Namba ya moduli 3: Uhamasishaji wa mawasiliano katika lugha ya ziada : Sehemu ya 1: Kuandaa mazingira asilia kwa ajili ya mazoezi ya lugha

By , in DIPLOMA/CHETI on .

Sehemu ya 1: Kuandaa mazingira asilia kwa ajili ya mazoezi ya lugha

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuwasaidia wanafunzi kufanya mazoezi ya muundo wa lugha katika mazingira asilia?

Maneno muhimu: usimamizi wa darasa; michezo; mapishi; maelekezo; mchakato

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Kutumia uongozi/utawala wa darasa kuwasaidia wanafunzi kujifunza lugha ya ziada;
  • Kutumia michezo na shughuli za kila siku kuimarisha wanafunzi kuhusu stadi za lugha na msamiati.

Utangulizi

Wanafunzi wako wana fursa gani kupitia –redio, vitabu, magazeti, wazungumzaji wa lugha na televisheni kwa lugha ya ziada ukilinganisha na ile inayotumika nyumbani?

Jawabu linaweza kuwa ni ‘fursa ndogo’. Wanaisikia na kuitumia kila siku darasani shuleni. Hii ina maana kuwa unawajibika kuwapa fursa ya kutumia lugha ambayo itawasaidia wanafunzi:

Kuitumia na kuwa wazungumzaji hodari katika matumizi ya msamiati mpya na muundo wa sarufi;

Kuwasiliana kwa kutumia lugha ya mazungumzo katika mazingira ya kijamii;

Kuimarisha na kuendeleza stadi zao za kusoma na kuandika.

Yote haya yanahitaji tafakuri ya hali ya juu, na upangaji na stadi makini. Sehemu hii itakupatia mikakati na mbinu za kukusaidia.

Somo la 1

Ukiwa mwalimu, utatoa maelekezo ya aina mbalimbali kwa wanafunzi wako.

Unaweza kutumia maelekezo ya kila siku kukuza msamiati mpya na stadi ya usikilizaji katika lugha ya ziada. Maelekezo hutumia muundo wa amri wa kitenzi. Wakiona muundo wa kuamuru katika kitenzi mara kwa mara katika mazingira yanayoleta maana, wanafunzi wataanza kuelewa na kujifunza muundo huo.

Wanafunzi wanapojifunza lugha mpya, usikilizaji huendelea haraka kuliko mazungumzo. Wanahitaji nafasi kubwa ya kusikiliza na kujibu katika lugha mpya. Katika hatua za mwanzo za ujifunzaji lugha (na baadaye pia), unaweza kutumia shughuli ambazo zinawahitaji kujibu kwa vitendo lakini haiwahitaji kujibu (kwa maneno) hadi wanapojisikia kuwa na uhakika zaidi. (Hii mara nyingi huitwa ‘mawazo ya mbinu jumuishi’- Angalia Nyenzo-rejea 1: Mawazo ya mbinu jumuishi .)

Uchunguzi kifani ya 1: Uongozaji wa darasa katika Kiingereza

Bibi Mujawayo anafundisha darasa la kwanza mjini Kigali, Rwanda. Anatumia Kiingereza katika uendeshaji wa darasa.

Asubuhi husalimiana na wanafunzi katika lugha zao za nyumbani, na huwauliza habari zao za nyumbani katika lugha zao.

Baada ya baraza, huanza kutumia Kiingereza darasani, ‘Pangeni mstari wanafunzi’ na huwaelekeza barazani, mahali ambapo wanapaswa kujipanga. ‘Ingia darasani’ husema huku akiwaonesha vitendo vya kuwaelekeza kuingia ndani. ‘Simameni karibu na madawati yenu.

Mwalimu na wanafunzi husalimiana kwa kutumia Kiingereza. Husema ‘Kaeni chini.

Hurejea tena katika lugha yao ya nyumbani ili kuanza kusimulia hadithi hadi anapowaweka katika vikundi, kwa ajili ya shughuli mbalimbali.

