SHAIRI : TESO

By , in Ushairi on .

1. Teso hili lanitesa, tena linanitafuna,
Kila kona lapapasa, amani ya kweli sina,
Teso linaninyanyasa, sijui kama tapona,
Penzi teso la harari, kama likikusariti.

2. Akili yavurugika, ufanisi tena sina,
Baroharo nateseka, penzi lenda mbali sana,
Penzi kwangu metoweka, tesoni ninapambana,
Penzi teso la hatari, kama likikusariti.

3. Ndoto zake za ajabu, ndizo zinanisonona,
Nipo mbali na tabibu, mateso kutoyaona,
Nateswa na mahabubu, mateso ya kutopona,
Penzi teso la hatari, kama likikusariti,

4. Naitika bila mwito, kichaa naonekana,
Nipo katika msoto, a hueni sijaona,
Nimekuwa kama toto, la kufanya sijaona,
Penzi teso la hatari, kama likikusariti.

5. Waungwana nipungeni, mwenzenu nataka pona,
Pepo hili nitoeni, pepo la kutesa sana,
Furaha nirejesheni, maisha yawe na mana,
Penzi teso la hatari, kama likikugeuka.

Na;
Mwl Jovin Kamugisha Felician
(Malenga chipukeni)
Coed-UDOM
0756882752

Facebook Comments
Recommended articles