MBINU ZA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI

By , in DIPLOMA/CHETI on . Tagged width:

Na. Nyandiba Carren

Masinde Muliro University of Science & Technology MMUST

AZIMA YA MODULA HII

Modula hii inaazimia kumwezesha mwanafunzi kufahamu mbinu na stadi za kufundisha Kiswahili, nadharia mbali mbali za ufundishaji wa lugha na vile vile zana na vifaa muhimu katika ufundishaji wa Kiswahili.

Kufikia mwisho wa kozi mwanafunzi aweze:

(a)    Kufafanua nadharia za kufundisha na kujifunza lugha .

 

(b)    Kubainisha umuhimu wa kufundisha Kiswahili katika mfumo wa elimu.

 

(c)    Kueleza sifa za njia za kufundishia vipengele mbalimbali vya lugha na fasihi.

 

(d)   Kutengeneza nyaraka na vyombo muhimu  katika somo la Kiswahili.

 

(e)    Kutayarisha na kufundisha aina mbalimbali za masomo kwa ufanisi

.

(f)     Kuandaa nyenzo anuwai za kufundishia Kiswahili.

 

 

(g)    Kutumia mbinu mbalimbali za kutathmini maendeleo ya wanafunzi.

 

 

 

MADHUMUNI

YALIYOMO

 

(a)     Nadharia za kufundisha na kujifunza lugha .

 

(b)     Umuhimu wa kufundisha Kiswahili katika mfumo wa elimu.

 

(c)     Sifa za njia za kufundishia vipengele mbalimbali vya lugha na fasihi.

 

(d)    Nyaraka na vyombo muhimu  katika somo la Kiswahili.

 

(e)     Kutayarisha na kufundisha aina mbalimbali za masomo kwa ufanisi.

 

(f)      Maandalizi ya nyenzo anuwai za kufundishia Kiswahili.

 

(g)     Mbinu mbalimbali za kutathmini maendeleo ya wanafunzi.

SURA YA KWANZA

UMUHIMU WA KUFUNDISHA LUGHA

1.1 Utangulizi

 Sura hii kinashughulikia Uumuhimu wa lugha na vile vile kufafanua umuhimu wa kufundisha lugha ya Kiswahili nchini Kenya.

Kufikia mwisho wa kitengo hiki, mwanafunzi aweze kutimiza yafuatayo:

1. Kufafanua maana ya ya lugha

2. Kueleza umuhimu wa kufundisha kiswahili nchini Kenya

3. Kueleza changamoto za ufundishaji wa Kiswahili nchini Kenya

 

1.2 MADHUMUNI YA KITENGO

1.3 MAANA YA  NA SIFA ZA LUGHA

Lugha hutawala maisha ya wanadamu. Lugha hutumika kueleza fikra za watu, kuendeleza mahusiano ya watu na hata kuhifadhi na kupitisha utamaduni wa watu. Bila lugha, historia ya mwanadamu haingekuwa jinsi ilivyo. Kwa hivyo, kama mwalimu wa lugha, ni muhimu kufahamu sifa muhimu za lugha.

Kwa mujibu wa wataalam mbalimbali wa Isimu, Lugha ni mfumo nasibu wa ishara za sauti wenye maana unaotumiwa na wanadamu katika kuwasiliana. Kutokana na fasili hii, tunaweza kubainisha sifa zifuatazo za lugha

a) Lugha ni mfumo

Ingawa binadamu ana uwezo wa kutamka sauti za aina nyingi, siyo sauti zote zinazotumiwa katika mawasiliano. Kila lugha ina idadi maalum ya sauti inazotumia katika mawasiliano ya lugha hiyo. Sauti hizo hazitumiwi kiholela, zinapangwa kwa utaratibu maalum ili kuleta maana katika lugha .Sauti za lugha ndizo hutumiwa katika kuunda maneno ambayo yanatumika katika mawasiliano. Maneno nayo huhitaji kupangwa kwa utaratibu maalum uliokubalika ili kuleta maana katika lugha. Kwa mfano mfuatano wa maneno ufuatao unaweza kukubalika katika Kiswahili mtoto mdogo analia, na walasio mdogo analia mtoto au katika Kiingereza my mother is beautiful ni sawa kuliko  beautiful mother my is.

b) Lugha ni maana

Utaratibu wa kupanga sauti na maneno katika lugha hautoshi kukamilisha maana. Mpangilio wa sauti lazima uwe na maana katika lugha husika. Kwa mfano mfuatano wa abab hauna maana yoyote katika Kiswahili lakini mfuatano wa baba una maana.Vivyo hivyo sentensi kama vile samaki amepika mamaimefuata mpangilio mzuri, lakini haina mantiki, kwa hivyo haiwezi kukubalika kama sentensi sahihi katika Kiswahili, tofauti na sentensi mama amepika samaki ambayo ina mantiki na hivyo basi inaweza kukubalika kama sentensi ya Kiswahili.

c) Lugha ni mfumo wa ishara nasibu za sauti

Ingawa tulikwisha kusema kuwa lugha ni mfumo wa ishara za sauti, tungependa kusema kuwa sauti zinazotumika ni nasibu tu, yaani hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya sauti zinazotumika kutaja kitu na kitu chenyewe. Kwa mfano, hakuna uhusiano wa moja kwwa moja kati ya neno paka na mnyama anayeitwa kwa jina hilo. Ingawa kuna maneno machache katika lugha yanayofuata milio ya vitu hivyo, kwa mfano, kengele kulia ngo ngo, maneno mengi katika lugha yoyote ile huwa hayana uhusiano wa moja kwa moja na kitu kinachoashiriwa.

d) Lugha ni ya binadamu

Lugha hutumika tu na binadamu. Kati ya viumbe wote duniani, binadamu ndiye aliyejaliwa kipawa cha kujifunza lugha. Lugha ya mwanadamu inatofautiana sana na mwasiliano ya wanyama na viumbe wengine kama vile nyuki, samaki n.k. Lugha ya wanadamu ni bunifu na hivyo humwezesha binadamu kubuni sentensi nyingi kuelezea hali mbalimbali na vile vile anaweza kufumia lugha kuzungumzia mambo yaliyopo, yajayo na yaliyopita na hata mambo ya kidhahania.

e) Lugha ni mawasiliano

Lugha huwasaidia watu katika kuwasiliana, yaani kupasha habari. Kwa  njia hiyo, lugha huwasaidia watu kuishi pamoja, kufanya kazi pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali. Lugha pia hutumika katika kuimarisha na kudumisha uhusiano kati ya watu, kwa mfano katika maamkuzi, kuombana msamaha, huelezana hisia za mapendi na kadhalika.

f) Lugha ni kioo cha utamaduni

Majina na vitendo vyote vinavyopatikana katika lugha hupatikana pia katika utamaduni wa watu.

Lugha inaashiria vitu, desturi, vitendo na matamanio ya watu wanaoishi katika utamaduni fulani. Mtu anayefahamu lugha hana budi kuelewa kuwa ufahamu mzuri wa lugha pia unahusisha ufahamu wa miiko ya lugha inayohusika. Matumizi ya lugha hutegemea mahusiano ya watu; kama ni marafiki, waajiriwa au watu wa ukoo mmoja. Kwa mfano mtu mzima hawezi kumuamkua mtoto mdogo kwa salamu za shikamoo katika utamaduni wa Waswahili.