Kila kikundi kina alfabeti. Husema kwa Kiingereza kwa kunyoosha mikono A na B nyosheni mikono. Kwa kuonesha katika kisanduku huwaambia ‘Chukueni vitabu kutoka katika kisanduku.’ ‘Kaa chini, na msomee mwenzio.’ Kama wanaonekana kutoelewa, wanaigiza wanachopaswa kufanya.

Baadaye hutoa maelekezo zaidi kwa Kiingereza, bila kutafsiri. Vikundi viwili vinapaswa kuonesha hadithi yao na kikundi kingine watasoma pamoja naye katika lugha yao ya nyumbani kutoka katika kitabu kikubwa.

Bibi Mujawayo anagundua kuwa wanafunzi wake wanaanza kuelewa haraka maelekezo katika Kiingereza, na mara huanza kusema maneno.

Shughuli ya 1: Simple Simon husema

Katika mchezo huu unaojulikana sana, wanafunzi hufuata kwa vitendo maelekezo. Unaweza kutumia njia hii kuongeza msamiati na stadi ya usikilizaji katika maeneo mbalimbali ya masomo.

Kiongozi hutoa amri na kuonesha vitendo wakati huohuo. Wanafunzi wanapaswa kufuata amri hiyo kutoka kwa Simple Simon. (Unaweza kubadilisha jina hili kwa kutumia jina la mtu ambaye ni mashuhuri kijijini.) Mchezo huchezwa kama hivi:

Kiongozi: Simple Simon anasema , ‘Ruka!’ (Kiongozi anaruka.)

Wanafunzi wanaruka.

Kiongozi: Simple Simon husema, ‘Shika vidole vya miguu !’ (Kiongozi anashika vidole vya miguu)

Wanafunzi wanashika vidole vya miguu.

Kiongozi: ‘Kuna pua yako!’ (Kiongozi anakuna pua yake.)

Baadhi hukuna pua zao. Wengine hawafanyi hivyo. Wale ambao wamekuna pua zao wanatoka (kwa sababu amri haikutoka kwa Simple Simon Na kuendelea hivyo….. Tumia maelekezo rahisi kwa wanafunzi wanaojifunza lugha ngeni, maelekezo magumu kwa wale ambao ni wanaielewa lugha zaidi. Anza polepole, lakini endelea kwa kasi zaidi. Mshindi ni yule aliyebaki.

Somo la 2

Ni jambo muhimu kuwapa wanafunzi nafasi ya asilia ya kuendeleleza stadi zao katika lugha ya ziada. Hapa tunapendekeza njia ambazo unaweza kuzitumia kushirikisha jamii na kutumia stadi za asilia na busara kama njia ya Nyenzo-rejea ya shughuli za darasani.

Umeona, katika Uchunguzi-kifani 1 na shughuli 1, namna maelekezo ya kila siku yanavyoweza kuleta muktadha asilia wa ujifunzaji lugha. Wanafunzi walisikiliza na kuonesha uelewa kwa vitendo. Katika sehemu hii tunashauri utumie mapishi ya asilia na mchakato kama njia ya muktadha wa mafunzo, ukiwapa nafasi wanafunzi kuzungumza (na kuandika) na vilevile kusikiliza.

Shughuli zilizotumika hapa zitaendelezwa mbele katika sehemu ya 5, ambapo darasa lako litaanza kutayarisha kitabu cha mapishi.

Uchunguzi kifani ya 2: Wanafunzi watu wazima hujifunza kwa vitendo

Baadhi ya wanafunzi wa Kiswahili walitumia muda wa siku nzima mjini kama sehemu ya kozi yao. Kila mwanafunzi alikuwa akifuatana na msaidizi wa lugha ambaye alikuwa mzungumzaji wa Kiswahili. Wasaidizi waliwasaidia wanafunzi walipokuwa wakijaribu lugha waliojifunza; wakinunua mboga kutoka kwa wauzaji wa barabarani na kuzungumza na familia zilizokuwa zinawasaidia.

