NUKUU ZA USHAIRI

By , in Ushairi on . Tagged width:
Kitengo Ushairi
 

Mashairi yanaweza kugawanywa katika aina mbalimbali kulingana na idadi ya mishororo katika kila ubeti.

Tanbihi: Aina za Mashairi ni tofauti na Bahari za Ushairi. Aina za mashairi huzingatia idadi ya mishororo katika kila ubeti ilhali Bahari za Shairi hutegemea na muundo wa shairi kwa kuzingatia vina, mizani, vipande na mpangilio wa maneno. Shairi moja haliwezi kuwa la aina mbili (k.v tarbia na takhmisa) lakini shairi linaweza kuwa katika bahari zaidi ya moja.

Zifuatazo ni aina za mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika kila ubeti

AINA MISHORORO
Umoja/tathmina 1 Tathmina au Umoja ni shairi lenye mshororo mmoja katika kila ubeti.
Tathnia 2 Tathnia ni shairi lenye mishororo miwili katika kila ubeti.
Tathlitha 3 Tathlitha ni shairi lenye mishororo mitatu katika kila ubeti.
Tarbia 4 Tarbia ni shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti. Mashairi mengi ni ya aina ya tarbia.
Takhmisa 5 Takhmisa ni shairi lenye mishororo mitano katika kila ubeti.
Tasdisa 6 Tasdisa ni shairi lenye mishororo sita katika kila ubeti.
Usaba 7 Usaba ni shairi lenye mishororo saba katika kila ubeti.
Ukumi 10 Ukumi ni shairi lenye mishororo kumi katika kila ubeti.
BAHARI ZA USHAIRI
Kitengo Ushairi
Aina za Mashairi
Uchambuzi wa Mashairi

Bahari za ushairi ni nyingi sana. Shairi huainishwa katika bahari fulani kulingana na mtindo wake, umbo lake na matumizi ya lugha.

Mifano ya Bahari za Ushairi

 1. Utenzi – shairi ndefu lenye kipande kimoja katika kila mshororo.
 2. Mathnawi – ni shairi la vipande viwili (ukwapi na utao) katika kila mshororo.

Ewe mtunga silabi, na sauti ya kinubi,
Majukumu hatubebi, maadamu hatushibi,
Mateso kwa ajinabi, kwa mabwana na mabibi
Ukija hayatukabi, karibia karibia

Ukawafi – ni shairi la vipande vitatu (ukwapi, utao na mwandamo) katika kila mshororo.

Nashindwa nikupe nini, nishukuru kwa malezi, mapenzi na riziki,
Ni pendo kiasi gani, lishindalo la mzazi, kweli mama hulipiki,
Ulinilinda tumboni, ukilemewa na kazi, ila moyo huvunjiki,
Kanilisha utotoni, mavazi pia malazi, ukitafuta kwa dhiki.

Mavue – Shairi la vipande vinne (ukwapi, utao, mwandamo na ukingo) katika kila mshororo.

Sisi walipa ushuru, wajenga taifa, tena kwa bidii, twahangaishwa,
Tumenyimwa uhuru, tuna mbaya sifa, hatujivunii, tunapopotoshwa,
Kila tunapopazuru, damu na maafa, hatutulii, hali ya kutishwa

Ukaraguni – shairi ambalo vina vyake vya kati na vya mwisho hubadilika kutoka ubetio mmoja hadi mwingine.

Vina Ubeti 1: —ni, —mi,
ubeti 2: —ta, —lo,
ubeti 3: —po, —wa,

Ukara – shairi ambalo vina vya kipande kimoja havibadiliki kutoka ubeti mmoja hadi mwingine, lakini vina vya kipande kingine hubadilika. Kwa mfano, vina vya kati vinafanana kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho lakini vina vya kipande cha mwisho vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.

vina Ubeti 1: —shi, —ma,
ubeti 2: —shi, —ko,
ubeti 3: —shi, —le,
ubeti 4: —shi, —pa

Mtiririko – shairi ambalo vina vyake vya mwisho na vya kati havibadiliki kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho.

kwa mfano vina vikiwa ( —ni, —ka) kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho.

Mkufu/pindu – Shairi ambalo neno la mwisho au kifungu cha mwisho cha maneno katika ubeti mmoja, hutangulia katika ubeti unaofuatia.

Hakika tumeteleza, na njia tumepoteza,
Nani wa kutuongoza, aliyepewa uweza,
Filimbi akipuliza, tusiyeweza kupuuza,
Bali twaisikiliza, bila ya kuzungumza,

Bila ya kuzungumza, wala mwendo kulegeza,
Tumwandame ja mwangaza, kututoa palipo giza,
Penye dhiki ya kuliza, bila sauti kupaza
Pengo hili kulijaza, ni nani anayeweza,

Kikwamba – Neno moja au kifungu cha maneno hurudiwarudiwa kutanguliza mishororo au ubeti katika shairi.

Jiwe hili lala nini, ila moshi na majani,
Jiwe linalala lini, litokapo vileoni,
Jiwe hili halineni, lina macho halioni,
Jiwe na tulibebeni, tulitupe mitaroni

Kikai – Shairi lenye kipande kimoja kifupi (chenye mizani chache kuliko kingine) Mfano (8,4)

Nani binadamu yule, adumuye,
Anayeishi milele, maishaye
Jenezani asilale, aluliye,
Kaburi liko mbele, sikimbiye.

Msuko – Shairi ambalo kibwagizo/mshororo wa mwisho ni mfupi kuliko mishororo mingineyo. K.v (8,8) (8,8) (8,8) (8).

Hawajazawa warembo, usidhani umefika,
Ukisifiwa mapambo, jinsi ulivyoumbika,
Akipata jipya umbo, ‘tabaki kihangaika,
Usidhani umefika.

 1. Mandhuma – shairi ambalo kipande kimoja hutoa hoja, wazo ama swali, huku cha pili kikitoa jibu/suluhisho.
 2. Malumbano – Mashairi mawili ambapo mshairi mmoja hutunga shairi akijibu au kupinga utunzi wa mshairi mwengine.
 3. Ngonjera – Shairi lenye wahusika wawili wanaojibizana. K.m. Ubeti wa kwanza, mwalimu, na wa pili, mwanafunzi.
 4. Sakarani – Shairi lenye bahari zaidi ya moja.
 5. Sabilia – Shairi lisilokuwa na kibwagizo. Kituo (mshororo wa mwisho) hubadilika kutoka ubeti hadi ubeti.
 6. Shairi huru – shairi lisilozingatia sheria za ushairi
 7. Shairi guni – shairi lenye makosa ya arudhi za shairi
FASIHI

Fasihi ni sanaa ya lugha. Fasihi hutumia lugha kutoa sanaa mbalimbali katika jamii.

Yaliyomo

 • Tanzu za Fasihi
  • Fasihi Simulizi
  • Fasihi Andishi
 • Tofauti kati ya Fasihi Andishi na Fasihi Simulizi
 • Umuhimu wa Fasihi Katika Jamii

Tanzu za Fasihi

Kuna tanzu mbili kuu za fasihi, na kila utanzu una vipera vyake: Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi:

Fasihi Simulizi

 1. Hadithi (Ngano) – hekaya, mighani, visasili n.k
 2. Nyimbo – za jandoni, za ndoa, za kazi n.k
 3. Maigizo – michezo ya kuigiza, ngomezi n.k
 4. Tungo Fupi – methali, vitendawili n.k

Fasihi Andishi

 1. Hadithi Fupi – hadithi isiyokuwa ndefu iliyochapishwa katika mkusanyiko wa hadithi nyingine
 2. Riwaya – hadithi ndefu iliyochapishwa katika kitabu chake pekee
 3. Tamthilia – mchezo wa kuigiza uliowekwa kwa maandishi
 4. Ushairi* – mashairi yaliyoandikwa

Tofauti kuu kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi ni kwamba Fasihi Simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo au matendo ilhali Fasihi Andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.

Tanbihi:Ushairi ni kipera cha nyimbo lakini pia mashairi yanaweza kuwa chini ya Fasihi Andishi, ikiwa yamechapishwa.

Tofauti kati ya Fasihi Andishi na Fasihi Simulizi

FASIHI SIMULIZI FASIHI ANDISHI
1. Huwasilishwa kwa njia ya mdomo na/au matendo. Huwasilishwa kwa njia ya maandishi
2. Ni mali ya jamii. Kazi andishi ni mali ya mwandishi (na mchapishaji)
3. Msimulizi anaweza kubadilisha sehemu fulani Kitabu kilichoandikwa hakiwezi kubadilishwa
4. Huhifadhiwa akilini Huhifadhiwa vitabuni
5. Kazi simulizi hubadilika na wakati Kazi andishi haibadiliki na wakati
6. Huhitaji msimulizi na hadhira yake wawe mahali pamoja wakati wa masimulizi Msomaji anaweza kusoma kitabu cha hadithi peke yake, mahali popote, wakati wowote
7. Mtu yeyote anaweza kutunga na kusimulia Ni lazima mwandishi na msomaji wawe na uwezo wa kusoma
8. Hutumia wahusika changamano (wanyama, watu, mazimwi n.k) Hutumia wahusika wanadamu.

Umuhimu wa Fasihi Katika Jamii

 • Kuburudisha jamii. Takribani vipera vyote vya fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira.
 • Kuelimisha. Fasihi hukusudia kuelimisha hadhira kuhusu jamii, mazingira n.k
 • Kudumisha maadili katika jamii kwa kuelekeza, kuonya na kunasihi hadhira jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii.
 • Kuunganisha jamii. Fasihi huleta pamoja watu katika jamii. Kwa mfano, katika nyimbo, miviga, vichekesho.
 • Kukuza lugha. Aghalabu tungo zote za fasihi hutumia lugha. Isitoshe, fasihi hutumia mbinu nyingi za lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na ukwasi wa lugha.
 • Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii. Aghalabu kazi za fasihi (hasahasa Fasihi Simulizi) huambatanishwa na desturi mbalimbali za jamii husika.
 • Kukuza uwezo wa kufikiri. Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. k.m vitendawili, ngano za mtanziko n.k
FASIHI ANDISHI
Utanzu wa Fasihi
Kiingereza Written Literature
Tanzu za Fasihi Andishi
 • Hadithi Fupi
 • Riwaya
 • Tamthilia
 • Ushairi – Mashairi Yaliyoandikwa
Angalia
 • Aina za Wahusika
 • Hadithi Fupi vs Riwaya
 • Tamathali za Usemi
Fasihi Simulizi
Ushairi

Fasihi Andishi ni aina ya sanaa ambayo hutumia maneno yaliyoandikwa kupitisha ujumbe. Ni sanaa inayopitishwa kwa njia ya maandishi

Yaliyomo

 • Tanzu za Fasihi Andishi
 • Sifa za Fasihi Andishi
 • Umuhimu wa Fasihi Andishi
 • Uchambuzi wa Fasihi Andishi
  • Aina ya Kazi Andishi
  • Wahusika
  • Maudhui na Dhamira
  • Mandhari
  • Mbinu za Lugha

Tanzu za Fasihi Andishi

Kuna tanzu nne kuu za Fasihi Simulizi:

 1. Hadithi Fupi – kazi andishi ya fasihi isiyokuwa ndefu sana
 2. Riwaya – kazi andishi ya fasihi ambayo huwa ndefu kuliko hadithi fupi
 3. Tamthilia- kazi andishi ya fasihi inayowasilisha mchezo wa kuigiza
 4. Mashairi – mashairi yaliyochapishwa huwa chini ya fasihi andishi.

Sifa za Fasihi Andishi

 1. Hupitishwa kwa njia ya maandishi
 2. Ni mali ya mtu binafsi
 3. Haiwezi kubadilishwa
 4. Hutumia mbinu za lugha na mbinu za sanaa

Umuhimu wa Fasihi Andishi

 1. Kuhifadhi kazi ya sanaa katika maandishi
 2. Kukuza lugha
 3. Kuburudisha
 4. Kuelimisha
 5. Kukashifu tabia zisizoandamana na maadili ya jamii
 6. Kuonya, kuelekeza, kunasihi

Uchambuzi wa Fasihi Andishi

Unapochambua kazi ya fasihi andishi zingatia:

Aina ya Kazi Andishi

 • Tambua aina au kipera cha kazi andishi ikiwa ni riwaya, hadithi fupi au tamthilia

Wahusika

 • Tambua wahusika katika kazi hiyo ya fasihi
 • Fafanua sifa za kila mhusika kwa kutumia vivumishi au virai vivumishi vinavyolingana na hulka za mhusika huyo.
 • Aidha, unapaswa kuyakinisha sifa hizo kwa kutolea mifano kutoka kwenye hadithi
 • Taja aina ya wahusika

Maudhui na Dhamira

 • Maudhui – ni nini kinachofanyika?
 • Dhamira – lengo/kusudi la kazi hiyo ni nini?

Mandhari

 • Hadithi inafanyika katika mazingira gani?
 • Mazingira hayo yanachangia vipi katika kisa hicho au sifa za wahusika?
 • Msanii ameunda hali gani? (hisia, n.k)

Mbinu za Lugha

 • Taja kwa kutolea mifano, fani za lugha zilizotumika ili kuifanya lugha iwe ya kuvutia zaidi
 • Fafanua mbinu za sanaa zilizotumika na utaje mifano mwafaka
FASIHI SIMULIZI
Utanzu wa Fasihi
Kiingereza Oral Literature
Tanzu za Fasihi Simulizi
 • Hadithi / Ngano
 • Nyimbo
 • Maigizo
 • Tungo Fupi
Tamathali za Usemi
Fasihi Andishi
VIPERA VYA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI
HADITHI / NGANO
 • Khurafa
 • Hekaya
 • Mighani / Visakale
 • Usuli / Visaviini
 • Visasili
 • Hadithi za Mtanziko
 • Hadithi za Mazimwi
NYIMBO
 • Mashairi
 • Kimai
 • Wawe/Hodiya
 • Nyimbo za Ndoa
 • Nyimbo za Kidini
 • Nyimbo za Kisiasa
 • Za Tohara/Jandoni
 • Nyimbo za Kizalendo
TUNGO FUPI
 • Methali
 • Vitendawili
 • Mafumbo
 • Vitanza Ndimi na Vichezea Maneno
 • Semi
 • Lakabu
 • Misimu
MAIGIZO
 • Michezo ya Kuigiza
 • Ngomezi
 • Miviga
 • Malumbano ya Utani
 • Mazungumzo/Soga
 • Ulumbi
 • Vichekesho
 • Maonyesho

Fasihi Simulizi ni utanzu wa fasihi ambao unawakilisha sanaa ya lugha inayopitishwa kutoka kwa kizazi hadi kizazi kwa njia ya maneno/masimulizi ya mdomo.

Sifa za Fasihi Simulizi

 1. Hupitishwa kwa njia ya mdomo
 2. Ufanisi wa sanaa katika fasihi simulizi hutegemea uwezo wa msimulizi, au wahusika
 3. Masimulizi yake yanaweza kuathiriwa na mazingira, hisia na hali
 4. Ni mali ya jamii. Hakuna mtu fulani anayemiliki sanaa katika fasihi simulizi.
 5. Inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, au mazingira mbalimbali kwa sababu hutegemea kumbukumbu ya msimulizi.
 6. Aghalabu huwa na funzo fulani

Umuhimu wa Fasihi Simulizi

 1. Kuburudisha – Hufurahisha na kuchangamsha hadhira
 2. Kunasihi- kutolea mawaidha na kuonyesha mwelekeo unaotarajiwa katika jamii
 3. Kuelimisha watu kuhusu vitu mbalimbali hasa mazingira yao
 4. Kutambulisha jamii – jamii mbalimbali husifika kutokana na sanaa zao katika fasihi simulizi kama vile nyimbo
 5. Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii
 6. Kuunganisha watu – huleta watu pamoja
 7. Kukuza lugha – fasihi huimarisha lugha kwa kuwa hutumia mbinu mbalimbali za lugha.
 8. Kuliwaza – hutoa huzuni na kuleta matumaini.
 9. Kupitisha muda – wakati mwingine fasihi simulizi hutumika kupitisha muda.

Isimu Jamii

Isimu Jamii (social linguistcs) – ni tawi la isimu (elimu ya lugha) linalochunguza namna lugha inavyotumika katika jamii na uhusiano baina yake. Tawi hili huzingatia matumizi ya lugha katika mazingira tofauti; aina mbali mbali za lugha na mazingira yake; uhusiano kati ya lugha na utamaduni wa jamii inayoitumia.

 • Istilahi za Isimu Jamii
 • Aina za Lugha

Istilahi za Isimu Jamii

 1. Isimu (linguistics) – ni mtalaa ambao huchunguza, huchanganua na pia kuchambua na kufafanua lugha kama mfumo wa mawasiliano baina ya wanadamu.
 2. Lugha – ni chombo cha mawasiliano baina ya watu. Lugha huzingatia mpangilio maalum wa sauti, maneno na sentensi.
 3. Sajili – ni mukhtadha/rejista mbalimbali au mitindo maalum ya lugha katika mazingira/hali mbalimbali. Mifano ya sajili ni kama vile lugha ya hospitalini, shuleni, sajili ya dini, biashara, kisiasa, michezo,
 4. Fonolojia – ni tawi la sayansi ya isimu linaloshughulikia uchunguzi wa mfumo wa sauti katika lugha fulani, kwa mfano ugawanyaji wa irabu na konsonanti. Fonolojia hutumika kuunda alfabeti katika lugha fulani. Aghalabu kila lugha hutumia mfumo fulani wa sauti mahususi katika lugha hiyo pekee.
 5. Fonetiki – huchunguza sauti zinazotamkwa na binadamu bila kuzingatia lugha yoyote.
 6. Mofolojia – (au sarufi maumbo) ni tawi la isimu linalochunguza maneno ya lugha fulani, aina za maneno katika lugha, hasa upangaji wa mofimu mbalimbali zitumikazo kwa ajili ya kuunda maneno hayo. Kwa mfano, lugha ya Kiswahili hutumia mbinu kadhaa kuunda maneno kulingana na mpangilio wa mofimu. Kwa mfano, neno ‘lima’ linaweza kutumika kuunda maneno mengine katika Kiswahili k.m mkulima, kilimo, nimelima, limika n.k Katika kubadilisha mofimu hizi, tunaweza kubadilisha neno moja kutoka aina moja(kitenzi) hadi nyingine (nomino) n.k
 7. Sintaksi – (au sarufi miundo) ni tawi la isimu au taaluma ya sarufi inayoshughulikia jinsi vikundi vya maneno na sentensi mbalimbali zinajengwa katika lugha. Sintaksia huangazia kanuni au sheria za lugha. Kila lugha huwa na sheria zake za kuambatanisha maneno kama vile jinsi ya kufuatanisha vitenzi, nomino na vielezi. Kwa mfano: Mtoto yako shiba ni sentensi isiyokuwa na sintaksi. Sentensi sawa ingekuwa: Mtoto wako ameshiba.
 8. Semantiki – ni tawi la isimu linalochunguza maana halisia (mantiki) ya maneno, kifungu au sentensi katika lugha. Sentensi isiyokuwa na mantiki ni sentensi inayotoa maana ambayo haiwezekani katika uhalisia. Sentensi inaweza kuwa sawa kisintaksia lakini iwe na makosa ya kimantiki. Kwa mfano: Kiatu cha mbwa kimefutwa kazi kwa sababu kumi ni kubwa kama hewa.

Aina za Lugha Katika Isimu Jamii

 1. Lafudhi – Ni upekee wa mtu katika matamshi (accent) unaoathiriwa na lugha ya mama, mazingira yake ya kijiografia au kiwango ujuzi wake wa lugha.
 2. Lahaja – ni vijilugha vinavyoibuka kwa lugha moja kuu kutokana na tofauti za kijiografia baina ya wazungumzaji wa lugha hiyo. Kwa mfano lugha ya Kiswahili ina lahaja kadhaa kama vile Kimtang’ata, Kilamu, Kimvita, n.k. Tofauti baina ya lufudhi ni kama msamiati, muundo wa sentensi au matamshi.
 3. Lugha rasmi – ni lugha inayotumika katika shughuli za kiofisi ama ya wakati wa mawasiliano rasmi katika taifa fulani. Kwa mfano, lugha rasmi nchini Kenya ni Kiingereza.
 4. Lugha rasimi – ni mtindo wa lugha uliotumiwa na mtu/watu fulani mashuhuri (zamani) na ambao huonekana kuwa mtindo bora wa lugha unaofaa kuigwa na wengine. Kwa mfano lugha ya Shakespeare.
 5. Lugha ya taifa – ni lugha inayoteuliwa na taifa fulani kama chombo cha mawasiliano baina ya wananchi, kwa maana inazungumzwa na wananchi wengi katika taifa hilo. Lugha ya taifa, nchini Kenya ni Kiswahili; Uganda ni Kiganda.
 6. Lugha Sanifu – Ni lugha iliyokarabatiwa na sheria zake (k.v muundo wa sentensi, msamiati, sarufi, n.k) kubainishwa na kuandikwa, na kwa hivyo huzingatia sarufi maalum na upatanisho sahihi wa sentensi. Kwa mfano: Kiswahili sanifu – ni lugha isiyokuwa na makosa ya kisarufi.
 7. Lingua Franka – Ni lugha inayoteuliwa miongoni watu wenye asili tofauti wasiozungumza lugha moja ili iwe lugha ya kuwaunganisha katika shughuli rasmi au za kibiashara.
 8. Pijini – ni lugha inayozaliwa kutokana na mchanganyo wa lugha zaidi ya moja. Kwa mfano. Sheng’ (lugha ya vijana mitaani nchini ni lugha iliyoibuka kutoka kwa Kiswahili na Kiingereza.
 9. Krioli – Ni pijini iliyokomaa na kukubalika.
 10. Lugha mame – hii ni lugha isiyokua na ambayo hubaki kati umbo lake la awali. Kwa mfano lugha ya Kilatini haibadiliki na hivyo hutumika katika kubuni majina ya kisayansi, n.k.
 11. Lugha azali – ni lugha inayozaa lugha nyinginezo.
 12. Misimu – ni lugha yenye maneno ya kisiri ambayo hutumiwa na kikundi fulani cha watu katika jamii, inayoeleweka tu baina yao. Misimu huibuka na kutoweka baada ya muda.

Kinyume

KINYUME
Kitengo Sarufi
NAVIGATION
Viungo Mbalimbali
Kukanusha

Maneno ya kinyume ni maneno yenye maana inayopingana. Inafaa ikumbukwe kwamba kuna tofauti kati ya kinyume na kukanusha. Kukanusha ni kukataa ujumbe wa sentensi bila kubadilisha maneno. Tunapokanusha, tunabadilisha viambishi pekee ili kupinga wazo la sentensi. Maneno ya kinyume huwa maneno mengine tofauti kabisa ambayo yanapingana kimaana bila kubadilisha maendelezo ya neno.

Kinyume cha Kawaida
Hisia, hali, dhana n.k
1. vita amani
2. furaha kilio
3. nuru giza
4. shibe njaa
5. mwanzo mwisho
Kinyume cha Sifa
Sifa zinazopingana kimaana
1. tamu chungu
2. kubwa dogo
3. nzuri mbaya
4. nyeupe nyeusi
Kinyume cha Jinsia (Uume – Uke)
Majina ya kijinsia moja yanabadilishwa na kuwa jinsia ile nyingine.
1. baba mama
2. mumewe mkewe
3. mjomba shangazi
4. kaka dada
5. babu nyanya
6. mvulana msichana
7. ghulamu banati
8. shaibu ajuza
Kinyume cha Uhusiano
Kinyume cha vitu au dhana mbili zinazohusiana.
1. mwalimu mwanafunzi
2. daktari mgonjwa
3. mzazi mwana
4. kiongozi mfuasi
Kinyume cha Vitenzi
Tunabadilisha vitenzi kwa kuweka vitenzi vingine vyenye maana ilnayokinzana
1. ongea nyamaza
2. penda chukia
3. sifu kashifu
4. simama keti
5. lia cheka
6. tabasamu nuna
7. enda kuja
Kinyume cha Kutendua
Vitenzi vinaweka katika kauli ya kutendua ili kuvikanusha.
1. fumba fumbua
2. ficha fichua
3. vaa vua
4. choma Choma

Kukanusha

 

Kukanusha ni kukataa au kukana kauli.

Mara nyingi tunapokanusha, tuanaongeza kiambishi ‘HA-‘ mwanzoni mwa kitenzi. Hata hivyo, kiambishi hicho hubadilika katika nafsi ya kwanza na ya pili umoja. Angalia jedwali lifuatalo.

