MISEMO YA KWENYE VYOMBO VYA USAFIRI

By , in Sarufi na Utumizi Wa Lugha on . Tagged width:

UKIWA NA MSONGO WA MAWAZO TAFUTA KITUO CHA DALADALA TU,UTAFURAHI NA ROHO YAKO AISEEE!!!

UTAWASIKIA AU KUSOMA NYUMA YA GARI:

1.Yatima hadeki
2.Utamu wa chips mimba
3.Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni
4. Usiyempenda kaja
5. Kobe hapimwi joto
6. Acha kazi uone kazi kupata kazi
7. Ukichezea koki utalowa
8. Heshima pesa kipara kovu tu!
9. Mtumbwi hauna saitimira.
9. Silaha pesa bastola mzigo
10. Hata uoge mjini huendi
11. Chezea mshahara usichezee kazi.
12. Ukiona manyoya ujue kaliwa
13. Ikisimama Panda
14. Pombe pombe tuu kunywea bar mbwembwe
15. Njia ya chooni haioti nyasi
16. Likizo ya maskini ugonjwa
17. When i grow up i want to be a scania
18. Hata bibi alikuwa binti
19. Kisigino hakikai mbele
20. Kama mapenzi pesa kaolewe na benki
21. Hata barabara ina matuta lakini huwezi panda viazi
22. Mavi hayana miba lakini ukikanyaga lazima uchechemee
23. Paka haishi kwa msela
24. Ukipendwa ujue kuna boya kaachwa
25. Nipo nipo kwanza
26. Mchana nzi ucku mbu
27. Usimshangae funza kukata viuno ndio mwendo wake
28. Kama umelipenda (gari) bonyeza nyota liwe lako
29. Supermarket hawauzi mkaa
30. We nisubiri mi nakungoja.
31. Zetu dagaa kuku tamaa
32. Hata uwe na heshima vipi huwezi kumpokea askari bunduki!!!!!!!!