SHAIRI : KIKAPU CHA MASHIKIO

By , in Ushairi on .

Napiga mbiu wendani,kwa Sauti isikike
Ipae yende angani,na miji yote ifike
Waelewe mafatani,wakiume na wakike
KILA MTU ANA YAKE,KIKAPU CHA MASHIKIO

Wambea wazungushao,ya umbea wasichoke
Wapakazia wenzao,makusudi waumbuke
Ni mengi walio nao,yaso nakifani chake
KILA MMOJA NA YAKE,KIKAPU CHA MASHIKIO

Namba na makisisina,maneno wayapulike
Wazingao na fitina,wenzao waazirike
Ni jambo gani la bina,liso namfano wake?
KILA MTU ANAYAKE,KIKAPU
CHA MASHIKIO

Kuwajuza yanipasa,nduzangu musiudhike
Mulo yafunua tasa,rudini muyafinike
Kobe kumteka kasa,ni nini faida Yake?
KILA MTU ANA YAKE,KIKAPU CHA MASHIKIO

Nimengi nilomfunda,nayeye abadilike
Namno nikajipinda,nayeye asitirike
Lakini punda ni punda,malipoye nimateke
KILA MTU UNAYAKE,KIKAPU CHA MASHIKIO

Watufanyia ya inda,kusudi tufedheheke
Yakwao yamewashinda, wameyawata yanuke
Ni dasturi ya yonda,huwa halioni lake.
KILA MTU ANA YAKE,KIKAPU CHA MASHIKIO

Tamati mangi tusambe,ngamia naakumbuke
Tusiyapigie pembe,niakiba tuyaweke
Kuteka nundu ya n’gombe,huwa ni ujinga wake
KILA MTU ANA YAKE,KIKAPU CHA MASHIKIO

Recommended articles