 

NADHARIA MBALI MBALI ZA UFUNDISHAJI WA LUGHA

Kunazo nadharia (mikondo) za ufundishaji wa lugha ya pili dunia ni mbalimbali ambazo zimewahi kuathiri, na ambazo mpaka sasa zinaathiri, ufundishaji wa lugha ya pili. Nadharia hizo ni nyingi.

Siyo madhumuni ya modula hii kuisifu ua kuitweza nadharia yoyote ya ufundishaji wa lugha ya pili. Lengo kuu hasa ni kumfafanulia mwalimu wa Kiswahili nadharia zilizopo katika ufundishaji wa lugha ya pili ili aweze kizielewa na baadaye kuchagua yale yaliyo muhimu katika ufundishaji wake. Mwalimu aliye na ufahamu mpana kinadharia ana nafasi nzuri ya kufanya maamuzi yanayofaa ufundishaji wake.

a) Nadharia ya ufundishaji wa moja kwa moja

Nadharia hii ilitumika sana Ulaya mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20. Nadharia hii ilisisitiza sana ufundishaji wa lugha ya pili kwa kuitumia lugha iyo hiyo. Iliwakataza walimu kutumia tafsiri ya aina yoyote katika ufundishaji wao. Katika nadharia hii, ilikuwa ni marufuku kutumia lugha ya mama katika ufundishaji wa lugha ya pili. Waasisi wa nadharia hii waliamini kuwa watu wanaweza kujifunza lugha ya pili namna wanavyo jifunza lugha ya kwanza, pasi na tafsiri au matumizi ya lugha nyingine yoyote. Kwao. Ujinzaji wa lugha ya pili ulikuwa ni sawa na kuzifuata nyayo za lugha ya kwanza ambapo yule anayejifunza huingiliana moja kwa moja na lugha anayojifunza bila tafsiri.

Nadharia ya ufundishaji wa moja kwa moja haikuhimiza uchambuzi wa sarufi au maelezo ya kisarufi kwa wanafunzi. Kwa mujibu wa nadharia hii, walimu walishauriwa kutotaja maneno kama’Nomino’, ‘Kitenzi’ na ‘Kivumishi’. Baada ya ufundishaji uliofanywa kwa uingizaji, na maonyesho ya vitu, kwa mfano, picha au vifaa vingine, wanafunzi walitakiwa kuzing’amua wenyeye sheria na kanuni za kisarufi. Wanadharia hii waliamini kuwa lugha hufunzika vizuri kwa kuitumia darasani na wala siyo kuichambua kisarufi.

Kwa mujibu wa nadharia hii, walimu walitakiwa kufundisha mazungumzo pamoja na ufahamu wa kusikiza. Mbinu ya maswali na majibu ilipendekezwa katika ufundishaji wa mazungumzo ambayo yalithaminiwa sana. Mwalimu aliuliza maswali nao wanafunzi waliyajibu. Kadhalika katika uzungumzaji wanafunzi walitakiwa kujifunza matamshi bora yaliyo sawa ya wazawa wa lugha ya pili waliyokuwa wakijifunza.

b) Nadharia ya utabia

Nadharia hii ilitumika sana katika miaka ya hamsini (1950) hadi miaka ya sitini (1960) kule Marekani. Baadhi ya vipengele vya nadharia hii vingali vinatumika mpaka leo. Nadharia hii imejengwa katika misingi ya nadharia ya Saikolojia iitwayo Utabia.

Wafuasi wa nadharia ya utabia walidhamiria kueleza namna tabia inavyojengwa. Waliamini kuwa tabia itadumu ikiwa itaigwa, itarudiwarudiwa, na kutuzwa, lakini tabia isiyorudiwa na isiyotuzwa hufifia.

Kwa hivyo walisisitiza ujifunzaji wa lugha ni sawa na ujifunzaji wa tabia yoyote ile ya binadamu,kama vile kuendesha baiskeli, kuogelea na kadhalika.Kwa hivyo walipendekeza mambo yafuatayo katika ufundishaji wa lugha:

i) Kukariri na kurudiarudia matamshi mazuri ya vipande vya mazungumzo , miundo ya sentensi      n.k

ii) Vipengele vya lugha vifundishwe kwa njia ya kusikiliza na kuongea kwanza kabla ya kuandikwa.

iii) Ufundishaji wa sarufi na vipengele vingine vya lugha usifanywe kwa kuchambua vipengele vya lugha. Mwanzoni wanafunzi wakariri na kurudia na kuiga vipengele hivyo kabla ya kuvizoea.

iv) Jukumu la mwanafunzi ni kufuata maagizo, ilhali lile la mwalimu ni kiongozi wa kila tukio darasani

 

c) Nadharia ya mawasiliano

Nadharia ya mawasiliano ilishika kasi na kupanuka nchini Uingereza katika miaka ya 1970. Lengo kuu la nadharia hii ni kukuza uwezo wa kuwasiliana, lakini siyo kukuza ujuzi wa miundo au vipengele vya lugha tu. Inakusudiwa kukidhi matakwa ya wale wanaojifunza lugha ya pili katika mawasiliano. Mawasiliano yanahusu mambo mengi kama vile, kusababisha mambo fulani yafanyike , kuboresha mahusiano kati ya watu, na kuonyesha hisia za watu na ubunifu wao. Kadhalika, nadharia hii inakusudiwa kuimarisha mbinu za ufundishaji ambazo zitasisitiza uhusiano uliopo kati ya miundo ya lugha mawasiliano.

Nadharia ya mawasiliano ina mihimili ifuatayo.

 I.  Maana ya miundo husisitizwa kwani lengo kubwa la nadharia hii ni mawasiliano. Kwa mujibu wa nadharia hii, madhumuni makuu ya lugha ni kuwasiliana, kwani lugha ni mfumo wa kueleza maana.

II. Vipashio muhimu vya lugha siyo vile vya kisarufi na kimuundo tu, lakini pia vile vya kimawasiliano.

 III. Malumbano (tamthilia fupi) zilitumiwa kufundishia huwa hazikaririwi.

 IV. Muktadha hupewa nafasi muhimu katika ufundishaji. Kwa mfano, maneno mapya au miundo fulani ya kisarufi huwekwa katika muktadha wa mawasiliano, kama vile katika sentensi, mazungumzo na makala.

    V. Drili zinafanywa lakini siyo za lazima kwa mujibu wa nadharia hii

 VI. Matamshi yanayoeleweka na watu wengi katika mazungumzo ndiyo lengo kuu.  Lengo siyo matamshi yanayofanana na yale ya wazawa wa lugha.

VII.Kanuni za kisarufi na mbinu nyinginezo zinatumiwa inapoonekana kuwa ni lazima.

VIII.  Wanafunzi wanaweza kuzungumza kuanzia siku ya kwanza.

 IX.            Lugha ya kwanza na tafsiri zinaweza kutumiwa ikiwa hapana budi, pale matumizi yake yanaposaidia ufafanuzi wa jambo.

    X.  Kusoma na kuandika kunaweza kuanza katika siku za mwanzo ikiwa ni muhimu.

 XI. Matumizi ya lugha kwa wingi darasani hupendekezwa kwani nadharia hii husisitiza kuwa mtu hujifunza lugha vizuri kwa kuitumia

XII.Jukumu muhimu la ujifunzaji wa lugha ni mawasiliano yanayofaa katika muktadha.

