SIFA NA MAADILI YA MFASIRI BORA

By , in TAFSIRI/UKALIMANI on .

 • Awe mahiri wa lugha mbili zinazohusika; kuwa mahiri katika lugha maana yake nini? Ni kujua vizuri nyanja mbalimbali za Isimu ya lugha husika kama vile; Fonolojia-Matamshi, Mofolojia-Maumbo, Sintaksia-Muundo na Semantiki-Maana.

 • Ajue vizuri utamaduni wa watu mbalimbali.

 • Ajue angalau lugha mbili

 • Awe na maarifa ya TEHAMA (ICT)

 • Awafahamu watu, jamii na utamaduni wao – mitazamo kuhusu watu, mitazamo – kuhusu wanyama.

 • Apende kujisomea na kujiendeleza kulingana na mabadiliko ya jamii. Mfano; kusoma vitabu, majarida, magazeti mbalimbali kusikiliza redio na kuangalia TV nk.

 • Awe mwandishi bora.

    MAADILI YA MFASIRI BORA (ETHICS)

 • Awe mwaminifu kwa matini na kwa mwenye matini; yaani asipotoshe habari au kusema uongo.

 • Awe mchapakazi (Kujituma/Bidii katika kazi)

 • Awe nadhifu – Unadhifu-mwonekano wa moyo, asiwe tapeli/laghai

 • Aelewe/kuelewa taratibu za kazi na kuzifuata. Mfano; bei ya kutafsiri kwa ukurasa au kwa maneno.

 • Ushirikiano/kushirikiana na watu mbalimbali wa fani mbalimbali, makundi mbalimbali ikiwa pamoja na wafasiri wenzake.

Facebook Comments
Recommended articles