SIMULLIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 14…

By , in Simulizi on . Tagged width:

…SEHEMU YA 14…
Ngome kubwa :6:20pm
Gavana Richald Robeni aliingia tena ndani kasri lake,alipotaka kuketi kwenye viti vyake,ghafla akasikia muungurumo wa helikopta, muungurumo ulikuwa mkubwa sana, bila shaka zilikuwa helikopta zaidi ya moja, akatoka nje haraka sana, akatazama juu ya anga la ngome yake, akatabasamu, helikopta tano zenye rangi nyeupe iliyopambwa na bendera za kichina,ziliwasili katika ngome yake, alifurahi sana, bila kutambua kuwa alikuwa amejichimbia kaburi yeye mwenyewe.

“,Welcome, karibuni sana kwenye makazi yetu …”,gavana alitoka nje ya kasri lake, akasogea mpaka kwenye kiwanja chao cha ndege, akawapokea askari wapya, akasalimiana na kiongozi wa jeshi hili wakapigiana saluti za heshima.

“,Asante, samahani sana kwa kuchelewa …”,kiongozi wa jeshi la kichina aliongea, akaomba samahani,mkononi alikuwa ameshika fimbo yake ya kijeshi, akiipiga piga mkononi.

“,Ondoeni shaka kabisa,hamjachelewa, kesho asubuhi na mapema tutaelekea vitani, “gavana aliongea.

“,Ok, can you give me the map of that forest? “,(sawa, unaweza kunipatia ramani ya huo msitu? “,kiongozi wa jeshi la kichina aliuliza, alitaka kuijua ramani, awapangie majukumu vijana wake. Gavana alijishika shika na mikono yake, akapekua mifuko ya nyuma ya suruali yake, hakuona ramani, akapekua mifuko ya shati lake, akaipata ramani katika mfuko upande wa kushoto, akampatia jenerali yule, wakashikana tena mikono, kila mmoja akachukua hamsini zake, gavana alirudi katika kasri lake, kiongozi wa jeshi la kichina akaongozana na vijana wake, mpaka kwenye vyumba vyao vya wageni.
…………………………………
Gano :Nusu saa iliyopita
Hwang lee alitabasamu,muda ambao aliusubili kwa hamu ulikuwa umewadia, alitamani sana kumiliki koloni la nchi ya Goshani, nchi ambayo ilijaa utajiri wa kila aina, madini, pembe za ndovu, ardhi yenye rutuba pamoja na nguvu kazi ya kutosha.

“,Lazima niwe mtawala wa Goshani,this is the only chance I was waiting for, lazima nitawale Goshani, lazima! “,Hwang lee aliongea yeye mwenyewe, ndani ya ofisi yake, akanyanyua simu ya mkonga, akapiga, baada ya dakika mbili, akakata simu, alikuwa amemaliza kufanya mazungumzo na mtu aliyekuwa anamuhitaji.

“,Ngo ngo, ngo ngo! “,mlango wa ofisi ya gavana wa kichina uligongwa, gavana katili aliyependa kutawala kila kona za dunia, huku akitumia jeshi lake kueneza utawala wake.

“,Get in!, ingia ndani ,mlango uko wazi …”,Hwang lee aliongea,mlango ukafunguliwa,kisha ukafungwa tena, mtu aliyekuwa amempigia simu alikuwa amesimama kwa heshima mbele yake, fimbo yake akiwa ameiweka na kuibana kwenye kwapa lake, akapiga saluti ya kijeshi.

“,Goshani wanapigana vita, waafrika they need to be free, wanataka uhuru wao, tumepigiwa simu na gavana Richald tukatoe msaada, muda mrefu tulitamani kumilika koloni hili, sasa muda umefika, chukua askari mia moja, nenda huko, fanya mbinu yoyote ile, gavana Richald auwawe, halafu uwa na hao waafrika walioanzisha vita! “,gavana Hwang lee alitoa maelekezo.

“,Sawa mkuu, nimekuelewa, kila kitu kitakwenda sawa,usiwe na shaka! “,jenerali na kiongozi wa jeshi la kichina aliongea, akapiga saluti, kisha akaondoka zake, tarumbeta kubwa ya kijeshi ikapigwa, katika ngome ya gavana, askari wote wakakusanyika..