Nadharia ya mawasiliano inapendekeza ufundishaji ambao unatumia shughuli zinazoedeleza mawasiliano. Hii ni kwa sababu wafuasi wa nadharia hii wanaamini kuwa ujifunzaji wa lugha huendelezwa na vitendo au shughuli zinazoendeleza mawasiliano badala ya ukaririshaji wa miundo. Vitendo kama vile ulinganishaji wa picha, maelezo yanayohusu ramani, maelezo ya ufanyaji wa shughuli fulani kwa mfano, kupika chakula fulani, kuonyesha njia, mazungumzo ya vikundi, tamthilia fupi, uingizaji, michezo, mijadala na usomaji wa magazeti hupendekezwa darasani. Katika darasa la aina hii, mwalimu huchukuliwa kama mratibu wa shughuli hiyo. Kazi yake muhimu huwa ni kuwezesha mawasiliano kuwapo kati ya wanafunzi darasani. Mwalimu pia huwapa wanafunzi ushauri ufaao.

Ni vizuri kutaja kwamba darasa linalotumia nadharia ya mawasiliano hushirikisha wanafunzi sana katika mawasiliano. Mwalimu hasemi yote na kutenda yoye. Jukumu lake huwa limebanwa kidogo. Wanafunzi huhimizwa kufanya mengi darasani.

d) Nadharia ya ufundishaji vitendo

Nadharia ya ufundishaji kwa vitendo ilianza nchini Marekani katika miaka ya 1920 na imetumiwa na baadhi ya walimu wa lugha ya pili kwa miaka mingi. Nadharia hii hudhamiria kufundisha lugha kwa matumizi ya vitendo. Wafuasi wa nadharia hii wanaamini pia kuwa wanafunzi hujifunza lugha ya pili vizuri katika mazingira na hali ambayo haina wasiwasi wala bughudha. Kwa hivyo dhima kuu ya nadharia hii ni kupunguza wasiwasi katika ufundishaji wa lugha ya pili. Nadhania hii pia hukusadia kuhitimisha wanafunzi wanaoweza kuwasiliana bila vikwazo kwa sababu.

       I.  Ufundishaji wa lugha ya pili kwa kutumia michezo na vitendo hupunguza wasiwasi wa mwanafunzi na huboresha mazingira ya ujifunzaji.

    II.  Ufundishaji wa mazungumzo wapaswa kucheleweshwa kidogo mpaka pale wanafunzi wa lugha ya pili watakapoimarisha ujuzi wao wa ufahamu na usikizaji.

 III.   Usikilizaji ukiimarika uzungumzaji unaimarika pia.

 IV.  Ufundishaji wa lugha ya pili wapaswa kusisitiza maana na wala siyo miundo.

    V.  Matumizi ya vitendo na amri ni muhimu katika ufundishaji wa lugha ya pili.

 VI.Mwanafunzi anaweza kujifunza vipande kikubwa kuliko sentensi.

VII. Drili na ukaririshaji vikiandamana na vitendo hupendekezwa darasani.

VIII.  Uigizaji wa mahali mbalimbali kama vile sokoni, hosipitali na dukani hupendekezwa.

 IX. Wanafunzi husikiza na kujibu kwa vitendo.

    X.Mwanzoni mwalimu asiwarekebishe sana wanafunzi wake lakini marekebisho yakue jinsi ujuzi wa wanafunzi unavyokua katika lugha.

e) Mwalimu aliye kimya

Katika mbinu hii, mwalimu anatakiwa kuwa kimya kwa muda mwingi darasani ilhali mwanafunzi anatakiwa kushirikishwa kuzungumza au kuandika kwa wingi kadiri iwezekanavyo. Mbinu hii ya ufundishaji imejengwa katika misingi ifuatayo:-

       I.Kwamba ujifuzaji wa lugha ya pili unafanikiwa ikiwa mwanafunzi anajigundulia mambo kwa ubunifu wake badala ya kurudiarudia na kukumbuka anachojifunza.

    II. Ujifunza wa lugha ya pili unafanikishwa na vifaa halisi vya ufundishaji (vitu ambavyo vinaweza kuonekana, kushikika).

 III. Ujifunzaji unafanikishwa na ushirikishaji wanafunzi katika kile anachofunza. Nadharia hii inashikilia kuwa wanafunzi ni mtendaji na siyo msikizaji tu.

Filosofia inayoongoza nadharia hii ya ufundishaji wa lugha ya pili ni ile isemayo:-

Mbinu za kufundishia Kiswahili

“Niambie na nitasahau”

Nifundishe na nitakumbuka

Nishirikishe na nitajifunza

Ø  Nadharia hii huwa inajaribu kuwaendeleza wanafunzi waweze kujitegemea na kuwajibika katika ujifunzaji wao lugha ya pili.

Ø  Mwalimu hawarekebishi wanafunzi sana kwani wanafunzi wenyewe wapaswa kukuza uwezo wao wao, wa kujirekebisha.

Ø  Wanafunzi wanahimizwa kujitegemea wao kwa wao, kwa hivyo wanapaswa kushirikiana badala ya kushindana.

Ø  Jukumu la mwalimu hasa ni kutayarisha mazingira yafaayo kwa ujifunzaji wa lugha; mazingira ambamo wanafunzi wake wataingiliana na kuwasiliana, mazingira ambamo mwalimu mwenyewe atajizuia kufanya au kusema yale wanafunzi wake wanaweza kufanya na kusema.

Ø   

f) Nadharia ya kijumuia na kibinadamu

Nadharia hii inapendekeza namna ya ufundishaji wa lugha ya pili ambapo mwalimu huwa ana jukumu la shauri na msaidizi wa wanafunzi. Wanafunzi nao huwa ni kama wasaidiwa na washauriwa. Kwa ufupi, nadharia hii ina mihimili ifuatayo:

–          Usalama wa wanafunzi ni muhimu sana, wanafunzi wakiwa na wasiwasi na kutojisikia salama hawawezi kujifunza lugha vizuri.

–          Kutomakinika kwa wanafunzi kwapaswa kupunguzwa hasa kwa matumizi ya majukumu tofauti tofauti katika ufundishaji.

–          Wanafunzi wakijifunza kitu wanapaswa kuhimizwa kuonyesha ujuzi wao darasani kwa mazungumzo au maandishi. Wanapaswa kujionyesha na kujivunia ujuzi wao; kwa hivyo mwalimu anatakiwa kuwapa fursa hiyo. 

–          Wanafunzi wanapaswa kujifunza lugha  kwa njia mbali mbali kama vile tafsiri, kujirekodi katika kanda za sauti, vikundi, uchambuzi usikizaji na mazungumzo ya jumla.

–          Ujifunzaji ni jukumu la jumuiya ya wanafunzi pamoja na mwalimu. Katika jumuiya hii, washiriki hujifunza kwa kuchangamana na wenzi wao. Kujifunza huwa si jukumu la mtu mmoja bali ni ushirikiano wa jumuiya.

 

ZANA/ VYOMBO VYA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI

Uandalizi wa somo la Kiswahili

Ni sheria ya maisha kwamba unapotaka kufaulu katika jambo lo lote maishani ni sharti ujitayarishe mapema kabla ya kulikabili jambo lenyewe. Katika taaluma ya ualimu, maandalizi Mwalimu anatakiwa kutayarisha mpangilio (taarifa) wa somo kutokana na ratiba (maaziimio ya kazi)  ambayo huwa imetayarishwa kutoka kwa silabasi.

 

a) Silabasi

Silabasi ni mpangilio wa kijumla wa mada zinazotakiwa kufuzwa katika darasa fulani kwa mwaka mzima katika somo mahsusi. Hivyo, silabasi humwongoza mwalimu kufahamu kitakachofunzwa . Aidha, silabasi hufafanua malengo ya somo na kutoa vidokezo vya mambo yanayotakikana kufundishwa ili kutimiza malengo hayo. Umuhimu mwingine ni kuwa ratiba ya kazi hutayarishwa kutokana na silabasi. Hili huwezeshe mwalimu kutafuta vifaa vya kufundishia na humwongoza katika utungaji wa mitihani na majaribio mengine.

