UCHUNGU (HADITHI FUPI)

By , in Fasihi Simulizi on . Tagged width:

Mbunda Msokile

I

Mpendwa Dora Charles,

Nilifurahi mno na hasa niseme nilipata maumivu makali na msisimko wa aina yake nilipokuona kwa mara ya kwanza ukiigiza mchezo wa Lina Ubani uliotungwa na P. Muhando, shuleni Kilakala, mjini Morogoro. Miondoko ya kuigiza kwako ulipokuwa ulingoni ilinichoma na kunipandikiza ari ya kutaka niwe nawe kwa kila hali. Naungama kwako kwa dhati kuwa siko tayari, wala sitakuwa radhi kuwa na mtu aitwaye mkc ambaye si wewe! Siku hiyo yaliyokuwa moyoni mwangu juu yako yalikuwa mengi. Nilishtushwa na umbo lako zuri. Nilifurahi.. U mzuri – macho makubwa na mazuri kama ya hua! Kwako wewe, jicho langu halitashiba kuona, wala sikio langu halitakinai kuisikiliza sauti yako! Kama sio ushujaa wa aina yake, naapa… ningewehuka! Maziwa yako mawili ni kama wanapaa wawili pacha… Mwili wako tebwere uliniteka mara moja!

Kama uwezo wa kubadilisha watu unaosemekana anao Mungu ungekuwa mikononi mwangu; naapa, nisingesita kukugeuza mara moja ili unifuate kwa kila hali. Aidha, nisingependa ulifikirie jambo hili kwa sasa wakati unapozongwa na kuzama sana katika kazi ya kuigiza, lakini nashauri ulifikirie kila pale unapopungukiwa na kazi hiyo.

Nina uwezo wa kutosha kifedha kama hilo pekee lingekuwa ndio kipimo chako cha kunikubali. Najua, kwako hili linaweza kukukera, linaweza kukuudhi ukafikiri kwamba mimi nimekuthaminisha na fedha! Lakini ningetamka lipi ambalo lingekutia zizi na zaa ya damu yako na kuamua kunifuata? Dora Charles, nisamehe kama kauli hii utaiona na kuiweka kuwa ni tusi kwako. Kwa kweli nimekosa neno lenye uzito unaosadifu dhamira yangu kwako!

Natamka waziwazi kuwa mimi si mjinga amhaye sijitambui kuwa sina utajiri, niko hohehahe kwa mtu wa aina yako. Lakini maskini naye hupenda, ana moyo wenye nguvu kuliko macho yanayoona. Maskini naye hupenda, kama wapendavyo wenye uwezo! Tcfauti huja kwa ule mtazamo tu. Nahlsi nttajikosesha haki kama siungami kwako kuwa umekuwa katika damu ya moyo wangu kwa siku nyingi sasa: miaka miwili si muda kidogo! Nimejifunza kukupenda katika dhiki na furaha, katika hali zote. Dora, kwa nini usiache kuitesa nafsi yangu vile na kuwa kitu kikamilifu kati yako nami? Unaowaona wanaishi katika majumba ya kifahari na kimaskini, walianza kama, mimi ninavyokuanza wewe. Ningekuwa na uwezo ningekuamuru uache kuwafurahisha watu wengine wasio hata na shukrani mbele yako!

Ukiwa rnkweli katika nafsi yako, nitakuwa tayari kabisa kulivumilia jibu lako. Nifanyie tajamali na haki ya kunijibu! Kwangu ndiyo au hapana, vyote nitavipokea na kuvivumilia baada ya kuvisubiri kwa hamu kubwa kama kipofa anayeona akategemea kupapasa kama kipofu asiyeona. Sitaacha kutumaini kuwa iko siku, au wakati utafika utakapoamua kufurahi nami ukiwa kama mke wangu, na ikishindikana nitaridhika uwe jirani, rafiki au mjuani!

Nilikuwa katika wasiwasi mkubwa, rnashaka mazito, lakini katika heshima ya aina yake… wakati wote huu. Nitaendelea kuwa hivyo! Nikiwa katika mguso mzito wa matumaini, naomba unielewe hivyo. Najikabidhi!

