SHAIRI: MWALIMU YAMENIKUTA

By , in Zote on . Tagged width:

Ninauleta mkasa, msada nahitajia.

Mwenzenu yalonifika, vema kuwahadithia.

Kichwa kinanichakata, mawazo wahida mia.

Mwalimu yamenikuta, nikubali nikatae?

 

Kipindi kilipofika, darasani naingia.

Nyanga zangu za hakika, madenti kuwakatia.

Sauti inasikika, hakuna asosikia.

Mwalimu yamenikuta, nikubali nikatae?

 

Sauti ilisikika, “Mwalimu ninaumia”.

Nyuma nilipogeuka, msichana maridhia.

Haraka nikamfika, niweze msaidia.

Mwalimu yamenikuta, nikubali nikatae?

 

Macho aliyazungusha, mahaba kuashiria.

Meno anang’ata kucha, ashindwa kunambia.

Miguu aitikisa, kama ataka kimbia.

Mwalimu yamenikuta, nikubali nikatae.

 

Ghafla kakurupuka, ili anikumbatie.

Mikono amenyoosha, kifuani kwangu mie.

Maneno yakimtoka, “maridhia nihurumie”.

Mwalimu yamenikuta, nikubali nikatae.

 

Libasi kaziangusha, moja hadi nyinginewe.

Pumzi akizishusha, zinakuja kwangu mie.

Kwa kweli amenichosha, manusura nizimie.

Mwa yamenikuta, nikubali nikatae?

 

“Mwalimu ninateseka, japo busu nitupie.

Wangu moyo umeteka, hadi napata kiwewe.

Nia yangu nimeweka, ticha unioe mie. ”

Mwalimu yamenikuta, nikubali nikatae?

 

Ghafla ninashtuka, kumbe naona ndoto.

Nilipofunua shuka, pembeni kuna kitoto.

Taratibu nainuka, na hapo mwisho wa ndoto.

Mwalimu yamenikuta, nikubali nikatae?.