 

Ili kujiandaa vyema kufundisha somo la Kiswahili lazima mwalimu afahamu matarajio ya silabasi ya Kiswahili. Lazima ayaelewe madhumuni ya somo ya Kiswahili na yale yote anayotarajiwa kufundisha, vyombo na vielelezo atakavyotumia katika kufundisha. Silabasi itamwezesha mwalimu kuwa na mwelekeo ulio sawa na mwalimu wengine wa somo hili.

 

Nchini Kenya, silabasi hutayarishwa na Taasisi ya Elimu ya Kenya (KIE) ikishirikiana na Baraza la kutunga Mitihani la Kenya (KNEC). Hii silabasi huwa ni moja na hutumiwa na shule zote na umma. Silabasi lazima iakisi na kukuza malengo ya elimu nchini Kenya malengo hayo ni :-

       I.            Kukuza umoja wa kitaifa

    II.            Kuendeleza ujenzi wa taifa kiuchumi na kijamii

 III.            Kumwendeleza mtu binafsi

 IV.            Kuhimiza usawa wa kijamii

    V.            Kutathmini na kukuza utamaduni wa Kenya

 VI.            Kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

 

b) Ratiba ya masomo (maazimio ya kazi)

Baada ya mwalimu kupokea silabasi ni lazima atayarishe ratiba ya masomo. Hii ni ratiba au mpangilio unaofafanua wazi jinzi mwalimu atakavyofunza tangu mwanzo wa mwaka au wakati anapoanza kulifunza darasa fulani hadi mwisho wa mwaka au mwisho wa muda wake wa kujifunza darasani hilo.

 

Itambidi mwalimu atambue uwiano uliopo kati ya vijisehemu mbalimbali vya yale yanayopendekezwa kufundisha baada ya kufanya hivyo atawajibika kuyapanga katika mtiririko mwema. Asifuate mpangilio wa silabasi ulivyo bila kutilia  maanani uhusiano wa mambo. Katika baadhi ya asasi, idara mbalimbali zinatayarisha ratiba ya masomo itakayofuatwa na walimu wote katika idara hiyo ili kuweko na ulinganifu katika madarasa yote ya darasa moja.

 

Madhumuni ya kuwa na ratiba ya masomo

Ø  Humwezesha mwalimu kuhitimisha silabasi kwa muda uliopendekezwa

Ø  Kumwezesha mwalimu kupanga ufundishaji wake ulingane  na ugumu wa mambo au ulingane na kiwango cha lugha ya wanafunzi na mpango wa mwalimu wa kutahini.

Ø  Humwezesha mwalimu kuamua namna ya kuhusisha mambo yanayohusiana na vilevile kuamua mambo ya kusisitiza.

Ø  Humwezesha mwalimu kufikiria na kuandaa vielelezo na vifaa mwafaka mapema.

Ø  Ratiba ya masomo hubainisha mahali mwalimu alipofika, alipotoka na anapoelekea.

Ø  Ratiba ya masomo ni kumbukumbu ya mafunzo ambayo inaweza kuhifadhiwa.

Kwa kawaida, ratiba ya masomo ya Kiiswahili huwa na vichwa vifuatavyo.

–          Wiki/Juma

–          Kipindi

–          Funzo

–          Mada

–          Shabaha

–          Marejeleo

–          Vifaa

–          Mbinu za kufundishia

–          Mazoezi /kazi

–          Maoni (hutolewa baada ya muda uliotengwa somo kupita)

c) Mpangilio wa somo /Taarifa ya somo

Mpangilio wa somo hutayarishwa kutokana na ratiba ya masomo. Mpangilio wa somo huwa ni maandalizi ya awali ya jinsi mwalimu atakavyolifunza somo lake katika muda uliotengwa somo hilo.madhumuni ya mpangilio wa somo ni:-

       I.            Humwezesha mwalimu kutimiza shabaha ya somo lake bila kwenda kombo au nje ya muda uliotengwa

    II.            Humwezesha mwalimu kuhusisha somo lililopita na lile analolifunza ikiwa ni lazima.

 III.            Humwezesha mwalimu ajiamini na hivyo hufundisha bila wasiwasi wala kuhangaika.

 IV.            Humwezesha mwalimu kutayarisha awali vielelezo atakavyotumia katika somo lake katika wakati ufaao.

Mwalimu pia huyatilia maanani mahitaji ya wanafunzi, udhaifu wao, na kutumia ustadi wao ili kuwafunza wote walio darasani. Ili kuzingatia hili, lazima mwalimu aiandike shabaha yake katika hali ya kutendeka na inayoweza kupimika na ieleze wazi litakaloweza kutendwa na wanafunzi baada ya muda uliotengwa, isiegemee upande wa mwalimu. Mada ihusu jambo litakaloshughulikiwa katika kipindi. Kwa mfano

i) Wanafunzi waweze kuandika madaftarini mwao jozi kumi za maneno yenye maana sawa.

ii)Wanafunzi waweza kutoa mifano isiyopungua mitano kwa kila tamathali ya usemi watakayofunzwa.

Shabaha hizi zinazomlenga mwanafunzi zimeandikwa katika hali ya kutendeka “ kuandika madaftarini ” na ” kutoa mifano .”Shabaha hizi pia zinatoa nafasi kwa mwalimu kutathmini somo lake linapomalizika. Mpangilio wa somo huwa na vichwa vifuatavyo:-

Tarehe ya somo                       Shabaha

–          Darasa                                             Muda

–          Wakati                                Vifaa

–          Funzo                                              Marejeleo

Ø  Kazi ya mwalimu. Hii hugawa katika hatua mbalimbali, kila hatua ikipewa muda wake. Kuna utangulizi, kiini na hitimisho

Ø  Kazi ya wanafunzi: sehemu hii inahusu jinsi mwalimu anavyotarajia kuwashirikisha. Wanafunzi wake.

Ø  Kazi ya mwanafunzi huenda sambamba, hatua kwa hatua na kazi ya mwalimu. Ikumbuke kuwa wakati mwingine ni vigumu kutenganisha kazi ya mwalimu na ile ya wanafunzi.

Ø  Kazi ya ubaoni. Huu ni mpangilio wa hoja muhimu ubaoni

Ø  Maoni. Mwalimu aeleze kufaulu kwa somo lake, kukamilika ua kutokamilika kwa hilo somo.

 

 

Mfano wa mpangilio wa somo

Tarehe Wakati Kidato Somo Idadi
19.6.2001 8.00-840 3 Kiswahili 42

Funzo              :           Kusikiliza na kuongea

Sehemu           :           Misemo

Shabaha

1.      Wanafunzi waweza kueleza maana ya semi mbalimbali za Kiswahili

Wanafunzi waweza kutumia semi mbalimbali kutunga sentensi sahihi

Marejeleo

1. Ya mwalimu

Ndalu na King’ei

Kamusi ya semi za Kiswahili KIE Kiswahili kwa kidato cha tatu mwongozo wa walimu uk. 39.