Ndimi,
Richard m’Banza

II

Kwako Richard,

Baada ya kuisoma barua yako nzito na kurnaliza yote, napenda kukuhakikishia kwa dhati kuwa nimeielewa sana. Aidha, nina kauli ya msingi kuhusu barua yako. Maafikiano yaliyofanywa mapema nilipotutuka titi kati yangu na mpenzi Mm. yameufanya moyo wangu ugande kwake. Sifikirii jambo liwalo duniani hapa litakalonibadilisha zaidi ya kifo! Tuliahidiana ndoa! Lini? Siku ya siku ikija, muda ambao yaliyo mbali yatakuwa yamekuja. Tunasubiri wakati. Lakini, kwa upande mwingine, ingawa tunasubiri muda, nyendo zetu zina ushahidi mkubwa wa maisha katika ndoa.

Ingawa naamua kulikataa ombi lako juu ya mapenzi yanayokusumbua kwangu, mimi si kwamba sina busara kiasi cha kutoheshimu ama kutothamini pendekezo kubwa na zito lenye lengo zuri kama hilo. Niamini nisemalo. Hivyo, naamini na pia kutumaini kuwa mawazo yote ya aina hiyo kutoka kwako juu yangu utayazima mara ukisha soma barua hii, na kwamba hutaanzisha tena upendo wa aina nyingine kwangu zaidi ya kupenda uigi.zaji wangu! Niamini, najivunia sifa zako nlizonitolea kwa moyo mkunjufu. Najinasua!

Ndimi,
Dora Charles

* * * *

Barua ya Dora imenikumbusha maudhi ya yule mwanamke Mwasi . Kwa hakika sijawahi kupata adha kama ya yule mwanamke! Kweli amenitenda… Nakumbuka alivyonilazimisha nimtumie fedha ili kutolea mimba yangu! Hapana, siwezi, nilimwambia. Nakumbukajinsi alivyokuwa ‘amekopakopa’ fedha za wanaume akina – Peter, akina… pale Mtwara, nami kudaiwa kumlipia madeni yote hayo! Tamaa imemshinda… Kwa kweli kupenda ni ubwege – ubwege na ujinga kabisa! Sikumbuki katika maisha yangu na mwanamke huyu kama aliwahi kunipa ‘asante’ yake, hata ya kinafiki baada kumletea zawadi rnbalimbali. Kila siku utasikia… oh khanga mimi sina, oh viatu sina, nataka gauni, nataka … mh, halafu nitumie fedha nikiwa kwetu! Tena lazima nisafir; kwa ndege… na kweli alikuwa akisafiri kwa ndege. Nakumbuka nilivyokuwa namtumia fedha pale chuoni wakati anasoma – sijawahi kumtumia fedha chini ya shilingi elfu moja – elfu moja wakati fedha za Tanzania zilipokuwa fedha! Mama mzazi… wala Baba mzazi hajawahi kupata fedha hizo! Lakini majibu yake? “Nimepata tufedha twako ulitotuma kwangu …” alisema! Kisha akaendelea “tena wewe mwanaume wa ajabu sana – huna akili! Umenifanya ‘nitembee’ na wanaume wengi, wakiwemo ‘mapadre’ wa hapa kwetu’ alisema.

Niliwazawaza tena kidogo. Ni kweli, mimi ni bwege. Kwa nini lakini mimi ni bwege hivyo? Hapana, ni maisha tu, hakuna shujaa wa mapenzi! Nilimpenda yule mwanamke, lakini nafikiri tatizo kubwa ni ‘tamaa’ kubwa kuliko uwezo aliyonayo yule mwanamke wa kwanza. Ni kweli, rnimi nimeonekaiia si chochote, akamfuata yule mwanaume anayeamini ana fedha – akabadili na dini! Ndiyo, amenikomoa, mimi bwege.. Lakini kwa nim niendelee kukaa bila mke? Ndiyo maana nimeamua kumtafuta mwenzi! Je, hii ndiyo ‘zawadi’ ya kutafuta mwanamke wa kuishi naye? Hapana, siwezi kukata tamaa. Dunia ndivyo ilivyo. Kusimama ni kinyume cha kuanguka na kulala! Kucheka ni kinyume cha kulia… Lakini mambo yote hayo ni muhimu katika kuukamilisha ulimwengu!

