Mimi ni nani ?

Mwalimu wa Kiswahili ni nani ?

Majina yangu ni Maeda Tumain, S mzaliwa wa mkoa wa Arusha, katika Mji wa Mto wa Mbu ulioko Wilaya ya Monduli. Nilisoma elimu ya msingi katika shule ya msingi Mto wa Mbu na kisha nilijiunga na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari Manyara. Baada ya hapo nilisoma masomo ya kidato cha tano na sita kwa mwaka mmoja.
Nilijiunga na masomo ya Shahada ya Elimu na sanaa (Bachelor of Arts with Education – BA Ed) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 2009.

Nimefundisha shule mbalimbali ikiwemo Green Acres, Cornelius Girls, Shule ya Sekondari Mbezi Beach na shule ya Sekondari Shaaban Robert. Pia nimekuwa nikifundisha somo la Kiswahili kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria tangu mwaka 2010.

Ni muasisi na mwenyekiti wa Umoja wa Walimu wa Somo la Kiswahili Tanzania (UWASOKITA), umoja ambao unalenga kuwaunganisha walimu wa somo la Kiswahili popote walipo ili kujadili na kutatua changamoto zinazowakabili katika ufundishaji wa somo la Kiswahili.

Kwa Mawasiliano :

(+255)717104507/766104507

mwalimwakiswahili@gmail.com

 

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!