SHULE YA SAIKOLOJIA

By , in ELIMUJAMII on .

πŸ‘‰1 Ukikuta watu katika mazungunzo, wakiwa wamesimama, kisha ukawasalimia kwa kuwapa mkono, tazama miguu yao. Endapo watageuza miguu na kiwiliwili basi ujue wako tayari ujiunge katika mazungunzo yao. Ikiwa watageuka kiwiliwili pekee, hawako tayari uungane nawo. Salimia uondoke ukitabasamu.

πŸ‘‰2 Zile sura mpya unazoona katika ndoto, sio sura mpya. Ni watu uliowahi kukutana nawo maishani lakini umewasahau kabisa.

πŸ‘‰3 Mtu anayependa na kufurahia hisia za kupendwa, huchelewa kuzeeka. Pia hupona majeraha /vidonda mapema kuliko mtu anayeteseka na mapenzi.

πŸ‘‰4 Tabia ya kuongea mwenyewe unapokuwa peke yako ni ishara ya kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri. Kuongea mwenyewe hadharani ni ishara ya maradhi ya akili.

πŸ‘‰5 Maamuzi yako yanaweza kuwa sahihi na ya haki zaidi unapotumia lugha mpya uliyojifunza kuliko unapotumia lugha yako ya kila siku.

πŸ‘‰6 Kukatishwa tamaa mara nyingi katika jambo moja kubwa, kunaweza kupelekea tabia ya kukata tamaa mwenyewe hata katika mambo mengine madogo zaidi. Ukijua hivyo utastuka.

πŸ‘‰7 Zungumza na mtu akiwa amechoka ili kupata ukweli kuhusu hisia zake. Ndio siri ya kuhoji watuhumiwa nyakati za usiku, na ndio sababu moja wapo ya kuwatesa wahalifu ili wazungumzie ukweli. Zingatia haki za binadamu.

πŸ‘‰8 Kimo cha mtu hurithiwa kutoka upande wa baba, wakati akili na hisia hutoka upande wa mama. Pata mke mwenye akili, pata mume mwenye kimo. 😎

πŸ‘‰9 Mtu anayezungumza akiwa na hasira, huzungumza ukweli karibu asilimia 90. Hasira huathiri kufikiria namna ya kuongopa

πŸ‘‰10 Ubongo una tabia ya kumzuia binadamu kufanya kazi kubwa ili asichoke. Mfano, Misuli ya binadamu ina nguvu ya kuweza kusukuma gari ndogo, lakini ubongo hauwezi kuruhusu. Baadhi ya watu wenye maradhi ya akili, ubongo wao hupoteza kazi hiyo na kuwafanya waonekane wana nguvu nyingi..

Facebook Comments
Recommended articles