SIKILI MIMI MASIKINI, UVIVU WANGU NYUMBANI…

By , in Simulizi on .

Sikili mimi maskini,
Uvivu wangu nyumbani,
Ukiwa huu njiani,
Nakufa hapa kwa nini?

Sadiki sasa ashiba,
Chakula kingi kwa Baba,
Nirudi tena kwa Baba,
Nakufa hapa kwa nini?

Naomba radhi nimekosa,
Nitakuwa mtoto mwema sasa,
Shambani tena sitakosa,
Baba na Mama nisameheni.

Nitalima kama Sadiki,
Nitalima wala sichoki,
Na nyumbani tena sitoki,
Baba na Mama nisameheni.

Recommended articles