Maisha ni mapambano. Lazima nijitahidi kumshauri Dora. Dora ni mtu -msichana tu kama walivyo wengine! Kama yule mwanamke Mwasi alizaliwa mzuri nikampenda, basi nitamkuta msichana wa sifa nizipendazo nikampenda! Nitaendelea kumshauri Dora…

III

Mpendwa Dora,

Lazima nikuambie kuwa leo asubuhi nilipopata barna yako, moyo wamgu umeingiwa na wasiwasi na mashaka makubwa! Wasiwasi, kwa sababu ya tamaa kubwa juu yako! Mashaka, kwa sababu ya tamaa kubwa juu yako! Mashaka, kwa sababu nahofia kukukosa. Juu ya hayo, nina uchungu mkali! Si hilo tu, barua yako kwa muda iliufanya moyo wangu upige kwa kishindo kama nyundo.

Baada ya kusoma katika barua yako kuwa huna mpango wowote wa kunikubali, na kwamba una mwanaume, kwa hakika moyo wangu ulipiga ‘pap’! kwa mgutusho, nikajiuliza.nimemkosea» nini Mungu? Kwa muda nilikaa kimya; tuli, kama kwamba ningekuwa nimenyang’anywa ulimi wangu wa nge! Katika kukupenda nimeongeza mzigo katika moyo wangu? Unawezaje kufanya hivyo? Jicho langu lachuruzika mito ya maji… Jicho langu latoka machozi. Lisikome… Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu! Ah! Dora, niokoe tafadhali!

Dora… amini usiamini, jina lako ni kama marhamu iliyomiminiwa kwangu. Niliweza kutoa kilio cha radi katika chumba changu kwa machungu! Kasoro hapakuwa na mtu wa kunisikiliza zaidi ya dhamiri yangu. Ushuhuda ungeusikia. Niliweza kuikumbuka ‘ndoto yangu njema, kuwa wewe nami tulikuwa tukifuatana pamoja mkono kwa mkono kamajogoo na tembe! Wakati mwingine wewe mbele mimi nyuma – kama kumbikumbi. Nimenyong’onyea baada ya kusoma barua yako, na hasa nikikumbuka kwa sasa mapenzi yangu kwako ni kama moto unaoenea haraka na kuzunguka kichaka kikavu wakati wa kiangazi. Siku zote nimekuwa nikimtafuta vuvu – tipwatipwa, nikawa nimemgundua katika wewe! Lakini sasa unaniumbua?

Dora… kwa sababu ya.kilio changujuu yako, machozi mengi nimeyapoteza – yametiririka kama maji ya masika! Kwa muda wa masaa machache tu nimepoteza afya yangu! Wewe unaelewa, umuhimu wa afya yangu ni kama mafuta katika utambi wa taa. Utambi usipokuwepo, taa haiwaki kama taa! Mwili bila afya njema, hauwezi kuishi!

Dora… maneno yako kwangu yamekuwa sawa na msumari wa moto juu ya donda ndugu. Unaelewa uzuri ulionao ndio ulionivuta, acha kiburi! Nimekupenda, nimekufia nguvu, la ajabu lipi? Kwa nini niwe kama mtu aliyefungiwa kidoto? Macho yangu yako wazi, nimekuona. Mapenzi sikuyaanza mimi. Nimeyakuta kama ulivyoyakuta wewe. Kwa nini kunitesa kwa kunijibu ovyo?

Naamini kama walivyosema walimwengu: Maisha ya dunia ni bahari, mtu asiyejua kuogelea katika bahari ya taabu za maisha, mwishowe hutoswa. Ya nmi unitose katika bahari tesi ya dunia, Dora? Huna uchungu? Dora…

Kumbuka… Mwenyezi Mungu aliruhusu watu alipomtabiria Nuhu na wanawe katika kitabu cha Mwanzo 9:1-2 kuwa waende duniani wakafanye nini? “Zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi. Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani; pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu.” Alisema BWANA Mungu. Bila shaka BWANA Mungu alisema haya kwa furaha. Na kupitia kauli ya Mhubiri 4: 9-11 wa Biblia, aliwahi kushauri nini? “Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja. Maana wapata ijara (tuzo) njema kwa kazi yao… Na tena wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua. Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto…” Dora, ushauri huu Mtakatifu unaudharau? Tazama Mungu anavyotupenda viumbe wake, wewc hukiri hilo?

Sikiliza ushauri mwingine alioutoa Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho juu ya suala la ndoa. Paulo anasema hivi kwa Wakorintho 7:2-5: “… ( ) kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane…”

Dora… ingawa mapenzi m majani na huota popote; siko tayari kwa sasa kumtafuta mwingine nikayaotesha mapenzi yangu! Wewe umekuwa liwazo langu, nyota yangu – hua tukufu katika moyo na nafsi yangu!

