Namba ya moduli 3: Uhamasishaji wa mawasiliano katika lugha ya ziada : Sehemu ya 2: Njia zijengazo ufasaha na usahihi

By , in DIPLOMA/CHETI on . Tagged width:

Sehemu ya 2: Njia zijengazo ufasaha na usahihi

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuwasaidia wanafunzi kujenga hali ya kujiamini katika utumiaji wa miundo ya lugha mahsusi?

Maneno muhimu: vitenzi; vielezi; urudiaji; mashairi; nyimbo; uhariri

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umewaongoza wanafunzi wako katika kuwapa ujuzi wa kudhibiti miundo ya lugha ya ziada;
  • umetumia urudiaji, nyimbo, mashairi na hadithi katika kufundisha miundo ya lugha;
  • umewasaidia wanafunzi wako kusimamia kazi yao wenyewe kadri wanavyotafuta maana na matumizi sahihi ya vitenzi.

Utangulizi

Ukiwa mwalimu wa lugha ya ziada, mara zote unatakiwa utafute mbinu mpya za kuwapa wanafunzi wako uzoefu wa lugha hiyo. Kama wanapewa fursa za kujizoeza lugha hiyo, matumizi yao ya lugha hiyo yatakuwa fasaha na sahihi zaidi.

Sehemu hii inakupatia mazoezi yanayofaa ambayo yanalenga katika kauli na miundo mahsusi.

Kumbuka kwamba vitendo utakavyovichagua ni lazima viwe vinafahamika kwa wanafunzi, ama kitendo chenyewe, au katika maisha yao (inapendelewa viwe vinavyohusu sehemu zote mbili).

Somo la 1

Kuwapatia wanafunzi wako fursa za kutumia miundo ya lugha mahsusi tena na tena ili waweze kuimudu, kunahitaji kuwa tendo la kufurahia.

Kuna nadharia isemayo kwamba watu hujifunza lugha kwa kuiga na urudiaji. Hapo zamani, kozi nyingi za lugha zilitumia sehemu kubwa ya urudiaji (mazoezi ya kurudiarudia). Siku hizi inadhaniwa kwamba vitendo vinavyowahusisha wanafunzi katika mawasiliano ‘halisi’ vinawasaidia zaidi kuliko urudiaji usiokuwa na maana. Hata hivyo, urudiaji bado unaweza kuwa wenye manufaa endapo wanafunzi watachomeka maana halisi katika sentensi. Inasaidia kama watawekewa urudiaji katika muziki.

Jaribu mawazo yaliyomo katika Uchunguzi-kifani 1 na Shughuli 1 kupima nadharia hizi.

Uchunguzi kifani ya 1: Urudiaji katika lugha unaohusu hadithi kutoka gazetini

Bwana Gasana anafundisha Kiingereza Darasa la 4 huko Butare, Rwanda. Mauaji yalitokea katika jiji lao, saa 2 usiku, siku mbili zilizopita. Aliwaonesha wanafunzi wake ripoti ya mauaji hayo kutoka kwenye gazeti. Alizungumza na wanafunzi wake (kwa lugha ya nyumbani) kuhusu jinsi askari wa upelelezi wanavyouliza watu wanapojaribu kutafuta mhalifu. Halafu akaweka sampuli ya swali na jibu ubaoni, kwa Kiingereza:

Q: Ulikuwa unafanya nini Jumanne saa 2 usiku, Kigeri?

A: Nilikuwa ninatazama runinga.

Aliwauliza wanafunzi wachache swali hilo hilo, ili kuhakikisha watatoa majibu yao wenyewe kwa utaratibu sahihi. Kisha, aliwaweka wanafunzi katika makundi ya wanafunzi sita sita. Kila mwanafunzi alitakiwa kuuliza swali kwa wanakikundi wake wengine watano, ambao kila mmoja atatoa jibu lake. Bwana Gasana aliwahimiza wanafunzi kusahihishana, na alitembea kuzunguka darasa, kusikiliza na kuongoza makundi.

Alimwambia kila mwanafunzi aandike ‘ripoti ya askari wa upelelezi’ kuhusu kundi lake. Kila moja kati ya sentensi sita zilionekana katika muundo ufuatao:

Saa 2 usiku Muteteli alikuwa anacheza na kaka yake.

Saa 2 usiku Erisa alikuwa anaandaa chakula.