Sehemu muhimu ya siku hiyo ilitumika kupika chakula. Mwanafunzi alipaswa kupika chakula, akielekezwa na msaidizi wa lugha. Upikaji ulikuwa umefanyiwa mazoezi na kuigizwa, na mara nyingi kuandikwa au kurekodiwa katika kinasa sauti, wiki moja kabla darasani. Wanaume walipewa maelekezo ya kutayarisha moto, wakati wanawake walitakiwa kupika chakula kama ugali, ndizi na nyama na kabichi. Walizungumzia pia jinsi ya kubadilishana nafasi ili kuwasaidia kujifunza lugha.

Wakati chakula kilipokuwa tayari, nyimbo za Kiswahili ziliimbwa, na wanafunzi walijifunza michezo ya asili ya Kiswahili ya watoto. Baada ya vyombo kusafishwa, kundi la wanafunzi wenye furaha na uchovu walijipakia katika teksi na kurudi nyumbani.

Shughuli ya 2: Kujifunza kwa vitendo vya shughuli za kijamii

Waambie wanafunzi wako kwamba watakwenda kutafuta jinsi shughuli za nyumbani zinavyotekelezwa na kueleza njia za mchakato katika lugha ya ziada. Watake wanafunzi kuleta taarifa kutoka nyumbani au mkaribishe mwenyeji shuleni kutoka katika jamii ili kuonesha stadi.

Wagawane wanafunzi katika jozi au katika vikundi (vikundi hivi vinaweza kuwa vya mchanganyiko wa uwezo tofauti), kufanya kazi, na ikiwezekana kuandika hatua za moja ya mchakato katika lugha ya ziada. Zungukia darasa na kuwasaidia msamiati mpya ambao watuhitaji.

Vipe vikundi muda wa kukariri na kufanya mazoezi ya hatua zinazotumika, katika kujitayarisha kuwasaidia wengine. Wanaweza kukusanya toka nyumbani vitu vinavyohitaji katika mchakato huo.

Siku inayofuata, mpe nafasi mwanafunzi mmoja kutumia lugha ya ziada kuelekeza mjumbe wa kikundi kingine, wakati huohuo darasa likiangalia k.m. kusafisha nyumba.

Wanafunzi wamefanyaje katika shughuli hiyo?

Unaweza kuitumia njia hiyo katika mchakato mwingine ili kukuza msamiati wao?

Kama jibu ni ndiyo, vipi?

Somo la 3

Lugha hutumika kwa mawasiliano, na ni muhimu uwe na sababu za wanafunzi kuzungumza, kusikiliza, kusoma na kuandika katika lugha ya ziada. Hii si rahisi ukiwa katika mazingira ambapo lugha ya ziada haizungumzwi. Hata hivyo, lugha ya ziada inaweza kuwa lugha ya vitabu na ya mawasiliano ya maandishi.

Duniani kote watu hubadilishana mawazo kuhusu ‘jinsi ya kufanya shughuli’; kwa mfano wanapeana maelezo ya upishi au sulubu ya utengenezaji wa nguo. Umekwisha kulifanya hili kwa mazungumzo; sasa wanafunzi wanaweza kufanya kwa maandishi. Waoneshe wanafunzi wako muundo wa kawaida wa maandishi ya maelezo ya upishi, katika lugha ya ziada. Maelezo ya upishi huandikwa kama mfululizo wa maelekezo.

Tunapoandika maelezo ya upishi, au kuelezea mchakato wake, hatujali nani atatenda, bali tunajali kuwa tendo linatendeka.

Uchunguzi kifani ya 3: Kuchora na kuandika maelezo ya upishi

Katika shule iliyopo Njombe, kusini mwa Tanzania wanafunzi wamekuwa wakibadilishana maelezo ya upishi. Walitaka kuchora maelezo ya upishi katika michoro na kubadilishana na marafiki zao. Bibi Masawda, mwalimu wao, alifikiri kuwa itakuwa vizuri kwao kujua njia mbalimbali za kuwasilisha taarifa. Aliwaonesha jinsi ya kuchora michoro ya kuonesha mifumo. Mara wanapokuwa wamekwisha chora na kuweka maelezo katika mchoro wa mfumo, waliandika mchakato kama pia maelezo (angalia kwa mfano Nyenzo-rejea 2: maelezo ya upishi ).

