SHAIRI : BWATUKO

By , in Ushairi on .

BWATUKO

Mtunzi: Abdul-razaq Rajabu Salimu
Shairi: Bwatuko
Tarehe: 05/07/2019

BWATUKO

1. Rajabu mwana Salimu, vita sasa nimeanza
Naongea mufahamu, maadili kuyatunza
Taongea musalimu, kwa wangu huu utunzi
Mbwatukaji nabwata, mambo mengi tabwatuka

2. Nabwata kwa mbwatuko, kusudi si kutukana
Nabwata kwa sikitiko, kusudi si kugombana
Nabwata kwa usikiko, sauti sikike sana
Nabwatukia vijana, wakike kwa wakiume

3. Vijana ninyi wa vyuo, ndio nawabwatukia
Tena nawashusha vyeo, hasa kwa kuwakamia
Mufanyayo huku vyuo, machafu kuyavamia
Huu mwanzo wa kubwata, sijui takoma lini

4. Wanikabu na hijabu, leo ninaanza nao
Wanamengi masaibu, ni wachafu pia hao
Kificho chao nikabu, wazinifu ndio wao
Mavazi wayaharibu, uchafu kila uchao

5. Wengine hutekenyana, mwili kusisimshana
Mwisho wao kudinyana, vijana kuchezeana
Eti ni kula ujana, kutwa kufanyiziana
Nabwata mbwatukaji, mchukiao kufeni

6. Wasichana nawachana, metolewa usichana
Mulikuja wasichana, munaondoka hamuna
Kazi yenu kujamana, chovywachovywa kwa sana
Nabwata kwa sikitiko, kusudi ni kuadili

Mimi ndio mswahili, wa kuenzi uswahili
Napenda mambo jamali, hasa yale ya halali
Leo meanza na hili, wenzangu tulijadili
Nimebwata kwelikweli, haya sasa kosoeni.

abuusalahuddiyn@gmail.com

Chungwa tamu ni la Tanga

Recommended articles