Nyenzo-rejea 1: Miundo mbadala ya somo inatoa sampuli zilizotumiwa na Bwana Gasana akiwa na wanafunzi wake wakubwa wa Darasa la 5.

Shughuli ya 1: Urudiaji katika bei mbalimbali

Tafuta au tengeneza tangazo la mauzo au orodha ya bei za mbogamboga za mahali hapo, ukionesha mapunguzo ya bei (angalia Nyenzo-rejea 2: Tangazo la bei kwa mifano). Kabla ya somo, tengeneza nakala kubwa ya tangazo au orodha ya bei ubaoni, au tayarisha tangazo moja au orodha ya bei kwa kila kundi katika darasa lako.

Andika mfuatano ufuatao wa swali na jibu ubaoni.

Q: .…. ni bei gani ?

A. Kabla ilikuwa shilingi …., lakini sasa ni shilingi …. tu.

 

Q: Hizo …. ni bei gani?

A: Kabla zilikuwa shilingi …., lakini sasa ni shilingi …. tu.

 

Wakati wa somo, onesha baadhi ya bidhaa, huku ukiuliza swali kulingana na bidhaa, na kuwaambia wanafunzi wachache wajibu.

Kisha, waweke wanafunzi katika makundi, ili waulizane na kujibizana kwa utaratibu huo huo.

Waambie kila kundi watunge na kuigiza wimbo wenye mistari yenye muundo huu: Kabla, hiyo …. ilikuwa shilingi …., lakini sasa ni shilingi …. tu.

Wanafunzi wako wamejifunza nini kutokana na shughuli hizi? Unajuaje? Je, utatumia aina hii ya zoezi tena?Kwa nini utalitumia tena, au kwa nini hutalitumia tena?

Somo la 2

Katika ufundishaji wa lugha ni muhimu kuzingatia maana ya lugha, kwa kukazia umuhimu wa mawasiliano, lakini wakati huohuo, kukazania ukuzaji wa uwezo wa kisarufi wa wanafunzi. Shughuli 2 inatoa mfano wa jinsi ya kutumia shairi la kusifu lililoandikwa kwa Kiingereza kufanyia kazi na wanafunzi kwa upande wa vitenzi na vielezi. Aina hii ya kazi inaweza kufanywa kwa kutumia matini za viwango mbalimbali, kwa kuzingatia viwango vya miundo mbalimbali. Vilevile, hakikisha kwamba unazingatia maana ya kipande cha maandishi, ingawa usitumie maana hiyo kwa urahisi tu kama nyenzo ya kufundishia sarufi. Ukiwa na wanafunzi wa umri mdogo, mkazo uwe kwenye maana na ufurahishaji.

Kwa kawaida hadithi hutumia njeo iliyopita, wakati maelezo aghalabu hutumia njeo iliyopo. Haya ni mazingira mazuri ya kuwapatia wanafunzi wako mazoezi ya njeo.

Kama hufundishi Kiingereza, fikiri kuhusu mada ya kisarufi ya lugha unayofundisha iliyo ngumu kwa wanafunzi, na utumie Shughuli 2 kulingana na lugha hiyo.

Uchunguzi kifani ya 2: Kujadili sarufi katika warsha ya walimu

Katika warsha iliyofanyika Tanga, walimu walikuwa na majadiliano changamfu kuhusu sarufi. Bwana Thomas Changae alishuhudia kuwa alisoma kwamba sarufi ni mifupa au kiunzi cha lugha na maneno mengine ni nyama. Vyote viwili mifupa na nyama vinachangia katika maana. Walimu walikubaliana kwamba wanafunzi wanahitaji kuendeleza welewa wao wa jinsi miundo ya lugha inavyofanya kazi, lakini pia walilalamika kuhusu wanafunzi kutopenda masomo ya sarufi.

Bi Susan Mkari alisema alijaribu kuhusisha shughuli ambazo zilikazia kwenye miundo ya lugha wakati wanafunzi wake wa Darasa la 6 wanaposoma hadithi na mashairi ya kuvutia. Kwa mfano, baada ya kufanya marudio ya njeo kuu za kitenzi cha Kiingereza, aliwaambia wanafunzi kutoa maoni yao kuhusu sababu za mwandishi wa hadithi au shairi kutumia njeo iliyopita, ya sasa au ya wakati ujao. Kisha, aliwaambia wanafunzi kuamua njeo ipi ya kitenzi au njeo zipi wanazihitaji katika kuandika hadithi au shairi lao wenyewe ili kuleta mvuto zaidi kwa wasomaji wao.

