Sifa za Vitendawili

By , in Fasihi Simulizi on . Tagged width:
  1. Vitendawili huwa na mwanzo maalum : Kitendawili  tega
  2. Hupitishwa baina ya watu wawili anayetega na anayetegua
  3. Vitendawili huwa na muundo maalum wa kuendelezwa (utangulizi, swali, (majaribio ya) jibu; wanaotegua wakishindwa anayetega huwa ameshinda, huitisha apewe mji/zawadi na kisha kutoa jibu)
  4. Huwa na vipande viwili swali na jibu. Mfano: Kila niendapo ananifuata  kivuli.
  5. Hutumia mbinu ya jazanda, kufananisha vitu viwili moja kwa moja. K.v. Nyumba yangu haina mlango  yai (yai limelinganishwa moja kwa moja na nyumba isiyo mlango)
  6. Hurejelea vitu vinavyopatikana katika mazingira na vinavyojulikana sana
  7. Vitendawili vilitegwa wakati maalum, hasa wa jioni
  8. Vitendawili hutumia tamathali za usemi (mbinu za lugha) kama istiara, tashihisi, tashbihi, jazanda, chuku, tanakali za sauti, n.k
  9. Vitendawili huwa na jibu maalum.