Vidahizo vya Fani ya Utengenezaji wa Karatasi, Matofali na Vigae

By , in Kamusi on . Tagged width:

Vidahizo vya Fani ya Utengenezaji wa Karatasi, Matofali na Vigae

Aa

alumini ji aluminium: metali nyeupe laini na nyepesi ambayo hutumika kutengeneza nyaya za umeme, mabomba na mabati.

alumu ji sulphate: msombo ambao hufanya vitu vihimili moto.

alamu ya alumini ji aluminium sulphate: msombo ambao hutumiwa kutuliza nyuzinyuzi za karatasi na kuongeza ugumu wake.

Bb

bakuli ji trough: chombo mfano wa hori kinachotumiwa kwa kupondea vitu.


bakuli

bapa kv flat: -enye uso uliosawazika.

buluu ji blue: taz. buluu: MIANZI, MKONGE, UFINYANZINAKSHI NA MABUYU.

Cc

chumba cha kukaushia ji drying chamber: sehemu ndani ya jengo yenye joto inayotumika kuwekea vitu vyenye majimaji ili viwe vikavu.

Dd

dai ji dye: kioevu kinachotumika kukipa kitu kingine (kama karatasi, ngozi, nguo, n.k.) rangi.

dai asilia ji natural dye: rangi awali inayopata kitu kabla ya kupata rangi nyingine.

dhibiti ubora kt control quality: kuhakikisha kuwa ubora wa bidhaa unabakia katika kiwango chake au kuwa bora zaidi.

diako ji diacol: kemikali ambayo huzifanya chembechembe za karatasi (grains) zijipange vizuri na zishikane.

dohani ji chimney: bomba maalumu la kutolea moshi nje ya tanuri au jiko.

dutu ji substance: kitu chochote chenye mata.

Ee

eneo la kinu karatasi ji effective area of paper making: mahali au sehemu ambapo mchakato wa kutengeneza karatasi hufanyika.


dohani

fueli ji fuel: dutu yoyote inayochomwa kuwa chanzo cha joto au nguvu, k.m., makaamawe au petroli.

funjo ji papyrus: mmea wenye majani yanayofanana na nyasi ambao huota kwenye sehemu za majimaji na hutumika kutengeneza karatasi.

fyatua kt mould: tengeneza tofali kwa kutumia kibao maalum.

Gg

gome ji bark sehemu ngumu ya nje ya mti, au pengine huitwa gamba.

Kk

kalibu ji mould: kifaa kinachoyapatia umbo maunzi yanayomiminwa ndani yake.

kalibu karatasi ji paper mould: mashine au kifaa cha kuweka tetefya ya karatasi ili ipate umbo maalum.

kamua kt press: minya kitu ili kutoa maji, k.m., kukamua karatasi rojorojo.

kapi ji pulley: kifaa duara chenye mfuo kukizunguka.

kapi bapa ji flat pulley: roda isiyo na nafuo mbinuko.

kemikali ji chemical: dutu inayotumika au kutengenezwa katika kemia.

kiawiza maji ji water discharger: sehemu ya kutolea maji nje.

kiawizi ji discharger: sehemu ya kutoka kitu nje, k.m., dohani.

kigae ji tile: kipande cha udongo kilichotengenezwa kutokana na udongo wa mfinyanzi na baadaye kuchomwa. Hutumiwa kuezekea nyumba.

kihero ji vat: chombo cha kuwekea tetefya ya karatasi ili baadaye ikaushwe na kuwekwa katika umbo linalotakiwa.

kipashio ji beltlace: kipande cha chuma kinachotumiwa kuunganisha ukanda.

kishikio ji anchor: kitu kinachotumiwa kushikilia kitu kilichotundikwa.

kitambaatenga ji felt: kipande cha nguo ambacho huwekwa tetefya ya karatasi wakati wa kukausha.

kivutio ji driver: kifaa kinachotumiwa kutoa kitu kingine, k.m., roda, bisibisi.

kivuvio ji hopper: kifaa ambacho hupuliza hewa ya kukaushia kitu au vitu haraka.

kiwanda ji factory: mahali ambapo vitu hutengenezwa, k.m. kiwanda cha karatasi, nguo.

kiwinga ji repellant: kitu kinachozuia kupenya kwa maji au kioevu kingine.

kiwinga maji ji water repellant: dawa ambayo hutumiwa kuzuia karatasi isinyonye maji au wino.

kuru ji roller: magurudumu yenye uwezo wa kusafirisha vitu yakirivingika.

Mm

mafutakaukia ji drying oil: mafuta ambayo ni rahisi kukauka. Hutumika kwenye wino wa kupigia chapa na rangi za mafuta.

makaamawe ji coal: madini meusi yanayotumika kama fueli.

malighafi ji raw material: vitu vitumiwavyo, aghalabu viwandani, kutengenezea bidhaa.

mashine ya kukamulia ji hydraulic press: mtambo wa kukamulia karatasi kutoa maji.

maunzi ji material: taz. maunzi: USINDIKAJI MAFUTA, MATUNDA NA UTENGENEZAJI SABUNI.

mchakato ji process: mlolongo mzima wa kufanya au kutengeneza kitu au vitu.

mfereji ji chanuel: mtaro au njia ambamo maji au vioevu vingine hupita.

mfinyanzi ji porter: mtu anayetengeneza vitu vya udongo.

mkanda ji belt: kipande kirefu cha nguo, ngozi au mpara kinachozungushwa katika oda.

mumiani ji formalydehyde: kemikali ambayo hutumika kama mputio wa kuhifadhia karatasi zisioze.

Pp

pararisha kt bleach: kufanya rangi ya kitu ififie, k.m., rangi ya nguo.

poda pararishi ji bleaching powder: ungaunga unaotumiwa kufifisha rangi ya kitu, aghalabu, nguo.

pondeo ji beater: mashine ya kumeng’enyea au kulainisha malighafi ya karatasi. Pia tetefya.

Rr

rangi ji colour: kemikali inayotiwa katika vitu vionekane tofauti na vilivyokuwa awali.

roda ji pulley: taz. kapi

rozini ji rozine: dawa inayozuia karatasi zisinyonye maji na kupunguza uzito.

Ss

sampuli ji sample: mfano halisi wa kitu.

Tt

tanuri ji kiln: jengo ambamo matofali au vigae huchomwa.

tetefi ji pulp: kitu laini kama ujiuji. Nayo tetefi ni malighali ya karatasi inayopondwapondwa na kuchanganywa na maji.

tofali ji block: bonge linalotengenezwa kwa kuchanganya saruji, mchanga na maji.

trei ji tray: chombo bapa cha kubebea vitu chenye kingo zilizoinuliwa.


trei

trei ya mali ghafi ji feeding tray: chombo bapa cha kuwekea malighafi iliyo tayari kuongezwa kwenye mashine.

Uu

umeme ji electricity: nishati inayoweza kubadilishwa kuwa nuru au joto.

Vv

vali ji valve: kifaa kinachomhusu uingiaji na utokaji wa vioevu na gesi kuelekea upande mmoja tu.

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!