Kwa kuwa Kiingereza ni lugha ya ziada kwa wanafunzi, Bi Mkari hutengeneza chati kubwa nyuma ya kalenda za zamani. Hii huwapa wanafunzi taarifa kuhusu njeo mbalimbali za vitenzi kuhusu wakati uliopo, uliopita na ujao. (Angalia Nyenzo-rejea 3: Chati za njeo za kitenzi kwa mfano rahisi ambao unaweza kutumia na wanafunzi wako.) Anawahimiza wanafunzi wake kusoma chati hizi wanapoandika.

Shughuli ya 2: Mchezo wa ugunduzi wa kitenzi na kielezi

Toa nakala za Nyenzo-rejea 4: Shairi la kusifu . Mahali ambapo mashine za kutolea nakala hazipo, nakili shairi ubaoni au sehemu ya nyuma ya kalenda.

Mara wanafunzi watakaposoma shairi na kulielewa, waache wafanye kazi kwenye makundi kwa kutafuta vitenzi vyote vilivyomo katika shairi. Wakumbushe wanafunzi kwamba vitenzi vingi ni maneno ‘yanayoonesha kutenda’. Waambie kila kundi kuripoti mbele ya darasa kuhusu vitenzi katika ubeti mmoja (angalia Nyenzo-rejea 5: Vitenzi na vielezi katika shairi ).

Waulize wanafunzi vitenzi viko katika njeo gani. Katika ubeti wa 1 na 2, vitenzi viko katika njeo iliyopo; baadhi ya vitenzi katika ubeti wa 3 viko katika njeo ijayo na vingine katika ubeti wa 4 viko katika njeo iliyopita. Kwa wanafunzi wa kiwango cha juu zaidi, jadili kwa nini njeo hizi zilitumika.

Waulize kuna tofauti gani kwenye maana inayosababishwa na utumiaji wa njeo tofauti na athari yake kwa shairi?

Unaweza kutumia mashairi na hadithi nyingine kwa njia zinazofanana na hizi.

Somo la 3

Yumkini utakuwa umegundua kwamba ni vigumu, wakati mwingine, kusahihisha kazi zilizoandikwa na wanafunzi, kwa sababu kuna makosa mengi sana ya lugha ndani yake. Hutakiwi kuwavunja moyo wanafunzi wako kwa kufanya masahihisho mengi kupita kiasi. Lakini pia hutakiwi kuwaacha waendelee na tabia mbaya. Tutatatuaje tatizo hili?

Njia mojawapo ni kuunganisha maana na miundo ya lugha. Andaa zoezi la kuandika ambalo lina maana kwa wanafunzi. Wahimize wahariri kazi zao kabla hawajazikusanya. Unaweza kuwaambia, wawili wawili, waandike ili waweze kusaidiana. Kisha wanaweza kurudishiwa kazi zao bila kuwa na maoni mengi ya kiusahihishaji.

Unaposahihisha kazi zao, zingatia kwenye maana na jambo linalopendelewa. Uzingativu wa pili, kazia kwenye kipengele kimoja cha muundo wa lugha –tahajia au pengine njeo za kitenzi au viunganishi. Kwa njia hii, maoni ya kiusahihishaji huwa si mengi na huelekeza sehemu maalum, na wanafunzi wana uwezekano mkubwa wa kuyaona na kuyazingatia.

Uchunguzi kifani ya 3: Kubadilishana uzoefu katika ‘Gurudumu la Waandishi’

Kozi ya kundi la walimu waliomo kwenye mafunzo kazini mjini Tabora walikuwa wakijaribu kuboresha uandikaji wao wenyewe. Wakufunzi waliwahimiza kuunda ‘Gurudumu la Waandishi’, ambako watasomeana kazi zao na kupeana maoni. Waliandika kuhusu uzoefu wao –kumbukumbu za utotoni, watu na mahali pa ajabu wanapopakumbuka, mambo ambayo hawatayasahau.

Wakufunzi waliwaongoza katika utoaji wa maoni, kwa kutumia vigezo mbalimbali kutegemeana na kitu kilichokuwa kimeandikwa. Hii hapa ni mifano:

Je, mwandishi anakisema akitakacho kwa ufasaha? Je, kuna sehemu ambazo zinahitaji kufafanuliwa?

