SABABU ZA ATHARI ZA KIMATAMSHI

By , in Sarufi na Utumizi Wa Lugha on . Tagged width:

Matamshi ya maneno katika lugha ya Kiswahili huathiriwa au hukosewa kutokana na sababu zifuatazo:

1. Athari za lugha ya kwanza/lugha mama, kwa mfano:

  • hachezagi badala ya huwa hachezi……………..Msukuma
  • karamu badala ya kalamu………………………..Mkurya
  • Dhawadi badala ya zawadi………………………Mzaramo/Mgogo
  • Ntoto badala ya mtoto……………………………Mmakonde
  • Fiatu fyangu badala ya viatu vyangu………..Mnyakyusa
  • Thithi thote badala ya sisi sote…………………Mpare

2. Kutokuwa na elimu

Mtu akikosa elimu au ufahamu wa kutosha kuhusu lugha fulani inaweza kusababisha kukosea matamshi ya maneno ya lugha husika.

3. Athari za lugha za kigeni

Mtu anapozungumza lugha za kigeni mara kwa mara katika mawasiliano yake humfanya awe na uzoefu na lugha husika. Hivyo, wakati anapozungumza lugha yake (lugha mama) hujikuta akiathiriwa kimatamshi na kimsamiati.

4. Mazoea

Wakati fulani mazoea ya mtu katika lugha yake humfanya aathiriwe katika vipengele fulani vya lugha anapozungumza lugha nyingine au na mtu mwingine akidhani ataeleweka. kwa mfano, zalau badala ya dharau, na zambi badala ya dhambi.

5. Athari za kimaumbile

Mtu anapokuwa na tatizo kwenye ala za sauti, hususan kuwa na kithembe, huweza kuathiri matamshi ya lugha sanifu. Kwa mfano, thalamu badala ya salamu.

6. Kasumba za wasomi

Mara nyingi wasomi wengi hupenda kuzungumza lugha za kigeni, ikiwemo Kiingereza, wakati wa mazungumzo yao wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo kutadhihirisha elimu au usomi wao mbele ya wengine.

 

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!