“,Tunaenda kwenye vita ya dharula,Goshani inapigana vita, koloni la Waingereza na waafrika, tunaenda kutoa msaada, na kuliweka koloni hili katika himaya yetu!,nahitaji askari mia moja tu wa kuondoka nao”,kiongozi wa jeshi la kikoloni alitoa maelekezo kwa jeshi lake, vijana wake wakaluka juu kwa shangwe, walipenda sana kupigana vitaa.

“,Iyeeeeee, “zilikuwa ni shangwe za kufurahia vita, askari mia moja wakaingia katika helikopta zao za kivita, bunduki zao zikiwa mikononi, baada ya dakika tano helikopta ikapaa angani,ikaiacha ardhi ya kisiwa cha Gano, ikaelekea bara,nchini Goshani, nchi zote zikipatikana Afrika ya mashariki.

…………………………………
Msitu wa mikoko :8:00
Jeshi la Waafrika lenye askari arobaini tu kwa sasa, hawakulala, waliendelea kujiandaa na mapambano,walitega mitego kama kawaida yao, walichimba shimo lingine katikati ya barabara nyembamba iliyoingia msituni, ndani ya shimo wakaweka miti iliyochongoka kama mikuki, kisha juu ya shimo wakaweka fito dhaifu zenye uwezo wa kukatika, wakatandaza nyasi, wakaweka udongo juu yake,wakasambaza, haikuwa rahisi kuutambua mtego huu,barabara ilisawazishwa vizuri kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu kutofautisha mahali penye mtego na pasipokuwa na mtego.

“,Vuta juu hilo gogo,lazima liwauee tena kama nzige …”,mzee Nyamigo aliongea,Mpuzu akiwa juu ya mti akalivuta vizuri gogo, juu ya mti, usawa wa barabara, gogo ambalo liliunganishwa na kamba mpaka barabarani, kisha kamba ikafukiwa, yoyote yule ambaye angepita barabarani kizembe na kujikwaa kwenye kamba, kamba ingefyatua mtego, gogo likamuangukia na kumuua palepale.

” ,Yes, well done, tumemaliza, kwa sasa tusikae kwenye miti, wameshajua mahali tulipojificha mwanzoni, watu ishirini wakae katika vichaka upande wa kushoto, wengine ishirini wakae vichakani upande wa kulia “,Angel Richald aliongea, hakuna aliyemuelewa, wote wakabaki wanamtazama, walikuwa hawajui kusoma, kuhesabu wala kuandika.

Mwamvua akaifanya kazi hiyo, alikuwa mtundu sana, siku zote alipenda kujifunza, alifahamu kila kitu mpaka lugha ya kizungu, bila hata kwenda shuleni, alijifunza kupitia wakoloni alioishi nao, alikalili kila kitu walichokifanya ambacho aliona kitamsaidia ,baada ya kumaliza kuwahesabu askari wa kiafrika, na yeye akakaa katika kundi moja lenye watu kumi na tisa,kisha wakaingia vichakani, pembeni ya barabara, wakajificha,kusubili vita…

…………………………………
Ngome kubwa :9:30pm
Kikao cha siri kiliendelea ndani ya vyumba vya wageni,askari wa kichina walipanga mipango yao ya siri kumuua gavana Richald Robeni, kisha waweze kuwa watawala wa Goshani.

“,Sisi tuna askari mia moja tu, wao wako wengi, japo hawazidi mia mbili, mimi nitaenda na gavana, katika gari moja, nitamteka na kumfunga kamba,mlinzi wake nitamuua, hana uwezo wa kupambana na mimi, kisha jeshi la Waingereza, tutawaambia watii amri zetu, kwenye vita na Waafrika,ili kuyaokoa maisha ya kiongozi wao, mtaenda vitani mkirudi mahali mlipotuacha, nikiwa nimemuweka mateka gavana, mtakuta nimemuua,akiwa ndani ya gari, bila wao kujua kama amekufa,nitawaambia waweke silaha chini kumpata gavana wao,wataweka silaha chini, kisha tutawashambulia kwa risasi, mchezo utaishia hapo! “,jenerali wa kichina alitoa maelekezo na mpango wake wa kufanya shambulio, wote wakamuunga mkono. Baada ya kikao, kila mmoja akajipumzisha kitandani, akiisubili kwa hamu asubuhi, siku inayofuata.

.……ITAENDELEA …

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!