SIMULLIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 12…

By , in Simulizi on .

…SEHEMU YA 12…
Msitu wa mikoko
Angel Richald alikuwa hana silaha yoyote ile,moyo wake ulikuwa na maumivu makali baada ya kumuua mama yake mzazi kwa mikono yake mwenyewe,nguvu zikamuishia, akajikuta ameiachia bunduki yake bila kupenda.Mpuzu Yahimana, mpenzi wake Angel, alihuzunika kwa kile kilichotokea, japo alikuwa vitani kupigania uhuru wa Mwaafrika, lakini hakuwahi kufikiria kuwaua wazazi wa Angel, viongozi wa serikali ya kikoloni, gavana Richald Robeni, pamoja na mke wake malikia Magreth hata siku moja, jeshi la kikoloni walizinyosha silaha zao juu ya mti, mahali risasi ilipotokea na kumuua malikia Magreth, mahali kilio cha Angel kilikuwa kinasikika…

“,Shoot them, kill all of them including my daughter, she has killed her mother, she has killed my wife ……”,( wapigeni na risasi, waueni wote akiwemo binti yangu, amemuua mama yake, amemuua mke wangu …)

Gavana Richald Robeni alitoa amri, akiwa amenyoosha silaha yake, akijiandaa kuvuta taiga ya bunduki yake, kuruhusu risasi,vijana wake, askari takribani mia moja hamsini waliosalia, wakajiandaa kuvuta taiga,kulishambulia jeshi la watu weusi waliokuwa wakidai uhuru wao kwa kuingia vitani.

“,Papaaa!paaa!paaa paaaa……”,jeshi la askari wa kikoloni walishambulia.

“,wafyatueni na mishale,lukeni,tokeni juu ya miti,tukimbilie vichakani……”,Mpuzu Yahimana aliwahimiza vijana wake,washuke juu ya mti kuzikoa nafsi zao,silaha zao za jadi zisingefua dafu mbele ya risasi za moto za askari wa kikoloni.

“,papaaa,paapaa…”,askari wa kikoloni waliendelea kushambulia,wakiutekeza mti mkubwa wa ubuyu,matawi na majani ya miti yakateketezwa,yakadondoka chini na kuwalaani wazungu.

“,Yalaaa,nakufaaa,uwiiii!,Mrungu turongole(Mungu tusaidie),tunakufaa……”Kelele za machungu zilisikika,mashujaa wa Kiafrika walipiga kelele za maumivu, risasi zilipenya katika miili yao,wengine tumboni,wengine kichwani,Ishimwe alimanusura apigwe risasi,lakini alimuona mlengaji aliyekuwa amemuweka kwenye tageti,akaruka upande wa pili wa mti,risasi ikamkosa,askari wa kikoloni akaikoki tena amshambulie Ishimwe,alichelewa sana,Ishimwe aliuvuta upinde wake mpaka mwisho,akaufyatua,mshale ukatoboa jicho la askari yule wa kikoloni,ukatokea upande wa pili wa kichwa chake,akafa palepale.Ishimwe akadaka tawi la mti,akaruka chini,akatokomea vuchakani,mahali walipoelekea wenzake walioruka juu ya mti kabla yake…

Angel aliiona bunduki ya baba yake ikielekea upande wake,bila shaka baba yake alitaka kumuua,akaangalia upande wa pili,askari wa kikoloni takribani kumi walijiandaa kumshambulia,hakuwa na hofu yoyote ile,aliona bora afe kuliko kubaki duniani,moyo wake ulimsuta,alijiona ana hatia kubwa kwa kumuua mama yake,hakuona haja ya kukimbia kama walivyofanya Waafrika,walioruka huku na kule,kuelekea mafichoni,katika vichaka virefu msituni.Mpuzu aliwashambulia askari wa kikoloni kwa mishale,yote ikaenda pembeni,hakuua askari hata mmoja,alipogeuka upande wa pili,akamuona mpenzi wake anataka kushambuliwa,alikuwa hajielewi kabisa,akamvuta,Angel akadondokea kifuani kwake,akamkumbatia,mkono wake wa kushoto ulimshika Angel kwa nguvu,mkono wake wa pili ukakamata tawi la mti,huku risasi zikiwakosa kosa,zikipita juu ya vichwa vyao kwa fujo,Mpuzu Yahimana akaruka chini,wakakimbila msituni,huku Angel akilia kilio cha kwikwi,walipogeuka nyuma,walishuhudia maiti nyingi za Waafrika,zikidondoka juu ya mti,wakahuzunika,wakapiga moyo konde,wakasonga mbele na kutokomea vichakani…

“,Kufa,kufa,poor race,i hate you,……”,askari mmoja wa kikoloni,alifoka kwa hasira,akipiga mateke maiti za askari wa Kiafrika,ambao walikuwa bado wakihangaika kukata roho,alizungusha vichwa vyao,akawamalizia,aliwachukia sana Waafrika.

“,Lets follow them,tuingie kwa vichaka kuwatafuta…”,askari mmoja aliongea,akawahimiza wenzake kusonga mbele,kuwafuata Waafrika mahali walipokimbilia.

