SHAIRI : NIANZE NA NINI

By , in Ushairi on .

Nimekunjato miguu, na mwili u tuli chini
Ba’da kupata nafuu, kwa tabu za maradhini
Nautunga wimbo huu, nambe nianze na nini?

Ni shura ya mimi nawe, nyongo mkaliya ini
Fikira zako zituwe, upimeto kwa makini
Nachotaka niambiwe, kwako nianze na nini?

Kama nianze na gari, sema ya aina gani
Lolote nipo tayari, benzi na isuzu jani
laazizi nishauri, kwako nianze na nini?

Ama nianze na nyumba, utakuwa furahani
Kwa wengine utatamba, kodi haulipi sini
Muhibaka nakuomba, nambe nianze nini?

Sema nianze na ndoa, kama kwako ndo amani
Ili nisikupe doa, ipande yako thamani
Kwa vyovyote nipo poa, nambe nianze na nini?

Hata kama utakalo, kwenye shairi huoni
Nambe nilifanye hilo, ewe wangu wa moyoni
Nataka neno ambalo, lasema nanze na nini?

Mwisho nafunga kauli, mjue muomba nani
Mwana wa mzee Ali, ambaye Moa nyumbani
Moto wenu Abtali, ambwaye Tanga mgeni

MBARUKU ALLY
MOTO WENU
ABTALI
MJAALA
0717199835
01/05/2019
Nikiwa Kigogo Dsm
Mzaliwa Moa Tanga

Facebook Comments
Recommended articles