SIFA ZA MTAMBAJI WA FASIHI SIMULIZI

By , in Fasihi Simulizi on . Tagged width: ,

SWALI: Kwa kutumia hoja tano, eleza sifa za mtambaji wa fasihi simulizi.

MAJIBU:

a) Asiwe mwoga ili kuweza kuzungumza mbele ya hadhira yake.
b) Asiwe na haya ili kuweza kuzungumzia mambo ya aibu inapobidi.
c) Awe na uelewa wa mazingira na masuala mtambuka katika jamii ili kuweza kuwasilisha dhana zisizopatikana katika mazingira yake k.m. kumtumia rais kuelezea dhana ya mfalme.
d) Awe na ufahamu mpana wa lugha ili aweze kuitumia kwa uhodari na kuwasilisha kwa wepesi kile anachosimulia.
e) Awe mchangamfu na mcheshi ili kunasa makini ya hadhira na kuzuia isikinai uwasilishaji wake.
f) Awe na ufahamu mpana wa utamaduni husika ili kuzuia kutumia maneno na ishara zinazoweza kuwaudhi au kupingana na imani za hadhira yake.
g) Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira k.v. kuimba na maswali ili hadhira isikinai, n.k.

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!