“,Stop!,don’t follow them,wacha fuata jinga hizi,let’s go back,turudi kwa great fort,we have to add more soldiers,askari yangu kufa nyingi sana……”,gavana Richald Robeni aliwazuia vijana wake kusonga mbele, askari wake wengi sana walikuwa wamepoteza maisha, jeshi lake lilikuwa limepungua, alitaka kurudi katika ngome yao kuongeza nguvu, askari wake wakatii amri yake, wakanyenyua mwili wa malikia wao kwa heshima, wakaupigia saluti, wakaanza safari ya kurudi katika ngome yao, wakiwa na majonzi makubwa …

…………………………………
Wanawake wa Kiafrika, wazee,watoto,pamoja na askari kumi waliokuwa pamoja nao kudumisha ulinzi,wakiwa juu ya mti wa ubuyu, mti uliokuwa umbali wa takribani mita kumi na eneo la vita, walisikia sauti za risasi, kelele za vilio na machungu zikipenya katika masikio yao, machozi ya huzuni yakawatoka, wakaa kimya, bila kutikisika juu ya mti, huku kila mmoja akiomba kwa mizimu, ndugu zao washinde na kurejea salama …

“,Twendeni tukawasaidie, twendeni ……”,askari mmoja, kati ya askari kumi waliokuwa juu ya mti, wakiwalinda wanawake, wazee na watoto, aliongea, alikuwa na shauku ya kutaka kutoa msaada kwa wenzake.

“,Hapana, hatujui wako mahali gani, tunaweza kushuka chini na kushambuliwa, isitoshe, kundi hili kubwa la Waafrika takribani wote, tuna waacha na nani? “,askari wa pili ,askari wa Kiafrika alimjibu mwenzake, akauliza tena swali.

“,Kweli kabisa, tuombe Mungu tu …”,askari wa tatu, akakubaliana na mwenzake, akaunga mkono, hawakua na haja ya kushuka chini ya mti wao wa maficho, wakatupilia mbali mawazo hayo, ghafla ukimya ukatawala tena msituni kwa mara nyingine tena …
…………………………………
Ngome kubwa :3;20pm
Magari kumi tu ndiyo yalirejea, magari ya askari wa kikoloni waliobakia, maiti zote ziliachwa msituni, zilikuwa nyingi sana, wakaziacha, wakiahidi kuzichukua watakaporejea msituni, wakiwa na kundi kubwa zaidi

Askari mia moja na hamsini tu ndio walirudi salama,wakiwa na mioyo iliyojaa huzuni, simanzi, pamoja na hasira juuu ya Waafrika.

“,Wamerudi, they are back! but why, ziko chache sana, zimekufa, they are killed ……”,

“,Hahahaaaa ……”,

Kundi la kwanza, kundi lililoenda kuwatafuta Waafrika katika majumba yao, makazi duni, wakawakosa na kushindwa kuwakamata, kisha wakawekwa rumande kwa amri ya gavana, waliongea kwa kejeli, wakacheka kwa dharau, walifurahi sana wenzao kurudi mikono mitupu,jeshi likiwa limepungua, askari wenzao wakiwa wameuawa kikatili …

“,Vizuri sana Africans, very good!very good! penda nyinyi sana ……”,

“,Hahaaa, haaaa, haaa …”,

Wakiwa wamesimama kwenye nondo za magereza yao, nondo ambazo ziliwawezesha kuona kila kitu kilichokuwa kinaendelea nje, waliwazomea, wakawakejeli askari wenzao, waliorudi wakiwa na nyuso za huzuni, huku baadhi wakiwa wamebeba mwili wa malikia wao, maneno ya kejeli na matusi yalipenya katika masikio ya gavana,akachukia, hasira zikampanda,askari wote waliokuwa pamoja naye wakachukia,sura zao zikakunjamana kwa hasira…

“,Firee them, I say fire them, kill them, uwa jinga yote ……,hypocrite people ……”,gavana Richald Robeni uvumilivu ulimshinda, akanyanyua bunduki yake, akaikoki, akavuta taiga, askari wake, askari waliokuwa pamoja naye, wakatii amri yake, wakageuka mahali yalipokuwa magereza ya wazungu, wakakoki bunduki zao, wakavuta taiga na kuanza kumimina risasi.

“,Paaaa, paaa, paaaa! ”
“,Aaaaa…ah, you have kill…ed us, mmetu…u…a, ”
“,paaaah, paaaah “,
“,Aaa…a…ah “,

Vilio vilisikika, askari wa kikoloni waliokuwa wamefungwa gerezani walikufa kama nzige,wakapiga kelele za maumivu, hakuna aliyesikia vilio vyao, ndani ya dakika tano tu, wote walikuwa wamepoteza maisha, ukimya ukatawala tena katika ngome ya wakoloni …

…………………………………
“,Let’s stop here, mimi choka sana, ”
“,Au ngoja nikubebe “,
“,No, no, hata wewe you have to rest, unapaswa kupumzika…”,
“,Mimi nashauri tupumzike, japo tumebaki wapambanaji arobaini tu, wengine wote wamekufa ……”,
“,Yes,wamekufa,by using this local guns,upinde na mishale, we can’t win the battle,hatuwezi kushinda kabisa, akili ikitulia, machungu ikipungua kwa moyo wangu, fundisha nyie kutumia guns, no way! I have killed my mum, I didn’t expect that, sikutegemea kabisa, I can’t go back,nikirejea kwa baba I will die, we have to win, tunapaswa kushinda,ili kuwakomboa na mimi jikomboa mwenyewe! “,,„Angel alipiga moyo konde, akajivika roho ya paka, akakubaliana na hali halisi, hakuwa na mama tena, baba yake hakumuhitaji tena, walikuwa maadui kwa sasa, hakua na jinsi zaidi ya kuungana na Waafrika kupigania uhuru kufa na kupona, hakua na jinsi kupigania maisha yake, bila hivyo baba yake pamoja na askari wake wa kikoloni watamuua, alipaswa kuwaua kabla hawajamuua …

…ITAENDELEA …
Wazungu kwa wazungu waeuana ndani ya ngome yao, Angel kadhamiria kusahau kila kitu kuhusu wazazi wake pamoja na rangi yake, nini kitaendelea? Usikose sehemu zijazo …

Facebook Comments
Recommended articles