VIGEZO VINAVYOSABABISHA UGUMU WA KUJIFUNZA LUGHA YA PILI

By , in Zote on . Tagged width:
                                          
          Vigezo
vinavyosababisha ugumu wa kujifunza lugha ya pili
1.     Hivyo
vipengele vitano vinavyojitokeza kurahisisha kujifunza lugha-mama huwa vigumu
kupatikana katika kujifunza lugha ya pili, yaani mazingira, muda, walimu,
mwingiliano na lugha nyingine, uhusiano na wengine.
1.     Mwingiliano
wa lugha-mama na lugha ya pili ni kigezo kikubwa sana. Mwanafunzi wa makabila
mbalimbali wanashindwa kukimudu Kiswahili kutokana na athari za lugha-mama zao.
Kuna matatizo ya:
(a)   
Kuchanganya sauti au kubadili sauti
k.m. chai (wanyakyusa)
kyai
(b)   Kuondoa
sauti
k.m. halafu (wahaya)
alafu
(c)   
Kuongeza sauti
k.m. mtu (wajaluo) mutu
(d)  
Kubadili sauti
k.m. thelathini
(wasambaa) selasini
Kila mtoto mwenye akili
timamu anamudu vizuri sana lugha-mama yake. Lakini inapofika lugha ya pili
panajitokeza matatizo mengi. Tutawezaje kupunguza matatizo hayo?
Kwanza, kujitahidi
kufuata kanuni zile za kujifunza lugha ya kwanza zinazowezekana k.m. kusikiliza
na kuzungumza kutangulie; kisha kusoma na kuandika.
Pili, ufundishaji ya
lugha ya pili pia uwe katika mazingira halisi. Mwalimu ujitahidi kutengeneza
mazingira halisi na kutumia mifano dhahiri. Kama vitu dhahiri kama nyoka,
waziri n.k. haviwezi kuletwa darasani basi picha na michoro dhahiri itumike.
Tatu, mwalimu utoe
mazoezi mengi na ya mara kwa mara. Mazoezi hayo yatajumuisha stadi zote za
kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika.
Nne, katika kufanikisha
kujifunza lugha ya pili, itabidi kuwa na marudio ya mara kwa mar. hii itasaidia
kujenga uzoefu na hivyo kuimarisha uzingatiaji.