KIAMBISHI MATUMIZI MFANO
SI nafsi ya kwanza si-ku-wa-on-a
HU nafsi ya pili hu-ni-faham-u
HA nafsi ya tatu ha-ta-chuku-a

Viambishi vya wakati na vya hali pia hubadilika kama ilivyoonyeshwa katika jedwali lifuatalo:

Kukanusha Wakati Uliopita (LI) => ‘KU’
1 Kajuta alimpigia kura. Kajuta hakumpigia kura.
2 Nilikupa nafasi yako. Sikukupa nafasi yako.
Kukanusha Wakati Timilifu (Uliopita Muda Mfupi) (ME) => ‘JA’
1 Maziwa ya nyanya yamemwagika. Maziwa hayajamwagika.
2 Viwete wametembea Viwete hawajatembea.
Kukanusha Wakati Uliopo (NA) => ‘-I’
1 Unasoma sentensi ya kwanza. Husomi sentensi ya kwanza.
2 Zinafanana na nyota. Hazifanani na nyota.
Kukanusha Wakati Ujao (TA) => ‘TA’
1 Jua litawaka sana. Jua halitawaka sana.
2 Watakaribishwa kwenye malango ya lulu. Hawatakaribishwa kwenye malango ya lulu.
Kukanusha Wakati wa Mazoea (HU) => ‘-I’
1 Polisi wa jiji kuu huchukua hongo. Polisi wa jiji kuu hawachukui hongo.
2 Bendera hufuata upepo. Bendera haifuati upepo.
Kukanusha Wakati Usiodhihirika (A) => ‘-I’
1 Anita ampenda Kaunda. Anita hampendi Kaunda.
2 Chema chajiuza, kibaya chajitembeza. Chema hakijiuzi, kibaya hakijitembezi.
Kukanusha KI ya Masharti (KI) => ‘SIPO’
1 Ukimwadhibu mtoto, atapata adabu njema. Usipomwadhibu mtoto hatapata nidhamu..
2 Bei yake ikishuka, nitainunua. Bei yake isiposhuka, sitainunua.
Kukanusha PO ya Wakati (PO) => ‘SIPO’
1 Uamkapo asubuhi ndugu yangu mshukuru Mungu. Usipo amka asubuhi ndugu yangu usimshukuru Mungu.
2 Mtoto aliapo mnyonyeshe. Mtoto asipo lia usimnyonyeshe
Kukanusha Hali ya Uwezekano (NGE) => ‘SINGE’
1 Ningekuwa nakupenda ningekwambia mapema. Nisingekuwa nakupenda nisingekwambia mapema.
2 Zingekuwa nyingi, wangeziiba. Zisingekuwa nyingi, wasingeziiba.
Kukanusha Hali ya Uwezekano (NGALI) => ‘SINGALI’
1 Khadija angalisoma kwa bidii angalikuwa na cheo kikubwa. Khadija asingalisoma kwa bidii asingalikuwa na cheo kikubwa
2 Yangalikuwa mabivu yangalianguka yenyewe. Yasingalikuwa mabivu yasingalianguka yenyewe
Kukanusha Amri/Agizo (-a/-e) => ‘SI’
1 Peleka kikapu hiki kwa nyanya. Usipeleke kikapu hiki kwa nyanya.
2 Chakula kiliwe. Chakula kisiliwe.
3 Mpende adui yako. Usimpende adui yako.
4 Waambieni watu wa mataifa yote. Msiwaambieni watu wa mataifa yote.
Kukanusha Viunganishi vya Kujumuisha (NA, KA) => ‘WALA’
1 Bafi alikuzaba kofi na kukupiga teke. Bafi hakukuzaba kofi wala hakukupiga teke.
2 Mama amepika chakula tukala pamoja. Mama hajapika chakula wala hatujala pamoja.

SARUFI: Matumizi ya Lugha

Sarufi ni sheria, kanuni au taratibu zinazopaswa kufuatwa katika lugha fulani. Kila lugha huwa na kanuni zake. Katika sarufi tutazingatia sauti(utamkaji), aina ya maneno, upatanisho wa maneno kisarufi, muundo wa sentensi za Kiswahili na kadhalika.

Ufuatao ni mukhtasari wa baadhi ya yale tuliyokuandalia katika matumizi ya lugha. Fungua kila ukrasa ili kusoma mada kwa kina.

Vipashio vya Lugha

Vipashio vya lugha ni viungo mbalimbali vinavyowekwa pamoja katika mpangilio fulani kisarufi, kuunda lugha:

 1. Sauti
 2. Mofimu
 3. Neno
 4. Sentensi

Kwa kuzingatia vipashio hivi vya lugha, tumekuandalia vipengele vifuatavyo katika sarufi:

Aina za Maneno

 • Nomino – majina, aina za nomino, uundaji wa nomino kutoka kwa maneno mengine, wingi
 • Vitenzi – vitendo katika sentensi, aina za vitenzi, mnyambuliko wa vitenzi
 • Viwakilishi – maneno yanayowakilisha nomino; aina za viwakilishi
 • Vivumishi – aina za vivumishi k.v vivumishi vya sifa, n.k
 • Vielezi – vielezi halisi, vielezi vya namna n.k
 • Viunganishi – a-unganifu, kuonyesha tofauti, sababu, sehemu n.k
 • Vihisishi – maneno ya kuonyesha hisia k.v hasira, mshangao n.k
 • Vihusishi – uhusiano wa nomino na mazingira yake
 • Kinyume – kinyume cha maneno mbalimbali

Muundo wa Maneno

 • Sauti na Silabi – aina za sauti(konsonanti, vokali), silabi, matamshi
 • Shadda na Kiimbo – mkazo katika maneno, kiimbo(intonation)
 • Viambishi – maana na aina za viambishi, uainishaji
 • Mofimu – mofimo huru, mofimu tegemezi
 • Viungo – Matumizi ya viungo k.v KWA, KU, JI, MA, NI, NA n.k

Upatanisho wa Maneno

 • Ngeli – ngeli mbalimbali za Kiswahili k.v A-WA, KI-VI n.k
 • Umoja na Wingi – wingi/umoja wa nomino, sentensi n.k
 • Ukubwa na Udogo – onyesha ukubwa/udogo wa neno au sentensi
 • Nyakati na Hali – nyakati(uliopita, uliopo, ujao, n.k), NGE, NGALI,
 • Kukanusha – kukanusha sentensi katika hali na nyakati mbalimbali

Sentensi

 • Aina za Sentensi – changamano, ambatano n.k
 • Uchanganuzi wa Sentensi – kikundi nomino, kikundi tenzi n.k
 • Virai na Vishazi – aina za virai, kishazi huru, kishazi tegemezi
 • Shamirisho na Chagizo – shamirisho yamwa, kitondo n.k
 • Uakifishaji – alama za kuakifisha k.v swali(?), kikomo(.) n.k
MAGHANI
Kitengo Ushairi
 
Uchambuzi wa Mashairi
Aina za Ushairi

Maghani ni tungo zinazotolewa kwa kughanwa (nusu kuimbwa nusu kukaririwa) Maghani yanaweza kuambatanishwa na ala za muziki au kughanwa kwa mdomo tu.

Aina za Maghani

Zipo fani mbali mbali za maghani ambazo zimeainishwa katika tanzu mbili kuu:

 1. Maghani ya Kawaida
 2. Maghani ya Masimulizi

Maghani ya Masimulizi

Lengo la maghani ya aina hii ni kusimulia kisa fulani, historia, n.k.

Kuna fani mbili za Maghani ya Masimulizi:

 1. a) Tendi

Tendi ni ushairi mrefu unaosimulia matukio ya kishujuaa. Tendi zinaposimuliwa huandamana na ala za muziki.

Sifa za Tendi:

 • Ni ushairi mrefu
 • Husimulia matendo ya kishujaa kwa njia kishairi
 • Husimuliwa badala ya kuimbwa
 • Huandamana na ala za muziki
 • Husimulia visa vya kihistoria
 • Hutungwa papo kwa hapo
 1. b) Rara

Hizi ni hadithi fupi za kishairi zenye visa vya kusisimua, zinazosimuliwa zikiambatanishwa na ala za muziki. Aghalabu hughanwa na watoto; na hutumika kama michezo ya watoto.

Sifa za Rara

 • Ni hadithi fupi za kishairi
 • Husimulia visa vya kusisimua
 • Zinaweza kuimbwa au kusimuliwa
 • Huambatana na ala za muziki
 • Aghalabu huwa ni visa vya kubuni

Maghani ya Kawaida (Sifo)

Maghani ya Kawaida ni maghani yanayosifia mtu, kitu au hali katika jamii

 1. a) Majigambo au Kivugo

Haya ni maghani ambayo mtunzi hujisifia (kujigamba) namna alivyo hodari katika nyanja fulani. Tungo hizi hutumia chuku na maneno ya kejeli kuwadunisha wapinzani wa mtunzi.

Sifa za Majigambo

 • Hutumia nafsi ya kwanza
 • Msimulizi hutumia maneno ya kujigamba
 • Msimulizi hutumia chuku kwa wingi ili kujisifu
 • Hutungwa kwa ubunifu mkubwa na hutumia mbinu kama sitiari, vidokezi, ishara n.k
 • Majigambo mengi huwa mafupi, lakini baadhi yake huwa marefu.
 • Huwa na matendo matukufu ya msimulizi
 • Huwa na ahadi za matendo kutoka kwa msimulizi
 1. b) Tondozi

Tondozi ni aina ya sifo ambayo husifia watu mashuhuri katika jamii kama vile viongozi

Sifa za Tondozi

 • Huwa ni ushairi wa kusimuliwa
 • Husifia mtu mwengine, mtu mashuhuri
 • Hutumia chuku
 • Hutumia mbinu kama sitiari, vidokezi, ishara n.k
 • Hutaja matendo makubwa ya kiongozi anayesifiwa

Pembezi

Pembezi ni maghani ya kumsifu mpenzi.

Sifa za Pembezi

 • Humsifu mpenzi wa mtu
 • Aghalabu huwa ushairi mfupi
 • Hutumia tamathali za lugha kwa wingi kama vile ishara kusimulia umbo la mpenzi
 • Pembezi zinaweza kuandamana na ngoma
 1. ii) Pembezi – tungo za sifa. Zinaweza kusifia kundi fulani la watu, wanyama, njaa, mvua, n.k
MAIGIZO
Utanzu wa Fasihi Simulizi
Vipera vya Maigizo
 • Michezo ya Kuigiza
 • Miviga
 • Ngomezi
 • Malumbano ya Utani
 • Ulumbi
 • Soga
 • Vichekesho
 • Maonyesho ya Sanaa

Maigizo ni sanaa katika fasihi simulizi ambayo watendaji huwa ndio wahusika. Maigizo hayasimuliwi kama mbinu nyingine za fasihi. Wahusika ndio huzungumza katika sehemu zao mbalimbali.

Mifano:

 1. Michezo ya Kuigiza (Jukwaani) – Haya ni maigizo ya jukwaani ambapo watendaji huiga maneno na matendo ya wahusika mbele ya hadhira.
 2. Miviga – Miviga ni sherehe mbalimbali katika jamii fulani. Watu hujumukika na sherehe hizi kulingana na tamaduni zao
 3. Ngomezi – ni sanaa ya ngoma. Midundo mbalimbali ya ngoma hutumika kuwasilisha ujumbe mbalimbali.
 4. Malumbano ya Utani – Malumbano ya utani ni mashindano ya kuongea jukwaani baina ya watu wa makundi au jamii mbili ambayo hutumia kejeli na chuku kukejeli tabia mbaya katika jamii au kundi fulani
 5. Ulumbi – Ulumbi ni uwezo wa kipekee wa kuzungumza mbele ya hadhira. Mtu mwenye uwezo huo wa kipekee wa kuzungumza jukwaani huitwa mlumbi.
 6. Soga – Soga ni mazungumzo baina ya watu wawili au zaidi ambayo aghalabu huwa hayana mada maalum.
 7. Vichekesho – Vichekesho ni aina ya sanaa ya fasihi simulizi ambayo watu hutoa vihadithi vifupi au sentensi zenye uwezo wa kuwafanya wasikilizaji wacheke.
 8. Maonyesho ya Sanaa – Maonyesho huhusisha watu wa jamii au kundi fulani wanaoonyesha taaluma, ujuzi au sanaa yao kwa watazamaji.

Mofimu

MOFIMU
Kitengo Muundo wa Neno
Aina Kuu
 • Mofimu Huru
 • Mofimu Tegemezi
 

Mofimu ni sehemu ndogo zaidi ya neno inayowakilisha maana ya neno hilo. Mofimu inaweza kuwa silabi moja au zaidi.
Kuna aina mbili za mofimu:

 1. Mofimu huru
 2. Mofimu Tegemezi
 1. Mofimu huru

Mofimu huru ni silabi moja au zaidi yenye maana kamili ya neno na inaweza kujisimamia yenyewe bila msaada wa viambishi au silabi nyingine. Aghalabu mofimu huru huwa nomino, vivumishi au vielezi visivyochukua viambishi vya ngeli.
Kwa mfano:daktari, ndoa, nyumba, Miranda

 1. Mofimu Tegemezi

Mofimu tegemezi ni mofimu ambazo huhitaji viambishi au mofimu nyingine tegemezi ili kuleta maana iliyokusudiwa. Mofimu hizi hujumuisha hasa mzizi wa neno (au shina la kitenzi), vivumishi, nomino au vielezi ambavyo vinahitaji viambishi viwakilishi vya ngeli ili kutoa maana iliyokusudiwa.
Shina la kitenzi au mzizi wa neno au kiini cha kitendo ni sehemu ndogo zaidi inayosimamia kitenzi chenyewe bila mnyambuliko, nyakati au viambishi vinginevyo. Viambishi ni mofimu tegemezi ya silabi moja inayowakilisha dhana fulani kama vile hali, ngeli, nafsi, wakati na kadhalika.

k.m:

mtangazaji => m-tangaz-a-ji
{m => mofimu ya ngeli ya M-WA kwa umoja
tangaz => mzizi wa neno, kiini cha kitendo cha kutangaza
a => kiishio cha kitenzi
ji => inaonyesha kazi au mazoea}

wametusumbua => wa-me-tu-sumbu-a
{wa => kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya tatu wingi
me => kiambishi cha wakati timilifu
tu => kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya kwanza wingi – kitendewa/mtendwa
sumbu => shina la kitendo cha kusumbua
a => kiishio}

wakulima => wa-ku-lim-a
{wa => kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya A-WA wingi
ku => kiambishi cha KU ya kitenzi jina
lim => mzizi wa kitendo cha kulima
a => kiishio}

Muundo wa Sentensi

 
 

 

 • Kiima, Kiarifa, Shamirisho na Chagizo
 • Kikundi Tenzi(KT) na Kikundi Nomino(KN)
  • Kikundi Nomino (Kiima): KN
  • Kikundi Tenzi (Kiarifa): KT
  • Shamirisho
  • Chagizo

Kiima, Kiarifa, Shamirisho na Chagizo

Sentensi huwa imeundwa na maneno mbalimbali. Vijenzi hivi vya sentensi ni Kiima, Kiarifa, Shamirisho na Chagizo

Angalia:

 • Aina za Sentensi => Sahili, Changamano, Ambatano
 • Virai na Vishazi
 • Uchanganuzi

Kikundi Tenzi(KT) na Kikundi Nomino(KN)

Hizi ndizo sehemu mbili kuu katika sentensi. Kila kundi kikundi kinaweza kuwa na maneno mbalimbali. Tutayachangua haya zaidi katika uchanganuzi wa sentensi.

Kikundi Nomino (Kiima): KN

Ni sehemu wa sentensi yenye nomino. Pia kikundi nomino kinaweza kushirikisha kikundi kivumishi au kishazi tegemezi.

k.m:

 1. Safari zawa salama bila misukosuko.
 2. Wanafunzi waliokuwa wametoroka shuleni, wamekamatwa na kuadhibiwa.
 3. Matunda matamu huvutia sana.

Kikundi Tenzi (Kiarifa): KT

Ni sehemu ya sentensi yenye kitenzi. Licha ya kitenzi, kikundi tenzi kinaweza kushirikisha kikundi kielezi au kikundi kivumishi. Aidha, kikundi tenzi kinaweza kuwa na kikundi nomino kama shamirisho kipozi au kitondo.

k.m:

 1. Mvua inarutubisha vitu vyote.
 2. Dunia huzunguka jua.
 3. Madawati yaliyokuwa yamechafuliwa yamesafishwa.

Shamirisho

Shamirisho ni mtendwa au mtendewa katika sentensi. Ni sehemu ya sentensi inayowakilisha kitu kilichofanyiwa kitu. Kuna aina tatu za shamirisho.

Shamirisho Kipozi – (direct object)

Ni sehemu inayowakilisha nomino inayopokea kitendo hicho moja kwa moja. Mtendwa

 1. Nyanya aliwasalimia wajukuu wake.
 2. Bustani la Kuzimu linawatisha watu wengi.
 3. Rita alimwandikia kakake barua kwa kalamu nyeusi.

Shamirisho Kitondo – (indirect object)

Huwakilisha ambaye kitendo kinafanywa kwa ajili yake au kwa niaba yake. Mtendewa

 1. Mama aliwapikia watoto ugali tamu.
 2. Bibi anawasimulia wasichana wadogo hadithi za kikale.
 3. Rita alimwandikia kakake barua kwa kalamu nyeusi.

Shamirisho ala kitumizi

Hurejelea ala au kifaa kinachotumika kutekeleza kitendo hicho

 1. Wetu wengine huvuna mahindi kwa panga.
 2. Mchungaji Thabiti alikufa kwa maji.
 3. Rita alimwandikia kakake barua kwa kalamu nyeusi.

Chagizo

Hutuelezea zaidi kuhusu kiima, kiarifa au shamirisho. Aghalabu chagizo huwa kielezi au kivumishi.

 1. Mama alimvalisha bintiye mavazi ya kupendeza.
 2. Mumbe ni msichana hodari sana.
 3. Kinyonga hupendelea kutembea polepole.
 4. Rita alimwandikia ka yake barua kwa kalamu nyeusi.

 NGE na NGALI

MATUMIZI YA NGE NA NGALI
Kitengo Sarufi
NAVIGATION
Ngeli za Kiswahili
Uakifishaji

Nge na Ngali hutumika kuonyesha uwezekano au majuto. Kitendo fulani hakikutokea kwa sababu ya kitendo au hali nyingine ambayo haikutimilika. Kwa kifupi, kuna vitendo au hali mbili zinazotegemena; kwa hivyo hali ya kwanza ikitokea kuna uwezekano wa kitendo cha pili kufanyika.

Ni hatia ya kisarufi kuchanganya NGA na NGALI katika sentensi moja. Ikiwa kipande cha kwanza kimetumia NGE, tumia NGE katika kipande cha pili n.k

 1. a) NGE

Nge hutumika kuonyesha kwamba kitendo fulani hakijafanyika na kwa hivyo jambo fulani halijatokea lakini kuna uwezekano wa kufanya kitendo hicho na jambo hilo litokee.

k.m

 1. Ningekuwa na pesa ningenunua simu => Sina pesa wala sikununua simu, lakini nikipata pesa saa hii, ninaweza kununua simu
 2. Ningejua nyumbani mwake ningemtembelea => Sijui nyumbani kwao wala sijamtembelea, lakini nikijua nitamtembelea.
 1. b) NGALI (au NGELI)

Ngali hutumika kuonyesha kwamba kitendo fulani hakijafanyika na kwa hivyo jambo fulani halijatokea wala hakuna uwezekano wa kufanya kitendo hicho. Hutumika hasa kuonyesha majuto.

k.m

 1. Ningalifika mapema ningalimpata kabla aondoke => Sikufika mapema, hivyo basi sikumpata, wala siwezi kumpata kwa sababu nishachelewa naye ashaondoka
 2. Ungalimsikiza mwalimu, ungalipita mtihani => Hukumsikiza mwalimu na hivyo basi hukupita mtihani, wala hakuna uwezekano wa kumsikiza wala kupita mtihani.

Kukanusha NGE na NGALI

Tunapokanusha NGE na NGALI, tunamaanisha kwamba kitendo cha pili kilifanyika tu kwa sababu kitendo cha kwanza kilikuwa kimefanyika. Kama jambo la kwanza halikundeka, jambo la pili halingetokea.

Tunakanusha kwa kuongeza kiungo ‘SI’ =>
{NGE => SINGE,
NGALI => SINGALI}

Mifano ya Ukanushaji

SENTENSI KUKANUSHA
1. Runinga ingeanguka, ingeharibika. Runinga isingeanguka isingeharibika.
3. Ungejua nini nichokiwaza, labda ingekuwa rahisi kukupata. Usingejua nini nichokiwaza, labda isingekuwa rahisi kukupata.
1. Changarawe ingalikuwa chakula, tungalishiba milele Changarawe isingalilikuwa chakula, tusingalilishiba milele
1. Laiti ningalijua, ningaliokoka nilipokuwa na wakati Laiti nisingalilijua, nisingaliokoka nilipokuwa na wakati

Maana: => kitendo kilifanyika kwa sababu kingine kilifanyika

 1. Nisingekuwa na pesa nisingenunua simu => Nilinunua simu tu kwa sababu nilikuwa na pesa; kuwa na pesa ndiko kulikoniwezesha kununua pesa.
 2. Mvua isingalinyesha, tusingalivuna. => Tulivuna kwa sababu mvua ilinyesha; kunyesha kwa mvua ndiko kulitufanya tuvune.

Ngeli za Kiswahili

NGELI ZA KISWAHILI
Kitengo Sarufi
 
 

Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Katika mfumo wa kisasa (na unaokubalika), ngeli huundwa kwa kuunganisha viambishi viwakilishi vya nomino.

Kwa mfano, neno kitabu. Tunasema, “Kitabu kimepotea – Vitabu vimepotea.”

Kwa kuunganisha kiambishi “KI”(umoja) na VI(wingi), tunapata ngeli ya KI-VI. Ni muhimu kusisitiza kwamba tunazingatia viambishi, wala si silabi ya kwanza.

Hivyo basi, maneno yasioyoanza kwa KI-VI kama vile chama -vyama yatakuwa katika ngeli ya KI-VI kwa kuwa yanachukua kiambishi KI => (Chama kimevunjwa – Vyama vimevunjwa.) Vivyo hivyo, kunayo majina yanayoanza kwa KI-VI yasiyokuwa katika ngeli ya KI-VI maadam yanachukua viambishi tofauti. k.v: kijana => A-WA (kijana amefika- vijana wamefika).

Tumekuandalia majedwali matatu kukupa mukhtasari wa ngeli zote za Kiswahili na jinsi baadhi ya maneno/viambishi vinavyobadilika kutoka ngeli moja hadi nyingine.

 1. a) Jedwali la kwanza linakupatia ngeli, maelezo yake, na mifano ya majina:
NGELI MAELEZO MIFANO
A-WA Hii ni ngeli ya majina ya viumbe wenye uhai k.v watu, wanyama, ndege, wadudu, miungu, malaika n.k Majina mengi katika ngeli ya A-WA huanza kwa sauti M- kwa umoja na sauti WA- kwa wingi. Hata hivyo baadhi ya majina huchukua miundo tofauti. mtu – watu
KI-VI Ni ngeli ya majina ya vitu visivyo hai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Pia ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo. k.v kitoto. kitu – vitu
LI-YA Hujumuisha majina ya vitu visivyo hai pamoja na yale ya ukubwa k.v jitu. Majina yake huchukua miundo mbalimbali. Baadhi yake huchukua muundo wa JI-MA (jicho-macho), lakini yanaweza kuanza kwa herufi yoyote. Kwa wingi, majina haya huanza kwa MA- au ME-. jani – majani
U-I Huwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M- (umoja) na MI(wingi). mti – miti
U-ZI Hurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti /u/’ k.v ukuta-kuta. Majina ya silabi mbili huongezewa /ny/ katika wingi. k.v ufa – nyufa ukuta – kuta
I-ZI Hutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (Wingi). Mengi yake huanza kwa sauti /u/, /ng/, /ny/, /mb/, n.k nyumba – nyumba
U-YA Ni majina machache mno yanayochukua kiambishi U(umoja) na YA(wingi). uyoga – mayoga
YA-YA Hii ni ngeli ya vitu visivyoweza kuhesabika (nomino za wingi). Hayana umoja. Mengi ya majina haya huanza kwa MA- lakini yanaweza kuchukua muundo wowote. maji
I-I Ni ngeli ya majina ya wingi ambayo huchukua kiambishi I- kwa umoja na pia kwa wingi. Majina haya hayana muundo maalum. sukari
U-U Majina ya nomino za wingi yanayoanza kwa sauti /u/ au /m/. Hayana wingi. unga
PA-PA Ni ngeli ya mahali/pahali – maalum. mahali
KU-KU Ngeli ya mahali – kwa ujumla. Aidha, hujumuisha nomino za kitenzi-jina uwanjani
MU-MU Ngeli ya mahali – ndani. shimoni
 1. b) Jedwali la pili linaangazia jinsi ngeli mbalimbali zinavyotumia “a-nganifu”, viashiria na viashiria visisitizi.
NGELI A- UNGANIFU VIASHIRIA VIASHIRIA VISISITIZI
KARIBU MBALI KIDOGO MBALI KARIBU MBALI KIDOGO MBALI
A-WA wa
wa
huyu
hawa
huyo
hao
yule
wale
yuyu huyu
wawa hawa
yuyo huyo
ao hao
yule yule
wale wale
KI-VI cha
vya
hiki
hivi
hicho
hivyo
kile
vile
kiki hiki
vivi hivi
kicho hicho
vivyo hivyo
kile kile
vile vile
LI-YA la
ya
hili
haya
hilo
hayo
lile
yale
lili hili
yaya haya
lilo hilo
yayo hayo
lile lile
yale yale
U-I wa
ya
huu
hii
huo
hiyo
ule
ile
uu huu
ii hii
uo huo
iyo hiyo
ule ule
ile ile
U-ZI wa
za
huu
hizi
huo
hizo
ule
zile
uu huu
zizi hizi
uo huo
zizo hizo
ule ule
zile zile
I-ZI ya
za
hii
hizi
hiyo
hizo
ile
zile
ii hii
zizi hizi
iyo hiyo
zizo hizo
ile ile
zile zile
U-YA wa
ya
huu
haya
huo
hayo
ule
yale
uu huu
yaya haya
uo huo
yayo hayo
ule ule
yale yale
YA-YA ya haya hayo yale yaya haya yayo hayo yale yale
I-I ya hii hiyo ile ii hii iyo hiyo ile ile
U-U wa huu huo ule uu huu uo huo ule ule
PA-PA pa hapa hapo pale papa hapa papo hapo pale pale
KU-KU kwa huku huko kule kuku huku kuko huko kule kule
MU-MU mwa humu humo mle mumu humu mumo humo mle mle
 1. c) Jedwali la pili linaangazia virejeshi(-o, amba-, -enye, -enyewe), ote, o-ote, ingi, ingine n.k kulingana na ngeli mbalimbali.
NGELI KIREJESHI O-REJESHI (AMBA-) ENYE ENYEWE OTE O-OTE INGI INGINE
A-WA ye
o
ambaye
ambao
mwenye
wenye
mwenyewe
wenyewe
wote
wote
yeyote
wowote
mwingi
wengi
mwengine
wengine
KI-VI cho
vyo
ambacho
ambavyo
chenye
vyenye
chenyewe
vyenyewe
chote
vyote
chochote
vyovyote
kingi
vingi
kingine
vingine
LI-YA lo
yo
ambalo
ambayo
lenye
yenye
lenyewe
yenyewe
lote
yote
lolote
yoyote
jingi
mengi
jingine
mengine
U-I o
yo
ambao
ambayo
wenye
yenye
wenyewe
yenyewe
wote
yote
wowote
yoyote
mwingi
mingi
mwingine
mingine
U-ZI o
zo
ambao
ambazo
wenye
zenye
wenyewe
zenyewe
wote
zote
wowote
zozote
mwingi
nyingi
mwingine
nyingine
I-ZI yo
zo
ambayo
ambazo
yenye
zenye
yenyewe
zenyewe
yote
zote
yoyote
zozote
nyingi
nyingi
nyingine
nyingine
U-YA o
yo
ambao
ambayo
wenye
yenye
wenyewe
yenyewe
wote
yote
wowote
yoyote
mwingi
mengi
mwingine
mengine
YA-YA yo ambayo yenye yenyewe yote yoyote mengi mengine
I-I yo ambayo yenye yenyewe yote yoyote nyingi nyingine
U-U o ambao wenye wenyewe wote wowote mwingi mwingine
PA-PA po ambapo penye penyewe pote popote pengine
KU-KU ko ambako kwenye kwenyewe kote kokote kwingi kwengine
MU- mo ambamo mwenye mwenyewe mote momote mengine

Nomino (N)

NOMINO
Kitengo Aina za Maneno
Kiingereza Nouns
NAVIGATION
Viwakilishi
 

Nomino ni maneno ambayo ni majinaya watu, vitu, hali n.k. Kuna nomino za kawaida na nomino za kipekee miongoni mwa aina nyingine za nomino.