Sehemu zipi zinavutia? Kitu gani kinazifanya zivutie? Sehemu gani zinachusha? Zinawezaje kuboreshwa?

Je, kila aya ina wazo kuu? Je, kuna baadhi ya mawazo makuu yanayohitaji kuendelezwa zaidi? Je, aya zinahitaji kupangwa tena?

Je, sentensi ni kamilifu? Je, ni ndefu sana au fupi sana? Je, zimewekewa alama za uandishi kwa usahihi? Je, tahajia za maneno ni sahihi?

Kazi hiyo imeandikwa kwa kutumia njeo ipi? Kagua ili kuhakikisha kwamba kila kitenzi kiko katika njeo stahili au kama kuna sababu ya msingi ya kutumia njeo nyingine.

Kitabu kiliwekwa pamoja kwa kujumuisha maandiko ya walimu hawa ambacho kilshirikishwa kwa familia na rafiki. Walimu waliamua kwamba baadhi ya mawazo haya yanaweza kutumika darasani, vikabadilishwa kulingana na umri na uwezo wa wanafunzi wao.

Shughuli muhimu: Uhariri wa kujifanyia mwenyewe na wa kubadilishana na wanadarasa kwa lengo la kuboresha uandishi

Waambie wanafunzi wako waandike kuhusu jambo linalotokana na uzoefu wao wenyewe. Jadili mawazo yatakayojitokeza ili kusisimua ubunifu wao. Kwa mfano, wanaweza kueleza kitu ambacho ni mali yao au mtu wa kuvutia wanayemfahamu. (Kwa kuwa uandishi huu ni wa kutoa maelezo, ni yumkini wakatumia njeo iliyopo.) Wanaweza kusimulia hadithi ya kutisha au tukio la kusisimua, au jambo la kijumuiya. (Kwa vile uandishi huu unajumuisha hadithi au masimulizi, ni yumkini wakatumia njeo iliyopita.) Wanafunzi wengine wanaweza kuona inasaidia zaidi kufanya kazi hii wawili wawili.

Kisha, waambie wafanye kazi katika makundi madogo madogo, kwa kusomeana maandishi yao. Watake watumie mojawapo au zote mbili kati ya seti za maswali zifuatazo ili kutoa maoni kwa kila kundi:

  • A.Sehemu zipi zinavutia? Kitu gani kinazifanya zivutie? Sehemu zipi zinachusha? Hizi zinawezaje kuboreshwa?
  • B.Uandishi huu umetumia njeo gani? Kagua ili kuhakikisha kwamba kila kitenzi kiko katika njeo stahili AU hakikisha kuwa kuna sababu ya msingi ya kutumia njeo nyingine.

Baada ya kupata maoni kutoka kwenye makundi, kila kundi liandike tena kazi yao. Kusanya kazi hizo, na tumia vigezo sawa kusahihisha kazi zote.

Utaratibu huu ulifanikiwa kwa kiasi gani? Je, utaurudia tena?

Je, hali ya uandishi wa wanafunzi wako ilipata ubora? Unajuaje?

Nyenzo-rejea ya 1: Miundo mbadala ya somo – iliyotumiwa na Bwana Gasana

Usuli/taarifa ya mwanzo/uelewa wa mwalimu

Mfuatano wa swali na jibu

S:     Je, Bibi Yuhi, ulisikia mlio wa bunduki?

J:      Ndiyo, wakati huo tulikuwa tunakula cha jioni.

au

S:     Je, Bwana Mulifi, ulisikia mlio wa bundukit?

J:      Hapana, wakati huo nilikuwa ninasafiri kwenda Nyanza.

Miundo ya ripoti ya askari wa upelelezi

Bibi Yuhi alisikia mlio wa bunduki wakati walipokuwa wakila chakula cha jioni.

au

Bwana Mulifi hakusikia mlio wa bunduki kwa sababu alikuwa safarini kwenda Nyanza.

Nyenzo-rejea  2: Tangazo la mauzo

Nyenzo ya Mwalimu ya kutumia na wanafunzi kwa ajili ya kupanga/kurekebisha

Kwa wanafunzi wenye umri mkubwa, unaweza kutumia mfuatano wa kiwango cha juu zaidi, kama vile:

S: Tazama shati ile! Hiyo ni bei rahisi.

J: Ndiyo, walikuwa wanaliuza kwa ShzT …. wiki iliyopita!

au

S: Ninakuonea huruma ulinunua hizo jeans wiki iliyopita!