Tazama – mti wa mahaba ulistawi kati ya Adamu na Hawa na ukatoa mizizi mikubwa, hadi ikawa vigumu kwao kutengana kwa dhiki na raha. Niliamini utakuwa pumzi ya uhai na maisha yangu, lakini kauli yako ya leo asubuhi imenikata maini. Imenikatisha tamaa na kunipanda uchungu! Kumbuka Dora, upendo una nguvu kama mauti, na wivu kwa binadamu ni mkali kama ahera kulivyo.

Dora, muda wa maisha ya mwanandamu ni mfupi mno. Mambo ya dunia ni ya kuja na kwenda. Kizazi huenda, kizazi huja, lakini dunia bado inaishi Jua lachomoza na kushuka mawioni. Upepo huvuma huko na kule na kurudia mzunguko wake. Wakati wanadamu tunapanga, tumwachie Mungu kupangua – Mungu anayesemekana mwenye kuweza yote! Kumbuka na ujue tuliyonayo leo, kesho hayapo. Maisha ya binadamu duniani ni mbegu za mche zikipeperushwa huko na huko angani. Iliyo nzuri hutua na kuota. Mimi nilipokufuata, mliamini kuwa ni muhimu kuwa pamoja (mume na mke) na kula maisha matamu leo kuliko kungoja kesho. Ujana ulionao ni sawa na moshi, ukienda haurudi! Dora nisamehe… Dora, nikubali! Walisema wahenga, ‘usifanye haraka kukasirika na kuchukia rohoni mwako. na aheri mvumilivu na msamehevu rohoni, kuliko mwenye roho ya kiburi.’

Dora… sina neno linalotosha kukushauri kama yote niliyokueleza hayajakushauri. Wanasema-nia njema ni tabibu! Nia mbaya huharibu! Sina nia mb aya kwako Dora…

Penzi halina uchaguzi: si mzee, si mtoto, si mkubwa, si maskini, na wala si tajiri, kila mtu hupenda. Mapenzi hayana digrii – msomi na asiyesoma, wote hupendana. Kila uchao, mapenzi yangu kwako yamezidi kuimarika. Ila nimekuwa nikikatishwa tamaa na majibu yako. Dora…

Dora, wakumbuke na wafikirie vipofu duniani walivyo… · wanapendana na kila mtu ana wake! Wanaonana vipi, Mungu anajua… Wafikirie viwete duniani – hujivuta na kujikokota matopeni, lakini kila mtu na mpenzi wake. Hawajui lini watasimama wapate kufaidi mapenzi yao kwa misakato ya rhumba! Wafikirie wagonjwa wa akili, kila mtu ana wake. Wakutanapo husahau maradhi yao, hawajitambui wakiwa ndani ya mapenzi. Wewe na mimi tuna akili timamu, kulikoni? Afadhali ningekutana na simba mwenye njaa ya siku kumi kuliko ukatili unaonifanyia! Mimi kisonoko? Na kisonoko naye hupenda…

Dora… nakuomba tena kwa mara ya mwisho na hali zote unikubalie. Tafadhali nikubalie. Nitakuwa mume mwema na mwaminifu. Na tazama, maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, na wala mifuriko ya mito haiwezi kuzamisha upendo. Nakushauri unifikirie kwa dhati. Nikubalie!

Ndimi
Richard m’Banza

IV

Kwako Richard,

Ni vema kutambua kwamba kila mtu katika maisha ana mipango yake. Tupende tusipende hili haliepukiki. Tena huukamilisha ulimwengu… Kama wewe unavyotamani na kupanga unioe mimi, nami pia nimepanga kukukana na kulizingatia penzi langu na Mm. Yawezekana hupendi kusikia hilo, lakini itakusaidia nini kutokukuambia ukweli? Tazama, Mhubiri 1:9-10 wa Biblia alikumbusha juu ya maisha na matendo ya mwanadamu hivi: “Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na ndiyo yatakayotendeka; walajambojipya hakuna chini ya jua. Je! kuna jambo lolote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi.” Kauli hizi zinaonyesha kuwa kati yetu yatakayotokea hayana upya wowote kwani yalikwisha kuwako.

Suala la upangaji wa mambo miongoni mwa binadamu ni muhimu. Aidha, si lazima kila linalopangwa linaweza kukubalika kwa wote. Kwako labda ungeshangilia kama mipango yangu na Mm ingeshindwa nawe kwa upande wa pili kushinda. Richard, ni kweli unanipenda. Lakini unajua wangapi wananipenda? Tazama, mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai. Pole, umenipenda, lakini sina la kukupa. Siwezi kukupenda.

