Sifa za Mkalimani

By , in TAFSIRI/UKALIMANI on .
  1.  Awe na ujuzi wa hali ya juu wa lugha anazoshughulika nazo pamoja na utamaduni wake.
  2. Ajue lugha zaidi ya mbili za kimataifa kwani kadiri unavyojua lugha zaidi ndivyo unavyokuwa   mkalimani bora zaidi. Pia lugha zaidi ya moja hasa za kimataifa zitamsaidia sana hasa kwenye mikutano/makongamano.
  3. Awe na ujuzi au maarifa ya kutosha juu ya mada, taaluma au uwanja unaozungumziwa. Inamaana kwamba kama wewe ni mkalimani wa masuala ya kiuchumi basi hupaswi kufasili masuala ya kisheria. Mfano; ukalimani wa mahakamani hufanywa na wanasheria, masuala ya tiba n.k
  4. Awe na ujuzi wa taaluma ya ukalimani; yaani awe amepata mafunzo ya ukalimani. Katika hayo mafunzo atajifunza mbinu za ukalimani aina, changamoto na namna ya kuzikabili changamoto hizo.
  5.  Awe na kipaji, yaani; Yaani uwezo wa kukumbuka kwa hali ya juu, Kuteua msamiati sahihi kwa haraka, Kipaji katika kuunda istilahi haraka haraka na kuitumia. Kipaji cha ulumbi/awe na ulumbi yaani kipaji cha kuongea na kuvuta/kushawishi watu.
  6. Awe mchapakazi, mdadisi na anayependa kujiendeleza na kupata  habari kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii mfano; magazeti, majarida, televisheni, facebook, twitter au kuzungumza na watu/kuchangamana na watu.
Recommended articles
error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!