NADHARIA YA UDHANAISHI/UTAMAUSHI (EXISTENTIALISM)

By , in Shahada on . Tagged width:
SWALI: Chagua nadharia yoyote unayoijua kisha ifafanue kwa undani ukionesha mwasisi au waasisi wa nadharia husika
JIBU:
UTANGULIZI
Sengo (2009:1) anafasili nadharia kuwa ni wazo kuu, fikra kuu, mwongozo mkuu wa mtu, watu au jamii ya pahala fulani, wakati fulani na kwa sababu fulani. Kwa mantiki hiyo nadharia ni dira na mwongozo wa kulikabili jambo kifalsafa, kidini, kimantiki, kijamii na kiutamaduni.
KIINI
NADHARIA YA UDHANAISHI/UTAMAUSHI
(EXISTENTIALISM)
DHANA YA UDHANAISHI
Kwa mujibu wa watalaamu mbalimbali kama vile Kimani Njogu na Rocha Chimera (1999) wanasema kwamba udhanaishi ni nadharia inayoshughulikia zaidi na “dhana ya maisha “.Swali la kimsingi katika nadharia hii ni maisha ni nini? Wadhanaishi huchunguza kwa undani nafasi ya mwanadamu ulimwenguni, .pia wanajishughulisha na uchunguzikuhusu uhusiano uliopo kati ya binadamu na mungu.Wamitila K.W (2003)katika kamusi ya fasihi na nadharia amefanunua udhanaishi kama dhanainayotumia kuelezea maono au mtazamo inayohusiana na hali ya maisha ya binadamu ,nafasi na jukumula binadamu ulimwenguni ,na uhusiano wake na mungu au kutokuwepo nauhusiano na mungu.Wanjala Simiyu (2012) katika kitabu kitovu cha fasihi simulizi udhainishi ni falsafa au mtazamo wamaisha ulio na kitovu chake
katika swala kuwa, maisha ni nini na yana maana gani kwa binadamu? Nikwa njia
gani mwanadamu anaweza kuyabadilisha maisha yake yaliyojaa na dhiki, mashaka na
huzuni..Kimani Njogu na Wafula L M katika nadharia za uhakiki wa
fasihi (2007) wanasema udhanaishi na falsafa kuhusu dhana ya maisha. Ni
falsafa inayo husiana na utamaushi kutokana na neno “kutamauka”.
Kutamauka ni kutokuwa
na furaha au kutokuwa na tamaa kwa kuhisi kutokuwa na matumaini
katikamaisha. Naye Camus (1984) udhanaishi ni falsafa inayoshugulikia
maswala kuhusu maisha; ni mtazamounaokagua kwa upembuzi hali ya nafasi ya mtu
katika ulimwengu anamoishi na pia ni falsafa inayozungumzia uhusianao uliomo
kati ya mtu na mungu na iwapo mtu anapaswa kuamini kuwepo
kwamungu. Nadharia hii inatusaidia kuhakiki maisha ya mwanadamu anayeishi
katika ulimwengu uliojaa shinda namatatizo mengi ambayo yanayosambambishwa na
binadamu mwenyewe. Matatizo anayoyapitia ni kamavita vya wenyewe kwa wenyewe
kwa misingi ya kidini, jaa na uchumi kuharibika, kukosa kazi,
ajali barabarani. Matatizo haya yanafanya mwanadamu kukata tamaa na
kushuku iwapo kweli mungu yuko.
WAASISI WA NADHARIA YA UDHANAISHI
Wamekuwa kwenye vitengo
vitatu
Wanaoamini
kuwepo kwa mungu
Soren Kierkegerd ni
mwanathiolojia wa kidenimaki aliyekuwapo kati ya mwaka wa 1813 hadi1855 aliweza
kuandika makala mbali mbali hasa;
·
The concept of dread
·
Fear and trembling
·
The sickness unto death
Wafula R.M na Kimani
Njogu (2007) naWamitila. W(2003)
Wasioamini kuwepo kwa
mungu
Wanafalsafa wa Kijerumani
wakiongozwa na FRIDRICK NIETZSCHE, MARTIN HEIDEGGER, GABRIEL MARCEL na KARL
JASPERS walitokea katika karne ya ishirini. (Wamitila K.W 2003)
Wasio
na uhakika wa kuwepo kwa mungu.