Yaloyomo

 • Aina za Nomino
  • Nomino za Kawaida
  • Nomino za Kipekee
  • Nomino za Jamii
  • Nomino za Wingi
  • Nomino za Vitenzi Jina
  • Nomino za Dhahania

Aina za Nomino

Kunazo aina mbalimbali za nomino katika lugha ya Kiswahili.

 • Nomino za Kipekee
 • Nomino za Kawaida
 • Nomino za Jamii/Makundi
 • Nomino za Kitenzi-Jina
 • Nomino za Dhahania
 • Nomino za Wingi

Nomino za Kawaida

Haya ni majina ya kawaida yanayoweza kutumiwa kurejelea vitu mbalimbali, watu, wanyama, mahali na kadhalika. Nomino hizi zinaweza kuwa katika umoja au wingi kulingana na ngeli yake.

k.m: nyumba, mbuzi, daktari, soko, kalamu, jua

Nomino za Kipekee

Haya ni majina maalum ya watu, mahali, bidhaa, kampuni, na kadhalika. Herufi ya kwanza ya nomino hizi huwa ni herufi kubwa. Nomino za kipekee haziwezi kubadilika, na hivyo basi hazina wingi.

k.m: Tanzania, Nairobi, Anita, Gafkosoft, Athi, Kimbo,

Nomino za Jamii

Nomino za jamii hurejelea kundi la vitu au wanyama, kwa ujumla. Aghalabu vitu vinavyorejelewa hutokea kwa makundi ya vitu mbili au zaidi. Nomino hizi hutumia wingi tu tunaporejelea makundi zaidi ya moja.

k.m: jozi la viatu, umati wa watu, bustani la maua, bunga la wanyama

Nomino za Wingi

Nomino hizi hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haziwezi kuhesabiwa. Vitu kama hivyo hutumia aina nyingine ya vipimo ili kurejelea kiasi chake. Nomino za wingi hazina umoja.

k.m: maji, maziwa, changarawe, pesa, nywele

Nomino za Vitenzi Jina

Nomino hizi huundwa kutokana na vitenzi kwa kuongeza kiungo KU mwanzoni mwa mzizi wa kitenzi.

k.m: kulima, kuongoza, kucheza, kulala

Nomino za Dhahania

Haya ni majina ya hali au vitu ambavyo havionekani wale haviwezi kushikika.

k.m: upendo, furaha, imani, elimu, ndoto, mawazo, maisha, usingizi.

Nyakati za Kiswahili

NYAKATI ZA KISWAHILI
Kitengo Sarufi
NAVIGATION
Kukanusha
Umoja na Wingi
Wakati Uliopita => LI
Hutumia kiambishi ‘LI’ na hurejelea kitendo kilichokamilika muda mrefu uliopita.
Ifuatayo ni mifano katika sentensi.
k.m: nilikwenda, tulilima, walikufukuza
1 Mama ataenda sokoni Mama alienda sokoni
2 Ndoto hiyo imenisumbua usiku kucha Ndoto hiyo ilinisumbua usiku kucha
Wakati Timilifu (Uliopita Muda Mfupi) => ME
Hutumia kiambishi ‘ME’ na hurejelea kitendo ambacho kimekamilika muda usio mrefu.
k.m: amepona, nimewachagua, zimechanganyika
1 Tutauona wema wake Bwana Mungu. Tumeuona wema wake Mungu wetu.
2 Dada yake alipagawa Dada yake amepagawa
Wakati Uliopo => NA
Hutumia kiambishi ‘NA’ kurejelea jambo linalotendeka sasa hivi.
k.m: anaugua, yanametameta, unatisha
1 Nilikupenda kwa yale uliyonitendea Ninakupenda kwa yale unayonitendea.
2 Nyumba zote zilibomolewa mwaka jana Nyumba zote zinabomelewa mwaka huu
Wakati Ujao => TA
Huchukua kiambishi ‘TA’ na hurejelea kitendo ambacho bado hakijafanyika lakini kinatarajiwa kufanyika..
k.m: atakupa, kitajulikana, utapokelewa
1 Mtoto amelifunga dirisha lililokuwa likiingiza hewa Mtoto atalifunga dirisha litakalokuwa likiingiza hewa.
2 Je, ulienda sokoni juzi? Je, utaenda sokoni kesho kutwa?
Wakati wa Mazoea => HU
Hutumia kiambishi ‘HU’ na hurejelea kitendo ambacho hufanyika mara kwa mara au kila siku n.k.
k.m: hutembea, husoma, huzilinda
1 Dkt. Matumbo alitibu wagonjwa. Dkt. Matumbo hutibu wagonjwa.
2 Mchungwa ule ulizaa machungwa matamu. Mchungwa ule huzaa machungwa matamu.
Wakati Usiodhihirika => A
Hutumia kiambishi cha ngeli au nafsi pamoja na kiungo ‘A’ kurejelea kitendo kinachoendelea kutendeka katika wakati usiodhihirika.
k.m: achukua, zapepea, twaangamia
1 Baba alitusubiri nyumbani. Baba atusubiri nyumbani.
2 Vitabu vyako vyote vimechomeka Vitabu vyako vyote vyachomeka
Wakati Timilifu Usiodhihirika => KA
Hutumia kiungo ‘KA’ kurejelea kitendo ambacho kinakamilika katika wakati usiojulika. Pia hutumika kurejelea kitendo kifanyika baada ya kingine. Hutumiwa katika masimulizi.
k.m: ikawalemea, tukazichukua, likampendeza
1 Latifa aliangalia mvunguni na kumwona nyoka.. Latifa akaangalia juu akamwona nyoka.
2 Aliwanyeshea mana wakiwa jangwani. Akawanyeshea mana wakiwa jangwani
Msamiati wa Nyakati na Saa

NYAKATI NA SAA
Kitengo Msamiati
MASOMO
Vitate, Vitawe, Visawe
Msamiati wa Majina ya Ukoo

Yaliyomo

 • Siku za Juma
  • Siku Zikilinganishwa na Leo
  • Miezi ya Mwaka
  • Masaa ya Siku
  • Kusoma Saa

Siku za Juma

Juma au wiki moja huwa na siku saba. Yafuatayo ni majina ya siku za juma. Kwa kuwa asili yake ni Kiarabu na Kiislamu, Jumamosi ndiyo siku ya kwanza ya wiki; nayo Ijumaa ndiyo siku ya saba.

SIKU YA JUMA KIINGEREZA
Jumatatu Monday
Jumanne Tuesday
Jumatano Wednesday
Alhamisi Thursday
Ijumaa Friday
Jumamosi Saturday
Jumapili Sunday

Siku Zikilinganishwa na Leo

Haya ni majina tunayotumia kurejelea siku zinazokaribiana na leo.

SIKU MAELEZO MFANO
juzi siku iliyotangulia jana ikiwa leo ni Jumatano, juzi ilikuwa Jumatatu.
jana siku iliyotangulia leo ikiwa leo ni Jumatano, jana ilikuwa Jumanne.
leo siku ambayo tuko sasa hivi
kesho siku inayofuata Ikiwa leo ni Jumatano, kesho itakuwa Alhamisi.
kesho kutwa siku itakayokuja baada ya kesho ikiwa leo ni Jumatano, kesho kutwa itakuwa Ijumaa.
mtondogoo siku itakayokuja baada ya kesho kesho kutwa. siku tatu kutoka leo ikiwa leo ni Jumatano, kesho kutwa itakuwa Jumamosi.

Miezi ya Mwaka

Jedwali lifuatalo linaonyesha majina ya miezi katika mwaka, na idadi ya siku katika kila mwezi.

# JINA MWEZI WA: SIKU
1 Januari kwanza 31
2 Februari pili 28
3 Machi tatu 31
4 Aprili nne 30
5 Mei tano 31
6 Juni sita 30
7 Julai saba 31
8 Agosti nane 31
9 Septemba tisa 30
10 Oktoba kumi 31
11 Novemba kumi na moja 30
12 Disemba kumi na mbili 31

Masaa ya Siku

Yafuatayo ni mafungu ya masaa au nyakati mbalimbali za siku.

WAKATI MAELEZO MASAA
mchana wakati wa siku wenye jua. kutoka saa kumi na mbili asubuhi hadi saa moja jioni hivi 6am – 7pm
usiku wakati wa siku usiokuwa na jua. kutoka saa moja jioni hadi saa kumi na mbili siku inayofuatia 7pm – 6am
alfajiri kati ya saa tisa na saa kumi na moja asubuhi 3am – 5am
macheo saa kumi na moja hadi saa kumi na mbili hivi jua linapochomoza 3am – 5am
asubuhi kutoka saa kumi na mbili hadi saa sita za mchana 6am – 12pm
adhuhuri saa sita za mchana hadi saa nane 12pm – 2pm
alasiri saa nane hadi saa kumi na moja hivi 2pm – 5pm
jioni saa kumi na moja hadi saa moja jioni 5pm – 6pm
machweo/magharibi saa kumi na mbili hadi saa moja jioni; jua linapotua 6pm – 7pm
usiku mchanga kati ya saa moja jioni na saa sita za usiku 7pm – 12am
usiku wa manane kutoka saa sita za usiku hadi alfajiri 12am – 3am

Kusoma Saa

Tunaweza kusoma saa tukitumia:

Mfumo wa Kiswahili

katika mfumo wa Kiswahili/Kibantu, siku huanza saa kumi na mbili asubuhi. Kwa hivyo, saa moja ya asubuhi inakuwa ndiyo saa ya kwanza(1) ya siku. Mfano:

 1. 5:00 asubuhi ⇒ saa tano kamili asubuhi
 2. 9:15 usiku ⇒ saa tisa na robo usiku.
 3. 11:30 jioni ⇒ saa kumi na moja unusu jioni
 4. 2:45 alasiri ⇒ saa tatu kasorobo au saa mbili na dakika arubaini na tano alasiri
 5. 10:23 alfajiri ⇒ saa kumi na dakika ishirini na tatu alfajiri

Mfumo wa Kimataifa/Kiingereza

Huu ndio mfumo unaokubalika kirasmi katika mataifa na lugha mbalimbali. Kulingana na mfumo huu, siku huanza saa sita za usiku. Hivyo basi, saa saba ya usiku inakuwa saa ya kwanza(1) ya siku.

Mfano:

 1. 6:00 macheo ⇒ saa kumi na mbili asubuhi kamili macheo
 2. 12:15 adhuhuri ⇒ saa sita na robo adhuhuri.
 3. 3:30 alasiri ⇒ saa tisa na nusu alasiri
 4. 6:45 jioni ⇒ saa moja kasorobo au saa kumi na mbili na dakika arubaini na tano jioni
 5. 11:08 usiku ⇒ saa tano na dakika nane usiku

 

 

 

 

 

 

 

 • MSAMIATI
 • Vitate, Vitawe, Visawe
 • Tarakimu
 • Akisami
 • Nyakati na Saa
 • Majina ya Ukoo
 • Mapambo
 • Malipo
 • Walemavu
 • Kazi Mbalimbali

Nyimbo Katika Fasihi Simulizi

NYIMBO
Utanzu wa Fasihi Simulizi
Kiingereza Songs
TANZU ZA FASIHI
Hadithi / Ngano
Maigizo
MBINU ZA SANAA
Upeo wa Chini
Tanakali

Nyimbo ni aina ya sanaa katika fasihi ambayo hutumia lugha teule, sauti na kiimbo maalum.

Aghalabu nyimbo hutumia ala za mziki kama vile ngoma. Nyimbo zinaweza kuimbwa na mtu mmoja au zaidi.

Wimbo hugawanywa katika beti na mishororo. Nyimbo nyingi huwa na kiitikio au mstari ambao hurudiwa rudiwa.

Yaliyomo

 • Sifa za Nyimbo
 • Umuhimu wa Nyimbo katika Fasihi Simulizi
 • Vipera/Aina za Nyimbo
  • Kulingana na Muundo:
  • Kulingana na Ujumbe/Maudhui:

Sifa za Nyimbo

 1. Hutumia kiimbo au sauti maalum
 2. Huweza kuendamana na ala za muziki
 3. Huimbwa na mtu mmoja au watu wengi; wakati mwingine nyimbo huimbwa kwa kupokezanwa.
 4. Hutumia lugha ya mkato
 5. Hurudiarudia (kukariri) maneno ili kusisitiza ujumbe katika wimbo

Umuhimu wa Nyimbo katika Fasihi Simulizi

 1. Kuburudisha
 2. Kuelimisha, kufunza, kuonya, kuelekeza
 3. Kuliwaza
 4. Kusifia kitu au mtu katika jamii
 5. Kuunganisha jamii
 6. Kudumisha/kuhifadhi tamaduni za jamii
 7. Kukuza talanta na sanaa katika jamii
 8. Hutumika katika mbinu nyingine za fasihi kama vile hadithi

Vipera/Aina za Nyimbo

Kulingana na Muundo:

 • Mashairi
 • Maghani

Kulingana na Ujumbe/Maudhui:

Nyimbo za Ndoa

Nyimbo za harusi huimbiwa bwana na bibi harusi kuwapongeza na kuwapa heko kwa kufunga ndoa yao. Aidha nyimbo hizi huwapa wawili hao mawaidha ya kutunza familia na watoto wao ili waishi pamoja.

Nyimbo za Jandoni/Tohara

huimbwa na vijana wanapopashwa tohara. Nyimbo hizi huonyesha ushujaa, na kuashiria kutoka kwamba anayetahiriwa amekuwa mtu mzima sasa.

Hodiya/Wawe

Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa na watu wanapofanya kazi ili kuwatia bidii wafanye kazi bila kuhisi machofu.

Kimai

Nyimbo za Mabaharia – Hizi ni nyimbo za wanabahari wanaposafiri baharini.

Nyimbo za Mazishi/Huzuni/Simanzi

Hizi ni nyimbo za kuliwaza na kuwapa pole walioachwa na marehemu. Nyimbo hizi huwapa matumaini waombolezaji.

Nyimbo za Kidini

Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa kumsifia Mungu, kuomba au kutoa mafunzo ya kidini.

Nyimbo za Kisiasa

Hizi ni nyimbo za kuwasifia viongozi wa kisiasa

Nyimbo za Kizalendo

Nyimbo za huonyesha uzalendo kwa kusifia taifa/nchi

Nyimbo za Mapenzi

Katika nyimbo za mapenzi, mwimbaji huimba kwa kumsifia mpenzi wake hasa kwa urembo na tabia zake.

Riwaya

RIWAYA
Utanzu wa Fasihi Fasihi Andishi
Kiingereza Novel
Mifano Kiu, Siku Njema, Mwisho wa Kosa
Angalia
 • Aina za Wahusika
 • Hadithi Fupi vs Riwaya
Tamthilia
Hadithi Fupi

Riwaya ni kazi ya fasihi andishi ambayo huwa ndefu na aghalabu riwaya moja hujaza kitabu kizima. Riwaya huwa na wahusika wengi na huangazia mawazo kadhaa. Aidha, riwaya hufanyika katika mazingira mbalimbali na aghalabu huchukua muda mrefu ikilinganishwa na hadithi fupi.

Yaliyomo

 • Aina za Riwaya
 • Mifano ya Riwaya

Aina za Riwaya

Kunazo aina kadhaa za Riwaya katika Fasihi Andishi:

 • Riwaya sahili – visa vyake husimuliwa moja kwa moja na huwa rahisi kueleweka
 • Riwaya changamano – hii ni riwaya ambayo huhitaji kusomwa kwa makini ili kueleweka. Aghalabu huwa na maudhui mengi na wahusika wengi ambao wanachangia katika tatizo kuu katika riwaya hiyo. Hujengwa kwa taharuki ili kuwavutia hadhira kutazamia jinsi tatizo kuu litakavyotatuliwa. Hutumia mbinu za taharuki na visengere nyuma/mbele.
 • Riwaya ya kibarua – hutumia muundo wa barua kuwasilisha ujumbe wake.
 • Riwaya kiambo – huhusisha maswala ya kawaida katika jamii

Mifano ya Riwaya

 • Kidagaa kimemwozea
 • Siku Njema
 • Mwisho wa Kosa

Sajili Katika Isimu Jamii

Sajili – ni mukhtadha/rejista mbalimbali au mitindo maalum ya lugha katika mazingira/hali mbalimbali.

Kuna sajili anuwai za matumizi ya lugha katika jamii. Hapa tutazingatia mifano michache ya sajili mbali mbali.Kila sajili huwa na sifa mbalimbali zinazoitofautisha sajili hiyo na nyinginezo. Ili kubaini sifa za lugha katika sajili fulani, ni muhimu kuzingatia baadhi ya maswali yafuatayo:

 • ni mazungumzo baina ya nani na nani?
 • kuna uhusiano gani baina ya wanaozungumza?
 • yanapatikana wapi?
 • yanatumika katika hali gani?
 • yana umuhimu ama lengo gani
 • ni istilahi zipi istilahi (maneno maalum) zinazopatikana katika mazingira hayo?
 • umaizi wa lugha baina ya wazungumzaji ni wa kiwango gani?
 • ni mtindo gani wa lugha unaotumika?

Sajili ya Ajali

Hii ni lugha inayotumiwa katika ambalo ajali imetokea. Wahusika wanaweza kuwa majeruhi, polisi, walioshuhudia au wananchi wengine n.k

Sifa za lugha inayopatikana katika sajili hii

 1. Msamiati wa kipekee unaohusiana na ajali kama vile majeruhi, hudumanya kwanza, damu, mkasa.
 2. Hutumia lugha ya kudadisi dadisi ili kubaini chanzo cha ajali.
 3. Huwa na masimulizi – walio na habari kuhusu kisa hicho hueleza waliyoshuhudia
 4. Kutokana na hali ya msukosuko, lugha hii haina utaratibu – watu huwa katika hali ya hofu, kwa juhudi za kuwaokoa majeruhi.

Mfano wa Sajili ya Ajali

Mwanakijiji 1: Nimesikia twa! Kisha kishindo kikubwa sana (akihema hema) Nikaambia kuna mlipuko tukimbie.
Mwanakijiji 2: Lilio la muhimu ni kuyaokoa maisha ya majeruhi kwa kuwapa huduma ya kwanza.
Mwanakijiji 1: Tuondoeni miili ya waliofariki kwanza.
Mwanakijiji 2: hatuwezi kuishika miili iliyobanwa katika gari hadi polisi wafike. Na ndio hao wanaokuja!
Mwanakijiji 1: (akikimbia) Ndio hao! Acheni kuiba mafuta! Polisi wanakuja!
Polisi: Wakitawanya wananchi walioliparamia gari kuiba bidhaa mbali mbali.Liinueni hili gari! Wapi dereva?
Dereva: (ambaye amelala akihema kwa maumivu, damu ikichuruzika miguuni na mikononi) Nilisitishwa na ng’ombe waliokuwa wakivuka barabara. Nilijsribu kukwepa lakini usukani ukanishinda gari likapoteza mwelekeo…
Abiria: Alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana. Tukampigia kelele apunguze mwendo lakini hakutusikia. Matunda yake…
Mwanakijiji 2: Niliona gari likibingiria mara kadhaa mpaka likaingia humu mtaroni, ndiyo tukakimbia kuwaokoa.
Polisi: Nyamazeni! Achieni polisi kazi iliyobaki. Ikiwa kuna yeyote anayejuana na waathiriwa aandamane nasi.

Sajili ya Biashara

Lugha ya biashara huzungumzwa na wauzaji na wanunuzi katika sehemu za kibiashara. Inapaswa ikumbukwe kwamba lugha hii inaweza kubadilika kidogo kulingana na mazingira. Kwa mfano, katika mikutano ya kibiashara, lugha rasmi hutumiwa ilihali katika soko, lugha ya mitaani inaweza kutumika.

Sifa za Lugha ya Biashara

 1. Hutumia msamiati wa kibiashara kama vile:
  • Fedha
  • Faida
  • Hasara
  • Bei
  • Bidhaa
 2. Hutumia misimu ili kuwavutia wanunuzi
 3. Ni lugha yenye malumbano hasa watu wanapojadiliana kuhusu bei
 4. Ni lugha legevu – haizingatii kanuni za lugha.
 5. Huchanganya ndimi kwa kuingiza maneno ya lugha za kigeni
 6. Ni yenye heshima na unyenyekevu kwa wanunuaji
 7. Msamiati katika lugha ya Kibiashara

Mfano wa Sajili ya Biashara

Mtu X: Tatu kwa mia! Tatu kwa mia! Leo ni bei ya hasara!
Mtu Y: Unauza hii briefcase kwa pesa ngapi?
Mtu X: Hiyo ni seventy bob mtu wangu
Mtu Y: Huwezi kunipunguzia. Niuzie hamsini hivi.
Mtu X: Haiwezekani mtu wangu. NItapata hasara nikiuza hivyo. Ongeza mkwaja, mama.
Mtu Y: Basi hamsini na tano.
Mtu X: Tafadhali ongeza kitu kidogo. Unataka nikule hasara leo? Fikisha sitini na tano.
Mtu Y: Basi sitanunua hii. Sina pesa hizo zote. Unajua uchumi ni mbaya siku hizi.
Mtu X: Tafadhali mtu wangu. Huu mkoba ni mzuri sana. Umetoka Germany. Angalia. Unaweka pesa hapa, kitambulisho hapa halafu unafunga hivi. Hauwezi kupoteza chochote ukiwa na mkoba huu. Angalia wewe mwenyewe. Hakuna mahali pengine utaweza kununua mkoba huu kwa bei ghali kama hii.
Mtu Y: Nimekwambia sina hizo pesa. Nitanunua baadaye ukipunguza bei.
Mtu X: Lete sixty bob. Lakini utakuwa umeniumiza. Nakufanyia hivyo kwa kuwa wewe ni customer poa.
Mtu Y: Sawa basi nitanunua. Shika sixty bob.
Mtu X: Asante Customer. Mungu akubariki. (akimfungia) Hey! Tatu kwa mia. Bei ya hasara! Tatu kwa mia!

Sajili ya Bungeni

Hii ni lugha inayozungumzwa wakati wa kikao cha bunge. Sajili hii ni tofauti na na sajili ya siasa, ambayo huhusisha wanasiasa wakipiga kampeni.

Sifa za Lugha ya Bungeni

 1. Ni lugha yenye ushawishi – wabunge hutumia vishawishi ili kuwahimiza wenzao waunge ama kupinga msalaba
 2. Ni lugha ya mjadala yenye waungao na wapingao.
 3. Ni lugha yenye heshima na nidhamu. Maneno ya heshima kama mheshimiwa, tafadhali na samahani hutumika sana.
 4. Hutumia maneno maalum yanayopatikana katika mazingira ya bunge kama vile kikao, mswaada, kuunga mkono, kujadili, kupitisha, n.k.
 5. Lugha ya bungeni ni rasmi na sanifu.
 6. Hulenga maswala mbalimbali ya kisiasa na maendeleo katika taifa.
 7. Huwa na maelezo kamilifu
 8. Ni lugha yenye maswali na majibu miongoni mwa wabunge.

Mfano wa sajili ya Bungeni

Spika: Waheshimiwa, muda unayoyoma. Nawaomba mfanye mazungumzo yenu sauti ya chini tumsikize huyu. Endelea mheshimiwa.
Mbunge 1: Asante Bwana spika. Hii siyo mara ya kwanza ya kuuwasilisha mswaada huu hapa. Kila mbunge anayethamini raia wa taifa hili ni lazima auunge mkono mswada huu. Katika kikao kilichotangulia, mliupinga mkidai kwamba hauna heshima kwa rais. Leo tumefanya ukarabati wote mliotaka. Hamna budi kuuunga mkono. Bwana spika….
Spika: Muda wako umekwisha tafadhali keti. Wabunge wataamua hatima ya mswada huu ikiwa utapitishwa kama sheria. Lakini kumbukeni uamuzi wa mwisho ni wa rais.