Bibi Masawda alijadiliana na wanafunzi wake ni kipi walichokiona ni rahisi kufanya, na kwa nini. Zaidi ya theluthi mbili za darasa waliona kuwa chati ya mfumo ilikuwa inafurahisha na ilikuwa rahisi kutengeneza kwa sababu waliweza kubadilisha maelezo ya upishi katika hatua na mchoro uliwasaidia kukumbuka na kuelewa maneno.

Bibi Masawda alitumia wazo hili la chati za mifumo katika masomo mengine, kwa kuwa hili lilionekana kuwasaidia wanafunzi wake kukumbuka zaidi.

Kwa mfano, katika somo la jiografia, alitumia chati ya mfumo kuandika kuhusu maelekezo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, na wanafunzi walichora picha za alama za mipaka ili kuifanya iwe rahisi kukumbuka maneno.

Shughuli muhimu: Kuandika maelezo ya upishi na mchakato wa maelezo

Watake wanafunzi kutafuta jinsi ya kupika vyakula vyao wanavyovipenda sana kutoka nyumbani na shirikiana mawazo hayo na darasa.

Wajulishe wanafunzi wako muundo wa maandishi ya mapishi kabla hawajafanya mfano wao (Angalia Nyenzo-rejea 2)

Watake wanafunzi kuandika maelezo ya mapishi vizuri, kila mmoja akijiandikia maelezo, na mwingine akitumia maelekezo ya mapishi ya kitabu cha darasani. Maelezo ya pili yanaweza kutumia muundo tofauti na ule wa kwanza (angalia Nyenzo-rejea 2 kwa ajili ya mitindo).

Watake wanafunzi wako wabadilishane kazi zao na kujadili maelezo ya mapishi.

Nyenzo-rejea ya 1: Mjumuisho wa mwitikio wa vitendo

Usuli/taarifa ya mwanzo/uelewa wa mwalimu

Kwa toleo la mtandaoni:

http://www.tpr-world.com/

Webu inatoa taarifa kuhusu mjumuisho wa mwitikio wa vitendo kama njia ya kufanya kazi katika ujifunzaji lugha. Kuna maelezo mengine ambayo unaweza kufuatilia.

Kwa ajili ya kuhariri matini

Unaweza kuwajulisha wanafunzi wako muundo wa lugha mbalimbali kutokana na vitendo vya kimchezo ambavyo vinawahitaji kufuata maelekezo kwa vitendo (mjumuisho wa mwitiko wa vitendo). Hapa kuna mifano ya namna ya maelekezo ambayo unaweza kuwapa wanafunzi. Weka mkazo katika aina moja ya maelekezo kwa wakati mmoja, ili wanafunzi waelewe jinsi lugha inavyofanya kazi

Mtingishiko wa mwili

Simama.

Cheka.

Kohoa.

Lia.

Gonga meza.

Vitendo na vifaa

Onesha mlango.

Okota kalamu.

Funga dirisha.

Nusa ua.

Onesha mlima.

Onesha mwanamke anayetengeneza keki.

Vitendo, vifaa na watu

Chukua kalamu na umpe Nuru

Tafuta kitabu na unipe

Okota karatasi na mpe Thimba.

Ongeza vimilikishi

Mpe Aida kitabu cha Thimba.

Leta peni ya Nuru kwangu

Mpe Kito kitabu chake.

Mpe Eshe miwani yake.

Hiki na kile; hapa na pale

Mpe hiki Adia.

Tafuta kile kutoka kwake.

Tafuta kalamu na iweke hapa.

Tafuta kitabu na kiweke pale.

Kuhusisha nafasi

Weka kalamu katikati ya vitabu viwili.

Weka kalamu karibu na rula.

Weka kifutio ndani ya kisanduku.

Weka rula juu ya kisanduku.

Jumlisha namba, ziweke rangi na ukubwa

Weka kalamu mbili ndani ya kisanduku.

Chukua mawe matatu nje ya kisanduku.

