UFUNDISHAJI WA KISWAHILI SEKONDARI : UTEKELEZAJI WA MUHTASARI WAKE

By , in WALIMU on .

Fulgence L. Mbunda

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

1.0 Utangulizi

Maandalizi ya ufundishaji wa somo lolote lile huanza kwa kudurusu muhtasari wake. Muhtasari ni matokeo ya malengo ya elimu pamoja na sera za nchi kuhusu elimu katika ngazi zake mbalimbali (chekechea, msingi, sekondari, vyuo). Hali kadhalika, unatokana na malengo na sera ambazo hubainisha masomo yake mbalimbali, Kiswahili likiwamo. Mada kwa kila somo huchaguliwa na kupangiliwa kufuatana na mahitaji na matakwa ya walengwa wake. Mbinu mbalimbali za kufundishia mada teule huainishwa, na hali kadhalika, tathmini yake huoneshwa kutokana na ufundishaji wa kila siku, mwezi, muhula na mwaka. Pamoja na hayo yote, muhtasari unaonesha pia vifaa mbalimbali vitakavyoendana na muhtasari huo, kama vile, vitabu vya kiada, ziada na vya rejea.

Muhtasari wa Kiswahili hauwezi kukwepa wasifu uliotajwa hapo juu. Fanaka katika utekelezaji wa muhtasari wowote ule, ukiwemo wa Kiswahili, inategemea sana kuwepo kwa sifa zote zinazostahili kila muhtasari kuwa nazo. Kazi ya mwalimu katika ufundishaji itarahisishwa sana iwapo muhtasari anaopaswa kuutumia umeundwa katika misingi toshelevu na una sifa zilizostahili. Mackey (1965:323-324) anaainisha sifa nne katika muhtasari wowote ule. BOFYA HAPA KUFUNGUA YOTE >>>>>>>>.UFUNDISHAJI WA KISWAHILI SEKONDARI UTEKELEZAJI WA MUHTASARI WAKE

Recommended articles