TATHIMINI YA MATINI ILI KUTAMBUA UBORA NA UDHAIFU WAKE KATIKA TAFSIRI

By , in Zote on . Tagged width:
 
Tuanze  na maana ya matini kwa mujibu wa
wataalamu mbalimbali kama vile :Wamitila (2003) ameeleza kuwa matini inaweza
kueleezwa kama kifungu cha maandishi au usemi wa lugha. Huweza
kuelezwa  kwa kuangalia maumbo  ya kazi yake.
Oxford dictionary (2000) inaeleza matini kuwa ni
andiko au chapisho linalohusu maudhui zaidi kuliko fani. Kutokana na maana hii
tunaweza kusema kuwa si matini zote huzingatia zaidi kipengele cha fani na
kuacha maudhui bali zipo ambazo huweka usawa katika vipengele hivyo na nyingine
kama za kisiasa na zile za kisayansi zinahusisha zaidi kipengele cha maudhui
kuliko fani. Hivyo kutokana na fasili zilizotolewa na wataalamu tunaweza
kufasili matini kuwa:
Ni wazo au mfululizo wa mawazo ambao unajitosheleza
kimaana. Au matini yaweza  ni neno moja, kirai, kishazi, sentensi,
aya, au kifungu cha habari ambacho kinajitosheleza kimaana chenye ujumbe au
wazo linalojitosheleza.
Katika tafsiri tunafanya tathimini ili kujua ubora
na upungufu wa tafsiri husika. Neno tathini wataalamu wanatueleza kama
ifuatavyo:
Wamitila (2003) anaeleza kuwa: kimsingi tunapotaja
tathmini kuhusina na kazi za kifasihi humanisha kupima ubora na udhaifu wa kazi
inayohusika. Mhakiki anaweza kupima kazi hiyo kwa kuiangalia maudhui yake au
muundo wake kwa ujumla.
Lakini kutathmini tafsiri ni zoezi la kupima kiwango
cha ubora wa tafsiri husika kwa kutumia mbinu zilizokubalika. Hivyo
tunavyofanya tathmini ya tafsiri tunaweza kupata makundi makuu manne. Makundi
hayo ni kama yafuatayo:
·         Tafsri
bora
·         Tafsiri
tenge
·         Tafsiri
finyu
·         Tafsiri
pana.
Katika kufanya tathmini kuna aina kuu mbili za
matini ambazo zinaweza kufanyiwa tathmini, matini hizo ni
kama  zifuatazo:
Matini lengwa zilizo katika mchakato wa kutafsiriwa.
Matini hizi ni zile ambazo hazijafikishwa kwa mteja. Katika matini hizi mfasiri
anaweza kutathmini tafsiri yake kwa lengo la kuiboresha kabla ya kuipeleka kwa
mteja.
Matini lengwa zilizo katika mikono mwa mteja. Matini
hizi mfasiri hufanya tathmini kwa lengo la kutoa maoni ambayo yatamwezesha
mfasiri kuboresha kazi nyingine atakazozifanya baadae au kama atatoa toleo
jingine.
Katika kufanya tathmini,  tamthiliya hii
ya “Black Hermit” iliyoandikwa na Ngugi wa Thiong’o (1968) na
kutafsiriwa kama “Mtawa Mweusi” na East African Educational
Publishers Ltd. (2008), tumetathmini kwa kuangalia vipengele vifuatavyo:
Sarufi: katika kipengele hiki tumeangalia uzingativu
wa vipengele vya kisarufi kama vile upatanisho wa kisarufi na upotoshaji wa
maana.
Jukumu la kwanza la mfasiri ni kuhakikisha kwamba
anazingatia na kuhifadhi upatanisho wa kisarufi wa matini chanzi. Lakini wakati
mwingine jukumu hili halitekelezeki mfano wafasiri wa tamthiliya ya “Black
Hermit”
iliyotafsiriwa kama “Mtawa Mweusi” hawajazingatia
upatanisho wa kisarufi na kufanya matini ya tafsiri ipoteze ubora wake.
      Mfano : Matini
chanzi:  sorting out beans spread  in a basin. (Uk
1)
          