Ya wanafunzi

KIE, Kiswahili kwa kidato cha tatu , mwongozo wa mwalimu uk 39

2 Ya wanafunzi

KIE, Kiswahili kwa kidato cha tatu kitabu cha wanarunzi uk 50-51

 MFANO WA MWENDELEZO WA MASOMO

Hatua Muda Kazi ya mwalimu Kazi ya wanafunzi
Utangulizi 1 Dakika 5 Kuwaongoza wanafunzi kueleza maana ya fumbo na aina za mafumbo Kueleza maana ya fumbo na kutaja aina mbalimbali za mafumbo
11 kiini Dakika 30 Kuwauliza wanafunzi wataje semi wanazo fahamu na maana zake  Wanafunzi watoe mifano ya semi na kueleza maana zake
    Kuwaeleza wanafunzi kutambua semi zinazorejelewa katika makala Wanafunzi wasome makala na kutambua semi zilizomo
Kueleza maana za semi zilimo katika Uk. 50 wa marejeleo ya wanafunzi na ukurasa 39 wa marejeleo ya mwalimu Wanafunzi wasome makala na kutambua semi zilizomo.
Mwalimu asahihishe kazi ya wanafunzi huku akiwasaidia walio na matatizo Wanafunzi maana ya semi zilizo katika ukurasa 50 wa marejeleo ya wanafunzi
Kurejelea yale yaliyofunza kwa ufupi Wanafunzi watunge sentensi madaftarini mwao wakitumia semi walizopewa
III HITIMISHO Dakika 5 Kurejelea yale yaliyofunza kwa ufupi Kusikiliza na kujibu maswali

 

MALENGO/ SHABAHA YA UFUNDISHAJI

Lengo au shabaha ya funzo

Aingiapo darasani kufunza mwalimu yeyote yule hutarajia kueleza au kufafanua mada au kitu fulani ili wanafunzi kuelewa anachotarajia kufunza katika kipindi fulani ili . Anachotajia kipindi fulani huwa ndio malengo au shabaha na malengo haya kufundisha yake yanaaishwa katika vipengele vitatu   kama ilivyo katika masomo mengine. Vipengele hivi ni:

a.       malengo tambuzi (cognitive objectives)

b.      malengo yenye athari/mguso/hisia(affective objectives)

c.       malengo ya musuli-mwendo nafsia(psychomotor objectives)

a)      Malengo tambuzi (cognitive objectives)

Haya ni malengo ya kumwezesha mwanafunzi kutambua,  kukumbuka na kutambua maarifa mapya na kuyajua ila aweze kuyaeleza akiuzwa. Anakuwa na uwezo wa kiakili wa kutambua stadi husika ili aweze kuzifafanua anapoulizwa. Malengo mengi ya walimu hupatikana katika kipengele hiki kwa sababu ni rahisi kutunga maswali ya utambuzi wa maarifa. Isitoshe, mifumo yetu ya elimu hasa lugha huzingatia sana utambuzi wa sarufi, mtindo, msamiati na kadhalika

b)     Malengo yenye athari/mguso au hisia

Haya nayo ni malengo yanayomwezesha mwanafunzi wa Kiswahili kupenda lugha fasaha na kuifurahia aisomapo popote pale. Anaweza pia akaathiriwa na wahusika shujaa na werevu, wajanja, wenye maadili mema na kadhalika. Haya hutokana na vitabu vya Kiswahili vinavyoweza kumuathiri mtu sana ili awe mwenye maadili mwema, mwenye kupenda kushirikiana na wenzake na kadhalika. Malengo yenye kuathiri tabia za wanafunzi ili ziwe nzuri zinazokubalika na jamii husika

c)      Malengo ya musuli-mwendo-nafsia (psychomotor objectives)

Malengo haya humwezesha mwanafunzi kufanyia  kazi misuli au sehemu za mwili wake kiustadi huku akionyesha umahiri wake. Kwa mfano anapotoa ulimi, ufizi, meno, nyuzi, sehemu za mdomo na kutamka maneno ya Kiswahili kwa ufasaha mkubwa .Ama  kwa mfano mwingine anapotumia mikono,uso,macho,kichwa,mabega na miondoko  mbalimbali kuwasilisha jumbe tofauti tofauti. Anapotumia viziada lugha (paralinguistic features) katika mawasiliano,

 

Matumizi ya malengo

 

Malengo ya somo au funzo hutumiwa kwa namna tatu muhimu

a.       Hutumiwa kutathmini ufundishaji. Kutathmini kama mwalimu amefundisha vyema ni kupima kama mwanafunzi / wanafunzi wameelewa kilichokuwa kinafundishwa. Kwa hivyo malengo hutueleza kile ambacho mwanafunzi ataweza kufanya baada ya  kipindi husika.

b.      Malengo huelekeza ujifunzaji wa wanafunzi au mwanafunzi. Huwambia matokeo ya ujifunzaji yatakuwa yapi ikiwa ufunzaji utafanikiwa .Kwa hivyo humpa au huwa kigezo ambacho kwacho wanaweza kujipima na kujua maendeleo yao ya ujifunzaji

c.       Malengo yanaweza kuwa kigezo cha upangaji wa kazi ama somo zima ama mwalimu anaweza kuyatumia kupimia kufaulu au kutofaulu  kwa somo lake  ili  abadilishe mbinu yaufundishaji. Kwa mfano atangulize mada na vijimada vipi? Ashughulikie na kuacha mada zipi? Awasilishe vipi hatua zake za ufundishaji? Ama atumie nyenzo na vifaa vipi ili afanikishe zaidi ufunzaji?

d.      Malengo huwasilisha jumbe kwa walimu wengine. Malengo huwezesha walimu tofauti kuwasiliana na wenzaokuhusu  vipindi, mada, masomo, na kozi wanazofundisha.Hii ni  kwa sababu matini yanayofundishwa ni sehemu tu ya mtaala mzima wa mfumo fulani wa elimu.

 

Vijisehemu/vijenzi vya malengo ya ujifunzaji (component of a learning objective)

Lengo la ujifunzaji lina vijenzi au vijisehemu vitatu navyo ni:

Ø  Tabia ya mwisho tarajiwa (terminal behavior)

Ø  Hali za kijarabati/majaribu (test conditions)

Ø  kiwango(standards)

 

a.Tabia ya mwisho tarajiwa

Hii ni sehemu ya lengo inayoeleza tabia ambayo mwanafunzi aliyeelewa afaa aidhihirishe.Ni tabia inaonyesha kile ambacho atakuwa na uwezo wa kufanya ili kudhihirisha kwamba amejifunza. Tabia hapa ni utendaji wowote au shughuli ambayo inaweza kutazamwa na kurudiwa. Mifano:

Taja sehemu za sentensi sahihi

Chora kinywa cha mtu anayetoa sauti aah

Tamka tangazo la kiashara 

Tabia ya mwisho tarajiwa huelezwa kwa kutumia vitenzi-vitendo(action verbs).Mifano ni eleza,pima,andika,chora,ainisha,tenganisha,tofautisha,linganisha,pango, taja orodhesha, toa sababu,pendekeza na kadhalika. Mwalimu anayeandaa malengo ya ufundishaji au ujifanzaji sharti ajaribu maswali yafuatayo:

1. Natarajia mwanafunzi kuwa na uwezo wa kufanya nini

2. Ni Kwa nini jinsi gani mwanafunzi atadhihirisha kwamba amejifunza

 3. Nitakubali kutekeleza kupi kwa mwanafunzi kama ushindi tosha kuwa   amejifunza?

 

b.Hali za kijarabati/mijarabu(test condition)

Hali nayo ni sehemu ya lengo inayoeleza hali ambayo kwayo mwanafunzi sharti adhihirisha tabia ya mwisho tarajiwa navyo ni:

I. Hali za vifaa anavyotarajiwa kuwa navyo kama nyenzo kama ramani,vitabu vya kiada,vikokotezi,rula,kalamu,karatasi na kadhalika .