J: Ndiyo, natamani ningesubiri punguzo la bei. Nimepoteza ShzT ….

Orodha ya bei za mboga mboga

Onesho hili linaweza kuwa lenye manufaa kama uko eneo la vijijini ili kuunda mazingira kwa ajili ya Shughuli 1.

Chanzo: Decade Volcano Photograph, Website.

BEI POA KABISA ZA LEO –NJOO UNUNUE!

MUHOGO siyo ShzT 2500 SASA ShzT 2000!

NYANYA siyo ShzT 1500 SASA ShzT 1200!

VITUNGUU siyo ShzT 1500 SASA ShzT 1100!

NDIZI siyo ShzT 1500 SASA ShzT 1000!

Nyenzo-rejea 3: Chati za njeo za kitenzi

Nyenzo ya Mwalimu ya kutumia na wanafunzi kwa ajili ya kupanga/kurekebisha

Njeo iliyopo Njeo iliyopita Njeo ijayo
Natembea Nilitembea Nitatembea
Nang’ata Niling’ata Nitang’ata
Nachagua Nilichagua Nitachagua
Nalima Nililima Nitalima
Nachora Nilichora Nitachora
Nakula Nilikula Nitakula
Nasahau Nilisahau Nitasahau
Nafahamu Nilifahamu Nitafahamu
Naona Niliona Nitaona
Nalala Nililala Nitalala
Naogelea Niliogelea Nitaogelea
Naandika Niliandika Nitaandika

Nyenzo-rejea 4: Shairi la kusifu

Kwa matumizi ya wanafunzi

Ngoma Yangu na Francis Faller

Inapiga

kwa uvumilivu

kama maji

yadondokayo

toka kwenye

bomba la

mfereji

au kwa majivuno

kama sauti ya mapigo ya maji ya bahari.

Ngoma yangu. Ngoma yangu.

Inaita upendo.

Inatwanga hasira.

Inahubiri uhuru.

Haisimami kamwe

Hata wakati hakuna mtu

anayesikia ngoma yangu

isipokuwa mimi.

Ngoma yangu inasalimia

kila kitu

kipitacho njia:

jua linalochomoza

mvua inayogongagonga

upepo unaovuma

familia ya korongo

makazi pote angani.

Inamsalimia chenene

Anayelia mlio mwembamba kwa sababu ya raha yake.

Inawasalimia wafanyakazi

ambao vifaa vyao vya kutobolea na kupasulia

vinachimba mashimo

kwa kuchosha.

Ninaifuatilia

katika kicheko

Ninaiongoza kuvuka

maumivu yanayopwita.

Ni shorewanda anayedonoa mbegu

ni ufito kando ya ukingo

ni risasi iendayo kasi.

Ngoma yangu. Ngoma yangu.

Inapiga kwa kiherehere

makaribisho

kwa ajili yako.

Je, utaisikia

kwa furaha?

Je, utakimbia kwa hofu?

Ngoma ni

ngozi na mbao tu

kwa hiyo utakuja?

Ni lazima uje.

Ni lazima uje.

Ngoma yangu kipenzi

ilikuwa jana dhaifu sana.

Leo inapiga.

Kwa nguvu.

Hakika haikutumika zaidi

duniani kote

kupiga bure.

Ingawa kamwe

haipati jibu

Nafikiri

sitaweza kuishi

kama wimbo

wa ngoma yangu

utakufa.

Chanzo asilia: My Drum – Meyerowitz, B., Copans, J. & Welch, T. (watunzi)

Nyenzo-rejea 5: Vitenzi na vielezi katika shairi – Ngoma Yangu na Francis Faller

Taarifa za msingi / welewa wa somo wa mwalimu

Katika tafsiri hii ya shairi vitenzi vimepigiwa mstari na vielezi vimewekewa wino uliokolezwa.

Inapiga

kwa uvumilivu

kama maji

yadondokayo

Dokezo 1: patiently ni kielezi cha namna, ambacho kinaeleza jinsi ngoma inavyopiga/lia: kwa utulivu, kwa kurudiarudia pasipo kuudhika au kuwa na hasira.
toka kwenye

bomba la

mfereji

Dokezo 2: dripping ni sehemu ya kitenzi kamili ‘is dripping’: kama maji [that is/ambayo] inadondoka – mshairi ameamua kutotumia ‘that is’.
au kwa majivuno

kama sauti ya mapigo ya maji ya bahari.