        Matini lengwa:  akichagua harage
katika bakuli.
 (Uk1)
                   Matini
chanzi: if this be a curse put upon me (uk4)
                   Matin
lengwa: kama hili ndilo laana nililopewa…(uk4)
Katika tafsiri ya kiswahili neno la kiingereza “beans” limefasiriwa
kama “harage” badala ya “maharage” na pia katika tungo
ya kiingereza “if this be a curse put upon me” limetafsiriwa
kama “kama hili ndilo laana nililopewa”badala ya “kama hii ndio
laana” 
tungo hizi zimefanya kukosekana kwa upatanisho wa
kisarufi katika matini lengwa.
Katika suala la maana yawezekana mfasiri akachagua
maana isiyo sahihi kati ya maana nyingi zilizo katika lugha lengwa za neno
katika lugha chanzi. Mfano
Matini
chanzi:                                                             Matini
lengwa
… in a basin
(uk1)                                                  :
…katika bakuli(uk1)
 …carrying                                                            …akichukua
Do without
husband                                          siwezi
kuishi bila mwanaume
I have tasted the pains of
beating               nimeona
maumivu ya mapigo
.
Katika tafsiri ya Kiswahili neno la kiingereza “basin” limefasiriwa
kama “bakuli” badala ya “beseni”, neno “carrying” limetafsiriwa
kama “akichukua”badala ya “akibebelea”, neno “do” limetafsiwa
kama “kuishi” badala ya “kufanya” na neno “tasted” limetafsiriwa
kama “nimeona”  badala ya “nimeonja”. Uteuzi wa
maana za  msamiati katika matini legwa umepotosha maana iliyokusudiwa
na mwandishi wa matini chanzi.
Kipengele cha pili ni muundo: kipengele hiki
kinahusu ulinganifu wa mpangilio kati ya matini chanzi na matini lengwa.
Tamthiliya ya “BlackHermit” ambayo ni matini chanzi imetumia
muundo sahihi wa tamthiliya ambapo majina ya wahusika yanatokea kushoto. Lakini
matini lengwa ambayo imetafsiriwa kama “Mtawa Mweusi” wafasiri
wameitafsiri kwa muundo wa filamu, ambapo majina ya wahusika yamejitokeza
katikati ya maelezo ya wahusika hivyo kukiuka muundo wa matini chanzi.
Vipengele vingine ambavyo tunaweza kuvifanyia
tathmini katika tafsiri hii ya “Mtawa Mweusi” ni kama vile
udondoshaji, upunguzaji na uteuzi mbaya wa maneno.
Udondoshaji: wafasiri wa matini hii kuna baadhi ya
maneno ambayo ni ya msingi kukamilisha wazo au habaha ya msanii au mwandishi
hayajitokeza ambayo yalikuwapo katika matini chanzi. Kwa mfano:
               
Matini chanzi:  This temptation harping on weak flesh (uk4)
               
Matini lengwa: Jaribu hili linalirudia rudia mwili wangu (uk.5)
                                                                      
Neno “weak” ambalo lipo kwenye matini
chanzi halijafasiriwa katika matini lengwa na lilipaswa kufasiriwe kama “dhaifu”.
Uongezaji: katika matini lengwa kuna baadhi ya
misamiati imeongezwa na wafasiri wakati katika matini chanzi haijatokea.
Mfano:
Matini chanzi:  A woman without a child
is not a woman.
  Uk.
4             
Matini  lengwa:  Mwanamke
bila mtoto si mwanamke timamu.   Uk 3
Neno “timamu” lililotumiwa na wafasiri
wa matini lengwa halipo kabisa katika matini chanzi.
Uteuzi m’baya wa msamiati: katika tafsiri ya “Mtawa
Mweusi”
 wafasiri wameteua na kutumia visawe ambavyo vimesababisha
upotoshaji wa ujumbe katika matini lengwa. Mfano wa viswe hivyo ni pamoja na :
Matinichanzi:  Have seen sunrise and
sunset. 
(pg. 3)
                        I
have tested the pains of beating.
 (pg. 3)
                        Together
with power of the tribe.
 (pg.
10)               
Matini  lengwa: Yameona  kuchomoza
na kuingia kwa jua
. (uk. 3)
                           Nimeona
maumivu ya mapigo. 
(uk. 4)
                           Pamoja
na nguvu ya taifa. 
(uk. 10)
Katika matini ya lengwa wafasiri wameteua na kutumia
visawe visivyokubalika kulingana na visawe vilivyotumika katika matini chanzi.
Wafasiri wametumia neno “I have tested” kama “nimeona” badala
ya “nimeonja” pia neno “tribe” likafasiliwa kama “taifa”.
Katika kufanya tathmini hususani katika kazi hizi
mbili za tamthiliya tafsiri iliyofanyika ina mapungufu katika kila kipengele
ambavyo ni msingi kuvizingatia wakati wa kufanya tafsiri. Vipengele hivi
vimewakumba wafasiri wa tamthiliya labda kutokana na sabau za kutofatiana
kiutamaduni, ujuzi wa lugha hizi kwa wafasiri wenyewe.
MAREJELEO
East African Educational Publishers Ltd (2008) Mtawa
Mweusi.
 Kenya: Sitima Printers  Stationers Ltd
Ngugi wa Thing’o (1968) Black Hermit.
Kampala-Uganda: East African Educational Publishers Stationers Ltd
Oxford Dictionary (2010) Oxford Advanced
Learner’s Dictionary of Current English
. New York: Oxford University
Press.
Wamitila, K.W (2003) Kamusi ya Fasihi:
Istilahi na Nadharia.
 Nairobi-Kenya:Focus: Publication Ltd.