SIMULIZI : Barua kutoka kwa marehemu mama kwa kijana wake siku ya 3 baada ya mazishi yake

By , in ELIMUJAMII on .

SIMULIZI : Barua kutoka kwa marehemu mama kwa kijana wake siku ya 3 baada ya mazishi yake

Mwanangu Mpendwa.

Napenda kujua kwa nini nimekufa kama mwanamke masikini ilihali nikiwa na kijana kama wewe.

Mwanangu nilitaka kukubariki kabla sijafa, lakini nimekufa na baraka zangu.

Chakula changu cha asubuhi na mchana kilikuwa kimoja tena nilikipata kwa taabu wakati nilipokuwa hai, lakini ulitapanya pesa zako kwa kila aina ya mapochopocho, chakula kama nyama na vinywaji siku ya mazishi yangu.

Mwanangu umetumia gharama kubwa na manukato ya gharama kuhifadhi mwili wangu lakini nilipokuwa hai ilinibidi niishi kwa kujipaka mafuta ya karanga.

Mwanangu uliuvalisha mwili wangu nguo na sanda za gharama wakati nilipokuwa hai hukinijali hata kwa vazi la mtumba.

Nilipokuwa mochwari ulikuja Mara kwa Mara kuutazama mwili wangu lakini kwa nini nilipokuwa hai hukufanya hivyo.

Kinachoniumiza zaidi ni jeneza la gharama ulimolaza mwili wangu wakati nilipokuwa hai niliishi kwenye pagara.

Ulipokuwa mtoto niliteseka mno kwa ajili yako ili upate chakula na uridhike. Nilivaa nguo moja tu ili uwe na nguo nyingi zenye kukutosheleza. Nilidhani ungenijali baada ya kuzeeka.

Ulikamilisha kujenda kaburi langu kwa wiki moja. Ukalipaka rangi na kuweka picha ya gharama ili uufurahishe mwili wangu.

Tena ukaandika msemo, “Nakupenda sana mama ulale mahala pema peponi” wakati nimekufa na moyo uliovunjika.

Mwisho.

Mwanangu Nimeandika haya kukumbusha kwamba hakuna mtu yeyote niliyempenda wakati wa uhai wangu kama nilivyokupenda wewe. Mwenyezi Mungu akusamehe.

Imeandikwa na mwalimu habelnoah

Tafadhali shirikisha wengine itukumbushe vijana kuwathamini wazazi wetu.

Recommended articles
error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!