Richard, sioni kwanini huwezi kunielewa. Wala sipendi ushindwe kunielewa. Siko tayari kushiriki majuto nawe.

Nashindwa kukukubalia kwa sababu mapenzi ya Mm yametandaa kona na kona ya moyo wangu. Ana umbo zuri… anatabianzuri… anautu… uso wake ni wa kirafiki na mcheshi, hunikaribisha kwa furaha hata kama kuna lindi la machungu! Mara zote hunikata kiu ya dhiki ya kila aina. Nami humfurahisha kwa wororo wa mwili wangu… humfurahisha kwa biwi la mapenzi linalotoa ndimi za moto! Vivyo Mm hunifurahisha. Tunakarnilishana. Siku zote huwa na furaha… furaha hunitambaa moyoni kilajua linaponikonyeza likijitokeza na kuramba ukungu na umande kwa miale yenye joto la asubuhi.

Yawezekana Richard umedanganywa na wanaume vijana wenzio kuwa ‘Dora’ ni ‘njia’ ama ‘uwanja wa mpira’ wa kumalizia mihati yako. Ikiwa hivyo ndivyo, waambie wenzako kuwa mmedanganyika. Mimi si chombo cha kumalizia matatizo ya mwili wako. Kama mapenzi yako ni mazito sana, basi utambue pia katika wingi wa mapenzi kuna huzuni. Nimekuambia wazi kuwa nafasi niliyonayo ya kupenda katika maisha yangu nimeshaitumia kwa mwingine. Lakini wewe huelekei kuelewa zaidi maelezo yangu. Naelewa, mapenzi yako kwangu ni mengi (unavyodai) kama mchanga wa bahari – ndiyo sababu labda unaniganda kama kupe juu ya damu ya mbwa mzee! Tafadhali usiniendeshe sana, nisije konda n’kawa mwembamba kama ufito. Tena, usije ukanirushia ndege wangu wa udi na uvumba! Nia yako ya urafiki kwangu yafanana na walimwengu wengine walivyo: wanakuganda kama sukununu ama umande wa asubuhi, najoto lajua likizidi, urafiki unapukutika!

Richard! Kwangu ni wazi mambo hayajakukalia vizuri! Tena, nakuomba na kukushauri uniache, usiutekenye polepole moyo wangu kwa maudhi ya machungu. Mtafute mwingine. Usikate tamaa! Jitahidi!

Ndimi
Dora Charles

V

Mpendwa Dora,

Siwezi kujizuia kutoa machozi ya uchungu. Ingawa nilitegemea jibu lolote kutoka kwako, jibu la kukataliwa linauma sana na kuipasua nyongo. Kukataliwa ni kubaya, walisema wahenga. Lakini uchungu utafaa nini kwangu ikiwa roho mwamuzi wako wa mwisho ameshatoa uamuzi wake? Najuta…

Nasita kukubali na kuamini kuwa jibu lako ni la mwisho, na kuwa limenikatisha tamaa. Nasema hivyo kwa misingi ifuatayo: Kwanza, ni kweli kuwa mmefanyiana ahadi ya ndoa na huyo Mm wako. Lakinihiini ahadi… Na ahadi ni ahadi, ni mwanzo wa tendo, bado si tendo! Dora… tuseme leo Mm ameuawa katika ajali, hungeweza kutafuta mwanaume mwingme atakayekufaa? Au itokee Mm amempata Mchuchu mwingine mwenye titi tute kifuani kama mdomo wa kuku, akaamua kukuacha, hutampenda mwingine badala yake? Na hutashikwa na mihati! Dunia ni kigeugeu, dunia ni tambara bovu, Dora! Dunia ni kinyonga, la jana kesho haliko, lililoshindikana likawezekana. Kwa kauli hizi, nakushauri tena kuwa usijisahau kabisa ukadhani ngamba kashika kamba! Pili, kwa jinsi nikuuguliavyo, sikulazimishi kufunga ndoa nami.

Nimesema nina hiyari kuwa rafiki, jirani au mjuani wa ndani! Labda ningeongeza la nne… niko radhi kuwa mume wako wa akiba, nisubiri kuchukua nafasi wenyewe wakiumia! Naungama tena kwako kuwa mimi sistahili bado kuusumbua moyo wako, lakini panapo ukweli unaogusa kwa njia yoyote ile, lazima tuuseme, ili kesho watakaosikia kilio changu wawe mashahidi na nguzo kubwa ya kauli zetu!