Sajili ya Hospitalini

Sifa za Lugha ya Hospitalini

 1. Hutumia msamiati wa hospitalini kama vile
  • dawa
  • magonjwa
  • Daktari
  • Wadi
  • Mgonjwa
  • Dawa
  • Kipimo
 2. Ni lugha yenye upole na heshima
 3. Huwa na maswali mengi hasa daktari anapotaka kutambua kiini cha ugonjwa unaomhadhiri mgonjwa wake
 4. Ni lugha yenye hofu na huzuni

Mfano wa Sajili ya Hospitalini

Daktari: Ulianza kuumwa hivi lini?
Mgonjwa: Kichwa kilianza kuniuma jana jioni baada ya chajio. Nilipoamka asubuhi nikatambua kwamba hata tumbo lilikuwa likiuma pia.
Daktari: Ulipoanza kuumwa na mwili mzima, ulichukua hatua gani? Hukunywa dawa yoyote?
Mgonjwa: Nilichukua tembe zilizokuwa zimepatiwa kakangu miaka mitano iliyopita alipokuwa akiumwa na malaria.
Daktari: Kila ugonjwa unahitaji matibabu mbalimbali. Tembe za malaria haziwezi kutumika kutibu maumivu ya kichwa na tumbo. Pia ni hatari kutumia dawa ambazo zimepitwa na wakati. Zinaweza kukuletea madhara zaidi.
Mgonjwa: (akikohoa) Sijui kama una tembe za kifua pia. Hii baridi inaniletea homa mbaya.
Daktari: Hatuwezi kukupatia dawa kabla ya kutambua ugonjwa ulio nao. Itabidi tupime joto lako, damu na pia mate yako ili kupata tatizo linalokusumbua. Kisha tutakupatia dawa. Je, una umri wa miaka mingapi?
Mgonjwa: Nikichukua hizo dawa nitapona?
Daktari: Matokeo hubadilika kutoka kwa mgonjwa mmoja hadi mwengine. Inaweza kuchukua muda. Huenda ukalazwa kwenye wadi kwa siku mbili tatu hivi. Umri wako, mama?

Sajili ya Kidini

Katika sajili ya kidini tunaangazia lugha inayozungumzwa na waumini/washiriki wa imani fulani wakati wa ibada, sala, katika nyumba takatifu au mahali popote pale ambapo wanazungumzia mambo yanayorejelea imani au Mwenyezi Mungu.

Sifa za Lugha ya Kidini

 1. Hutumia msamiati wa kidini kama vile
  • Bibilia
  • maombi
  • mbinguni
  • jehanamu
  • Madhabahu
  • Paradiso
  • Mbinguni
  • Mwenyezi Mungu
  • Mwokozi
 2. Ni lugha inayonukuu sana hasa wazungumzaji wanaporejelea Kitabu kitakatifu
 3. Lugha yenye heshima, upole na unyenyekevu
 4. Lugha sanifu
 5. Ni lugha iliyojaa ahadi nyingi kwa wanaoandamana na mafunzo ya kidini na vitisho kwa wanaoenda kinyume na mafundisho
 6. Huwa imejaa matumaini
 7. Ni lugha yenye kutoa maneno ya sifa, kumtukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu

Mfano wa Sajili ya Kidini

Boriti: Bwana asifiwe Bi…
Bi Rangile: Amina, mchungaji. Watoto wanaendeleaje?
Boriti: Karita hana neno. Mwenyezi Mungu ametunyeshea rehema na neema zake. Je, wajukuu wako wa hali gani?
Bi Rangile: Wanaendelea vizuri isipokuwa hawataendelea na masomo. Sijui nilimfanyia Mungu dhambi gani.
Boriti: Nasikitika sana kusikia hivyo. Mungu atawalinda mayatima hao. Yeye ndiye baba wa mayatima. Mungu ni mwenye huruma.
Bi Rangile: Sijui hayo, mchungaji. Hata sijui maana ya kuishi hapa duniani. Kila siku ni matatizo.
Boriti: Usife moyo. Mungu anasema katika kitabu cha Yohana 14:18, “Sitawaacha nyinyi kama mayatima…” Kwa hivyo, ukiwa na imani, Mungu atakuonekania.
Bi Rangile: Basi niombee mchungaji ili Saumu na Neema wapate karo ya kurudi shuleni.
Boriti: Funga macho tusali. Ewe Rabuka uliyejaa neema na baraka tele. Tunakushukuru na kulitukuza Jina lako takatifu kwa baraka zako za ajabu. Tunajua kwamba wewe ndiye Mungu uliyewatoa wana wa Israeli kutoka Misri. Sisi wenye dhambi tunakuja mbele yako tukiomba ukafanya miujiza katika nyumba hii ya Bi Rangile……
Wote: Amina.

Sajili ya Kisayansi

Sifa za Lugha ya Kisayansi

 1. Hutumia msamiati wa kipekee unaoambatana na taaluma inayorejelewa.
 2. Huwa na maelezo kwa ukamilifu.
 3. Huwa na mpangilio maalum na maendelezo ya hoja na ujumbe.
 4. Huchanganya ndimi na kutumia maneno ya kisayansi au lugha mbalimbali.
 5. Hutumia lugha sanifu.
 6. Ni lugha yenye udadisi mwingi (wakati wa kufanya utafiti)

Mfano wa Lugha ya Kisayansi

Kwa sababu zisizoweza kuepukika, kikundi chetu hakitamaliza utafiti ulioratibiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi ujao. Hii ni kwa sababu ya changamoto kadhaa ambazo tumekutana nazo. Kwanza, viluwiluwi, ambao ndio tunaotafiti wamekuwa haba sana wakati huu wa ukame. Pili, kutokana na kufungwa kwa maabara ya kisayansi katika taasisi hii, ni muhali kufanya majaribio yoyote ya kazi yetu. Tatu, kumekuwa na pingamizi kubwa kutoka kwa baadhi ya wanakijiji kwamba kukusanya viluwiluwi kunawatia hofu. Aidha, tume yetu imepungukiwa na fedha baada ya serikali kusitisha kudhamini utafiti huu.

Baada ya kujadiliana kwa vikao tatu mfululizo, tume yetu inapendekeza haya: Muda wa kufanya utafiti uongezewe kwa kipindi cha miezi sita; serikali kupitia kwa taasisi hii ifadhili wachunguzi. Wananchi wahamasishwe kuhusu umuhimu wa kuwafanyia viwavi utafiti na maabara ya utafiti ikaraatiwe haraka iwezekanayo.

Sauti za Kiswahili

SAUTI ZA KISWAHILI
Kitengo Muundo wa Neno
Aina Kuu
 • Konsonanti
 • Irabu
NAVIGATION
Mofimu
Shadda na Kiimbo

a, b, ch, d, e, f, g, h, i, k, l, m, n, o, p, r, s, t, u, v, w, y, z

Kuna aina mbili za Sauti katika lugha ya Kiswahili:

 1. Irabu
 2. Konsonanti

Irabu (Vokali)

a, e, i, o, u

Irabu zinapotamkwa, hewa haizuiliwi katika ala za matamshi.
Jedwali lifuatalo litakuonyesha jinsi ya kubainisha vokali kulingana na sehemu ya ulimi inayoachilia hewa, na jinsi midomo inavyobadilika

Irabu Sehemu ya Ulimi Midomo
e,i Mbele Midomo imetandazwa
a Katikati; ulimi huinuka na kutandaza Midomo imetandazwa
o,u Nyuma Midomo imevirigwa

Konsonanti

b, ch, d, f, g, h, j, k, l, m, n, p, r, s, t, v,w, y, z

Konsontanti zinapotamkwa, hewa huzuiliwa katika ala za matamshi ( ulimi na midomo).
Kuna aina mbili kuu za sauti za konsonanti:

 1. Sauti Ghuna => konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa hutikisa nyuzi za sauti
 2. Sauti Sighuna => konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa haitikisi nyuzi za sauti

Jedwali lifuatalo litakuonyesha aina za konsonanti kulingana na mahali zinapotamkiwa na sauti (ghuna au sighuna)

Midomo Midomo + Meno Meno + Ulimi Ufizi Kaakaa + ufizi Kaakaa gumu Kaakaa Laini Koo Aina ya Sauti
Vipasuo p
d
t
d
j k
g
sighuna
ghuna
Vikwamizo / Vikwaruzo f
v
th
dh
s
z
sh kh
gh
h sighuna
ghuna
Kipasuo – kwamizo ch Sighuna
Nazali / Ving’ong’o m n ny ng’ Ghuna
Kitambaza l Ghuna
Kimadende r Ghuna
Viyeyusho / Nusu Irabu y w Ghuna

Vipasuo ( p,b,k,g,t,d )

Hutamkwa kwa kukutanisha ala za kutamkia ili kufungilia hewa na kisha kuiachilia ghafla

 • Vipasuo sighuna (p, k, t ) – hutamkwa bila kutikisa nyuzi za sauti
 • Vipasuo ghuna (b, g, d ) – hutamkwa kwa kutikisa nyuzi za sauti

/p/ na /b/ hutamkwa kwa kukutanisha midomo katika meno:

 • /p/ – papa, pepea, pipi, popo, pua
 • /b/ – baba, bebea, bibi, bobo, bubu

/t/ na /d/ hutamkwa kwa kukutanisha ufizi na ncha ya ulimi

 • /t/ – taa, tetea, titi, toto, tua
 • /d/ dada, doa, dua

/k/ na /g/ hutamkwa kwa kukutanisha nyuma ya ulimi na kaakaa laini

 • /k/ – kaka, koko, kuku
 • /g/ – gae, gege, gogo, gugu

Vikwamizo ( d f,v,dh,th, s,z,sh,h,gh)

Pia huitwa Vikwaruzo Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kisha kuachilia hewa kupitia katika mwanya mwembamba

 • Vikwamizo sighuna (f,th,s,kh,h,sh) – hewa haitikisi nyuzi za sauti
 • Vikwamizo ghuna (v, dh,z,gh) – hewa hutikisa nyuzi za sauti

/f/ na /v/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa chini na wa juu na kuachilia hewa kidogo kupita

 • /f/ – faa, fee, fua
 • /v/ – vaa, vua

/s/ na /z/ hutamkwa kwa kukutanisha sehemu ya kati ya ulimi na kaakaa gumu

 • /s/ – sasa, sisi
 • /z/ – zaa, zeze, zizi, zuzu

/dh/ na /th/ hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na meno ya juu

 • /dh/ – dharau, dhani
 • /th/ – thubutu

/gh/ na /kh/ hutamkwa kwa kukutanisha kaakaa laini na kilimi

 • /dh/ – dharau, dhani
 • /th/ – thubutu

/h/ hutamkwa kwa kukutanisha kilimi na koo na kuachilia hewa kwa nguvu

 • /h/ – haha, hii, huu

Kipasuo-kwamizo: ( ch )

Pia huitwa kituo-kwamizo – Hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, na kuachilia hewa

 • /ch/ – chacha, chechea, choo

Ving’ong’o / Nazali ( m,n,ng’,ny )

Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kuzuia hewa kupitia kinywani; hewa hupitia puani.
/m/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa juu na wa chini, ili kuzuia pumzi kupita kinywani

 • /m/ – mama, umeme, mimi,

/n/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, ili hewa ipitie puani

 • /n/ – nana, nene, nini, nono, nunua

/ny/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa gumu

 • /ny/ – nyanya, nyenyea, nyinyi, nyoa, nyunyu

/ng’/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa laini

 • /ng’/ – ng’ang’a, ng’oa

Kitambaza ( l )

Hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na ufizi huku hewa ikipitia kwenye pande za ulimi bila kukwaruza ufizi

 • /l/ – lala, lea, lilia, lo! lulu

Kimadende ( r )

Hutamkwa kwa kupigapiga na kukwaruza ufizi haraka haraka kwa ncha ya ulimi.

 • /r/ – rai, rarua,

Viyeyusho ( y,w )

Pia huitwa nusu-irabu. Hutamkwa kwa utaratibu kwa kuleta ala za matamshi karibu sana lakini kuachilia hewa bila kuikwaruza.
/w/ hutamkwa midomo ikiwa wazi

 • /w/ – wawa, wewe,

/y/ hutamkiwa kwenye kaakaa gumu

 • /y/ – yaya, yeye,

Ala za Kutamkia

Hizi ni sehemu za mwili zinazotumika wakati wa kutamkia maneno:
Meno, Ulimi, Midomo, Pua, Chemba cha Pua, Ufizi, Kaakaa gumu, Kaakaa laini, Kimio , Chemba cha Kinywa, Ncha ya ulimi, Bapa la ulimi, Shina la Ulimi, Koromeo, Kidakatonge, Kongomeo, Nyuzi za Sauti, Koo, Njia ya Chakula

Sentensi za Kiswahili

AINA ZA SENTENSI
Kitengo Lugha
NAVIGATION
Muundo wa Sentensi
Virai na Vishazi

Sentensi ni kundi la neno moja au maneno zaidi yenye kiima na kiarifa na inayofuata kanuni za sarufi.

Yaliyomo

 • Aina za Sentensi
  • 1. Sentensi Sahili
  • 2. Sentensi Ambatano.
  • 3. Sentensi Changamano

Aina za Sentensi

 1. Sentensi Sahili

Hizi ni sentensi zenye kishazi kimoja na huwakilisha wazo moja tu.

 1. Sentensi sahili kutokana na kikundi tenzi pekee:
  1. Ninasoma => KT(T)
  2. Hajakuandikia barua => KT(T + N)
  3. Tulimwona nyoka mkubwa =>KT(T + N + V)
  4. Alikimbia haraka sana => KT(T + E + E)

Kikundi Nomino + Kikundi Tenzi

  1. Sakina anaimba. => KN(N) + KT(T)
  2. Latifa na Kanita wamejipamba vizuri. => KN(N + U + N) + KT(T + E)
  3. Jua kali liliwaka mchana kutwa. => KN(N + V) + KT(T + E + E)
  4. Runinga ya Bwana Kazito imeharibika tena. => KN (N + V + N + N) + KT (T + E)
 1. Sentensi Ambatano.

Sentensi ambatano ni sentensi zenye zaidi ya kishazi huru kimoja na huwakilisha mawazo mawili au zaidi. Aghalabu sentensi hizi hutumia viunganishi(U) au alama za uakifishaji kama vile kituo(,) na nukta-nusu (;) ili kubainisha wazo moja toka nyingine.

 1. Kuunganisha Sentensi Mbili:
  1. Chesi alisoma kwa bidii. Chesi alianguka mtihani. =>Ingawa alisoma kwa bidii, Chesi alianguka mtihani.
  2. Dadangu amerudi nyumbani. Dadangu amelala. =>Dadangu amefika nyumbani na kulala.
 2. Mifano mingine:
  1. Tulifika, tukaona, tukapiga na tukatawala.
  2. Leo inaonekana Karimi amejipamba akapambika.
 1. Sentensi Changamano

Hizi ni sentensi zinazoundwa kwa kuunganisha kishazi huru pamoja na kishazi tegemezi au sentensi mbili kwa kutumia o-rejeshi ili kuleta zaidi ya wazo moja.

 1. Kuunganisha Sentensi:
  1. Juma amenilitelea kitabu. Nilikuwa nimetafuta kitabu hicho kwa muda mrefu. => Juma ameniletea kitabu ambacho nilikuwa nimekitafuta kwa muda mrefu.
  2. Yeye ni mwizi. Alipigwa jana jioni. => Yeye ndiye mwizi aliyepigwa jana jioni.
 2. Mifano Zaidi:
  1. Nimemuona yule ninayemtafuta na neema zake.
  2. Ndoto zinazotisha ni za kishetani.

Tanbihi: Ili kutofautisha sentensi ambatano na changamano kwa urahisi, sentensi changamano hutumia o-rejeshi (k.m ambacho, ambaye, niliye- , nililo- n.k.

Shadda na Kiimbo

SHADDA NA KIIMBO
Kitengo Muundo wa Neno
KIINGEREZA
Shadda Stress
Kiimbo Intonation
NAVIGATION
Sauti za Kiswahili
Uainishaji

Shada(Shadda) na Kiimbo ni namna ya kutamka neno au fungu la maneno kwa namna tofauti kuleta maana mbalimbali.

Shadda / Shada – (Stress)

Shadda ni mkazo wa silabi. Maneno ya Kiswahili huwa na silabi moja ambayo hutamkwa kwa nguvu zaidi kuliko silabi nyingine. Unapotamka silabi iliyotiwa mkazo (shada), sauti hupandishwa juu kiasi.

Maneno mengi ya Kiswahili, hasa yale yenye asili ya Kibantu hutia mkazo katika silabi ya pili kutoka mwisho.

Kwa mfano:ma’ma, sandu’ku, kita’bu, tulikoto’ka, buruda’ni, baraba’ra (njia)

Baadhi ya maneno yenye asili ya kigeni, huwa na shada katika silabi nyingine.

Kwa mfano:bara’bara (sawa sawa), mukhta’sari,

Kiimbo – (Intonation)

Kiimbo ni sauti maalum inayojitokeza unapotamka maneno fulani. Kiimbo husaidia kuleta maana kamili ya sentensi iliyokusudiwa. Kwa kutamka sentensi kwa sauti fulani ‘ya kiwimbo’, tunaweza kubainisha kauli ya kawaida, swali, hisia n.k.

Sentensi au maneno yanapotamkwa kwa viimbo mbalimbali, hutoa dhana tofauti. Katika uandishi, Viimbo husaidiwa na alama za uakifishaji ili kumwelekeza msomaji asome kwa kiimbo kilichokusudiwa.

 1. a) Kuulizia Swali (?)

Tunainua sauti tunapouliza swali ili kulitofautisha na sentensi ya kawaida.
k.m Ulisoma kitabu nilichokupatia?

 1. b) Kuonyesha Hisia (!)

Tunapotoa hisia, aghalabu kiimbo huenda juu.
k.m Ajabu!

 1. c) Kutoa Kauli (.)

Tunapotoa kauli (sentensi ya kawaida), aghalabu sauti huenda chini katika neno au silabi ya mwisho. Hata hivyo, sauti inaweza kubadilika kulingana na neno linalotiliwa mkazo katika sentensi.

Tamathali za Usemi

TAMATHALI ZA USEMI
Aina
 • Mbinu/Fani za Lugha
 • Mbinu za Sanaa
Kiingereza Figures of Speech
Ushairi
Fasihi Simulizi

Tamathali za Usemi ni matumizi ya maneno kwa namna fulani ili kuifanya lugha iwe ya kuvuitia na kuifanya kazi ya sanaa iwe ya kupendeza. Kuna aina mbili za tamathali za usemi:

 1. Mbinu au Fani za Lugha- Ni uteuzi wa maneno ili kuifanya lugha iwe ya kupendeza na kuvutia. Pia, Mapambo ya Lugha. Fani za Lugha zinaweza kutambulikana moja kwa moja bila kusoma kifungu kizima.
 2. Mbinu za Sanaa- Ni ubunifu wa kisanaa unaojitokeza baada ya kusoma au kusikiliza masimulizi. Angalau unahitaji kusoma sentensi kadhaa au hata hadithi nzima ili kutambua mbinu ya sanaa iliyotumika.

Yaliyomo

 • Mbinu za Lugha
 • Mbinu za Sanaa

Mbinu za Lugha

 • Tanakali za Sauti -Ni mbinu ya kutumia maneno yanayoiga sauti au hali fulani au namna kitendo kilivyofanyika. Milio.
 • Tashbihi -Hii ni mbinu ya lugha inayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha; ‘kama’, ‘mithili ya’, ‘sawa na’, ‘ja’. Tashbiha. Similes.
 • Istiara -Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kutumia kiungo ‘ni’ ama ‘kuwa’. Istiari. Sitiari. Imagery
 • Jazanda – Ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi.
 • Taashira -Ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika kumaanisha kitu kingine chenye uhusiano na kile kilichotumiwa. Symbolism
 • Taswira – Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji.
 • Tashihisi -Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai (sifa za kibinadamu). Uhuishaji. Personification.
 • Chuku -Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe fulani au kusifia kitu. Kutilia Chumvi. Hyperbole
 • Takriri -Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. Repetition
 • Tanakuzi-Tanakuzi ni mbinu ya kusisitiza ujumbe kwa kuambatanisha maneno ya kinyume au yanayokinzana. Ukinzani
 • Majazi – Majazi ni pale tabia za wahusika zinapoambatana na majina yao halisi.
 • Lakabu – Ni mbinu ya mhusika kupewa/kubadikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia/sifa zake.
 • Semi – Ni fungu la maneno linapotumika kutoa maana nyingine, badala ya ile ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha ukali wa maneno au kupamba lugha. Kuna aina mbili za semi:
  • Nahau – huwa na vitenzi
  • Misemo – haina vitenzi
 • Methali – Methali ni misemo ya hekima yenye maana iliyofumbwa. Mhusika, mwandishi wa fasihi anaweza kutumia methali kupitisha ujumbe.
 • Maswali ya Balagha -Tashititi au maswali ya balagha ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika ambayo hayahitaji jibu. Mubalagha. (Rhetorical questions)
 • Uzungumzi Nafsiya – Mhusika hujizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.
 • Ritifaa – Mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa (au asiyekuwepo) kana kwamba yuko pamoja nawe.
 • Utohozi – Kutohoa ni mbinu ya kuswahilisha maneno ya lugha nyingine, yatamkike kama ya Kiswahili.
 • Kuchanganya Ndimi – Kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili.
 • Kuhamisha Ndimi – Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu.

Mbinu za Sanaa

 • Kinaya – Kinaya ni mambo katika sanaa kuwa kinyume na matarajio ya hadhira. Irony
 • Kejeli -Kejeli ni mbinu ya sanaa inayotumia maneno kudharau au kukemea kitendo au mtu fulani.
 • Taharuki -Taharuki ni mbinu ya kusimulia au kuandika riwaya/hadithi kwa kufanya hadhira na/au wahusika wajawe na hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye; hamu ya kutaka kuendelea kusoma/kusikiliza. Baadhi ya hadithi huishia kwa taharuki na kuilazimisha hadhira yake ijikamilishie au ibaki ikijiuliza maswali. Suspense
 • Sadfa – Sadfa ni kugongana kwa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vilikuwa vimepangwa, japo havikuwa vimepangiwa. Coincidence
 • Kisengere Nyuma – Mwandishi ‘hurudi nyuma’ na kuanza kusimulia kisa kilichokuwa kimetendeka kabla ya alichokuwa akisimulia. Aidha, mwandishi hubadilisha wakati wa masimulizi na kuwa wakati wa kisa hicho. Hutumika sana kuonyesha mhusika anapokumbuka kitu, au kutupatia msingi wa jinsi mambo yalivyoanza. Mbinu Rejeshi. Flashback
 • Kisengere Mbele – Mwandishi anapobadilisha wakati na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni; au kutumia lugha isiyo moja kwa moja kutabiri yatakayojiri. Utabiri. Foreshadow
 • Njozi au Ndoto – Mwandishi hutumia ndoto kutabiri jambo litakalofanyika au kufumbua jambo lililokuwa limefumbwa.
 • Upeo wa Juu – Ni sehemu ya hadithi ambayo matukio yanafanyika kulingana na mapenzi ya hadhira au msomaji. Climax
 • Upeo wa Chini – Ni sehemu ya hadithi ambayo matukio yanafanyika kinyume na mapenzi ya hadhira au msomaji. Aghalabu upeo wa chini hutokea baada ya upeo wa juu. anti-climax
 • Nyimbo – Nyimbo na/au mashairi yanaweza kutumika katika hadithi kwa madhumuni mbalimbali.

Tamthilia

TAMTHILIA
Utanzu wa Fasihi Fasihi Andishi
Kiingereza Play
Mifano
 • Mstahiki Meya
 • Kifo Kisimani
 • Shamba la Wanyama
Angalia
 • Wahusika
 • Michezo ya Kuigiza
Hadithi Fupi
Riwaya

Tamthilia au tamthiliya ni sanaa ambayo huwasilisha mchezo wa kuigiza kwa njia ya maandishi. Majina ya wahusika huandikwa katika upande wa kushoto, kisha koloni, halafu hufuatiwa na maneno halisi yaliyotamkwa na mhusika huyo.

