MFANO WA ANDALIO LA SOMO (KISWAHILI)

By , in AZIMIO LA KAZI I-IV on .

Mfano wa Andalio la Somo 

Tarehe Darasa Somo Vipindi Muda Idadi ya wanafunzi
07/01/2019 Kidato

cha IB

Kiswahili 1&2 02:00-3:20 asubuhi Waliosajiliwa Waliohudhuria
KE ME JUMLA KE ME JUMLA
20 28 48 15 20 35

 

Ujuzi: Uwezo wa kutofautisha matumizi ya aina mbalimbali za maneno katika miktadha tofauti.

Mada Kuu: AINA ZA MANENO.

Mada ndogo: Ubainishaji wa aina za maneno.

 

Lengo kuu: Kubainisha matumizi sahihi ya maneno katika tungo mbalimbali za Kiswahili.

 

Malengo mahususi: Baada ya kumalizika kwa mada hii mwanafunzi aweze:

  1. kubainisha aina saba (7) za maneno.
  2. kutofautisha aina mbalimbali za maneno katika tungo.

Zana/vifaa: Chati za ukutani za aina za maneno na ufafanuzi wake, vitu halisi, chati ya sentensi mbalimbali.

Rejea: Kiswahili kidato cha kwanza, TET (2006)

 

HATUA ZA SOMO

HATUA MUDA SHUGULI ZA UFUNDISHAJI SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI TATHMINI
1. Utangulizi Kuuliza maswali mafupi mafupi kwa mdomo kuhusu somo lililopita Kujibu maswali hayo kwa mdomo Kuchunguza kama mwanafunzi anaweza kujibu maswali hayo kwa usahihi.
2. Maarifa mapya a) Kuwaongoza wanafunzi kutunga sentensi mbalimbali kwa kutumia vitu halisi.

 

b) Kuwaongoza wanafunzi katika jozi kubaini maneno (yaani: nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi, kihisishi, kiwakilishi na kiunganishi) kwa kutumia chati ya sentensi mbalimbali.

a) Kutunga sentensi mbalimbali kwa kutumia vitu halisi.

 

 

b) Kubaini maneno (yaani: nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi, kihisishi, kiwakilishi na kiunganishi) kwa kutumia chati ya sentensi mbalimbali.

Kuchunguza kama wanafunzi wameweza kutunga sentensi hizo.

Kuchunguza kama mwanafunzi wameweza kubaini  aina saba (7) za maneno.

3.Kukazia maarifa Kuwaongoza wanafunzi katika makundi kuchora chati za ukutani na kubainisha aina za maneno. Kuchora chati za ukutani na kubainisha aina za maneno. Kuchunguza kama mwanafunzi ameweza kubainisha aina za maneno kwa usahihi.
 

4.Tafakuri

Kutoa zoezi kwa wanafunzi la kubainisha maneno katika sentensi na kusahihisha. Kufanya zoezi la kubainisha maneno katika sentensi kwa kuandika. Kuchunguza kama mwanafunzi ameweza kubainisha maneno katika sentensi.
5.Hitimisho Kuuliza maswali ya mdomo kwa wanafunzi juu ya somo na kutoa ufafanuzi panapohitajika. Kujibu maswali kwa mdomo, na kuuliza maswali kwa mdomo juu ya somo hasa panapohitaji ufafanuzi. Kuchunguza kama mwanafunzi ameweza kijibu maswali kwa usahihi.

 

Tathmini ya wanafunzi: …………………………………………….…………….…………………………………………………………………..

Tathmini ya mwalimu: ………………………………………………………………………………………………………………………………..

Maoni: ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………

Facebook Comments
Donate
Recommended articles