SIFA ZA INSHA NZURI

By , in Kidato I-IV Kidato V-VI on . Tagged width:

Insha nzuri huandikwa kwa kuzingatia mambo muhimu yafuatayo:

 1. Kuzingatia uteuzi mzuri wa mada: mwandishi wa insha hana budi kuteua mada ambayo ataweza kuielezea kwa kina na kwa ufasaha kulingana na lengo la mada hiyo. Kushindwa kufanya hivyo, insha haitaeleweka, hukosa mvuto na hupoteza maana kwa wasomaji au wasikilizaji.
 2. Kuzingatia muundo wa insha: Insha nzuri hugawanywa katika sehemu kuu nne (4) ambazo ni kichwa cha insha, utangulizi,kiini, hitimisho.
 3. Kuzingatia matumizi sahihi ya alama za uandishi, kama vile nukta, mkato, nukta pacha, alama ya kuuliza, alama ya kushangaa, mabano, kistari, ritifaa, herufi kubwa, alama za mtajo, n.k.
 4. Kuzingatia ufasaha wa lugha: Lugha inayotakiwa kutumiwa katika uandishi wa insha ni lazima iwe sanifu na fasaha.
 5. Kuzingatia mantiki (mtiririko mzuri wa mawazo): Hii ni pamoja na kuzingatia/kupanga nini cha kuanza au nini kiwe mwanzo na nini kiwe kati na mwisho wa insha.
 6. Kila aya ibebe wazo kuu moja
 7. Kuepuka matumizi ya lugha ya mkato, kama vile n.k (na kadhalika au na kuendelea), pia mf. (mfano).
 8. Kuhusianisha mada inayojadiliwa na uhalisia wake katika jamii ya sasa.
 9. Kuepuka matumizi ya maneno au tungo zenye utata (maneno au tungo zenye maana zaidi ya moja).
 10. Kuzingatia matumizi sahihi ya nyakati au muda. Hii hujumuisha matumizi ya wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao.
 11. Kutumia sarufi ya lugha husika ipasavyo.