OSW 224 : FASIHI SIMULIZI JARIBIO KUU – MAALUMU (JUNI, 2015) MAJIBU

By , in MITIHANI SHAHADA on . Tagged width:
OSW 224 : FASIHI SIMULIZI JARIBIO KUU – MAALUMU (JUNI, 2015) MAJIBU
1.     Fasihi
simulizi ni hai. Jadili

MAJIBU

Fasihi
Simulizi ni sanaa ya maneno teule inayofikisha ujumbe kwa njia ya masimulizi yam
domo. Uhai wa fasihi simulizi unajikita katika vipengele mbalimbali kama vile:
     ·
Kuwepo kwa hali ya utendaji ambao
hushirikisha hadhira na fanani.
     ·
Kubadilika kulingana na wakati na
mazingira.
     ·
Kuwepo kwa mtendaji ambaye ndiye mtendaji
mkuu wa fasihi simulizi, huyu ndiye anayerithisha kazi za fasihi simulizi toka
kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
·
Kuwepo kwa hadhira .
·
Kuwepo kwa utegemezi katika fasihi
simulizi huifanya iwe hai.
·
Huzaliwa, hukua na mwisho hufa
kulingana  na maendeleo ya jamii
Kwa
ujumla uhai wa fasihi simulizi ni dhana pana inayoifanya fasihi yenyewe
iendelee kudumu katika jamii hasa kutokana na uwezo wake wa kujigeuza kulingana
na mabadiliko ya jamii.
2. Fanani na hadithi hushiriki pamoja katika utendaji
wa fasihi simulizi. Thibitisha ukweli huu kwa mifano maridhawa.

MAJIBU

Ushirikiano
wa fanani na hadhira ni moja wapo ya sifa za fasihi simulizi. Hadhira huweza
kushiriki kutegemeana na ubunifu wa fanani katika uwasilishaji wa kazi husika
ya fasihi. Umuhimu wa ushirikiano huu ni kama ifuatavyo:
Hadhira,
hufuatilia kwa makini mwanzo hadi mwisho na kupata ujumbe uliokusudiwa, bila
hivyo hadhira huweza kusinzia.
Vilevile,
hadhira inaposhiriki humthibitishia fanani juu ya kufanikiwa au kutofanikiwa
mbele ya hadhira. Mfano unapotenda halafu hadhira imenuna ni dhahiri kuwa
fanani hajafanikiwa kuiteka hadhira yake.
Ushiriki
wa hadhira pia huipa uhai kazi nzima ya fasihi inayotendwa mbele ya hadhira. Vionjo
kama makofi na vigelegele toka kwa hadhira hunogesha uwasilishaji.
Ushiriki
wa hadhira pia humuongezea fanani kujiamini hasa hadhira inapotoa mwitiko
chanya kwa kushangilia au kupiga makofi. Kujiamini kwa fanani huchochea
mbwembwe na madoido ya kisanii.
Ushirikiano
wa fanani na hadhira katika uwasilishaji wa kazi ya fasihi, kwa mfano sehemu za
kuitikia katika masimulizi hufanikiwa vizuri iwapo hadhira itashiriki.
Kwa
ujumla ukamilifu wa fasihi simulizi hauwezi kutokea iwapo fanani ataachwa peke
yake wakati wa uwasilishaji.
3.     Je, fasihi simulizi ina umuhimu kwa jamii? Kama upo, ni upi?