Yaliyomo

 • Aina za Tamthilia
 • Mifano ya Tamthilia

Aina za Tamthilia

Kunazo aina kadhaa za tamthilia katika fasihi andishi:

 1. Tamthilia Cheshi/Komedia – ni mchezo wa kuchekesha. Maudhui yake huundwa kwa lengo la kutumbuiza hadhira.
 2. Tamthilia Simanzi/Trejedia – ni mchezo uliojaa huzuni, mikasa, mikosi, visa vya kutisha na aghalabu baadhi ya wahusika wakuu hufa.
 3. Tamthilia Simanzi-Cheshi/Trejikomedia – ni mchezo wenye visa vya kuhuzunisha lakini pia unawasilisha kwa njia ya kuchekesha. Aghalabu wahusika hutumia kejeli kuchekesha hadhira ijapokuwa kuna shida fulani inayowakabili. Baadhi ya wahusika wakuu hukumbwa na mikasa.
  Mfano: Kifo Kisimani (na Kithaka Wa Mberia)
 4. Tamthilia Tatizo – ni mchezo wa kuigiza ambapo wahusika huwa na tatizo/shida kuu wanalotaka kulitatua. Tamthilia hii aghalabu hutumia mbinu ya taharuki ili kuwafanya hadhira wawe makini ili kuona jinsi tatizo hilo litakavyoishia.
 5. Tamthilia ya Domestiki Drama – ni mchezo unaoangazia maisha ya kawaida ya watu kama vile familia, urafiki, ndoa n.k
 6. Tamthilia ya Melodrama – ni mchezo ambao husisitiza sifa za wahusika kwa kuunda wahusika kuunda wahusika wenye sifa zilizopigiwa chuku na zisizobadilika. Tamthilia hizi huundwa kwa namna inayowafanya hadhira wawapende wahusika fulani na wawachukie wahusika wengine. Kwa mfano:
  • Shujaa ambaye hushinda kila mara
  • Wahusika wabaya ambao hubakia wabaya kutoka mwanzo hadi mwishi
  • Wahusika wazuri ambao hufanya vitendo vizuri kutoka mwanzo hadi mwisho
  • Wapenzi ambao hata wakitenganishwa bado watapendana
  • Aghalabu huishia kwa raha mustarehe

Mifano ya Tamthilia

 1. Kifo Kisimani
 2. Shamba la Wanyama
 3. Mstahiki Mey

 Tungo Fupi

TUNGO FUPI
Utanzu wa Fasihi Simulizi
Vipera vya Tungo Fupi
 • Methali
 • Vitendawili
 • Mafumbo
 • Semi (Nahau na Misemo)
 • Vitanza Ndimi na Vichezea Maneno
 • Lakabu
 • Misimu
Maigizo
Hadithi / Ngano

Tungo Fupi ni kipera cha Fasihi Simulizi kinachojumulisha sanaa simulizi zinazoundwa kwa maneno machache; sentensi moja au mbili hivi. Tungo Fupi nyingi huwa na sehemu mbili na aghalabu huhitaji kujibizana ambapo mtu mmoja hutoa pendekezo au swali; halafu mtu mwengine hutoa jawabu – k.m vitendawili na mafumbo. Baadhi ya tungo fupi husemwa na mtu mmoja tu kama vile methali.

Aghalabu vipera vyote vya tungo fupi hutumiwa katika kazi nyingine za fasihi ( na lugha kwa ujumla ) kama mapambo ya lugha.

Vipera vya Tungo Fupi

 1. Methali
  Methali ni tungo fupi za sentensi moja ambazo hutoa funzo fulani kwa njia ya mafumbo. Methali huwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza hutoa hoja nayo sehemu ya pili hutoa suluhisho. Methali hutumika kwa minajili ya kutoa funzo kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Methali nyingine huhitaji hekima ili kujua maana yake.
 2. Vitendawili
  Vitendawili ni tungo fupi ambazo huwa na swali fupi na jibu kwa makusudi ya kupima ufahamu wa hadhira kuhusu mazingira yake. Anayetoa kitendawili huulizia swali lake kwa kutoa maelezo mafupi yanayorejelea umbo la kitu hicho, sauti, harufu au kukifananisha na kitu kingine. Anayejibu huhitajika kufikiria haraka na kutoa jawabu ambalo huwa la neno moja au maneno mawili hivi. Vitendawili huwa na mianzo maalum kulingana na jamii yake.
 3. Mafumbo
  Mafumbo hutumika kuupima uwezo wa mtu kufikira na kufumbua swali ambalo huwa na maelezo marefu. Majibu ya mafumbo huhitaji maelezo na aghalabu hukusudia kujua jinsi mtu anavyoweza kutatua tatizo fulani ambalo linahitaji kufikiria sana.
 4. Vitanza Ndimi
  Vitanza ndimi huwa ni sentensi zinazotumia maneno yanayomkanganya msomaji katika matamshi. Vitanza ndimi huhitaji kutamkwa haraka haraka na kurudiwa rudiwa mara kadhaa kwa kusudi la kukuza uwezo wa kutamka.
 5. Vichezea Maneno
  Ni maneno yanayokaribiana kimatamshi au kimaana hutumika katika sentensi moja kama njia ya kuonyesha ukwasi wa lugha au kuburudisha. Pia hutumika kama vitanza ndimi.
 6. Misimu
  Misimu ni maneno ambayo huzuka miongoni mwa kundi fulani katika jamii na hueleweka tu miongoni mwa watu katika kundi hilo. Misimu hukua na kutoweka baada ya muda.
 7. Lakabu
  Lakabu ni majina yanayobandikwa watu kutokana na sifa zao, maumbile, hulka au mambo yanayowahusu. Lakabu pia ni mbinu ya sanaa.
 8. Semi (Nahau na Misemo)
  Semi ni mafungu ya maneno ambayo hutumika kuleta maana tofauti na maana halisi ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha maneno makali kwa kutumia maneno mengine. Aidha semi zinaweza kutumika tu kwa minajili ya kupamba lugha. Kuna aina mbili za semi: Nahau na misemo

Uainishaji wa Neno

UAINISHAJI WA MANENO
Kitengo Muundo wa Neno
NAVIGATION
Shadda na Kiimbo
Viambishi

Kuainisha ni kugawa neno katika viambishi vyake mbalimbali. Tunapoainisha neno, tunaonyesha mzizi wa neno pamoja na viambishi vyote vilivyofungamanishwa kuunda neno hilo.

Angalia:

 • Viambishi
 • Uchanganuzi wa Sentensi

Mifano:

Ainisha maneno yafuatayo:

 1. nitasoma → ni-ta-som-a

{ni → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja
ta → kiambishi kiwakilishi cha wakati ujao
som → shina la kitenzi cha kusoma
a → kiishio}

 1. walipozipata → wa-li-po-zi-pat-a

{wa → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili wingi
li → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopita
po → kiambishi kiwakilishi cha po ya wakati au cha ngeli ya mahali PO
zi → kiambishi kiwakilishi cha kitendwa, ngeli ya I-ZI wingi
pat → shina la kitenzi cha kupata
a → kiishio}

 1. vimeshikamana → vi-me-shik-aman-a

{vi → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya KI-VI wingi
me → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopita muda mfupi
shik → shina la kitenzi cha kupata
aman→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendamana
a → kiishio}

 1. mnayemkimbilia → m-na-ye-m-kimbi-li-a

{m → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili wingi
na → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopo
ye → kiambishi kirejeshi cha nafsi ya tatu
m→ kiambishi kiwakilishi cha mtendewa, nafsi ya tatu umoja
kimbi → mzizi wa kitenzi cha kukimbia
li → kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendea
a → kiishio}

 1. yakimwagika → ya-ki-mwag-ik-a

{ya → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya YA-YA
ki → kiambishi kiwakilishi cha KI-ya masharti au au cha KI-ya kuendelea
mwag → mzizi wa neno mwaga
ik→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendeka
a → kiishio}

 1. hawakukushibisha → ha-wa-ku-ku-shib-ish-a

{ha → kiambishi kiwakilishi cha kukanusha
wa → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya tatu wingi
ku → kiambishi kiwakilishi cha kukanusha wakati uliopita
ku → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili mtendewa
shib → mzizi wa kitenzi cha kushiba
ish→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendesha
a → kiishio}

 1. lililolililia → li-li-lo-li-li-li-a

{li → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya LI-YA umoja
li → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopita
lo → kiambishi kirejeshi cha ngeli ya LI-YA umoja
li→ kiambishi kiwakilishi cha mtendewa, ngeli ya LI-YA
li → shina la kitenzi cha kulia
li → kiambishi kiishio cha kauli ya kutendea
a → kiishio

Alama za Uakifishaji

ALAMA ZA UAKIFISHAJI
Kitengo Sarufi
NAVIGATION
NGE na NGALI
Viungo Mbalimbali

Kunazo alama kadhaa zinazotumika kuakifisha maneno na sentensi za Kiswahili.

Alama ya Kikomo au Kituo Kikuu(.)
1. Kuonyesha mwisho wa sentensi.
 1. Huu ndio mwisho wa sentensi hii.
 2. Kioo kimevunjika.
2. Katika kufupisha maneno
 1. U.N.O, K.B.C, Y.C.S
 2. Dkt. Maktaba, Bw. Msumari
3. Kuonyesha Saa
 1. Misa ilianza saa 4.30 za asubuhi.
 2. Hivi sasa ni saa 10.20.
4. Katika hesabu kuonyesha sehemu isiyo nzima
 1. Ukigawa tatu mara mbili, utapata 1.5
 2. Mtoto huyo ana uzani wa kilo 8.27
5. Kuonyesha senti katika pesa
 1. Bei yake ni shilingi 12.50.
 2. Karo ya shule mwaka huu ni 80,000.00
Alama ya Kituo, Kipumuo au Koma (,)
1. Kuorodhesha vitu zaidi ya mbili
 1. Nimenunua simu, saa, redio na viatu.
 2. Kina mama waliimba, wakapiga ngoma na kunegua viuno vyao.
2. Kugawanya mawazo katika sentensi.
 1. Baada ya sala za jioni, Mzee Makosa alitoka nje na kuwasha sigara yake.
 2. Nilipomwuliza kama alimjua binti yule, aliniangalia tu na kucheka
 3. Ingawa kitabu hiki ni kizito, sina budi kukibeba.
3. Kutoa maelezo zaidi.
 1. Shabiba, mmojawapo ya wanawake wajawazito, amejifungua mtoto wa kike.
 2. Shati hili, ingawa nalichukia, nitalivalia tu.
4. Katika tarakimu, kugawa elfu.
 1. Shilingi 209, 408, 000 ziliporwa na serikali.
 2. Dawa hiyo iliua takribani mbu 61, 247.
Alama ya Kinukuu (‘ na “)
1. Kunukuu usemi halisi
 1. “Ukitaka kufua dafu,” mama akamwambia mwanawe, “lazima utie bidii.”
 2. Alimtazama kisha akamwuliza, “Unadhani nimechanganyikiwa kama wewe?”
2. Kunukuu kichwa cha kazi ya sanaa k.v kitabu, wimbo, kipindi n.k
 1. Saumu na Neema ni wahusika katika riwaya “Hamu ya Sumu Tamu”.
 2. Rose Muhando ndiye aliyeimba “Mteule Uwe Macho”.
3. Kuonyesha maneno yasiyo ya Kiswahili unapochanganya ndimi katika sentensi
 1. Huyu ndiye mchezaji “number one”
 2. Amesema “keyboard” ya “computer” yake haifanyi kazi..
4. Kuonyesha maneno yanayowakilisha maana tofauti na maana yake ya kawaida au kinaya.
 1. Lesi alipoenda kwenye ‘maktaba’ alipata mimba.
 2. Rais wetu ‘mtukufu’ amewatisha mawaziri wake.
 3. Moto ulioteketeza shule hiyo ulitokana na kusudi la wanafunzi la ‘kumshtua’ mwalimu wao.
5. Kuonyesha herufi iliyoachwa nje au kufupisha maneno katika ushairi hasa kwa kusudi la kutosheleza idadi ya mizani
 1. ‘takufuata popote wendapo,
 2. ‘liapo ya mgambo, lazima kuna jambo
6. Katika maendelezo ya sauti ya ung’on’g’o (ng’)
 1. Ng’ombe wa Ng’ang’a wanang’ang’ania nini?
 2. King’ang’i anapenda kunung’unika ovyo ovyo.
Alama ya Kiulizi (?)
1. Kuulizia swali
 1. Je, utamtembelea lini?
 2. Ariana anaishi wapi?
2. Kuonyesha pengo lililoachwa wazi
 1. Ndama ni mwana wa ng’ombe ilhali ___?___ ni mtoto wa mbuzi.
 2. __?__ mpokee mke wako, __?__, siku ya leo umepata jiko.
Alama ya Hisi (!)
1. Kuonyesha hisia kama vile hasira, mshangao, furaha n.k
 1. Lo! Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.
 2. Pepo nyeusi! Shindwa! Chomeka! Kwenda kuzimu!
2. Kuigiza Tanakali za Sauti
 1. Amejikwaa sasa ameanguka pu!
 2. Moyo ulidunda ndu! ndu!
Alama ya Nukta-Mbili au Koloni (:)
1. Kutanguliza orodha
 1. Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wa wengi: wake kwa waume; wadogo kwa wakubwa; wazee kwa vijana.
 2. Kuna aina kadhaa za vivumishi: vivumishi vya sifa, vivumishi vya idadi, vivumishi viwakilishi na kadhalika
2. Kuelezea sababu au kuonyesha matokeo ya kitu.
 1. Saumu alipoingia chumbani alipigwa na butwaa: mamake alikuwa amekufa.
 2. Baba alinipatia zawadi nzuri sana: nilirukaruka kwa furaha.
3. Kuonyesha saa
 1. Wimbo huo unachukua dakika 4:45.
 2. Aliingia saa 5:15
4. Kunukuu ukurasa wa Bibilia
 1. Padre alisoma Luka 2:1-6
 2. Katika kitabu cha Mwanzo 5: 2-7, Bibilia inasema…
5. Kuonyesha maneno ya msemaji katika tamthilia au mchezo wa kuigiza
 1. Mzee Mwanyati: Unafikiria mimi ni nyanyako?
 2. Kadogo: (akitetemeka) Tafadhali naomba unisamehe.
6. Kuonyesha mada katika barua au kumbukumbu za mkutano
 1. KUH: Ombi Lako la Kujiuzulu.
 2. RE: Barua ya tarehe 3/2/1999.KUM: 2/321/2000 Mbinu Mpya za Kunyamazisha Raia
7. Katika kumbukumbu za mkutano
 1. KUM 2/321/2000: Mbinu mpya za kunyamazisha raia.
 2. Ajenda 2: Kusomwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia.
Alama ya Nukta-Kituo au Semi Koloni (;)
1. Kuorodhesha vitu hasa vinapokuwa na zaidi ya neno moja
 1. Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wa wengi: wake kwa waume; wadogo kwa wakubwa; wazee kwa vijana.
 2. Wakati wa likizo tulitembelea sehemu kadhaa: Mombasa, Kenya; Dodoma, Tanzania; Kampala, Uganda na tukamalizia hapa Nairobi, Kenya.
2. Kuunganisha vishazi huru viwili au kuonyesha mawazo mawili.
 1. Tuliwasili darasani tukiwa tumechelewa; mwalimu alitukaribisha kwa kiboko.
 2. Usiwe na wasiwasi; nitakuwa pamoja nawe siku zote.
Alama ya Kistari Kifupi (-)
1. Kuunganisha maneno mawili
 1. Mbwa-koko aliuma mwana-haramu.
 2. Nawatuma kama wana-kondoo miongoni mwa mbwa-mwitu.
2. Kuonyesha hadi, au mpaka
 1. Bei imepanda kutoka shilingi 20 – 30
 2. Tutasoma kitabu cha Matendo 2: 3 – 7
3. Kama alama ya kupunguza au kutoa katika Hesabu
 1. 9 – 7 = 2
 2. 4 – 5 = -1
4. Kuonyesha neno ambalo halijakamilika litaendelezwa katika msitari ufuatao
 1. Ukitaka twende kwetu nyumbani nitaku-
  peleka ukamwone mamangu.
 2. Kuna migumo kumi na mitatu kati-
  ka Bustani la Kuzimu.
5. Kuonyesha tarehe
 1. Watu wengi walikufa tarehe 07-08-1998.
 2. Marehemu alikufa tarehe 06-06-2006
Alama ya Kistari Kirefu (‒)
1. Kutoa maelezo zaidi
 1. Nilipokutana na Zakido ‒ ambaye aliripotiwa kupotea miaka miwili iliyopita ‒ nilimsalimia lakini hakunitambua.
 2. Hatimaye nimeshinda ‒ baada ya kujaribu kwa masaa matatu.
2. Kuorodhesha hoja au vitu
 1. Umuhumu wa fasihi simulizi:
  ‒ kuburudisha
  ‒ kuelimisha
  ‒ kuunganisha jamii
Alama ya Mabano au Parandesi ()
1. Kutoa maelezo zaidi
 1. Z. Anto (aliyeimba Binti Kiziwi) ametoa wimbo mpya.
 2. Shangazi yangu (ambaye ni naibu wa waziri) amenitumia zawadi.
2. Kutoa neno jingine lenye maana sawa
 1. Dhamira (nia) ya mshairi huyu ni kutushauri tusikimbilie maisha.
 2. Mabanati (wasichana) hao hutembea uchi jijini usiku wa manane.
Alama ya Kinyota (*)
1. Kuonyesha neno ambalo litaelezewa zaidi chini ya ukrasa(foot note)
 1. Alipopata nafasi ya kuingia shule ya upili ya Starehe*, mwanafunzi huyo alijawa na furaha tele.

*Starehe ni mojawapo ya shule zinazofanya vizuri zaidi barani Afrika.

2. Kuficha herufi/silabi katika neno ili kupunguza ukali wa maneno yasiyo na nidhamu.
 1. Rais aliwaita wananchi m**i ya kuku.
 2. Aidha, alisema kwamba nyote ni wapu***vu.
Alama ya Mlazo (/)
1. Kuonyesha ‘au’
 1. Mkutano huo utahutubiwa na Rais/Waziri Mkuu.
 2. Wazungumzaji wengi wa Kiswahili wanatoka Kenyz/Tanzania.
2. Kuonyesha neno au fungu la maneno lenye maana sawa.
 1. Sheila amepewa cheo cha katibu/mwandishi.
 2. Hawa ndio wanaotapatapa ovyo/wasio na mbele wala nyuma.
3. Katika hesabu kuonyesha kugawanya au akisami.
 1. 5/7 ya siku za juma ni siku za kazi.
 2. 12 / 6 = 2
4. Katika tarehe
 1. Shule zilifunguliwa tarehe 08/01/2012
 2. Kamati hiyo ilikubaliana kwamba, Mwokozi alizaliwa tarehe 25/12
Alama ya HERUFI KUBWA
1. Kuanzisha sentensi’
 1. Fisi hula mizoga.
 2. Huu ndio mwanzo wa sentensi hii.
2. Kuonyesha Nomino za Kipekee
 1. Bi Rangile anatoka Vikwazoni.
 2. Nchi ya Tanzania imebarikiwa na Mlima Kilimanjaro unaowavutia wageni kutoka Ulaya.
3. Kuonyesha Kichwa au Mada
 1. ALAMA ZA UAKIFISHAJI
 2. UFAHAMU
 3. Njia Tano za Kuua Mbu
4. Kuonyesha maneno yaliyofupishwa
 1. UKIMWI ni Ukosefu wa Kinga Mwilini.
 2. TUKI ni Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
Alama ya Kikomo au Kituo Kikuu(.)
1. Kuonyesha mwisho wa sentensi.
 1. Huu ndio mwisho wa sentensi hii.
 2. Kioo kimevunjika.
2. Katika kufupisha maneno
 1. U.N.O, K.B.C, Y.C.S
 2. Dkt. Maktaba, Bw. Msumari
3. Kuonyesha Saa
 1. Misa ilianza saa 4.30 za asubuhi.
 2. Hivi sasa ni saa 10.20.
4. Katika hesabu kuonyesha sehemu isiyo nzima
 1. Ukigawa tatu mara mbili, utapata 1.5
 2. Mtoto huyo ana uzani wa kilo 8.27
5. Kuonyesha senti katika pesa
 1. Bei yake ni shilingi 12.50.
 2. Karo ya shule mwaka huu ni 80,000.00
Alama ya Kituo, Kipumuo au Koma (,)
1. Kuorodhesha vitu zaidi ya mbili
 1. Nimenunua simu, saa, redio na viatu.
 2. Kina mama waliimba, wakapiga ngoma na kunegua viuno vyao.
2. Kugawanya mawazo katika sentensi.
 1. Baada ya sala za jioni, Mzee Makosa alitoka nje na kuwasha sigara yake.
 2. Nilipomwuliza kama alimjua binti yule, aliniangalia tu na kucheka
 3. Ingawa kitabu hiki ni kizito, sina budi kukibeba.
3. Kutoa maelezo zaidi.
 1. Shabiba, mmojawapo ya wanawake wajawazito, amejifungua mtoto wa kike.
 2. Shati hili, ingawa nalichukia, nitalivalia tu.
4. Katika tarakimu, kugawa elfu.
 1. Shilingi 209, 408, 000 ziliporwa na serikali.
 2. Dawa hiyo iliua takribani mbu 61, 247.
Alama ya Kinukuu (‘ na “)
1. Kunukuu usemi halisi
 1. “Ukitaka kufua dafu,” mama akamwambia mwanawe, “lazima utie bidii.”
 2. Alimtazama kisha akamwuliza, “Unadhani nimechanganyikiwa kama wewe?”
2. Kunukuu kichwa cha kazi ya sanaa k.v kitabu, wimbo, kipindi n.k
 1. Saumu na Neema ni wahusika katika riwaya “Hamu ya Sumu Tamu”.
 2. Rose Muhando ndiye aliyeimba “Mteule Uwe Macho”.
3. Kuonyesha maneno yasiyo ya Kiswahili unapochanganya ndimi katika sentensi
 1. Huyu ndiye mchezaji “number one”
 2. Amesema “keyboard” ya “computer” yake haifanyi kazi..
4. Kuonyesha maneno yanayowakilisha maana tofauti na maana yake ya kawaida au kinaya.
 1. Lesi alipoenda kwenye ‘maktaba’ alipata mimba.
 2. Rais wetu ‘mtukufu’ amewatisha mawaziri wake.
 3. Moto ulioteketeza shule hiyo ulitokana na kusudi la wanafunzi la ‘kumshtua’ mwalimu wao.
5. Kuonyesha herufi iliyoachwa nje au kufupisha maneno katika ushairi hasa kwa kusudi la kutosheleza idadi ya mizani
 1. ‘takufuata popote wendapo,
 2. ‘liapo ya mgambo, lazima kuna jambo
6. Katika maendelezo ya sauti ya ung’on’g’o (ng’)
 1. Ng’ombe wa Ng’ang’a wanang’ang’ania nini?
 2. King’ang’i anapenda kunung’unika ovyo ovyo.
Alama ya Kiulizi (?)
1. Kuulizia swali
 1. Je, utamtembelea lini?
 2. Ariana anaishi wapi?
2. Kuonyesha pengo lililoachwa wazi
 1. Ndama ni mwana wa ng’ombe ilhali ___?___ ni mtoto wa mbuzi.
 2. __?__ mpokee mke wako, __?__, siku ya leo umepata jiko.
Alama ya Hisi (!)
1. Kuonyesha hisia kama vile hasira, mshangao, furaha n.k
 1. Lo! Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.
 2. Pepo nyeusi! Shindwa! Chomeka! Kwenda kuzimu!
2. Kuigiza Tanakali za Sauti
 1. Amejikwaa sasa ameanguka pu!
 2. Moyo ulidunda ndu! ndu!
Alama ya Nukta-Mbili au Koloni (:)
1. Kutanguliza orodha
 1. Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wa wengi: wake kwa waume; wadogo kwa wakubwa; wazee kwa vijana.
 2. Kuna aina kadhaa za vivumishi: vivumishi vya sifa, vivumishi vya idadi, vivumishi viwakilishi na kadhalika
2. Kuelezea sababu au kuonyesha matokeo ya kitu.
 1. Saumu alipoingia chumbani alipigwa na butwaa: mamake alikuwa amekufa.
 2. Baba alinipatia zawadi nzuri sana: nilirukaruka kwa furaha.
3. Kuonyesha saa
 1. Wimbo huo unachukua dakika 4:45.
 2. Aliingia saa 5:15
4. Kunukuu ukurasa wa Bibilia
 1. Padre alisoma Luka 2:1-6
 2. Katika kitabu cha Mwanzo 5: 2-7, Bibilia inasema…
5. Kuonyesha maneno ya msemaji katika tamthilia au mchezo wa kuigiza
 1. Mzee Mwanyati: Unafikiria mimi ni nyanyako?
 2. Kadogo: (akitetemeka) Tafadhali naomba unisamehe.
6. Kuonyesha mada katika barua au kumbukumbu za mkutano
 1. KUH: Ombi Lako la Kujiuzulu.
 2. RE: Barua ya tarehe 3/2/1999.KUM: 2/321/2000 Mbinu Mpya za Kunyamazisha Raia
7. Katika kumbukumbu za mkutano
 1. KUM 2/321/2000: Mbinu mpya za kunyamazisha raia.
 2. Ajenda 2: Kusomwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia.
Alama ya Nukta-Kituo au Semi Koloni (;)
1. Kuorodhesha vitu hasa vinapokuwa na zaidi ya neno moja
 1. Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wa wengi: wake kwa waume; wadogo kwa wakubwa; wazee kwa vijana.
 2. Wakati wa likizo tulitembelea sehemu kadhaa: Mombasa, Kenya; Dodoma, Tanzania; Kampala, Uganda na tukamalizia hapa Nairobi, Kenya.
2. Kuunganisha vishazi huru viwili au kuonyesha mawazo mawili.
 1. Tuliwasili darasani tukiwa tumechelewa; mwalimu alitukaribisha kwa kiboko.
 2. Usiwe na wasiwasi; nitakuwa pamoja nawe siku zote.
Alama ya Kistari Kifupi (-)
1. Kuunganisha maneno mawili
 1. Mbwa-koko aliuma mwana-haramu.
 2. Nawatuma kama wana-kondoo miongoni mwa mbwa-mwitu.
2. Kuonyesha hadi, au mpaka
 1. Bei imepanda kutoka shilingi 20 – 30
 2. Tutasoma kitabu cha Matendo 2: 3 – 7
3. Kama alama ya kupunguza au kutoa katika Hesabu
 1. 9 – 7 = 2
 2. 4 – 5 = -1
4. Kuonyesha neno ambalo halijakamilika litaendelezwa katika msitari ufuatao
 1. Ukitaka twende kwetu nyumbani nitaku-
  peleka ukamwone mamangu.
 2. Kuna migumo kumi na mitatu kati-
  ka Bustani la Kuzimu.
5. Kuonyesha tarehe
 1. Watu wengi walikufa tarehe 07-08-1998.
 2. Marehemu alikufa tarehe 06-06-2006
Alama ya Kistari Kirefu (‒)
1. Kutoa maelezo zaidi
 1. Nilipokutana na Zakido ‒ ambaye aliripotiwa kupotea miaka miwili iliyopita ‒ nilimsalimia lakini hakunitambua.
 2. Hatimaye nimeshinda ‒ baada ya kujaribu kwa masaa matatu.
2. Kuorodhesha hoja au vitu
 1. Umuhumu wa fasihi simulizi:
  ‒ kuburudisha
  ‒ kuelimisha
  ‒ kuunganisha jamii
Alama ya Mabano au Parandesi ()
1. Kutoa maelezo zaidi
 1. Z. Anto (aliyeimba Binti Kiziwi) ametoa wimbo mpya.
 2. Shangazi yangu (ambaye ni naibu wa waziri) amenitumia zawadi.
2. Kutoa neno jingine lenye maana sawa
 1. Dhamira (nia) ya mshairi huyu ni kutushauri tusikimbilie maisha.
 2. Mabanati (wasichana) hao hutembea uchi jijini usiku wa manane.
Alama ya Kinyota (*)
1. Kuonyesha neno ambalo litaelezewa zaidi chini ya ukrasa(foot note)
 1. Alipopata nafasi ya kuingia shule ya upili ya Starehe*, mwanafunzi huyo alijawa na furaha tele.

