SHAIRI : NAKUENZI KAMBARAGE

By , in Ushairi on . Tagged width:

SHAIRI : NAKUENZI KAMBARAGE
**********
Siwezi kukukumbuka,
kimya kimya mtukuka,
mwelekezi muafaka,
u wa maana hakika,
ut’endelea tajika,
milele yote milele.
****
Kwa dhati toka moyoni,
ni shahidi Maanani,
Baba ali mhisani,
wa wanyonge niamini,
alikuwa ni makini,
wa haki za binadamu.
****
Nyerere wetu shujaa,
Afrika aliifaa,
wasifa wake wajaa,
yote yote mataifaa,
mengi mema ulifanzaa,
nakuenzi Kambarage.
****
Shukurani Maanani,
kunigea tungo hini,
nikimtaja mwendani,
aliyeko mtimani,
kulla wa bora imani,
amkumbuke Nyerere.
***

Rwaka rwa Kagarama,
Mshairi Mnyarwanda.