NUKUU 10 MUHIMU ZA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE KUTOKA KATIKA KITABU CHAKE “TUJISAHIHISHE- MEY 1962”

By , in Kavazi on .

  1. “Kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo.”
  1.  “Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu ya mambo kama mafuriko,nzige,kiangazi,n.k., matatizo yao mengi hutokana na unafsi.
  1. Nitasema kweli daima.Fitina kwangu ni mwiko.
  1. Wengine humwona mwenzao anafanya kosa.Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya.Lakini hawanyamazi kimya kabisa! Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri siri.
  1. “Wengine hugawa watu katika mafungu.”Fulani” japo akifanya kosa kubwa sana hasemwi.Lakini “Fulani” wa pili akifanya kosa japo dogo, kosa lile hukuzwa likawa kama mlima Kilimanjaro.”
  1. “Ukweli una tabia moja nzuri sana.Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki.Kwake watu wote ni sawa.”
  1. “Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua kuwa hana makosa.”
  1. “Kosa jingine ni kutojielimisha.Kanuni yetu moja inasema: Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.Wengine hufikiri kuwa kujielimisha ni kujua kusoma na kuandika.Hilo ni kosa, lakini si kubwa kama la pili.Wengi wetu, hasa baadhi ya viongozi, hufikiri kuwa tunajua kila kitu na hatuna haja kujifunza jambo lo lote zaidi.”
  1. “Watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu, wala hawana haja kujifunza zaidi.Hii ni tabia mbaya ambayo huzuia kabisa maendeleo.”
  1. “Uvivu wa kutumia akili unaweza kutufanya tutumie dawa kuondoa matatizo ambayo si ya dawa hata kidogo.Daktari asipojua ugonjwa wangu na sababu zake hawezi kujua dawa yake.Akinipa dawa nikapona, atakuwa kaniponya kwa bahati tu, kwa desturi daktari wa namna hiyo hawezi kumponya mgonjwa, na ni daktari wa hatari sana.”
Facebook Comments
Recommended articles