*Starehe ni mojawapo ya shule zinazofanya vizuri zaidi barani Afrika.

2. Kuficha herufi/silabi katika neno ili kupunguza ukali wa maneno yasiyo na nidhamu.
 1. Rais aliwaita wananchi m**i ya kuku.
 2. Aidha, alisema kwamba nyote ni wapu***vu.
Alama ya Mlazo (/)
1. Kuonyesha ‘au’
 1. Mkutano huo utahutubiwa na Rais/Waziri Mkuu.
 2. Wazungumzaji wengi wa Kiswahili wanatoka Kenyz/Tanzania.
2. Kuonyesha neno au fungu la maneno lenye maana sawa.
 1. Sheila amepewa cheo cha katibu/mwandishi.
 2. Hawa ndio wanaotapatapa ovyo/wasio na mbele wala nyuma.
3. Katika hesabu kuonyesha kugawanya au akisami.
 1. 5/7 ya siku za juma ni siku za kazi.
 2. 12 / 6 = 2
4. Katika tarehe
 1. Shule zilifunguliwa tarehe 08/01/2012
 2. Kamati hiyo ilikubaliana kwamba, Mwokozi alizaliwa tarehe 25/12
Alama ya HERUFI KUBWA
1. Kuanzisha sentensi’
 1. Fisi hula mizoga.
 2. Huu ndio mwanzo wa sentensi hii.
2. Kuonyesha Nomino za Kipekee
 1. Bi Rangile anatoka Vikwazoni.
 2. Nchi ya Tanzania imebarikiwa na Mlima Kilimanjaro unaowavutia wageni kutoka Ulaya.
3. Kuonyesha Kichwa au Mada
 1. ALAMA ZA UAKIFISHAJI
 2. UFAHAMU
 3. Njia Tano za Kuua Mbu
4. Kuonyesha maneno yaliyofupishwa
 1. UKIMWI ni Ukosefu wa Kinga Mwilini.
 2. TUKI ni Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
Alama ya Kikomo au Kituo Kikuu(.)
1. Kuonyesha mwisho wa sentensi.
 1. Huu ndio mwisho wa sentensi hii.
 2. Kioo kimevunjika.
2. Katika kufupisha maneno
 1. U.N.O, K.B.C, Y.C.S
 2. Dkt. Maktaba, Bw. Msumari
3. Kuonyesha Saa
 1. Misa ilianza saa 4.30 za asubuhi.
 2. Hivi sasa ni saa 10.20.
4. Katika hesabu kuonyesha sehemu isiyo nzima
 1. Ukigawa tatu mara mbili, utapata 1.5
 2. Mtoto huyo ana uzani wa kilo 8.27
5. Kuonyesha senti katika pesa
 1. Bei yake ni shilingi 12.50.
 2. Karo ya shule mwaka huu ni 80,000.00
Alama ya Kituo, Kipumuo au Koma (,)
1. Kuorodhesha vitu zaidi ya mbili
 1. Nimenunua simu, saa, redio na viatu.
 2. Kina mama waliimba, wakapiga ngoma na kunegua viuno vyao.
2. Kugawanya mawazo katika sentensi.
 1. Baada ya sala za jioni, Mzee Makosa alitoka nje na kuwasha sigara yake.
 2. Nilipomwuliza kama alimjua binti yule, aliniangalia tu na kucheka
 3. Ingawa kitabu hiki ni kizito, sina budi kukibeba.
3. Kutoa maelezo zaidi.
 1. Shabiba, mmojawapo ya wanawake wajawazito, amejifungua mtoto wa kike.
 2. Shati hili, ingawa nalichukia, nitalivalia tu.
4. Katika tarakimu, kugawa elfu.
 1. Shilingi 209, 408, 000 ziliporwa na serikali.
 2. Dawa hiyo iliua takribani mbu 61, 247.
Alama ya Kinukuu (‘ na “)
1. Kunukuu usemi halisi
 1. “Ukitaka kufua dafu,” mama akamwambia mwanawe, “lazima utie bidii.”
 2. Alimtazama kisha akamwuliza, “Unadhani nimechanganyikiwa kama wewe?”
2. Kunukuu kichwa cha kazi ya sanaa k.v kitabu, wimbo, kipindi n.k
 1. Saumu na Neema ni wahusika katika riwaya “Hamu ya Sumu Tamu”.
 2. Rose Muhando ndiye aliyeimba “Mteule Uwe Macho”.
3. Kuonyesha maneno yasiyo ya Kiswahili unapochanganya ndimi katika sentensi
 1. Huyu ndiye mchezaji “number one”
 2. Amesema “keyboard” ya “computer” yake haifanyi kazi..
4. Kuonyesha maneno yanayowakilisha maana tofauti na maana yake ya kawaida au kinaya.
 1. Lesi alipoenda kwenye ‘maktaba’ alipata mimba.
 2. Rais wetu ‘mtukufu’ amewatisha mawaziri wake.
 3. Moto ulioteketeza shule hiyo ulitokana na kusudi la wanafunzi la ‘kumshtua’ mwalimu wao.
5. Kuonyesha herufi iliyoachwa nje au kufupisha maneno katika ushairi hasa kwa kusudi la kutosheleza idadi ya mizani
 1. ‘takufuata popote wendapo,
 2. ‘liapo ya mgambo, lazima kuna jambo
6. Katika maendelezo ya sauti ya ung’on’g’o (ng’)
 1. Ng’ombe wa Ng’ang’a wanang’ang’ania nini?
 2. King’ang’i anapenda kunung’unika ovyo ovyo.
Alama ya Kiulizi (?)
1. Kuulizia swali
 1. Je, utamtembelea lini?
 2. Ariana anaishi wapi?
2. Kuonyesha pengo lililoachwa wazi
 1. Ndama ni mwana wa ng’ombe ilhali ___?___ ni mtoto wa mbuzi.
 2. __?__ mpokee mke wako, __?__, siku ya leo umepata jiko.
Alama ya Hisi (!)
1. Kuonyesha hisia kama vile hasira, mshangao, furaha n.k
 1. Lo! Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.
 2. Pepo nyeusi! Shindwa! Chomeka! Kwenda kuzimu!
2. Kuigiza Tanakali za Sauti
 1. Amejikwaa sasa ameanguka pu!
 2. Moyo ulidunda ndu! ndu!
Alama ya Nukta-Mbili au Koloni (:)
1. Kutanguliza orodha
 1. Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wa wengi: wake kwa waume; wadogo kwa wakubwa; wazee kwa vijana.
 2. Kuna aina kadhaa za vivumishi: vivumishi vya sifa, vivumishi vya idadi, vivumishi viwakilishi na kadhalika
2. Kuelezea sababu au kuonyesha matokeo ya kitu.
 1. Saumu alipoingia chumbani alipigwa na butwaa: mamake alikuwa amekufa.
 2. Baba alinipatia zawadi nzuri sana: nilirukaruka kwa furaha.
3. Kuonyesha saa
 1. Wimbo huo unachukua dakika 4:45.
 2. Aliingia saa 5:15
4. Kunukuu ukurasa wa Bibilia
 1. Padre alisoma Luka 2:1-6
 2. Katika kitabu cha Mwanzo 5: 2-7, Bibilia inasema…
5. Kuonyesha maneno ya msemaji katika tamthilia au mchezo wa kuigiza
 1. Mzee Mwanyati: Unafikiria mimi ni nyanyako?
 2. Kadogo: (akitetemeka) Tafadhali naomba unisamehe.
6. Kuonyesha mada katika barua au kumbukumbu za mkutano
 1. KUH: Ombi Lako la Kujiuzulu.
 2. RE: Barua ya tarehe 3/2/1999.KUM: 2/321/2000 Mbinu Mpya za Kunyamazisha Raia
7. Katika kumbukumbu za mkutano
 1. KUM 2/321/2000: Mbinu mpya za kunyamazisha raia.
 2. Ajenda 2: Kusomwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia.
Alama ya Nukta-Kituo au Semi Koloni (;)
1. Kuorodhesha vitu hasa vinapokuwa na zaidi ya neno moja
 1. Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wa wengi: wake kwa waume; wadogo kwa wakubwa; wazee kwa vijana.
 2. Wakati wa likizo tulitembelea sehemu kadhaa: Mombasa, Kenya; Dodoma, Tanzania; Kampala, Uganda na tukamalizia hapa Nairobi, Kenya.
2. Kuunganisha vishazi huru viwili au kuonyesha mawazo mawili.
 1. Tuliwasili darasani tukiwa tumechelewa; mwalimu alitukaribisha kwa kiboko.
 2. Usiwe na wasiwasi; nitakuwa pamoja nawe siku zote.
Alama ya Kistari Kifupi (-)
1. Kuunganisha maneno mawili
 1. Mbwa-koko aliuma mwana-haramu.
 2. Nawatuma kama wana-kondoo miongoni mwa mbwa-mwitu.
2. Kuonyesha hadi, au mpaka
 1. Bei imepanda kutoka shilingi 20 – 30
 2. Tutasoma kitabu cha Matendo 2: 3 – 7
3. Kama alama ya kupunguza au kutoa katika Hesabu
 1. 9 – 7 = 2
 2. 4 – 5 = -1
4. Kuonyesha neno ambalo halijakamilika litaendelezwa katika msitari ufuatao
 1. Ukitaka twende kwetu nyumbani nitaku-
  peleka ukamwone mamangu.
 2. Kuna migumo kumi na mitatu kati-
  ka Bustani la Kuzimu.
5. Kuonyesha tarehe
 1. Watu wengi walikufa tarehe 07-08-1998.
 2. Marehemu alikufa tarehe 06-06-2006
Alama ya Kistari Kirefu (‒)
1. Kutoa maelezo zaidi
 1. Nilipokutana na Zakido ‒ ambaye aliripotiwa kupotea miaka miwili iliyopita ‒ nilimsalimia lakini hakunitambua.
 2. Hatimaye nimeshinda ‒ baada ya kujaribu kwa masaa matatu.
2. Kuorodhesha hoja au vitu
 1. Umuhumu wa fasihi simulizi:
  ‒ kuburudisha
  ‒ kuelimisha
  ‒ kuunganisha jamii
Alama ya Mabano au Parandesi ()
1. Kutoa maelezo zaidi
 1. Z. Anto (aliyeimba Binti Kiziwi) ametoa wimbo mpya.
 2. Shangazi yangu (ambaye ni naibu wa waziri) amenitumia zawadi.
2. Kutoa neno jingine lenye maana sawa
 1. Dhamira (nia) ya mshairi huyu ni kutushauri tusikimbilie maisha.
 2. Mabanati (wasichana) hao hutembea uchi jijini usiku wa manane.
Alama ya Kinyota (*)
1. Kuonyesha neno ambalo litaelezewa zaidi chini ya ukrasa(foot note)
 1. Alipopata nafasi ya kuingia shule ya upili ya Starehe*, mwanafunzi huyo alijawa na furaha tele.

*Starehe ni mojawapo ya shule zinazofanya vizuri zaidi barani Afrika.

2. Kuficha herufi/silabi katika neno ili kupunguza ukali wa maneno yasiyo na nidhamu.
 1. Rais aliwaita wananchi m**i ya kuku.
 2. Aidha, alisema kwamba nyote ni wapu***vu.
Alama ya Mlazo (/)
1. Kuonyesha ‘au’
 1. Mkutano huo utahutubiwa na Rais/Waziri Mkuu.
 2. Wazungumzaji wengi wa Kiswahili wanatoka Kenyz/Tanzania.
2. Kuonyesha neno au fungu la maneno lenye maana sawa.
 1. Sheila amepewa cheo cha katibu/mwandishi.
 2. Hawa ndio wanaotapatapa ovyo/wasio na mbele wala nyuma.
3. Katika hesabu kuonyesha kugawanya au akisami.
 1. 5/7 ya siku za juma ni siku za kazi.
 2. 12 / 6 = 2
4. Katika tarehe
 1. Shule zilifunguliwa tarehe 08/01/2012
 2. Kamati hiyo ilikubaliana kwamba, Mwokozi alizaliwa tarehe 25/12
Alama ya HERUFI KUBWA
1. Kuanzisha sentensi’
 1. Fisi hula mizoga.
 2. Huu ndio mwanzo wa sentensi hii.
2. Kuonyesha Nomino za Kipekee
 1. Bi Rangile anatoka Vikwazoni.
 2. Nchi ya Tanzania imebarikiwa na Mlima Kilimanjaro unaowavutia wageni kutoka Ulaya.
3. Kuonyesha Kichwa au Mada
 1. ALAMA ZA UAKIFISHAJI
 2. UFAHAMU
 3. Njia Tano za Kuua Mbu
4. Kuonyesha maneno yaliyofupishwa
 1. UKIMWI ni Ukosefu wa Kinga Mwilini.
 2. TUKI ni Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

Uchambuzi wa Mashairi

BAHARI ZA USHAIRI
Kitengo Ushairi
Bahari za Ushairi
Maghani

Yafuatayo ni mambo muhimu unayohitajika kuzingatia kila unapochambua shairi.

 1. Muundo/Umbo la shairi
 2. Uhuru wa Mshairi
 3. Maudhui
 4. Dhamira
 5. Mtindo wa / Mbinu za Lugha

Muundo/Umbo la Ushairi

Katika umbo wa shairi, tunaangazia jinsi shairi lilivyoundwa kwa kuangazia mizani, vina, mishororo n.k Aidha, ni muhimu kutaja aina na bahari za shairi zinazohusiana na kila sifa uliyoitaja.

 1. Idadi ya mishororo katika kila ubeti – Tumia idadi ya mishororo kubainisha aina ya shairi hilo.
  Kwa mfano: Shairi lina mishororo minne katika kile ubeti, kwa hivyo ni Tarbia
 2. Idadi ya mizani katika kila mshororo na katika kila kipande cha mshororo.
  Kwa mfano: Kila mshororo una mizani kumi na sita: nane katika utao na nane katika ukwapi.
 3. Idadi ya vipande katika kila mshororo – Taja ikiwa shairi lina kipande kimoja, viwili, vitatu au vinne kisha utaje bahari yake.
 4. Kituo, kiishio au kibwagizo – Ikiwa mstari wa mwisho umerudiwa rudiwa, basi shairi lina kibwagizo au kiitikio, la sivyo lina kiishio.
 5. Vina – Zingatia vina vya kati na vya mwisho kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Kisha utaje ikiwa ni Mtiririko, Ukara au Ukaraguni

Uhuru wa Mshairi

Mshairi hafungwi na kanuni za kisarufi za lugha katika utunzi wa shairi. Anaweza kufanya makosa ya kisarufi kimakusudi ili shairi lizingatie umbo fulani. Zifuatazo ni njia mbalimbali ambazo mtunzi wa shairi anaweza kutumia kuonyesha uhuru wake.

 1. Inkisari – kupunguza idadi ya silabi katika neno ili kusawazisha idadi ya mizani katika mshororo.
  mfano: kubadilisha nimeona aliyenipenda kuwa meona alenipenda.
 2. Mazda – kuongeza silabi katika neno ili kusawazisha idadi ya mizani katika mshororo.
  mfano: afya ukijaliwa kuwa afiya ukijaliwa .
 3. Tabdila – kubadilisha silabi ya mwisho ili kustawazisha urari wa vina katika kipande bila kuathiri mizani.
  mfano: yahuzunisha dunia kuwa yahuzunisha duniya .
 4. Kuboronga Sarufi -ni mbinu ya kupangua mpangilio wa maneno ili kuleta urari wa vina au mdundo wa ushairi.
  mfano: siku hiyo ikifika kuwa ikifika hiyo siku .
 5. Utohozi – Kuswahilisha Maneno – Wakati mwingine mshairi anaweza kubadilisha neno la lugha nyingine litamkike kwa Kiswahili ili kudumisha mdundo wa kishairi na pia kupata neno mwafaka litakalotimiza arudhi za kiushairi.
  mfano: tukapata intaneti badala ya tukapata ‘internet’ ama mtandao wa tarakilishi.

Maudhui

Maudhui ni jumla ya ujumbe na mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika shairi fulani. Haya ni mambo yanayotajwa katika hadithi na yanaweza kujumuisha mawazo zaidi ya moja. Maudhui husaidia kujenga dhamira ya shairi.

Dhamira

Dhamira ni lengo, dhumuni au nia ya mtunzi wa shairi. Mtunzi wa shairi anaweza kuwa na kusudi la kutuonya, kututahadharisha au kutunasihi kuhusiana na jambo fulani.

Mtindo wa Lugha

Mtindo wa lugha hurejelea namna mbalimbali ambazo mshairi anatumia mbinu za lugha. Mshairi anaweza kutumia mbinu za lugha. kama vile: Tanakali za Sauti, Istiara, Takriri, Semi n.k

Angalia: Mbinu za Lugha katika Fasihi

 Uchanganuzi wa Sentensi

UCHANGANUZI WA SENTENSI
Kitengo Lugha
NAVIGATION
Virai na Vishazi
Muundo wa Sentensi

Kuchanganua sentensi ni kugawa sentensi kulingana na makundi ya maneno na aina ya maneno.

Kuna njia tatu za kuchanganua sentensi:

 1. matawi
 2. jedwali
 3. mishale

Content

 • Mifano
  • Kuchanganua Sentensi Sahili
  • Kuchanganua Sentensi Ambatano
  • Kuchanganua Sentensi Changamano

Mifano

Kuchanganua Sentensi Sahili

 1. Nimefika.
 1. Matawi
 2. Jedwali
S
KT
T
Nimefika
 1. Mishale

S → KT

KT → T

T → Nimefika

 1. Jiwe Limeanguka.
 1. Matawi
 2. Jedwali
S
KN KT
N T
Jiwe limeanguka
 1. Mishale

S → KN + KT

KN → N

N → Jiwe

KT → T

T → limeanguka

 1. Mvua nyingi ilinyesha jana usiku.
 1. Matawi
 2. Jedwali
S
KN KT
N V T KE
T E E
Mvua nyingi ilinyesha jana usiku
 1. Mishale

S → KN + KT

KN → N + V

N → Mvua

V → nyingi

KT → T + KE

T → ilinyesha

KE → E1 + E2

E1 → jana

E2 → usiku

Kuchanganua Sentensi Ambatano

 1. Barua ilitumwa lakini haikumfikia Shakila.
 1. Matawi
 2. Jedwali
S
S1 U S2
KN1 KT1 U KT2 KN2
N1 T1 U T2 N2
Barua ilitumwa lakini haikumfikia Shakila
 1. Mishale

S → S1 + U + S2

S1 → KN1 + KT1

KN1 → N1

N1 → Barua

KT1 → T1

T1 → ilitumwa

U → lakini

S2 → KT2 + KN2

KT2 → T2

T2 → haikumfikia

KN2 → N2

N2 → Shakila

 1. Mwalimu alikunja shati lake na kuwachapa wanafunzi kwa kiboko.
 1. Matawi
 2. Jedwali
S
S1 U S2
KN KT U KT KN
N T KN U T KN KE
N T N V U T N U N
Mwalimu alikunja shati lake na kuwachapa wanafunzi kwa kiboko
 1. Mishale

S → S1 + U + S2

S1 → KN1 + KT1

KN1 → N

N → mwalimu

KT1 → T + KN2

T → alikunja

KN2 → N + V

N → shati

V → lake

U → na

S2 → KT2 + KN3 + KE

KT2 → T

T → kuwachapa

KN3 → N

N → wanafunzi

KE → U + N

U → kwa

N → kiboko

Kuchanganua Sentensi Changamano

 1. Wote waliokufa watafufuka
 1. Matawi
 2. Jedwali
S
KN KT
W S T
Wote waliokufa watafufuka
 1. Mishale

S → KN + KT

KN → N + s

W → wote

s → waliokufa

KT → T

T → watafufuka

 1. Wanafunzi ambao hawatasoma vizuri wataanguka mtihani
 1. Matawi
 2. Jedwali
S
KN KT
N s T N
N V KT T N
N V T E T N
Wanafunzi ambao hawatasoma vizuri wataanguka mtihani
 1. Mishale

S → KN + KT

KN → N + s

N → wanafunzi

s → V + T + E

V → ambao

E → hawatasoma

KT → T + N

T → wataanguka

E → mtihani

 Ukubwa na Udogo

UKUBWA NA UDOGO
Kitengo Sarufi
NAVIGATION
Umoja na Wingi
Ngeli

Maneno huwekwa katika ukubwa au udogo yanapozidi kiasi cha wastani kinachotarajiwa. Hali ya ukubwa na udogo hutumika hasa unaposifia au kudharau kitu.

Ukubwa

Nomino zote katika hali ya ukubwa huwa katika ngeli ya LI-YA. Tunaweka maneno katika ukubwa kwa kuongeza kiungo JI na/au kutoa kiwakilishi cha ngeli.

Udogo

Maneno huwekwa katika udogo ili kusifia udogo wao au kudharau kiasi chake. Nomino zote katika hali ya udogo huwa katika ngeli ya KI-VI. Maneno huwekwa katika udogo kwa kuongeza kiungo ki- au kiji-. Katika baadhi ya maneno, kiambishi kiwakilishi cha ngeli huachwa nje tunapoweka maneno katika udogo.

Wastani

Hii ni hali ya kawaida/katikati ya nomino. Si kubwa si ndogo.

WASTANI UDOGO UKUBWA
1. Mtu kijitu Jitu
2. mto kijito Jito
3. kitu kijikitu Jikitu
4. mtoto kitoto / kijitoto toto / jitoto
5. mlango kijilango Lango
6. mwiko kijimwiko / kijiko Jimwiko
7. chungu kijichungu Jungu
8. nyumba chumba / kijumba Jumba
9. kikapu kijikapu kapu / jikapu
10. mji kijiji jiji

Umoja na Wingi

UMOJA NA WINGI
Kitengo Sarufi
NAVIGATION
Nyakati
Ukubwa na Udogo

Sentensi za Kiswahili zinaweza kubadilishwa kutoka kwa umoja hadi wingi, kulingana na ngeli yake. Baadhi ya ngeli hubaki sawia katika umoja na wingi.

Mifano ifuatayo itakuonyesha umoja na wingi wa sentensi katika ngeli mbalimbali.

Ngeli ya A-WA
1. Mtoto huyu ni mvivu sana. Watoto hawa ni wavuvi sana.
2. Mwizi aliyeiba ng’ombe wa mzee mkongwe amekamatwa na mwananchi. Wezi walioiba ng’ombe wa wazee wakongwe wamekamatwa na wananchi
Ngeli ya KI-VI
1. Kitabu chako kiko juu ya kitanda Vitabu vyenu viko juu ya vitanda
2. Chumba kile kidogo kimeangukia chungu Vyumba vile vidogo vimeangukia vyungu.
Ngeli ya LI-YA
1. Jani lile linaficha tunda kubwa ambalo limeiva Majani yale yanaficha matunda makubwa ambayo yameiva.
2. Jiko lolote lenye kaa moto litolewe nje Meko yoyote yenye makaa moto yatolewe nje.
Ngeli ya U-I
1. Mtaa huo hauna mti wowote Mitaa hiyo haina miti yoyote.
2. Huu ndio mto uletao maji katika mji wetu Hii ndiyo mito iletayo maji katika mito yetu.
Ngeli ya U-ZI
1. Ukuta mwingine umepigwa kwa upembe Kuta nyingine zimevunjwa kwa pembe.
2. Ubao mrefu uliokuwa kwenye ua wetu ulikatwa kwa upanga mweusi Ndefu ndefu zilizokuwa kwenye nyua zetu zilikatwa kwa panga nyeusi.
Ngeli ya I-ZI
1. Nyumba iliyo karibu na barabara ile imefungwa Nyumba zilizo karibu na barabara zile zimefungwa.
2. Ndoo yenye maji imewekwa juu ya mbao kubwa Ndoo zenye maji zimewekwa juu ya mbao kubwa.
Ngeli ya U-YA
1. Uyoga uliokuwa hapa umeoza. Mayoga yaliyokuwa hapa yameoza.
2. Mhindi wa kuchoma umeibiwa. Mahindi ya kuchoma yameibiwa.
Ngeli ya YA-YA
1. Mafuta na maji hayawezi kuchanganyika Mafuta na maji hayawezi kuchanganyika.
2. Damu ni nzito kuliko maji Damu ni nzito kuliko maji.
Ngeli ya I-I
1. Sukari imemwagika kwenye changarawe hii. Sukari imemwagika kwenye changarawe hii.
2. Ugali ni tamu lakini mboga haina chumvi. Ugali ni tamu lakini mboga haina chumvi.
Ngeli ya U-U
1. Uji uliopikwa kwa unga wa wimbi ni mtamu kuliko ule wa mtama. Uji uliopikwa kwa unga wa wimbi ni mtamu kuliko ule wa mtama.
Ngeli ya PA-PA
1. Mahali ambapo palipandwa maua panapendeza sana Mahali ambapo palipandwa maua panapendeza sana.
Ngeli ya KU-KU
1. Huku niliko hakuvutii kama kwangu Huku tuliko hakuvutii kama kwetu
2. Kukimbia huku kunachosha. Kukimbia huku kunachosha.
Ngeli ya MU-MU
1. Nyumbani humu mna giza totoro. Nyumbani humu mna giza tororo

 Ushairi

USHAIRI
Utanzu wa
 • Fasihi
 • Nyimbo
 • Fasihi Andishi
Kiingereza Poetry
Tutaangazia
 • Aina za Mashairi
 • Bahari za Ushairi
 • Uchambuzi wa Mashairi
 • Maghani
Fasihi Andishi
Tamathali za Usemi

Ushairi ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha teule na mpangilio fulani wa maneno badala ya kutumia lugha natharia(mflulizo).

