Vidahizo vya Fani ya Usindikaji Mafuta na Matunda, na Utengenezaji wa Sabuni

By , in Kamusi on . Tagged width:

Vidahizo vya Fani ya Usindikaji Mafuta na Matunda, na Utengenezaji wa Sabuni

Aa

asidi ji acid: kemikali ambayo ikitendana (ikimenyuka) na besi hutoa chumvi na maji, na ina uwezo wa kubadili litimasi kuwa nyekundu.

Bb

besi ji base: kemikali ambayo ikitendana na asidi hutoa chumvi na maji, na hubadili litimasi kuwa buluu.

Cc

chachuka kt ferment: kubadilika kikemikali kwa vitu vya kikaboni kwa kutendana na viumbe hai kama bakteria, n.k.

Ff

fua kt dehydrate: ondoa maji yote yaliyomo ndani ya kitu.

Hh

hasi kt sterilize: 1. ua vijidudu na viumbe vinavyosababisha maradhi. 2. fanya kiumbe kisiwe na uwezo wa kuzaa.

hatimiliki ji patent: kibali anachopewa mtu na serikali cha kumruhusu kutengeneza, kuuza kitu kwa muda maalum.

Kk

kabohidrati ji carbohydrate: msombo wa kaboni, hidrojeni na oksijeni, kama vile uwanga, sukari na selulosi.

kakamaza kt stabilize: fanya kitu tepetepe kuwa kigiumu kwa kutulizana.

kichochezi ji catalyst: dutu inayozidisha kasi ya mmenyuko.

kihawilijoto ji heat exchanger: kitumi cha kuhamisha joto la kioevu kimoja kwenda kwenye kioevu kingine bila ya kuchanganyika pamoja.

kihifadhi ji preservative: kitu kinachozuia uharibikaji au udhurikaji wa dutu.

kimeng’enya ji enzime: kichochezi ambacho kwa kawaida ni protini kinachotengenezwa na selihai.

kimeng’enywa ji substrate: dutu inayosahilishwa kwa ajili ya matumizi ya kujenga, kulinda na kutia joto mwilini.

kindaoksidishi ji antioxidant: kemikali inayozuia athari za ubabuzi wa metali, k.m., kupata kutu kwa chuma.

kinu ji mill: mashine itumikayo kuponda au kusaga mbegu za mafuta au nafaka.

kioevu ji liguid: kitu kama maji, maziwa, mafuta, au soda kinachoweza kumiminwa.

kioevu babuzi ji caustic lye: kioevu kinachotumika kutengeneza sabuni, nacho huunguza au huharibu kwa amali ya kemikali.

kiolwa ji object: kitu kinachoweza kuonekana, kusikika, kuhisika au kuguswa.

kitako ji base: sehemu ya chini kabisa ya kitu, hasa ile sehemu ambayo kitu husimamia.


kitako

kitambulisho ji label: kipande cha karatasi au maunzi kinachoambatishwa ili kukijulisha kitu fulani ni nini, cha nani au wapi kinatoka au kinapelekwa.

kiwangomchemko ji boiling point: halijoto ya kioevu kinapoanza kuchemka. Hali hii hutofautiana kutegemea kanieneo ya angahewa ya mazingira.

kiwangomyeyuko ji melting point: halijoto ambapo dutu hubadilika kutoka mango kuwa kioevu.

koleza kt concentrate: fanya kioevu kuwa thabiti kwa kuongeza kumumunyishwaji au kwa kupunguza kiasi fulani cha maji.

Mm

mafutaghafi ji crude oil: mafuta ambayo hayajapitia mchakato wowote wa usafishaji.

mafuta haradali ji mustard oil: mafuta yaliyokamuliwa kutokana na mbegu za haradali.

mafuta laini ji soft oil: mafuta ambayo yamesafishwa sana.

mafuta mahindi ji corn oil: mafuta yaliyotengenezwa kutokana na kukamua mahindi.

mafuta mimea ji vegetable oil: mafuta yanayotokana na usindikaji wa mbegu za mimea, k.m., alizeti, n.k.

mafutauto ji oil: mafuta ya majimaji yasiyoganda kwenye baridi.

magadi ji soda ash: kemikali inayounguza; inayochoma; inayomomonyoa mwili na vitu vingine. Fomula NaCh.