Okota kalamu nyekundu na mpe Thimba.

Weka kitabu cha kijani mezani.

Chukua kitabu kidogo na mpe Nuru.

Weka kitabu kikubwa ndani ya kisanduku.

Maelekezo na maelezo, pamoja mazungumzo kiasi

Fanya na kusikiliza

Wanafunzi wanafanya tendo. Mwalimu (au mwanafunzi mwingine) husema wanachofanya (k.m. ‘Umesimama.’)

Sikiliza na kufanya

Mwalimu (au mwanafunzi mwingine) anamuelekeza mwanafunzi (k.m. Simama.’ Mwanafunzi anafuata amri, kwa kufanya tendo.

Sahihi au si sahihi

Mwanafunzi anajifunza kusema ‘sahihi’ na ‘si sahihi’. Mwalimu (au mwanafunzi mwingine) anatenda tendo, na kutoa tamko ‘lililo sahihi’ au ‘lisilo sahihi’ kuhusu anachofanya (k.m. ‘Nimekaa.’) Wanafunzi wanasema ‘kweli’ au ‘si kweli’

Sikiliza, igiza na tenda

Mwalimu (au mwanafunzi mwingine)anamuelekeza mwanafunzi. Mwanafunzi anarudia yaliyosemwa na halafu anatenda amri hiyo.

Eleza, sikiliza na igiza

Mwanafunzi hutenda na kueleza wanachofanya (k.m. ‘Nimesimama.’) Mwalimu ( au mwanafunzi mwingine) anaeleza kile kilichosemwa na mwanafunzi na anatekeleza kitendo.

Kwenda nje au kutumia picha ili kuongeza msamiati

Mwanzoni, unahitaji kutumia maneno yanayojulikana na maelekezo mapya. Baada ya msamiati wa darasa kujulikana, unaweza kutumia msamiati wa nje ya darasa, k.m.:

Gusa jani.

Onesha mbingu.

Unaweza pia kuongeza msamiati kwa kutengeneza kadi zenye maneno au picha, k.m. picha za aina ya chakula:

Chukua nyama na mpe Nuru.

Tafuta mkate wa Kapuki na unipe.

Zimetolewa kutoka: Total Phsyical Response Worldwide, Website

Nyenzo-rejea 2: Mapishi

Nyenzo ya Mwalimu ya kutumia na wanafunzi kwa ajili ya kupanga/kurekebisha

Hapa kuna njia tatu za kuonesha mapishi ya aina moja

Kutengeneza supu ya pilipili (mchoro mfumo)

Osha na kata nyama katika vipande vidovidogo

Pika/Chemsha nyama katika maji ya moto

Kata vitunguu, nyanya na pilipili

Weka vitunguu vilivyokatwa, nyanya na pilipili kwenye nyama na koroga

Tia maji mengi ya kutosha kiasi cha kufunika mchanganyiko na iache ichemke katika moto mdogo

Safisha, osha, katakata na kuongeza mboga nyinginezo

Iache ichemke polepole hadi nyama inapokuwa laini

Kula kwa wali

Kutengeneza supu ya pilipili (maelezo ya mchakato)

Wakati supu ya pilipili unapotayarishwa, 0.5 ya nyama inasafishwa na kukatwa katika vipande vidogo vidogo. Nyama inapikwa katika maji moto, na vitunguu, nyanya, mboga na pilipili zinaongezwa. Zinachemshwa hadi zinakuwa laini; halafu zinaliwa kwa wali.

Kutengeneza supu ya pilipili (viungo na mbinu)

Viungo:

0.5 kg ya nyama (iliyooshwa na kukatwa katika vipande vidogo)

Vitunguu 4

Nyanya 8

Pilipili zilizokaushwa 4 hadi 5

Mboga nyinginezo, zinazopatikana

Lita 1.5 ya maji

Mbinu: Weka maji katika sufuria na yachemshe Ongeza vipande vya nyama na chemsha Ongeza vitunguu vilivyokatwa, nyanya, pilipili na mboga nyinginezo, koroga na acha ichemke.

Recommended articles