Ushairi unaweza kuwa kipera cha fasihi simulizi (nyimbo) na pia katika fasihi andishi kwa sababu mashairi yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya kukariri na pia kwa njia ya maandishi. Mashairi yanayoghanwa badala ya kuimbwa huitwa maghani.

Yaliyomo

 • Uchambuzi
 • Istilahi za Kishairi
 • Sifa za Ushairi
 • Umuhimu wa Mashairi

Uchambuzi

Katika ushairi, tutaangalia:

 • Aina za Mashairi – Kuainisha mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika kila ubeti.
 • Bahari za Ushairi – Muundo wa shairi kulingana vina, idadi ya mizani, vipande, mpangilio wa maneno n.k.
 • Uchambuzi wa Mashairi – Mambo muhimu unayohitajika kuzingatia unapochambua shairi
 • Uhuru wa Mshairi – Ukiukaji wa kanuni za sarufi
 • Istilahi za Kishairi – Msamiati unaotumika katika ushairi km vina, mizani n.k
 • Sifa za Ushairi – Sifa zinazobainisha ushairi kutokana na aina nyingine za sanaa.
 • Umuhimu wa Ushairi – Umuhimu wa ushairi katika jamii.

Istilahi za Kishairi

Haya ni baadhi ya maneno ambayo hautakosa kukutana nayo unapozingatia ushairi. Ni muhimu mwanafunzi kuyajua vizuri.

 1. Shairi – ni sanaa ya maneno (utunzi maalum wa lugha ya kisanaa) unaotumia mpangilio na uteuzi maalum wa maneno na sauti ili kupitisha ujumbe fulani.
 2. Vina – ni silabi za mwisho katika kila kipande.
 3. Mizani – ni idadi ya silabi katika kila mshororo.
 4. Mshororo – ni msitari mmoja wa maneno katika shairi.
 5. Ubeti – ni kifungu cha mishororo kadhaa.
 6. Vipande – ni visehemu vya mshororo vilivyogawanywa kwa alama ya kituo(,)
 7. Ukwapi – kipande cha kwanza katika mshororo
 8. Mwandamo – Kipande cha tatu katika mshororo
 9. Ukingo – kipande cha nne katika mshororo
 10. Utao – kipande cha pili katika mshororo
 11. Mwanzo – mshororo wa kwanza katika ubeti
 12. Mloto – mshororo wa pili katika ubeti
 13. Kimalizio/Kiishio – mshororo wa mwisho katika ubeti usiorudiwarudiwa katika kila ubeti.
 14. Kibwagizo – mshororo wa mwisho katika ubeti unaorudiwarudiwa kila ubeti.

Sifa za Ushairi

 1. Huwa na vina, mizani, mishororo na beti
 2. Hutumia lugha teule
 3. Hufupisha au kurefusha maneno ili kutosheleza idadi ya mizani
 4. Mashairi hayazingatii kanuni za kisarufi. (Angalia uhuru wa mshairi)
 5. Hutumia mbinu za lugha

Umuhimu wa Mashairi

 1. Kuburudisha
 2. Kuhamasisha jamii
 3. Kukuza sanaa na ukwasi wa lugha
 4. Kuliwaza
 5. Kuelimisha
 6. Kuonya, kutahadharisha, kunasihi na kuelekeza
 7. Kupitisha ujumbe fulani
 8. Kusifia mtu au kitu
 9. Kukejeli au kukemea mambo yanayoenda kinyume na maadili ya jamii

Viambishi

VIAMBISHI
Kitengo Muundo wa Neno
Aina Kuu
 • Viambishi Awali
 • Viambishi Tama
NAVIGATION
Uainishaji
Mofimu

Kiambishi ni silabi inayofungamanishwa na mzizi wa neno ili kuleta maana iliyokusudiwa. Viambishi havina maana kamilifu peke yake: huhitaji kufungamanishwa na mzizi wa neno. Kwa hivyo, kiambishi ni mofimu tegemezi inayoongeza maana fulani katika neno kama vile ngeli, wakati, hali, mnyambuliko wa kitendo n.k

Angalia: Uainishaji wa Neno

Kuna aina mbili kuu za viambishi:

 1. Viambishi Awali
 2. Viambishi Tama

Viambishi Awali

Viambishi hivi hutokea kabla ya mzizi ya neno / shina la kitenzi. Kuna aina kadhaa za viambishi hivi kama vile viambishi viwakilishi vya nafsi, ngeli, mahali, wakati, hali n.k

Viambishi Viwakilishi vya Ngeli

Hizi ni silabi zinazowakilisha ngeli katika neno. Mfumo wa ngeli unaokubalika hutumia viambishi hivi kubainisha ngeli mbali mbali.

k.m:

a-me-avy-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya A-WA(umoja)
zi-ta-pasuk-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli I-ZI wingi
ki-li-pote-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya KI-VI(umoja)
ya-na-angaz-iw-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya LI-YA(wingi)

Viambishi Viwakilishi vya Nafsi

hivi ni viambishi ambavyo huonyesha nafsi katika neno. Kuna aina mbili za viambishi viwakilishi vya nafsi:
a) Viambishi Viwakilishi vya Nafsi ya Mtendaji/Mtenda

=> Hutumika kuonyesha aliyefanya kitendo katika neno. Kama viambishi vya Ngeli ya Mtendaji, viambishi hivi ndivyo vinavyotangulia viambishi vingine katika kitenzi.

NAFSI UMOJA WINGI MFANO
YA KWANZA NI TU ni-na-andik-a, tu-li-shind-a
YA PILI U M u-me-kasir-ik-a, m-na-pig-w-a
YA TATU A WA a-li-simam-a, wa-ta-p-ew-a
 1. b) Viambishi Viwakilishi vya Nafsi ya Mtendewa/Mtendwa => Hutumika kuonyesha nafsi ya aliyeathirika na kitendo katika neno. Kama viambishi viwakilishi vya ngeli ya mtendewa, mara nyingi viambishi hivi huwekwa punde kabla ya shina la kitenzi.
  Viambishi viwakilishi vya mtendewa ni sawa na viambishi viwakilishi vya mtendaji isipokuwa:
NAFSI YA MTENDEWA KIAMBISHI MFANO
YA PILI UMOJA KU zi-me-ku-fik-i-a
YA PILI WINGI M, MU, WA ni-na-wa-tum-a
YA TATU UMOJA M ni-ta-m-tambu-a

 

Viambishi Viwakilishi vya Wakati/ Hali

Hivi ni viambishi ambavyo vinapowekwa kabla ya shina la kitenzi, vinatufahamisha wakati kitendo hicho kilipofanyika.
Viambishi hivi ni:

KIAMBISHI HUWAKILISHA: MFANO
LI wakati uliopita kili-chom-ek-a
ME wakati timilifu (uliopita muda mfupi) zi-me-anguk-a
NA wakati uliopo tu-na-ku-subir-i
TA wakati ujao wa-ta-ni-ju-lish-a
HU wakati wa mazoea hu-som-e-a
A wakati usiodhihirika a-tu-pend-a
KA wakati usiodhihirika zi-ka-teket-e-a
PO PO ya wakati a-li-po-wasil-i
KI KI ya masharti ni-ki-zi-angali-a

Viambishi Viwakilishi vya Kukanusha Wakati

Viambishi hivi hutumika kukanusha kitenzi katika sentensi kulingana na wakati au hali

KIAMBISHI HUKANUSHA: MFANO
KU wakati uliopita haku-ingi-a
JA wakati timilifu (uliopita muda mfupi) si-ja-ku-uliz-i-a
-I* wakati uliopo na wa mazoea ha-som-i
TA wakati ujao ha-ki-ta-maliz-ik-a

Tanbihi: * Tunapokanusha wakati uliopo, wakati wa mazoea na wakati usiodhihirika, tunatumia kiambishi kiishio(I) badala ya kutumia kiambishi tamati.
k.m:si-ku-ju-i, ha-pat-ik-an-i

Viambishi Viwakilishi vya Kukanusha Nafsi

Tunapokanusha kitenzi, kiambishi cha kwanzwa hubadilika kulingana na nafsi.

KIAMBISHI MATUMIZI MFANO
SI nafsi ya kwanza si-ku-wa-on-a
HU nafsi ya pili hu-ni-faham-u
HA nafsi ya tatu ha-ta-chuku-a

Viambishi Virejeshi vya Ngeli

Hurejelea ngeli ya mtendewa au mtendwa na hutumika hasa katika vishazi tegemezi (vyenye o – rejeshi)
k.m:

 • wa-li-cho-nitum-i-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya KI-VI
 • ni-ta-ka-ye-m-salim-i-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya A-WA
 • u-li-ko-ji-fich-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya mahali KU
 • tu-li-po-pa-safish-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya mahali PO

Viambishi Tama

Viambishi tama hutokea baada ya shina la kitenzi na hutumika kutuarifu kauli au myambuliko wa kitenzi hicho.

Viishio

Katika kauli ya kutenda, vitenzi vyenye asili ya Kibantu huishia kwa sauti “-a”. Kwa mfano: a-na-omb-a, tu-li-zo-andik-a

Tanbihi: Tunapokanusha vitenzi hivi vyenye asili ya Kibantu katika wakati uliopo na wakati wa mazoea kiishio “-a” hubadilika na kuwa “-i” Kwa mfano: Ha-pat-ik-an-i, Si-ku-ju-i

Vitenzi vyenye asili ya kigeni huchukua viishio tofauti kama vile e, i na u katika kauli ya kutenda. Kwa mfano: ha-wa-ja-tu-jib-u, a-na-tu-subir-i, ni-me-ku-sameh-e

Hata hivyo katika kauli nyinginezo (isipokuwa kauli ya kutenda) vitenzi hivi vya kigeni huchukua kiishio “a”. k.m harib-ik-a, tu-me-jib-iw-a

Viambishi Viwakilishi vya Kauli ya Kitenzi

Hubadilika kulingana na mnyambuliko wa kitenzi.

KAULI KIAMBISHI MFANO
KUTENDEA e, i omb-e-a, pig-i-a,
KUTENDEANA ean, ian omb-ean-a, pig-ian-a,
KUTENDWA w som-w-a
KUTENDEWA ew, iw omb-ew-a, pig-iw-a
KUTENDEKA ek pend-ek-a
KUTENDESHA esh, ez, ish, iz kom-esh-a, ing-iz-a
KUTENDANA an finy-an-a

Kwa mifano zaidi, angalia mnyambuliko wa vitenzi.

 Vielezi (E)

VIELEZI
Kitengo Aina za Maneno
Kiingereza Adverbs
NAVIGATION
Viunganishi
Vivumishi

Vielezi ni maneno yanayotoa habari zaidi kuhusu kitendo kilivyofanyika. Pia vielezi hutoa habari zaidi kuhusu hali, vivumishi au vielezi vingine.

Yaliyomo

 • Aina za Vielezi
  • Vielezi vya Mahali
  • Vielezi vya Wakati
  • Vielezi vya Idadi
  • VIelezi Vya Namna

Aina za Vielezi

Vielezi vya Mahali

Vielezi vya mahali hutoa habari kuhusu mahali ambapo kitendo kilifanyika. Aghalabu vielezi hivi huundwa kwa kutumia jina la mahali au kwa kuongeza kiungo -NI mwishoni mwa neno linaloashiria mahali.

k.m: nyumbani, kazini, shuleni

 • Mtoto huyo hajatulia nyumbani tangu alipotoka Mombasa.
 • Msipitie sokoni mkienda kanisani.

Vielezi vya Wakati

Huelezea zaidi kuhusu wakati kitendo kipofanyika

k.m: jioni, jana, asubuhi, saa saba, mwaka juzi

 • Mzee Kasorogani amesema kwamba ataoga mwaka ujao
 • Musa alilazimishwa kuchimba mtaro saa sita usiku
 • Kisaka na Musa watakutana kesho

Vielezi vya Idadi

Vielezi vya idadi hutulezea kitendo kilifanyika mara ngapi

 1. a) Idadi Kamili

Vielezi vya Idadi Kamili hutaja idadi kamili ya mara ngapi kitendo kilifanyika.

k.m: mara mbili, siku mbili kwa juma, mara kumi

 • Gibi alimzaba kofi mara tatu na kisha akakimbia.
 • Daktari alimwagiza mama huyo achukue dawa mara tatu kwa siku na arudi hospitalini siku mbili kwa mwezi
 1. b) Idadi Isiyodhihirika

Vielezi vya Idadi Isiyodhirika huelezea kiasi ambacho kitendo kilifanyika bila kutaja kiasi kamili

k.m: chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani

 • Mwizi wa kuku alipigwa mara kadhaa kabla ya kuokolewa na polisi.
 • Yeye hunipigia simu mara kwa mara

VIelezi Vya Namna

Huelezea jinsi au namna kitendo kinavyofanyika. Kitendo kinaweza kufanyika kwa namna mbalimbali. Hivyo basi kuna aina mbalimbali za vielezi vya namna:

a) Vielezi vya Namna Halisi

Hutufahamisha jinsi kitendo kinavyofanyika kwa kutumia maneno halisi (bila kuambatanishwa na maneno mengine au viambishi vingine).

k.m: vizuri, ovyo, haraka

 • Kioo cha bibi harusi kilianguka na kuharibika vibaya
 • Mama alipika chakula upesi
 • Amepigwa kalamu kwa kufanya kazi kiholela

b) Vielezi vya Namna Hali

Hutufahamisha hali ambayo kitendo kilifanyika. Vielezi hivi hujihusisha na tabia ya kitu/mtendaji wa kitendo

k.m: kwa furaha, kwa makini,

 • Bibi harusi aliingia kanisani kwa madaha
 • Mtoto alilia kwa maumivu mengi

c) Vielezi vya Namna Kitumizi/Ala

Hutoa habari kuhusu kifaa, ala au mbinu iliyotumiwa kufanya kitendo fulani

k.m: kwa kisu, kwa jembe, kwa meno, kwa moto, kwa maji

 • Mkulima aliangusha mti mkubwa kwa shoka
 • Mzee huyo alimpiga mke wake kwa bakora kabla ya kuchoma nguo zake kwa makaa

d) Vielezi Vikariri

Husisitiza kitendo kinavyofanyika kwa kutaja kielezi kinachorejelewa mara mbili mfululizo.

k.m: haraka haraka, ovyo ovyo, juu juu

 • Polisi walipoingia, wezi walitawanyika haraka haraka.
 • Wanafunzi wengi hufanya kazi yao ovyo ovyo

e) Vielezi vya Ki-Mfanano

Vielezi mfanano hutumia KI-mfanano kuelezea kitendo kinavyofanyika kwa kulinganisha.

k.m: kitoto, kiungwana,

 • Babake huongea kiungwana.
 • Harida hutembea kijeshi

f) Vielezi Viigizi

Vielezi hivi huigiza sauti au mlio wa kitu, kitendo kitendo kilipofanyika kwa kutumia tanakali za sauti

k.m: tuli, chubwi, tifu, chururu

 • Mwanafunzi alitulia tuli mwalimu alipomzaba kofi pa!
 • Kaswimu aliangusha simu changaraweni tifu na kujitumbukiza majini chubwi

g) Vielezi vya Vielezi

Vielezi hivi hutumika kuelezea kielezi kingine. Hivyo basi, hutanguliwa na kielezi badala ya kitendo

k.m: sana, kabisa, hasa, mno

 • Mamake Kajino alitembea polepole sana.
 • Chungu kilivunjika vibaya kabisa

h) Vielezi vya Vivumishi

Hutoa habari zaidi kuhusu kivumishi

k.m: sana, kabisa, hasa, mno

 • Yeye ni mrefu sana
 • Mtoto wake ana tabia nzuri mno

 Vihisishi (I)

VIHISISHI
Kitengo Aina za Maneno
Kiingereza Injections
NAVIGATION
Nomino
Vihusishi

Vihisishi ni maneno yanayotumika kuonyesha hisia kama vile hasira, furaha, mshangao, kusifia, kushangilia n.k. Vihisishi hutambulishwa katika sentensi kwa kuambatanishwa na alama ya mshangao (!). Kihisishi kimoja kinaweza kutumika kutoa hisia tofauti kulingana na muktadha.

Mifano ya Vihisishi

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maneno yanayotumika kuonyesha hisia. Hata hivyo, maneno mengine yoyote yanaweza kutumika kama vihisishi, kulingana na mukhtadha. k.v Potelea mbali!

Kihisishi Mfano katika Sentensi Hisia
Lo! Lo! Maajabu ya Musa haya! mshangao
Salaale!, Masalaale! Salaale! Angalia watu wote hawa waliofika mahali hapa! mshangao
Kumbe! Nilidhani wewe ni rafiki yangu. Kumbe! mshangao
Po! Sijawahi kuona kijana mjeuri kama wewe. Po! hasira
Ng’o! Omba msamaha utakavyo, lakini unachoka bure. Ng’o! kiburi
Hata! Bwanake hakumwachia chochote! Hata! kusifia, kupuuza
Akh!, Aka! Mtoto mpumbavu huyu! Akh! hasira, kukashifu
Ah! Ah! Sikuyaamini macho yangu. mshangao
Ala! Ala! Umefika tayari! mshangao
Haha! Haha! Umenivunja mbavu, bwana! kicheko
Ehee!, Enhe! Enhe! Endelea, ninaipenda sana hadithi hiyo! kuitikia
Hmmm! Hmmm! Chakula kitamu hicho! kuitikia, kusifia
Ebo! Ebo! Tabia gani hiyo. kukashifu, hasira
Kefule! Kefule! Umenifedhehesha sana. hasira
Wee! Katamu alinegua kiuno na kucheza kwa madaha. Wee! Wavulana wakaduwaa. kusifia
La!, Hasha! La! Sitaki kusikiliza upuuzi wako tena. kukataa
Hoyeee! Wamama wote, hoyee! Hoyee! kushangilia
Huraa! Huraa! Tumeshinda. kushangilia

Vihusishi (H)

VIHUSISHI
Kitengo Aina za Maneno
Kiingereza Prepositions
NAVIGATION
Vihisishi
Viunganishi

Vihusishi ni maneno yanayotuarifu zaidi kuhusu uhusiano wa nomino na mazingira yake.

Yaliyomo

 • Aina za Vihusishi
  • Vihusishi vya Mahali
  • Vihusishi vya Wakati

Aina za Vihusishi

Vihusishi vya Mahali

mbele ya, nyuma ya Kuna mzoga nyuma ya jengo hilo.
chini ya, juu ya Joto lilipozidi, watoto waliketi chini ya mti ule.
kando ya Kando ya mito ya Babeli ndipo tulipoketi.
karibu na, mbali na Fisi aliambiwa asile mifupa karibu namtoto yule.

Vihusishi vya Wakati

kabla ya Ni vizuri kusali kabla ya kula chakula.
baada ya Watoto safi hupiga meno mswaki baada ya kila mlo.

Vitenzi (T)

VITENZI
Kitengo Aina za Maneno
Kiingereza Verbs
NAVIGATION
Vivumishi
Viwakilishi

Vitenzi ni maneno yanayosimamia kitendo. Kila kitenzi huwa na shina la kitenzi (sehemu ndogo zaidi ya kitenzi ambayo ndiyo huwakilisha tendo hilo). Shina la kitenzi huambatanishwa na viambishi ili kutoa maana iliyokusudiwa kama vile mtendaji, mtendewa, wakati kitendo kinafanyika na pia kauli ya kitenzi hicho.

Aina za Vitenzi

 1. Vitenzi Halisi
 2. Vitenzi Visaidizi + Vitenzi Vikuu
 3. Vitenzi Vishirikishi
 4. Vitenzi Sambamba

Vitenzi Halisi

Hivi ni vitenzi vinavyorejelea kitendo moja kwa moja. Vitenzi halisi vinapoambatanishwa na vitenzi vidogo katika sentensi, huitwa vitenzi vikuu.

k.m: soma, kula, sikiza

 • Waziri Mwasimba aliwasili jana kutoka ng’ambo.
 • Kawia atapikia wageni.
 • Funga mlango wa dirisha.

Vitenzi Visaidizi

Vitenzi visaidizi hutangulia vitenzi halisi (vitenzi vikuu) katika sentensi ili kuleta maana inayokusudiwa kulingana na wakati au hali.

k.m: -kuwa, -ngali,

 • Jua lilikuwa limewaka sana.
 • Bi Safina angali analala

Vitenzi Vishirikishi

Vitenzi vishirikishi hutumika kuelezea hali iliyopo au mazingira. Kuna aina mbili za vitenzi vishirikishi:

a) Vitenzi Vishirikishi Vipungufu – havichukua viambishi vyovyote.

k.m: ni, si, yu

 • Kaka yako ni mjanja sana.
 • Huyo si mtoto wangu!
 • Paka wake yu hapa.

b) Vitenzi Vishirikishi Vikamilifu – huchukua viambishi vya nafsi au ngeli. Vitenzi hivi vinaweza kusimama peke yake au vinaweza kufuatiliwa na vitenzi vikuu.

k.m: ndiye, ndio, ndipo

 • Sanita ndiye mkurugenzi wa kampuni
 • Huku ndiko kulikoibiwa

Muundo wa Vitenzi

Kwa kuzingatia muundo wa vitenzi, tunaweza kuweka vitenzi katika aina zifuatazo:

 1. Vitenzi vya Silabi Moja
 2. Vitenzi vya Kigeni
 3. Vitenzi vya Kibantu

Vitenzi vya Silabi Moja

Hivi ni vitenzi vyenye silabi moja pekee. Ili kuleta maana kamili, vitenzi hivi huambatanishwa na kiungo KU- katika kauli ya kutenda. Kama vitenzi vingine, vitenzi vya silabi moja vinaweza kunyambuliwa.

k.m: soma, kula, sikiza

 • -cha – kucha – jua linapochomoza asubuhi k.m kumekucha
 • -fa – kufa – kuacha kupumua, kupoteza uhai k.m amekufa
 • -ja– kuja – fika mahali hapa k.m nimekuja
 • -la– kula – kutia chakula mdomoni k.m anakula
 • -nya– kunya – kutoa mabaki ya chakula toka tumboni k.m mtoto amekunya
 • -nywa– kunywa – kutia kinywaji kama vile maji au maziwa mdomoni k.m ninakunywa uji
 • -pa– kupa – kumkabithi/kumpatia mtu kitu k.m amenipa pesa
 • -pwa– kupwa – kujaa hadi pomoni – k.m kisima kimekupwa maji
 • -twa– kutwa – jua linapozama magharibi na usiku kuingia k.m kumekutwa
 • -wa– kuwa – kutokea katika hali au mahali fulani k.m alikuwa

Vitenzi vya Kigeni

Hivi ni vitenzi vyenye asili kutoka kwa lugha nyingine badala ya Kibantu. Baadhi ya lugha hizo ni Kiarabu, Kizungu, Kireno, Kihispania n.k. Vitenzi hivi havifuatilii muundo wa kawaida wa vitenzi vya Kiswahili ambavyo huishia kwa sauti -a. Badala yake, vitenzi hivi huishia kwa sauti nyingine kama vile -e, i, -o, na u

k.m: haribu, tubu, shukuru, salimu, thamini, amini, samehe, baleghe

Vitenzi vya Kibantu

Hivi ni vitenzi vyenye asili ya Kibantu na ambavyo huishia kwa sauti -a. Kitengo hiki hujumuisha asilimia kubwa zaidi ya vitenzi vya Kiswahili

k.m: simama, shika, tembea, beba, soma, lia

 Viunganishi (U)

VIUNGANISHI
Kitengo Aina za Maneno
Kiingereza Conjunctions
NAVIGATION
Vihusishi
Vielezi

Viunganishi ni maneno yanayoutumika kuunganisha, kulinganisha au kuonyesha uhusiano wa dhana mbili au zaidi.

Aina za Viunganishi

Zifuatazo ni aina mbalimbali za viunganishi kulingana na matumizi yake

Kuonyesha Umilikaji

A-Unganifu Kiatu cha Mzee Sakarani kimepasuka.
KWA (umilikaji wa mahali) Mbinguni kwa kuna makao mengi.

Kujumuisha

na Baba, mama na watoto huunda familia kamili.
pamoja na Mwizi aliiba runinga pamoja na redio
fauka ya, licha ya Fauka ya mapigo yote, Kafa alikatakatwa kwa kisu.
zaidi ya, juu ya Unataka nini tena zaidi ya mema yote niliyokutendea?
pia, vilevile Alimpiga mkewe na bintiye vilevile
mbali na Mbali na hayo nitakujengea nyumba ya kifahari.
aidha Keti akitoka shuleni atapika. Aidha atampelekea nyanya sukuma wiki.
wala (kukanusha) Ndege wa angani hawalimi wala hawapandi.