magadi babuzi ji sodium hydroxide: aina ya kemikali inayounguza, inayochoma, inayomomonyoa mwili au vitu vingine.

majinyongo ji brine: maji yenye madini mengi ya chumvi.

mango ji solid: kitu kisichokuwa kioevu au gesi.

maunzi ji material: chochote ambacho kutokana nacho kitu chaweza kutengenezwa.

menyu kv pure: isiyo na uchafu au mchanganyiko wa dutu yoyote nyingine.

midia ji medium: dutu inayoingilia kati ambayo inabidi kani au athari fulani ipite ndani yake, mathalani, hewa maji, metali, n.k.

mikrobiolojia ji microbiology: mtaala wa kisayansi wa viumbehai vidogovidogo sana kama vile bakteria, virusi, protozoa, kuvu, n.k.

mituamo ji statics: elimu ya jinsi ya vitu vinavyokaa katika hali tuli na kani za msawazisho.

mjao ji volume: kipimo cha nafasi kinachokaliwa na kitu.

msibiko ji contamination: hali ya kuwa chafu kutokana na kuguswa au kuingiwa na kitu.

mtovu kv centripetal: -enye kuelekea kwenye nukta.

mumunyisha kt disssolve: fanya kioevu kwa kutia ndani ya kioevu.

mvuke ji vapour: hali mojawapo ya mata ambapo dutu inakuwa katika hali ya gesi.

mvukemaji ji steam: maji katika hali ya gesi inayotokana na kuchemka.

myuko ji convection: msogeo ndani ya gesi au kioevu unaosababishwa na kioevu au gesi fukuto inayopanda juu na gesi au kioevu baridi kinachoshuka chini.

Nn

neli ji tube: mrija mwembamba

nishati ji energy: nguvu, na uwezo wa kufanya kazi.

nururisha kt radiate: piga kiolwa kwa miali ya nuru, joto, n.k.

Oo

ombwe ji vacuum: nafasi bila ya hewa au gesi ndani yake.

Pp

pimamchepuko ji refractometer: chombo cha kupimia kiasi cha mchepuko na kipeomchapuko.


pimamchepuko

pepetaka ji foreign matters: takataka ambazo huvunwa pamoja na mbegu zinazotoa mafuta; nazo hutolewa kabla ya ubanguaji.

Rr

regesha kt recycle: rudisha katika hali ya kwanza ili kitumike tena.

Ss

sabuni ya kimetali ji metallic soap: chumvi isiyomumunyika iundwayo na metali pamoja na asidi shahamu. Hutumika kuvifanya vitambaa visipenyeke na maji kwa urahisi na pia kama kikaushio cha rangi.

safisha kt refine: toa uchafu, k.m., kutoka kwenye sukari, metali, na mafuta.

shahamu ji fats: mafuta yanayotokana na wanyama, aghalabu ya kuganda.

Tt

themometa ji thermometer: ala ya kupimia halijoto.


themometa

Uu

uchepukaji ji refraction: badiliko la uelekeo wa mnururisho wakati wa kupita, kutoka na kuingia midia nyingine kutokana na mnururisho kuwa na kasi tofauti katika midia hizo.

ujazo ji capacity: nafasi inayopimwa kwa kuzidisha urefu kwa upana kwa kina.

ukebeshaji ji canning: hifadhi ya chakula katika makopo.

uoksidishaji ji oxidation: utaratibu au kitendo cha kuongeza oksijeni, kupunguza hirojeni au kupunguza eleletroni kwenye kemikali yoyote.

upasterizaji ji pasteurilization: kuua bakteria katika maziwa kwa kuchemsha hadi kufikia halijoto ya 60°C.

usindikaji ji milling: ukamuaji wa mbegu au tunda ili kutoa umajimaji uliomo.

utokaji ji emission: kutoka kwa kitu katika kitu kingine.

uvukizaji ji evaporation: ubadilishaji wa kioevu kuwa mvuke.

uzito wiani ji relative desinty: uwiano kati ya masi ya mata katika mjao fulani na masi ya maji yenye mjao sawa.

Vv

vitamini bandia ji artificial vitamin: taz. vitamini: SAYANSI KIMU.

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!