UTUNGAJI WA TAMTHILIYA

By , in Kidato I-IV Kidato V-VI on . Tagged width:

Dhima ya Tamthiliya

Tamthiliya ni kazi ya fasihi iliyoandikwa kwa lengo la kuonyeshwa jukwaani, ambapo wahusika huzungumza na kutenda vitendo mbalimbali. Tamthiliya huigiza maisha ya kila siku.

Kwa kuwa tamthiliya imeandikwa kwa lengo la kuigizwa huwa imeandikwa na maelezo ya jukwaani, maelezo yanayoonesha nini kifanywe na nani na kwa namna gani. Tamthilya hugawanywa katika maonyesho kama ambavyo riwaya inavyogawanywa katika sura.

Tamthiliya imegawanyika katika aina zifuatazo:

Tanzia;ni aina ya tamthiliya ambapo mhusika mkuu/shujaa anapata anguko kubwa au kifo ambacho huwafanya hadhira(walengwa) kuwa na huzuni.

Ramsa: ni tamthilia ambayo hulenga kufundisha kwa njia ya kuchekesha ili kuleta ujumbe mzito.

Vichekesho/Futuhi: ni aina ya tamthiliya ambayo lengo lake kuu ni kuchekesha kwa kutumia mbinu ya kutia chumvi mambo, kudhihaki na kukejeli.

Utungaji wa Tamthiliya

Katika utunzi wa tamthiliya kuna mambo kadhaa ya kuzingatia, mambo hayo ni kama yafuatayo:

  • Chagua jambo unalotaka kuandikia
  • Panga namna msuko wa visa na matukioa utakavyokuwa
  • Buni wahusika wako kulingana na kile unachotaka kukiandika
  • Chagua mandhari yanayofaa kulingana na visa zako
  • Tumia mtindo wa majibizano kati ya wahusika
  • Gawa tamthiliya katika maonyesho
  • Weka maelekezo ya jukwaa. Haya huelezea kile kinachotendeka kwa wakati ule. Maelezo ya jukwaa huwa katika maandishi ya italiki.

 

 

 

 

  1. MUUNDO WA HADITHI

 

MTIRIRIKO UCHAMBUZI           KINACHOLENGWA
Matukio yanayofuata mda Matukio yanafuatana kama yalivyojiri Kuelewesha hadithi moja kwa moja
Matukio ya mda mmoja Kuonyesha matukio yanavyojiri maeneo tofauti kwa mda mmoja au kuonyesha namna tukio moja linatokana na lingine Kujenga hisia au pingamizi
Flash back Tukio limeshawishika na tukio moja lililopita(kumbukumbu) Kutoa mwangaza kuhusu mahusiano, vyanzo vya tukio pamoja ya kujenga hisia kati ya wakati wa sasa na uliopita.
Maishara Kutoa mwangaza kwa kufuatisha tukio na ishara au maelezo( mf; one months later) Kuleta ukaribu na mkusanyiko wa mawazo pamoja.
  1. KASI YA TUKIO
  2. MDA BUBU: Ni mda wa kati ya scene mbili usiokua na tukio lolote, mda huu unabeba mda au eneo, unaweza ukabeba sekunde, dakika, saa, siku…

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!