Kutofautisha

lakini, ila Ongea nayeilausimwambie mipango yetu.
bila Tasha aliondoka bila kusema lolote.
bali Sitawaacha kama mayatima bali nitawatumia msaidizi.
kinyume na, tofauti na Jana kulinyesha kinyume na utabiri wa hali ya hewa.
ingawa, ingawaje Nitamtembelea ingawa sijui nitamwambia nini.
japo, ijapokuwa Nakuomba upokee nilichokileta japo ni kidogo sana.
ilhali Fungo zimepotea ilhali zilikuwa zimewekwa vizuri.
minghairi ya Waliendelea kutenda dhambi minghairi ya kuhubiriwa kanisani.
dhidi ya Vita dhidi ya gonjwa hilo vingali vinaendelea.

Kuonyesha Sababu

ili Hanna aliumizwa ili asikumbuke aliyoyaona.
kwa, kwa vile Emili alinyamaza kwa vile kugombana na rafikize.
kwa maana, kwa kuwa Aria alipigwa na butwaa kwa maana mpenzi wake aligeuka kuwa mwalimu wake.
kwani Melisa alijificha kwani hakutaka kuonekana na Spensa.
kwa minanjili ya Chali alitembea mwendo huo wote kwa minanjili ya kuongea na Katosha.
maadam Wanawake katika familia hiyo hawali maini maadam mama mkongwe alilaani maini katika familia hiyo.
madhali Madhali sote tuko hapa, tunaweza kuanzisha mkutano mapema

Kuonyesha Matokeo

basi, hivyo basi Umekula ng’ombe mzima, hivyo basi huna budi kumalizia mkia.
kwa hivyo Alipatikana na makosa ya kumnajisi bintiye, kwa hivyo akahukumiwa miaka kumi gerezani.
ndiposa Mama Kelele alipenda kuongea sana, ndiposa wakamkata midomo.

Kulinganisha

kama, sawa na Kunywa pombe ni kama kujichimbia kaburi mwenyewe.
kulingana na Mwalimu Makunza hafanyi kazi kulingana na maadili ya shuleni.
kuliko, zaidi ya Talia ni mfupi kuliko Nuru
vile Mganga Daimoni hutibu vile alivyofunzwa na Mganga Kuzimu.

Kuonyesha Kitu kimoja kama sehemu ya kingine

kati ya Vitatu kati ya vitabu hivi vimepigwa marufuku.
miongoni mwa Miongoni mwa walioachiliwa, ni Ngiri na Mende.
baadhi ya Baadhi ya wasichana kutoka Vikwazoni hawaheshimu miili yao.
mojawapo Mojawapo ya maembe uliyochuma yameoza.

Kuonyesha Kitu kufanyika baada ya kingine

kisha Soma mfano huu kisha usome sentensi ifuatayo.
halafu Alichukua kisu halafu akatokomea gizani.

Kuonyesha Kitu kufanyika badala ya kingine

badala ya Mapepo yalimchukua Shakawa badala ya bintiye
kwa niaba ya Mama Roga alitoa hotuba kwa niaba ya mumewe.

Kuonyesha Uwezekano

labda, pengine Sina pesa leo, labda uje kesho.
ama, au Ama Anita au Katosha anaweza kuja.
huenda Huenda kesho ikifika, Mungu atende miujiza.

Kuonyesha Masharti

bora, muradi Sitakuuliza bora tu usichelewe.
ikiwa, iwapo Ikiwa huna jambo muhimu la kusema, nyamaza.

 Vivumishi (V)

VIVUMISHI
Kitengo Aina za Maneno
Kiingereza Adjectives
NAVIGATION
Vielezi
Vitenzi

Vivumishi au visifa ni maneno yanayotuelezea zaidi kuhusu nomino. Aghalabu vivumishi hutanguliwa na nomino.

Yaliyomo

 • Aina za Vivumishi
  • Vivumishi vya Sifa
  • Vivumishi Vimilikishi
  • Vivumishi vya Idadi
  • Vivumishi Visisitizi
  • Vivumishi Viashiria / Vionyeshi
  • Viwakilishi Viulizi
  • Vivumishi Virejeshi
  • Vivumishi vya KI-Mfanano
  • Vivumishi Vya A-Unganifu

Aina za Vivumishi

Vivumishi vya Sifa

Hivi ni vivumishi ambavyo hutoa sifa ya kitu, mtu, mahali, n.k

k.m: kizuri, kali, safi, mrembo

 • Yule mama mweusi hupika chakula kitamu.
 • Mvulana mkorofi aliadhibiwa na mwalimu kutokana na tabia zake mbaya.
 • Sauti nzuri humtoa nyoka mkali pangoni

Vivumishi Vimilikishi

Vivumishi hivi hutumika kuonyesha nomino inamiliki nyingine. Mizizi ya vivumishi hivi huundwa kulingana na nafsi mbalimbali ( -angu, -ako, -ake, -etu, -enu, -ao).

k.m: changu, lako, yake, kwetu, vyenu, zao

 • Nitatumia talanta zangu kwa manufaa ya taifa letu.
 • Aliweka kitabu chako sebuleni mwako
 • Katosha amepata nguo yake miongoni katika sanduku lao.

Vivumishi vya Idadi

Hutueleza zaidi kuhusu kiasi, au idadi ya nomino. Kuna aina mbili za vivumishi vya idadi.

a) Idadi Kamili

hutumia nambari kuelezea idadi ya nomino.

k.m: tatu, mbili, kumi

 • Msichana mmoja amewauwa nyoka wawili
 • Siku kumi zimepita tangu Bi Safina alipojifungua watoto watatu

b) Idadi Isiyodhihirika

huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja idadi kamili

k.m: chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani

 • Watu wachache waliohudhuria mazishi ya Kajuta walikula chakula kingi sana.
 • Baba yao alikuwa mateka kwa miaka kadhaa.

Vivumishi Visisitizi

Husisitiza nomino fulani kwa kurudia rudia kivumishi kiashiria

k.m: yuyu huyu, wawa hawa, kiki hiki, papo hapo, mumu humu,

 • Jahazi lili hili
 • Wembe ule ule
 • Ng’ombe wawa hawa

Vivumishi Viashiria / Vionyeshi

Vivumishi viashiria hutumika kuonyesha au kuashiria nomino kulingana na mahali.

Karibu hapa, huyu, hiki, hili, huku, haya, ule, wale, pale
Mbali kidogo hapo, huyo, hiyo, hicho
Mbali zaidi pale, lile, kile
 • Msichana huyu ni mkubwa kuliko yule
 • Jani hili la mwembe limekauka
 • Tupa mpira huo

Viwakilishi Viulizi

Vivumishi viulizi hutumika kuuliza swali.

Baadhi ya vivumishi viulizi huchukua viambishi vya ngel

k.m: -ngapi?, -pi?

 • Ni walimu wangapi wamefukuzwa? – kuulizia idadi
 • Je, ni dawati lipi lenye funguo zangu?

Kunavyo vivumishi viulizi vingine ambavyo havichukui viambishi vyovyote.

k.m: wapi?, gani?, nini?, vipi?

 • Unazungumza kuhusu kipindi gani?
 • Je, mmefika mahali wapi? – kuulizia mahali

 

Vivumishi Virejeshi

Hivi ni vivumishi ambavyo hurejelea nomino. Vivumishi hivi vinaweza kuwa vivumishi vya O-rejeshi au vivumishi viashiria vinapotumika kurejelea nomino.

k.m: ambaye, ambao, ambalo, ambacho,

 • Msichana ambaye alikuja ni Sheila
 • Sauti ambayo uliisikia ilikuwa ya Mzee Kasorogan

Vivumishi vya KI-Mfanano

Vivumishi vya KI- ya Mfanano hutumika kulinganisha sifa ya nomino na hali au tabia nyingine. Vivumishi hivi hutanguliwa na nomino, kiunganishi cha A-unganifu na huchukua kiungo KI.

k.m: wa kifalme, za kijeshi, ya kitajiri, n.k

 • Chifu wa Vikwazoni anaishi maisha ya kimasikini
 • Chali anapenda kusikiliza mziki wa kizungu
 • Bi Naliza huvulia mavazi ya kifalme.

Vivumishi Vya A-Unganifu

Vivumishi hivi hutuelezea zaidi kuhusu nomino kwa kuonyesha kitu kinachomiliki nomino hiyo. Huundwa kwa kuambatanisha kiambishi cha nafsi/ngeli pamoja na kiambishi -a cha a-unganifu, kisha nomino

k.m: cha, la, kwa, za, ya

 • Watoto wa mwalimu mkuu wana tabia nzuri
 • Chai ya daktari imemwagika

 Viwakilishi (W)

VIWAKILISHI
Kitengo Aina za Maneno
Kiingereza Pronouns
NAVIGATION
Vitenzi
Nomino

Viwakilishi vya Nomino ni maneno yanayotumika badala ya nomino. Kiwakilishi hakiwezi kuambatanishwa na nomino inayorejelewa.

Yaliyomo

 • Aina za Viwakilishi
  • Viwakilishi vya Nafsi
  • Viwakilishi Viashiria
  • Viwakilishi Visisitizi
  • Viwakilishi vya Sifa
  • Viwakilishi vya Idadi
  • Viwakilishi Viulizi
  • Viwakilishi Vimilikishi
  • Viwakilishi Virejeshi (O-Rejeshi)
  • Viwakilishi Vya A-Unganifu

Aina za Viwakilishi

Viwakilishi vya Nafsi

Viwakilishi hivi hutumika kwa niaba ya nafsi kwa umoja na kwa wingi.

k.m: mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi, wao

NAFSI UMOJA WINGI
Nafsi ya Kwanza Mimi Sisi
Nafsi ya Pili Wewe Ninyi/Nyinyi
Nafsi ya Tatu Yeye Wao
 • Sisi tuliwatangulia nyinyi kufika hapa.
 • Mimi si mjinga kama vile yeye anavyofikiria

Viwakilishi Viashiria

Viwakilishi viashiria (vionyeshi) hutumika badala ya nomino kwa kutumia kuonyesha nomino inayorejelewa bila kuitaja.

k.m: huyu, yule, hapa, n.k

 • Hiki hakina maandishi yoyote.
 • Hao hawajui tofauti ya viwakilishi na vivumishi
 • Tumekuja hapa ili kuwaburudisha kwa nyimbo tamu tamu.

Viwakilishi Visisitizi

Husisitiza nomino inayowakilishwa kwa kurudiarudia kiashiria chake.

k.m: yuyu huyu, wawa hawa, kiki hiki, papo hapo, mumu humu,

 • Zizi hizi ndizo zilizovunjika wiki jana
 • Yule yule aliyekamatwa juzi, ameiba tena.

Viwakilishi vya Sifa

Husimama badala ya nomino kwa kurejelea sifa yake.

k.m: ‘-eupe, -zuri, -tamu, -embamba, -rembo, safi’

 • Vyekundu vimehamisha
 • Warembo wamewasili.
 • Kitamu kitaliwa kwanza.

Viwakilishi vya Idadi

Hutumika kusimama badala ya nomino kwa kurejelea idadi yake.

a) Idadi Kamili– hutumia nambari kuelezea idadi ya nomino.

k.m: ‘saba, mmoja, ishirini’

 • Wawili wamepigwa risasi polisi leo jioni.
 • Alimpatia mtoto wake hamsini kununua chakula

b) Idadi Isiyodhihirika– huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja idadi kamili

k.m: ‘chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani’

 • Tutazungumza na wachache kabla ya kuanzisha maonyesho yetu.
 • Kadhaa zimeripotiwa kupotea.

Viwakilishi Viulizi

Viwakilishi viulizi hutumika kwa niaba ya nomino katika kuulizia swali.

Baadhi ya viwakilishi viulizi huchukua viambishi vya ngeli

k.m: ‘ -ngapi?, -pi?’

 • Vingapi vinahitajika? – kuulizia idadi
 • Zipi zimepotea?

Kunavyo viwakilishi viulizi vingine ambavyo havichukui viambishi vyovyote.

k.m: ‘wapi?, gani?, nini?, vipi?’

 • Gani imefunga bao hilo?
 • Wapi hapana majimaji?
 • Yule mvulana alikupatia nini?
 • Uliongea naye vipi? – kuulizia namna

Viwakilishi Vimilikishi

Viwakilishi hivi hurejelea nomino kwa kutumia vimilikishi.

k.m: ‘-angu, -ako, -ake, -etu, -enu, -ao ‘

 • Kwetu hakuna stima.
 • Lake limekucha.
 • Zao zimeharibika tena

Viwakilishi Virejeshi (O-Rejeshi)

Hutumia O-rejeshi kurejelea na kusimamia nomino

k.m: ‘ambaye, ambao, ambalo, ambacho, huyo, yule’

 • Ambalo lilipotea limepatikana.
 • Ambaye hana mwana, aeleke jiwe

Viwakilishi Vya A-Unganifu

Huwakilishi nomino kwa kutaja kinachomiliki nomino hiyo. Huundwa kwa kuambatanisha kiambishi cha nafsi/ngeli pamoja na kiambishi -a cha a-unganifu, kisha nomino nyingine

k.m: ‘cha, la, kwa, za, ya’

 • Cha mlevi huliwa na mgema
 • Za watoto zitahifadhiwa.

 Virai na Vishazi

VIRAI NA VISHAZI
Kitengo Lugha
NAVIGATION
Aina za Sentensi
Uchanganuzi wa Sentensi

Sentensi huwa na vifungu mbalimbali. Baadhi ya vifungu hivi ni vishazi na virai.

Yaliyomo

 • Virai (phrase)
  • Kirai Nomino:
  • Kirai Kiwakilishi
 • Kirai Kivumishi
 • Kirai Kielezi
 • Vishazi (clause)
  • Kishazi Huru (Independent Clause)
  • Kishazi Tegemezi (Dependent Clause)

Virai (phrase)

Kirai ni fungu la maneno lisilokuwa na kitenzi.Phrase

Kuna aina nne za virai:

Kirai Nomino:

Kirai Nomino ni fungu la maneno katika sentensi lenye nomino (Kikundi Nomino/Kiima)

 1. Redio na runinga hutumika kutupasha habari.
 2. Bintiye Mchungaji Boriti anapenda kuwasaidia watu.
 3. Miembe mirefu itakatwa.

Kirai Kiwakilishi

Kirai Kiwakilishi ni fungu la maneno linalowakilisha nomino katika sentensi

 1. Zenyewe zimekwishaharibika.
 2. Watakaovumilia hadi siku ya mwisho wataokolewa
 3. Yeye alijitumbukiza majini na kufariki papo hapo.

Kirai Kivumishi

Kirai Kivumishi ni fungu la maneno katika sentensi linalotupa habari zaidi kuhusu nomino.

 1. Matokeotuliyokuwa tukiyasubiri yametangazwa.
 2. Duka zenye bei nafuu zimefungwa.
 3. Msichana mrembo kama malaika ameolewa.

Kirai Kielezi

Kirai Kielezi ni fungu la maneno linaloelezea zaidi kuhusu kitenzi au kivumishi.

 1. Walevi wana mazoea ya kupayuka ovyo ovyo.
 2. Viumbe vyote vyenye uhai vinamshangilia kwa furaha milele na milele.
 3. Kwaya ya Chuo Kikuu cha Nairobi huimba kwa sauti za kimalaika

Vishazi (clause)

Kishazi ni sehemu ya sentensi yenye kitenzi. Kuna aina mbili za virai:

Kishazi Huru (Independent Clause)

Kishazi Huru huwa na maana kamili na kinaweza kujisimamia chenyewe kama sentensi.

 1. Amina ameanza kuimba baada ya kumaliza kusali.
 2. Watakaopatikana wakichekacheka ovyoovyo, watang’olewa meno.
 3. Nitakupatia nusu ya ufalme wangu, iwapo utanipigia magoti.

Kishazi Tegemezi (Dependent Clause)

Kisha Tegemezi huhitaji kuunganishwa na kishazi kingine ili kuleta maana iliyokusudiwa. Aghalabu huwa na kirejeshi k.v amba-, -enye n.k

 1. Amina ameanza kuimba baada ya kumaliza kusali.
 2. Watakaopatikana wakichekacheka ovyoovyo, watang’olewa meno.
 3. Nitakupatia nusu ya ufalme wangu, iwapo utanipigia magoti.

Vitate, Vitawe na Visawe

VITATE, VITAWE NA VISAWE
Kitengo Msamiati
MASOMO
N/A
Tarakimu

Baadhi ya maneno ya Kiswahili yanaweza kuwa na maana sawa, maana zaidi ya moja au matamshi yanayotatiza. Vikundi hivi vitatu ni:

 1. Vitate – maneno yanayotatiza kimatamshi. ⇒ Vitate hutatiza kimatamshi
 2. Vitawe – maneno yenye maana zaidi ya moja. Vitawe hugawanywa kwa matawi au maana zaidi
 3. Visawe – maneno tofauti yenye maana sawa. Visawe huwa na maanasawa ”

Vitate

Maneno yanayotatiza kimatamshi.

 1. ndoa na doa :
  1. ndoa ⇒ kuungana kwa watu wawili na kuishi pamoja kama mume na mke
  2. doa ⇒ alama ya uchafu, kasoro au dosari
 2. baba na papa :
  1. baba ⇒ mzazi wa kiume
  2. papa ⇒ mnyama wa baharini
 3. fua na vua :
  1. fua ⇒ osha nguo, tengeneza vyuma
  2. vua ⇒ shika samaki kutoka majini; toa nguo
 4. faa na vaa :
  1. faa ⇒ inayostahili, inayopaswa
  2. vaa ⇒ weka nguo juu ya mwili
 5. ngoma na goma :
  1. ngoma ⇒ ala ya muziki itoayo sauti inapopigwa
  2. goma ⇒ acha kufanya kazi
 6. shinda na shida :
  1. shinda ⇒ ongoza katika makabiliano, mashindano
  2. shida ⇒ taabu au matatizo
 7. shindano na sindano :
  1. shindano ⇒ makabiliano baina ya watu wawili au zaidi ili kutambua atakayeongoza
  2. sindano ⇒ kifaa kinachotumika kushonea vitu
 8. pinga na piga :
  1. pinga ⇒ kutokubaliana na jambo fulani
  2. piga ⇒ kugonga au kuchapa
 9. fahali na fahari :
  1. fahali ⇒ ng’ombe wa kiume. pia ndume
  2. fahari ⇒ kujivunia, furaha
 10. haba na hapa :
  1. haba ⇒ kisichokuwa kingi
  2. hapa ⇒ mahali karibu

Vitawe

Mano yenye maana zaidi ya moja

 1. paa :
  1. kwea (enda juu)
  2. mnyama wa porini anayefanana na mbuzi
  3. sehemu ya juu ya nyumba
 2. shinda :
  1. kaa au ishi mahali/wakati fulani
  2. ongoza katika shindano
  3. tupu
 3. kaa :
  1. sehemu yenye moto ya kuni
  2. mnyama wa majini
  3. keti chini
  4. kuwa mahali fulani kwa muda
 4. mbuzi :
  1. mnyama anayefugwa kama ng’ombe
  2. chombo cha kukunia nazi
 5. mlango :
  1. ukoo au watu wenye asili smoja
  2. sehemu ya kuingia kwenye nyumba
  3. kitu kinachotumika kifunga nyumba
 6. fua :
  1. unda vyombo/vifaa mbalimbali kwa kupiga chuma
  2. osha nguo
 7. vua :
  1. toa nguo kutoka mwilini
  2. toa samaki kwenye maji
 8. kiboko :
  1. mnyama mkubwa wa baharini
  2. silaha inayotumika kwa kuchapa au kupiga
 9. tembo :
  1. aina ya ndovu
  2. aina ya pombe

Visawe

Maneno tofauti yenye maana sawa.

 1. msichana au banati : ⇒ kijana wa jinsia ya kike
 2. mvulana au ghulamu : ⇒ kijana wa jinsia ya kiume
 3. huzuni au majonzi : ⇒ hali ya kilio na huruma
 4. mazishi au matanga : ⇒ shughuli za kumzika marehemu
 5. wakati au mwia : ⇒ wakati au muda
 6. mtu au mja : ⇒ mnyama atembeaye kwa miguu miwili mwenye uwezo wa kuongea na kufikiri kimantiki
 7. barua au waraka : ⇒ kartasi inayoandikwa na kutumwa ili kuwasilisha ujumbe fulani
 8. siri au faragha : ⇒ jambo lisilopaswa kujulikana na mtu mwengine
 9. macho au maninga : ⇒ sehemu za mwili zinazotumika kuangalia na kuona
 10. mwangaza au nuru : ⇒ miyale inayowezesha watu kuona vitu
 11. Mungu au Mola au Rabana au Jalali au Rabuka : ⇒ Majina ya Mwenyezi Mungu

Wahusika Katika Fasihi Andishi

WAHUSIKA KATIKA FASIHI ANDISHI
Kiingereza Characters
Angalia
 • Tamthiliya
 • Hadithi Fupi
 • Riwaya

Fasihi Andishi hutumia wahusika wanadamu, kinyume na Fasihi Simulizi ambayo hutumia wahusika changamano (watu, wanyama, mazimwi n.k). Kunazo aina kadhaa za wahusika katika kazi ya fasihi andishi kama vile: tamthilia, riwaya na hadithi fupi.

Aina za Wahusika

 1. Wahusika Wakuu ⇒ hawa ni wahusika ambao wanahusishwa na takribani visa vyote katika riwaya/tamthilia. Wahusika huhusishwa kutoka mwanzo hadi mwisho. Aghalabu mhusika mkuu hafi isipokuwa katika trejedia/simanzi au hufa kifo cha ushujaa.
 2. Wahusika Wasaidizi ⇒ hawa ni wahusika wanaosaidia kujenga mhusika mkuu. Hutokeza mara nyingi katika hadithi. Wahusika wasaidizi wanaweza kuwa na visa vyao. Kwa mfano marafiki na aila za wahusika wakuu.
 3. Wahusika Wadogo ⇒ ni wahusika ambao wanafanya kazi ndogo sana katika fasihi kama vile kujenga maudhui au mandhari. Wahusika hawa wakitolewa, riwaya/tamthilia inaweza kuendela bila kubadilika sana. Kwa mfano mwenye duka ambalo mhusika alinunua kitu fulani.
 4. Wahusika Bapa ⇒ hawa ni wahusika wasiobadilika kutoka mwanzo hadi mwisho. Kwa mfano, mhusika mbaya anabakia kuwa mbaya kutoka mwanzo hadi mwisho. Sifa za wahusika bapa huweza kutambulika mwanzoni mwa hadithi/riwaya. Wahusika bapa hawawakilishi sifa halisia za binadamu. Nia yao ni kujenga tabia moja tu.
  Kuna aina mbili za wahusika bapa:
 • Wahusika bapa-sugu – huoenyesha msimamo wao kulingana na masimulizi ya msanii.
 • Wahusika bapa-vielelezo – msimamo wao hutambulika kulingana na majina yao. Msanii hutumia mbinu ya majazi au lakabu kuwapatia wahusika majina yanayolingana na sifa zao. Kwa mfano: Mhusika Rehema ni mwenye huruma na neema kutoka mwanzo hadi mwisho.
 • Wahusika Duara ⇒ mhusika duara hubadilika kitabia katika fasihi. Hawana msimamo thabiti. Hubadilika kulingana na maudhui na mazingira. Kwa mfano, msichana aliyeanza kama mpole na mwadilifu anapobadilika na kuwa mtovu wa nidhamu, kahaba na asiyeshirikiana na mtu yeyote.
 • Wahusika Wafoili ⇒ huwa katikati ya wahusika bapa na wahusika duara. Wanaweza kuchukua msimamo fulani katika maswala fulani lakini pia wanaweza kubadilisha msimamo huo wakati mwingine kulingana na hali. Wahusika hawa hutegemea wahusika duara na wahusika bapa ili kutoa sifa zao. Kwa mfano, wakiishi na mhusika bapa, wanaweza kuchukua msimamo wa mhusika huyo lakini wakikaa sana na mhusika mwengine, wanabadilika. Wahusika hawa aghalabu huwakilisha uhalisi wa binadamu.

 

 • FASIHI
 • Fasihi Simulizi
 • Fasihi Andishi
 • Ushairi
 • Tamathali za Usemi
 • FASIHI SIMULIZI
 • Hadithi / Ngano
 • Nyimbo
 • Maigizo
 • Tungo Fupi
 • FASIHI ANDISHI
 • Hadithi Fupi
 • Riwaya
 • Tamthilia
 • Aina za Wahusika
 • USHAIRI
 • Aina za Mashairi
 • Bahari za Ushairi
 • Uchambuzi

 AINA ZA MANENO

 • Nomino (N)
 • Viwakilishi (W)
 • Vitenzi (T)
 • Vivumishi (V)
 • Vielezi (E)
 • Viunganishi (U)
 • Vihusishi (H)
 • Vihisishi (I)
 • VIJENZI VYA NENO
 • Sauti za Kiswahili
 • Mofimu
 • Viambishi
 • Uainishaji
 • Shadda na Kiimbo
 • UPATANISHO WA SARUFI
 • Ngeli za Kiswahili
 • Ukubwa na Udogo
 • Umoja na Wingi
 • Nyakati
 • Kukanusha
 • Kinyume
 • Viungo Mbalimbali
 • Uakifishaji
 • NGE na NGALI
 • SENTENSI
 • Aina za Sentensi
 • Muundo wa Sentensi
 • Uchanganuzi wa Sentensi
 • Virai na Vishazi