JEAN PAUL SATRE
aliyetokea baada ya vita vikuu vya dunia na alikuwa mwanafalsafa wa kifaransa. Kimani
Njogu na Rocha chimera (1999)
HISTORIA FUPI
Udhanaishi unahusishwa
kwa kiasi kikubwa na mwanathiololojia wa ki-denimaki kwa jina Soren Kieregaard
(1813-1855), katika maandishi yake mbalimbali Soren Kieregaard (1844) The
concept of dread Soren Kieregaard (1843) Fear and trembling Soren Kieregaard
(1849) The sickness unto death Kieregaard anaeleza kuwa mtu haishi kwa nguvu
zake mwenyewe, kuna nguvu zinazomtawala ambozo ni za Mungu. Binadamu anapoishi
hutenda dhambi na ili apate utulivu wa kiroho inambidi atubu dhambi hizo.Wanaamini
kuwepo kwa mungu kwa binadamu wote. Anaeleza kuwa binadamu ni kikaragosi cha nguvu
zilizomuumba ni katika kuzicha. Anaendelea kusema kwamba udhanaishi ni dhana ya
hofu pale ambapo binadamu huogopa adhabu kutoka kwa Mungu kwa hivyo amefunikwa na
wasiwasi, hataki kumkosea Mungu. Anasisitiza binadamu ni mtu binafsi (hali ya kujijali).
Binadamu hupata
kimbilio kutoka kwa mivutano ya maisha kupitia kwa Mungu. Imani hii ilishika
nguvu sana kwenye ukristo, huu ukawa mwanzo wa udhanaishi wa ukristo. (christian
existentialism) Kwa mujibu wa Wamitila .K.W (2003) kamusi ya fasihi, istilahi
na nadharia asema kuwa katika karne ya ishirini, udhanaishi ulipata
msukumo mpya kutoka kwa mwanafalsafa wa kijerumani Friedrich Nietzsche na
wengine kama Martin Heidegger, Gabriel Marcel na Karl Jaspers.
Nietzche (1927) “joyful
wisdom” anadai kuwa mungu amekufa. Tamko hili pamoja na misimamo ya wenzake
vinakuwa misingi muhimu ya kuzuka kwa udhanaishi wa ukanaji Mungu (atheistic existenialism)
Kwa mujibu wa tovuti, Martin Heidegger, mwanafalsafa wa kijerumani na
mwanafunzi wa Husserl aliamini kuwa neno “nitakufa” si katika dunia ya
ukweli.
 Kwa mujibu wa
kimani Njogu na Rocha Chimera (1999) wanaelezea kuhusu mwanafalsafa wa
kifaransa Jean Paul Satre ambaye ndiye mwasisi mkuu wa udhanaishi. Baada ya
vita vikuu vya dunia anadai kuwa mtu huzaliwa au hujipata ametumbukia katika
ombwe la aina fulani. Vilevile mtu yuko huru kuishi tu na kukabiliana vilivyo
na ulimwengu unaomzunguka. Isitoshe kwa vile binadamu hana uwezo kwa yale
anayoyapitia maumivu na mateso anaweza kukata tamaa.
Katika mhadhara
alioutoa Jean Paul Satre, (1946) “Existentialism and Humanilism” alisisitiza
kuwa “kuzimu ni ya watu wengine”. Hii ni ishara kuwa ana uwezo wa kuchagua
na uhuru wa kila mtu anaweza athiri watu wengine, alisisitiza pia dini haiwezi
kutatua shinda za binadamu isitoshe aliegemea katika suala la ubinafsi wa mtu.
MIHIMILI YA UDHANAISHI
Waandishi mbalimbali
wameweza kutoa mihimili ya udhanaishi, kwa kuwarejelea Wafula .R.M na Kimani
Njogu (2007) wao wameainisha mihimili hiyo kama ifuatavyo;
·
Wanatilia mkazo matatizo halisi
yanayomsimbu mwanadamu na kwanakwepa imani ya kinjozi juu ya imani ya
kuishi.
·
Hawaamini uwepo wa Mungu na uumbaji wake
wa ulimwengu.
·
Juhudi za mtu binafsi kujisaka au
kupambana na maisha huishia katika mauti.
·
Maudhui yanayotajwa na wadhanaishi ni
kama vile uhuru wa mtu binafsi, uwezo wake wa kujifikiria na kujiamulia.
Kwa ujumla udhanaishi
ni nadharia inayochochea uhakiki wa kazi za fasihi kifalsafa zaidi ili kuweza
kutathmini ukweli kuhusu maisha kupitia wahusika mbalimbali ambao huwakilisha
sifa na tabia za wanadamu katika maisha halisi.

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!