2. Muda wa kujibu maswali,dakika tano,kumi, thelathini n.k

3. Jinsi ya kuwasilisha majibu: kumaongezi kuorodhesha, kutaja,kuandika insha kuchora,majedwali,michoro,kupanga, kivitendo n.k

 

c.Kiwango (standands)

Hii nayo ni sehemu inayoonyesha kiwango cha chini cha utendaji ambacho ni kubalifu kuwa ni ushandi kwamba ujifunzaji wa kilichotarajiwa umetokea. Mifano:

1. Toa sababu sita za

2. Andika vivumishi vyovyote tano

3. Andika insha”mwizi” isiyupungua maneno mia mbili.

STADI ZA LUGHA

Katika ufundishaji wa lugha yoyote ile ikiwemo Kiswahili, stadi zinazozingatiwa ni nne, nazo ni;

Kusikiliza, kuongea na kusoma na kuandika. Kila mojawapo ya stadi hizi ina umuhimu wake katika kufanikisha ujifunzaji wa lugha.

Kusililiza

Hii ndiyo stadi ya kwanza na ya kimsingi . Ili kuzikuza stadi zile zingine, ni lazima mtu aweze kusikiliza yanayosemwa, ni vigumu kwa mtu asiyekuwa na uwezo wa kusikiliza kuweza kusema/ kuongea.

Kuongea

Hii ndiyo stadi ya pili na ya kimsingi kufunzwa . baada ya mtu kusikiliza anaweza kuongea kwa kuiga sauti zile ambazo amezisikia.Ni muhimu hata hivyo huku kuongea kusiwe tu ni kutoa sauti za maneno , ni sharti ziongozwe na kanuni za lugha ili mawasiliano yaeleweke.satdi za kusikiliza na kuongea huambatana sana.

Kusoma

Hii ndiyo stadi ya tatu muhimu kukuzwa katika ujifunzaji wa lugha. Kusoma kunahusu kutambua na kufahamu yale yaliyoandikwa kwa kuyatamka kimya , kwa sauti au kwa kuguza

( kwa vipofu). Stadi ya kusoma hukuzwa katika viwango mbalimbali kutegemea kiwango cha mwanafunzi, umri wake, na darasa la mwanafunzi.

 

Kuandika

Hii ndiyo stadi ya nne kukuzwa baada ya kusoma. Kuandika ni uwezo wa kunukuu ishara za lugha na kubuni mawasiliano kwa ishara hizo. Stadi ya kuandika ni changamano mno na huhusisha sehemu kadhaa za mwili. Msingi bora katika stadi zile zingine ni muhimu katika kukuza satdi hii ya kuandika.

 

UJIFUNZAJI WA KISWAHILI

Mtu anaweza kujifunza au kufunzwa Kiswahili kama lugha ya kwanza, ya pili au ya tatu.Tutashughulikia ujifunzaji wa kiswahili kama lugha ya pili au ya tatu.

 

Lugha ya Pili

Hii ni lugha ambayo mtu anajifunza baada ya kujifunza lugha ya kwanza. Mbinu za ufundishaji au ujifunzaji walugha ya pili ni tofauti kabisa na za lugha ya kwanza.Tofauti ni kuwa ili kuifunza lugha ya pili, ni lazima ifanywe kuonekana kukaribiana na lugha ya kwanza kama iwezekanavyo.

MBINU NA STADI ZA KUFUNDISHIA

 

Ufundishaji wa Kiswahili kama ulivyo wa lugha nyinginezo huhitaji mwalimu kutumia mbinu kadhaa ilimuradi ufundishaji wake ulete matokeo mema. Sababu ni kuwa mwanafunzi wa Kiswahili katika kiwango chochote kile anahitajika kutamka maneno mapya ipasavyo;kuyaendeleza vilivyo; kujua maana yake, kuunda vishazi(clauses) na virai (phrases) ;kuunda sentensi ambatano  compound sentenses) n.k.

Haya yote hufanywa kupitia matamshi sahihi na fasaha na kuandika Kiswahili sanifu na fasaha. Mwalimu hutumia mbinu na stadi nyingi ambazo zina ubora na udhaifu wake. Akijua ubora anaweza kuutumia ipasavyo ili afanikishe kufundisha kwake. Kwa upande mwingine akijua udhaifu wa kila mbinu anaweza kukwepa au kupunguza athari za udhaifu husika kwa somo lake. Baadhi ya mbinu hizi ni kama zifuatazo;

 

Mbinu ya mdahalo (discussion method)

Mdahalo ni mbinu ambapo wanafunzi hushugulika katika majadiliano ya hoja kiusomi huku wakisimamiwa na mwalimu. Wanafunzi hubadilishana hoja na mitazamo ilmuradi wafikie uamuzi au hitimisho fulani. Mdahalo huwa na sifa uamuzi bainifu zifuatazo:

1.      Kuna kubadilishana kwa hoja au mawazo kati ya mwalimu na mwanafunzi wake na hata miongoni mwa wanafunzi wenyewe.

2.      Mwanzoni mada huwasilishwa kwa wanafunzi ambayo wanaenda kuijadili

3.      Kila mwanafunzi darasani au kupitia vikundi hutoa hoja, sababu,maoni na kadhalika ili kuimarisha kujadili kwake.

4.      Mwalimu huwa ni kiongozi wa kuelekeza mdahalo, yaani kiongozi mkuu

5.      Wakati mdahalo umetolewa hoja na maoni tosha kikundi au darasa hufikia hitimisho

6.      Mwalimu hutumia mdahalo kupata hoja, mifano na maoni. Anaweza akafafanua baadhi ya mawazo ili yaeleweke wazi

Ubora wa mbinu ya mdahalo

Husaidia  kuleta uwazi wa masuala. Husaidia wanafunzi kutafakari na kugandisha (weka pamoja mawazo) huku wakitambua dhana muhimu. Huwazoesha wanafunzi kuelewa kuwa maoni tofauti sio kosa ni usomi tu na pia wanaelewa kuwa watu huuitaji vitu sawa kwa sababu tofauti ambazo zote labda ni kubalifu kwa jamii husika. Mijadala humwezesha mwanafunzi kuvumbua yale ambayo hajajua.Mijadala humfunza kutumia ushawishi badala ya vitisho na propaganda.Humwezesha kustahimili maoni yaliyo tofauti na yake. Kupitia mijadala kikundi hufanzana pamoja, hutoa maelekezo hugawana majukumu,huonyesha ilihamu zao,heshima na mawazo yao huku wakiziwasilisha maarifa yao kama hitimisho.

Udhaifu Wa Mbinu Ya Mdahalo

Udhaifa mkubwa ni kwamba mbinu hii huhitaji muda mrefu sana ambao ni nadra kupatikana katika harakati  za ujifunzaji wa lugha. Wanafunzi  wasioelewa Kiswahili vyema huchukizwa na midahalo kwa   sababu inawahitahi kutumia lugha yao hiyo mbovu huku wakichekwa na wenzao. Kwa hivyo wanafunzi wandani (introverts) na wasiofurahia Kiswahili huenda wasishiriki vilivyo.