Dora, nakuomba fikiria upya juu ya suala lote. Nimeweka ahadi kuwa mwaka huu lazima niamue kuwa na mtu wa aina yako. Ingawa umeshanipa jibu lililonichoma moyo na kuniumiza, nakuhakikishia kuwa sijakata tamaa. Natumaini!

Ndimi
Richard m’Banza

VI

Kwako Richard,

Naambiwa kuna baadhi ya makabila ya dunia hii – yasemekana baadhi ya makabila ya sehemu za Mashariki ya Mbali – mke mmoja huolewa na wanaume zaidi ya mmoja na wote huishi pamoja katika nyumba moja. Nimehakikishiwa kuwa hizi ni habari za kuaminika na kwa hiyo zisipuuzwe! Lakini huko ni Mashariki ya Mbali; kuna misingi yake ya maisha ya kisiasa na kitamaduni. Tujifunze, lakini tusichukue kila kitu chao!

Nimekueleza mifano hii, Richard, ili kukuongoza wapi unaweza kutafuta wanawake wanaoelekeana na tabia na mawazo yako! Wanawake wa akiba… Mimi sma nafasi ya kuwa na mwanaume wa akiba!

Katika kabila letu sisi tunafundishwa kuwa mume mmoja huwa na mke mmoja. Uvunjaji wa uaminifu wa ndoa husababisha watu kuuana! Baadhi ya watani zangu huko Kusini mwa Tanzania hufundishwa katika unyago kuwa sifa ya uzuri wa mwanamke inatokana na kupendwa na kuwa na wanaume wengi siku hadi siku. Jitahidi kuangalia huko, labda utafanikiwa kuopoa mmoja! Naambiwa wanawake wa huko huweza kusafiri hata maili tano wakati wa usiku ili kuwafuata wanaume. Jaribu bahati yako huenda utafanikiwa.

Suala la ajali kwa mpenzi wangu Mm silijali. Kwanza – nani ana uhakika na maisha yake? Je, unaweza kusema utakuwaje saa moja tu inayofika mbele yako? Ajali ni ajali – haiteui siku wala sura. Haijali rangi wala cheo… Hata wewe ukinioa inawezekana nikafa siku hiyo kabla hatujaishi. Nani atakuwa amepata au kupatikana?

Jitulize, Banza! Poa moyo! Huna bahati nami! Pole!

Ndimi,
Dora Charles.

VII

Dada Dora,

Watu husema: “Asiyekubali kushindwa si mshindani.” Usemi huu ni mzito, nami naelekea kuupokea na kuuamini bila badiliko lolote lile. Nimekubali kushindwa juu yako, japo hili silipendi aslan. Lakini kutopenda kwangu kutasaidia nini? Nakutakia heri. Nina masikitiko yasiyoneneka. Lazima nitaomboleza! Nitaomboleza mchana na usiku nitaomboleza! Nitaomboleza leo, na kila siku nitaomboleza… Nitaomboleza!

Mimi ni mtu aliyeona mateso
Kwa fimbo ya ghadhabu yake
Ameniongoza na kuniendesha katika giza
Wala si katika nuru
Hakika juu yangu angeuza mkono wake
Mara kwa mara mchana wote

Amechakaza nyama yangu na ngozi yangu
Ameivunja mifupa yangu
Na kunizungusha uchungu na uchovu
Amenikalisha penye giza
Kama watu waliokufa zamani

Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka
Ameufanya mnyororo wangu mzito
Naam, nikilia na kuomba msaada
Huyapinga maombi yangu
Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa

Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye
Kama simba aliye mafichoni
Amezigeuza njia zangu, na kunirarua-rarua
Amenifanya ukiwa
Ameupinda upinde wake
Na kunifanya niwe shabaha kwa mshale

Amenichoma viuno
Kwa mishale ya podo lake
Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote
Wimbo wao mchana kutwa
Amenijaza uchungu
Amenikinaisha kwa pakanga

Amenivunja meno kwa changarawe
Amenifunika majivu
Umeniweka nafsi yangu mbali na amani
Nikisahau kufanikiwa
Umetufanyakuwa takataka, na vifusi
Katikati ya mataifa

Nitajuta!

MAOMBOLEZO, 3:1 – 17:45

Ndimi,
Richard m’Banza

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!