SHAIRI : UDINI NA UKABILA

By , in Ushairi on .

SHAIRI : UDINI NA UKABILA
——————————
1.
Itikadi ya udini, na ile ya ukabila.
N’kifikiri kwa makini, naona tupu balaa.
Ukabila na udini, maovu haya masuala.
Yeyote mpenda kheri, aepuke dhana hizi.

2.
Ukishamiri udini, hata ukabila pia.
Vikakujaa moyoni, weye ‘mepotoka ndia.
Mtego wake shetani, tayari ‘meng’ang’ania.
Weye umeharibika, hatari kwa jamii yako.

3.
Kama kheri waitaka , kwako na jamaa zako.
Na zake Mola baraka, Hata kwayo nchi yako.
Kataa kwa uhakika, kwawo wote moyo wako.
Kuyashabikia haya, udini na
ukabila.

4.
Kumbuka jamii zetu, ziliishi kwa amani.
Wahenga mababu zetu, wali na zao imani.
Tukifanya mambo yetu, salama u salimini.
Yeo tunachafuana, kisa udini ‘kabila.

5.
Shemeji muisilamu, aidha na dada yangu.
Miye siyo mwisilamu, kama hao ndugu zangu.
Na n’na wajibu maalumu, kwa kaya ya jamaa’angu.
Niwache wajibu huo, sababu Waisilamu?

6.
Kwanza nikitafakari, wa Ukiristo asili.
Halafu nikifikiri, wa Usilamu asili.
Hatimaye ninakiri kuwa si ya kaya mbili.
Asili’ze kaya moja, ya babu Aburahamu.

7.
Hizo yeo dini zetu, zili na bora imani.
Zalenga kwa Mungu wetu, wa salama na amani.
Tukatae katukatu, Tulio makanisani.
Kuchukia ndugu zetu, walio misikitini.

8.
Tuitafute salama, huku twathaminiana.
Tulinde yetu jamaa, huku twaheshimiana.
Udini mbaya jama, ukabila ni laana.
Kuyashabikia haya, yakini uhayawani.
—————————

Rwaka rwa Kagarama (Mshairi Mnyarwanda)
Jimbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare, RWANDA.

Recommended articles