 

Mbinu ya kuwapa kazi (assignment method)

Katika mbinu hii mada  za ujifunzaji hugawanywa katika vijimada na vijimada hivyo hugeuzwa kuwa kazi za kushughulikiwa na wanafunzi katika makundi.  Kila kikundi hutafitia  vijimada walivyopewa na kuwasilisha kazi iliyoandikwa kama makala. Kazi hizi(makala) huwasilishwa darasani na kutathiminishwa na darasa zima ikiongozwa na  mwalimu. Marekebisho hufanyiwa kazi zilizowasilishwa na kisha wanafunzi kusoma na kujifunza zaidi kazi zilizoboreshwa kazi andishi husaidia kupanga maarifa na upataji wa mambo makuu miongoni mwa wanafunzi. Husaidia pia katika maandalizi mema ya  kufanya mitihani. Ni mbinu faafu ya kufundishia masomo au vipengee vingi kwa wanafunzi viwango vya juu na  walio werevu na makini. Kuna aina nne za kazi. Nazo ni:

(i)                 Kazi za kimaandalizi (preparatory assignment)

Wanafunzi hupewa kazi za kuwaandaa kufanya kazi za baadaye. Baada ya kazi hizi mwalimu huongoza wanafunzi kujua urahisi wa kufanya kazi nyinginezo ambazo ni ngumu kiasi.Hizi ni kama kazi za awali.

 

(ii)               Kazi zinazo-wezesha kudurusu zaidi (study assignments)

Wanafunzi hupewa kazi za kuwawezesha kudururusu zaidi katika makundi ama kila mwanafunzi kibinafsi kazi hizi zinaweza kutofautiana kulingana na mahitaji na uwezo wa wanafunzi au kikundi. Kazi hizi zinaweza kuwa ukurasa mmoja; aya moja  sura moja, mada, mradi, zoezi, ripoti au jaribio (experiment). Mwalimu, huelekeza wanafunzi tu katika kuitekeleza.

(iii)             Kazi za kimazoezi (Revision assignment)

Kazi hizi ni za kuthibitisha (prove) au kurudiarudia zoezi (drill) la kazi ambayo tayari imefanywa na wanafunzi ili wamakinike kwayo zaidi. Kupeleleza na kupima usahihi ( check) wa mambo wanayo jua kupeleleza na kupima usahihi wa kuelewa kwao. Kazi za kimazoezi huandaliwa kimbele na mwalimu kwa kuzingatia malengo maalumu ya yaliyomo katika mafunzo yanayofanyiwa mazoezi.

(iv)             Kazi za kurekebisha.(Remedial assignments)

Lengo la kazi hizi ni kuondosha kuelewa kubaya na hoja dhai miongoni mwa wanafunzi kuhusu yaliyofundishwa. Hii ina maana sharti mwalimu achunguze na kufahamu, kuelewa kubaya na hoja  dhaifu za wanafunzi kabla hajawapa kazi za marekebisho. Sharti mwalimu ajihusishe na wanafunzi wadhaifu na wasiofanya vyema ajue matatizo yao na kuyapangia kazimarekebisho.

Sifa za kazi nzuri

sharti kazi ziwe wazi dhahiri zenye kuvutia na ziwekwe mipaka kabisa. Kazi hizi ziwe na changamoto tosha za kusisimua ilhamu ya wanafunzi. Sharti ziwe na uhusiano tosha na mada kuu zilizo kwenye silabasi. Sharti zivute upekuzi, udadisi na uchunguzi wa wanafunzi ama hamu zao za kukuza ilhamu nzuri kazi zisiwe pana sana kiasitcha kuwanyongonyeza na  kuwaletea uchoshi wanafunzi.

 

Mbinu ya  kudurusu ambako kumesimamiwa.(administered study method)

Katika mbinu hii wanafunzi husoma na kujifunza mambo mapya huku wakisimamiwa na kuelekezwa na mwalimu. Wanafunzi hujisomea na smara wanapokabiliwa na  shida kama kutoelewa sentenzi, neno, semi, method n.k. huenda mwalimu kwa  ufafanuzi zaidi au uelekezaji wake. Kama mwalimu haulizwi chochote yeye hutazama na  kuchunguza michakato ya kudurusu na kuwashauri.

Mbinu hii ni kama kufundisha na kuendeleza hali bora kabisa kabisa za  ujifunzaji huru wanafunzi hufundishwa jinsi ya kudurusu na  kuelekeza bidii zao za kiusomikatika kipindi maalumu cha kudurusu. Ni mchakato wa  kuwazoesha wanafunzi jinzi ya kudurusu huku mwalimu akidurusu nao na kusaidia wanafunzi wadhaifu katika kipindi cha kudurusu. Lengo kubwa huusisha kuwawezesha wanafunzi kupata na kutumiastadi mwafaka za kudurusu na kuwa wafundishaji wema.

Shughuli katika kudurusu kulikosimamiwa

Mwalimu huandaa mpango wa kivitendo ikiwa anatarajia kufaulu na kupata matokeo mema ya kutumia mbinu ya kudurusu. Anaweza kuandaa jinzi anapanga kufanya yafuato:-

i.                    Kuelekeza wanafunzi wapate mambo muhimu kutoka vitabuni.

ii.                  Kuwaelekeza wanafunzi jinsi ya kutumia vyema vitabu, ramani, michoro, piha, majedwali, chati duara zilizomo n.k. ikiwa watanikuta  vitabuni.

iii.                Kuwaelekeza wanafunzi jinsi ya  kuandika kumbu kumbu/ mambo makuu yanayotokana na wanayoyasoma. hili linawezesha wanafunzi kuandika hasa mihtasari ya wanayoyasoma ambayo nayo hurahisisha kuelewa kwao.

iv.                kuwafundisha kupitia uelekezaji jinsi ya kusoma haraka haraka na kuandika au kusimulia ripoti ya kilichosomwa.

v.                  Kugundua ilihamu maalum;uwezo maalum na tofauti za kibinafsi za wanafunzi wake na jinsi anapanga kutumia ugunduzi huo.

Ubora wa mbinu hii

(i)                 Stadi fulani muhimu za kufaulu kutumia mbinu ya kudurusu hupatika tu kupitia mazoezi yaliyosimamiwa. mwalimu huwezeshwa kutazama wanafunzi wake wakidurusu huku ukirekebisha udhaifu wao na  kuimarisha kufaulu kwao.

(ii)               Wanafunzi hufaidika kwa kushughulikiwa binafsi na  mwalimu. Na mwalimu huwaelewa wanafunzi wake kila mmoja na matatizo yake au mazuri/vipawa vyake kwa  kutambua mazoea yao.

(iii)             Utambuzi wa mazoea na tofauti z kibinafsi humwelekeza mwalimu jinsi ya kukabili mada za kufundishwa baadaye katika mipango ya mafunzo ya baadaye.

(iv)             Kusimamiakwa mwalimu huwezewsha mwanafunzi kutumia vitabu, makala na mada wazisomazo ipasuavyo.

(v)               Mbinu hii hukuza  uhusiano na uelewano mwema kati ya  mwalimu na mwanafunzi wake.

udhaifu

walimu wavivu wasioandaa wanaweza kujificha katika mbinu hii na kupoteza nafsi za ujifungaji za wanafunzi.

Mbinu ya maigizo na michezo(simulation and games) role playing and games

igizo ni kuchukua nafasi dhima ya mhusika fulani na kujifanya kuwa yeye.stadi za kutumika viziada lugha na kuandika hukuzwa kupitia mbinu ya kuigiza na kucheza. Mwalimu na wanafunzihuigiza nafasi ya mtufulani na  kuitenda. Ni kama kuchunguza dhima na nafasi za viongozi wachezaji wanawake, wanaume waoga, wajisiri wenye majikwezo wenye vitambi na na kuigiza dhima zao kwa lengo la kujifunza lugha au kuchewa na kufurahisha tu.