Ngoma yangu. Ngoma yangu.

Inaita upendo.

Inatwanga hasira.

Dokezo 3: proudly vilevile ni kielezi ambacho kinaeleza jinsi ngoma inavyolia: kwa kujipenda, kama kwamba inajifurahia sana.
Inahubiri uhuru.

Haisimami kamwe

Hata wakati hakuna mtu

anayesikia ngoma yangu

isipokuwa mimi.

Dokezo 4: never ni kielezi cha wakati ambacho kinaongezea taarifa kwenye kitenzi ‘stops’: ngoma haiwezi kusimama hata mara.
Ngoma yangu inasalimia

kila kitu

kinachopita njia: jua

Dokezo 5: battering ni sehemu ya kitenzi kamili ‘is battering’: mvua [that is/ambayo] inagongagonga.
linalochomoza mvua

igongayo upepo

unaovuma familia ya

korongo makazi

Dokezo 6: monotonously ni kielezi cha namna ambacho kinaeleza jinsi kazi ya kuchimba inavyoendelea kwa namna inayochosha na ya kurudiarudia
pote angani.

Inamsalimia chenene

Anayelia mlio mwembamba kwa sababu ya raha yake.

Dokezo 7: It’s ni kifupi cha It is na ‘is’ ni kitenzi, ingawa si kitenzi kinachoonesha tendo.
Inawasalimia wafanyakazi

ambao vifaa vyao vya kutobolea na kupasulia

vinachimba mashimo

Dokezo 8: Nervously ni kielezi cha namna ambacho kinaeleza jinsi ngoma inavyolia: kama kwamba ngoma ina hamu au ina woga kidogo.
kwa kuchosha. Dokezo 9: ‘will come’ ni iko katika njeo ijayo lakini iko katika muundo wa swali, ‘will you come?’
Ninaifuatilia katika

kicheko Ninaiongoza

kuvuka maumivu

yanayopwita.

Ni shorewanda anayedonoa mbegu

You should ni muundo uliofupishwa wa You should come – vilevile ni tendo katika njeo ijayo.
ni ufito kando ya ukingo Dokezo 10: was ni njeo iliyopita ya ‘is’.
ni risasi iendayo kasi.

Ngoma yangu. Ngoma yangu.

Dokezo 11: Strong kwa kawaida ilitakiwa iandikwe ‘strongly’: hiki ni kielezi ambacho kinaeleza jinsi ngoma inavyolia.
Inapiga kwa kiherehere

makaribisho

kwa ajili yako.

Dokezo 12: wasn’t stretched ini kitenzi kilicho katika njeo iliyopita.
Je, utaisikia

kwa furaha?

Je, utakimbia kwa hofu?

Dokezo 13: never ni kielezi cha wakati (tazama Dokezo 4).
Ngoma ni

ngozi na mbao tu

kwa hiyo utakuja?

Ni lazima uje.

Ni lazima uje.

Dokezo 14: could not live na should die ni vitenzi ambavyo vinarejelea katika wakati ujao kwa sababu vinaashiria kwamba mshairi hataweza kuishi hapo baadaye bila ngoma.
Ngoma yangu kipenzi ilikuwa jana dhaifu sana. Leo inapiga.

Kwa nguvu.

Hakika haikutumika zaidi

duniani kote

kupiga bure.

Ingawa kamwe

Dokezo 15: Wanafunzi wanaweza kukanganywa na maneno yanayoishia na ‘ing’. Wakati mwingine maneno haya ni sehemu ya kitenzi, mfano: ‘I am singing. Pengine maneno haya ni nomino, mfano: ‘The singing’ of the choir was excellent. Pengine, ni vivumishi ambavyo vinafafanua nomino, mfano: ‘The singing canaries’ flew to the top of their cage. Katika shairi hili dripping, battering, chirping, digging, pecking, beating ni sehemu za vitenzi. The pounding ni nomino. Throbbing ni kivumishi kinachofafanua pain.
haipati jibu

Ninafikiri

sitaweza kuishi

kama wimbo

wa ngoma yangu

utakufa.

Everything ni kiwakilishi ambacho kinasimama mahali pa nomino ambazo zinakifuatia katika ubeti wa 2. For nothing ni msemo ambao unamaanisha ‘without payment/bila malipo’ au ‘for no reason/bila sababu’.
error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!