SHAIRI : UWARIDI

By , in Ushairi on .

Uwaridi uwa zuri, mwenzenu nimelipata,
limi andiko nakiri, nimeshaweka ukuta,
Nimenukia uturi, kiroho kusitasita,
Nimesahau ya zama, ya nyuma sitaki tena.

Udongo tapalilia, na samadi shindilia,
Maji nitamwagilia, magugu nitayatoa,
Uzio taliwekea, haribifu kuzuia,
Nimesahau ya Zama, ya nyuma sitaki tena,

Ua Lina rangi nzuri, haijawahi tokea,
Ua lacheza kachiri, upepo ukipipea,
Linanipa umahiri, kwa kalamu kusifia,
Nimesahau ya Zama, ya nyuma sitaki tena.

ยฉNyerere Ideas ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
๐Ÿ’š๐Ÿ’š๐Ÿ’š
๐ŸŒณ๐Ÿฆ’
0656-498341

Facebook Comments
Recommended articles