MAJIBU

Fasihi simulizi ni sanaa
isiyopitwa na wakati. Umuhimu wa fasihi simulizi ni wa vizazi vyote na utakoma
pale jamii itakapoamua kuachana na yale yasemwayo, kuelezwa au kusimamiwa na
fasihi hiyo. Umuhimu huo wa fasihi simulizi unajikita katika vipengele
vifuatavyo:
(i) Kuburudisha
Fasihi simulizi huweza kutumiwa kama burudani kwenye mkusanyiko wa jamii.
Tanzu kama hadithi, ushairi, semi (methali, vitendawili, nk.) aghalabu hutumiwa
ili kuwaburudisha waliokusanyika katika jamii. Kwa mfano, watoto
wanapokusanyika kucheza, aghalabu hutegeana vitendawili kama njia ya
kujiburudisha. Hadithi, ngano, hekaya au hata hurafa huweza pia kutambwa kama
njia ya burudani.
(ii) Kuelimisha   
Kwa kutumia fasihi simulizi, wanajamii wanaweza kuzielimisha thamani za
kijamii, historia yao, utamaduni na mtazamo wao kilimwengu kutoka kizazi kimoja
hadi kingine.
(iii) Kuipa
Jamii Muelekeo
Kwa njia ya kuelimishana kimawazo yanayohusiana na tamaduni na desturi za
jamii husika, wanajamii wanahakikisha kwamba jamii, kwa kutumia fasihi
simulizi, inapata muelekeo utakaowabainisha wao mbali na wengine.
(iv)  Kuhifadhi Historia na Utamaduni
Katika kuhifadhi amali muhimu za  kijamii, fasihi simulizi
inakuwa nyezo muhimu. Aidha, wanajamii hufahamishwa kifasihi simulizi historia
yao – wao ni nani na wanachimbukia wapi. Maarifa haya ni muhimu kwa kila
mwanajamii, kwani yanamsaidia sio tu kujielewa, bali pia kujitambua.
(v)  Kuunganisha Vizazi vya Jamii                 
Fasihi simulizi ni msingi mkubwa wa kuwaunganisha wanajamii waliopo na
waliotangulia mbele ya haki. Kwa kutambiwa hadithi, vitendawili, methali na
nyimbo zao, umbali wa kiwakati kati ya vizazi vilivyotangulia mbele ya haki,
vilivyopo na vijavyo unafupishwa kwa kiasi kikubwa sana.
(vi) Kufundisha  
Jamii ina jukumu la kuwafundisha vijana wake maadili ya jamii ile ambayo
yana adili  yaani funzo au ujumbe unaowaelekeza, kuwaadibu, kuwaonya
na kuwaongoza kwenye matarajio ya jamii ile. Kwa hiyo, jamii nyingi hutumia
fasihi simulizi kama njia ya kuwaelekeza na kuwafundisha vijana wake mwenendo
mzuri, maadili na falsafa ifaayo ili kutunza jina na heshima ya jamii ile. Kwa
mfano, katika vita dhidi ya Nduli Iddi Amini 1978/1979 nyimbo za kwaya, nyimbo za
muziki wa dansi, tenzi, mashairi n.k. zilitumika kuongeza hamasa kwa askari
wetu waliokuwa mstari wa mbele vitani kuwaongezea ari ya kumwadhibu adui yetu.
Kitendo cha kushindwa kwa Iddi Amini katika vita vile tunaweza kusema kwamba
kazi hizo za fasihi simulizi zimefaulu katika dhima yake ya kuelimisha ili
kuongeza hamasa kwa askari wetu. Umuhimu wa fasihi unaonekana katika kufaulu
kutatua matatizo yetu katika jamii.
                                                             
(vii) Kuukuza Ushirikiano         
Ilivyo ni kwamba fasihi simulizi ni mali ya jamii wala sio ya
mtu binafsi. Hadithi inaposimuliwa kwa hadhira kubwa, vitendawili vinapotegewa
kundi pana, ni kwa sababu kimsingi fasihi simulizi ndivyo ilivyokusudiwa
itumike katika muktadha wa kuvihusisha sio vikundi vidogo vidogo tu, bali pia,
na hasa jamii nzima.kwa jumla.
(viii)  Kuzikuza na Kuziendeleza Stadi za Lugha         
Kwa kuwa fasihi simulizi hutegemea usemi na matamko, hatuwezi
kushiriki katika kusimulia hadithi, kutegeana vitendawili, kuimba, nk. bila ya
kuongea au kutamka au kuimba. Kwa sababu hii, fasihi simulizi ina mchango
mkubwa wa kuboresha uwezo wetu wa kuzimiliki na kuzimudu stadi za lugha. Kwa
mfano, tanzu za vitanza ulimi zilisaidia kuhakikisha kwamba utamkaji ni mzuri;
utegeanaji wa vitendawili na majibu yake sahihi huukuza uwezo wa kuwaza haraka
haraka na kwa usahihi. Hadithi huukuza ule uwezo wa kukumbuka maudhui.
Kwa jamii ya sasa
fasihi simulizi ni muhimu sana kwa jamii kwa sababu jamii inakengeuka sana na
kuacha amali muhimu.
4.     Tanzu
za fasihi simulizi ni hadithi na semi tu! Jadili.

MAJIBU

Fasihi simulizi ni sanaa ya lugha yenye
tanzu mbalimbali zikiwemo hadithi na semi. Kwa uchambuzi wa wataalamu wengi wa
fasihi simulizi kama vile Mulokozi, anaainisha tanzu nne ambazo ni Hadithi,
semi, ushairi na sanaa za maonesho. Tanzu hizo na vitanzu vyake huweza
kuoneshwa katika mchoro ufuatao.
Soga
Tarihi/Visakale
Lakabu
Maigizo
Kwa ujumla mgawanyo wa
tanzu za fasihi simulizi bado unahitaji mjadala kwa sababu wataalamu wenyewe
bado hawajakubaliana na aina moja, kila mmoja ana aina yake ya uainishaji.