Michakato ya kutumia mbinu ya maigizo na michezo

i.                    Kutambua igizo au mchezo wenyewe. kwa mfano mwanasiasa au  “shairi la ngonjera.”

ii.                  Kuteua na kujadili stadi, maneno, semi, methali maswali, viziada lugha vitumiwavyo na wanasiasa  au katika michezo ya ngonjera.

iii.                Kuteua wanafunzi wahusika katika igizo husika au ngonjera husika.

iv.                Upangaji wa igizo au ngonjera. Mhusika gani aanze wahusika wapi waendeleze au hatua zipi zikuze igizo au igizo au ngonjera. mhusika yupi atamatishe.

v.                  kuamua michakato ya kutadhimini igizo au ngonjera. uasili, uhalisia, sauti, ufasaha na ulinganishi na hali halisi. muda mafunzo yapatikanayo vipengele vya upataji lugha; ilihamu na mvuto n.k

vi.                michezo sharti iwe na mafunzo ya kijumla nay awe changana endelevu. sharti ikuze lugha kimsamiati kimuethali ruwaza za sentenzi kiufasaha n.k

Mambo muhimu: tahadhari

a.       Igizo au mchezo uwe na shabaha maalumu za kielimu.

b.      Igizo au mchezo ushirikishe wanafunzi wengi. vikundi ili kuwa na washiriki wengi.

c.       Muda uwe wa kutosha kipindi husika

d.      Mwalimu afanye zoezi la awali kuhakisha muda hautoshi au kupunguza muda ili apate muda unaohirajika.

e.       Igizo au mchezo unaweza kufanywa katika awamu kuwa mrefu sana.

Ubora wa maigizo

i.                    Huwapa wanafunzi fursa ya kusuluhisha matatizo ambayo wanakumbana nayo wakati wa kuigiza.

ii.                  wanafunzi huridhika wakati wanatambua umairi wao mpya wa kuzua mawazo na dhana mpya maigizoni.

iii.                uigizaji humweka mwanafunzi katika  mazingira halisi ya kutumia Kiswahili kama kinavyotumiwa na wengine.

iv.                mwanafunzi humotishwa kwa kushiriki kivitendo katika  uigizaji toshelevu.

Udhaifu wa maigizo

i.                    Ni vigumu kupima hisia za wanafunzi Kiswahili kuhusu maigizo.

ii.                  Uigizaji na michezo huchukua muda mrefu.

iii.                Ni vigumukutumia maigizo ili kutatua  tatizo.

iv.                Wakati mwengine sio rahisi kupata waigizaji shupavu miongoni mwa wanafunzi.

v.                  Sio rahisi kufundisha maigizo na michezo ya kukuza lugha kama mwalimu hana ujuzi wa kufaragua.

Mbinu ya kufundisha kwa zamu. (team teaching method)

Katika mbinu hii walimu kadhaa hufundisha darasa moja katika vipindi tofauti. ama wanafunzi waweze kuwekewa katika vikundi kulingana na kuelewa kwao uwezo wao ilihamu zao wielekeo yao matatizo yao ya kilugha nakadhalika, kisha wakafundishwa kila kikundi na mwalimu aliyestadi sana. Kila malimu kuingiliana ipasuavyo na kikundi chake na kutatua matatizo ya kila mmoja wao. Walimu hawa huandaa shabaha za kufundishia kila kikundi ambazo zinasawazishwa na mwalimu kiongozi. Idadi na utaalamu wa walimu husika hufiwa maanani ili ulingane na mahitaji ya vikundi au na vijimada. Muda wa kila kikundi husawazishwasharti yalinganishwe na shughuli za ujifunzaji za kila kikundi. Madazinazogawiwa walimu zilingane na taaluma na ilihamu yao. Kiwango na mtindo wa ufundishaji uwe faafu kwa kikundi.

Ubora wa mbinu ya kufundisha kwa timu/zamu.(heuristic or discovery method)

Katikambinu hii mwanafunzi huachiwa nafasi ili atatue matatizo yake mwenyewe. Mwanafunzi huhitajika kutumia kudadisi dadisi mazingira kutokana na uwezo wake wakimaumbile (Instinet). Hupata elimu kupitia kupekuapekua kwa yanayomzunguka. Anajitazama kuchunguza mazingara huku akifanya majaribio. Wanafundishwa na mwalimu jinsi ya kuvumbua mambo, kanuni na sheria, jinsi kuweka katika mfumo maarifa ajifunzayo na kufikia majumui kupitia bidi yao mwenye.

wanafunzi wawapo darasani wanaweza kupewatatizo lililo sawa ili wote walitatue. kila mwanafunzi hujua jukumu la kutafuta njia za kutatua tatizo. kila mwanafunzi huruhusiwa kutembea darasani akiongea na wenzake jinsi ya kutatua tatizo waliopewa. Mwanafunzi huhimizwa kuuliza maswali mengi iwezekanavyo ambayo majibu yake yeye mwenyewe huyatafuta. Wanafunzi hutumia stadi za  kujitazama kimakini huku wakifanya majaribio na kurekodi matokeo. baadaye hufiia majumui na  mifumo ya maarifa waliyojifunza wao wenyewe.

Walimu wanatarajiwa kuwa na ghala la maarifa na habari. lakini wasaidie wanafunzi padogo sana. Anatakikana awe mwelekezaji mzuri;akiwapa uelekezaji mdogo tarajiwa. Awaulize tu maswali ya kuelekezahuku wakati mwengine ikihurumia tu wale wanaoshindwa kutatua matatizo. wanafunzi wanaweza kuuliza wagundue sheria zinazohusu:-

i.                    Uundaji wa maneno ya Kiswahili       –           K+V+K+V

K+I+K+I

ii.                  Uundaji wa sentensi sahihi

iii.                Utohozi wa istilahi za Kiswahili

iv.                Minyambuliko ya vitenzi vya  Kiswahili

 

Ubora wa mbinu ya uvumbuzi.

a.       Mbinu ya uvumbuzi husaidiakatika ukuzaji wa mielekeo ya kisayansi na moyo wakuchunguza kufanya majaribio.

b.      Mbinu hii hukuza utendaji kazi kwa bidii miongoni mwa walimu na wanafunzi wao.

c.       Michakatoya kujifunza hukuza  kujitegemea kujiamini, na  kujishughulisha miongoni mwa wanafunzi.

d.      Maarifa hupatikana kupitia tajriba zilizotoka na mikutadha faafu.

Udhaifu wa mbinu ya uvumbuzi

a.       Huchukua muda mrefu huku ikiruhusu makosa mengi kufanywa yanayomuhusu mtu hoja na kuhakikisha kunakoendelea bila kusahihishwa haraka.

b.      mbinu hii haifai kwa wanaoanza kujifunza tu.

c.       mbinu hii ni ya kiteknikali na kisayansi mno kiasi kwamba ni vigumu musali wa kiwango wastani kuitunia vyema.

 

UFUNDISHAJI WA FASIHI

Utangulizi

Kimsingi, ufundishaji wa fasihi ni daraja ya juu ya ufundishaji wa kusoma kwa ziada. Kwa hivyo, masomo haya mawili na malengo yanayoingiliana na hutumia mbinu sawa.

Kuna aina mbili za fasihi. Fasihi simulizi na fasihi andishi. Madarasa ya fasihi yanamuweka mwanafunzi katikati ya taarifa za midomo na maandishi. Anaelekezwa jinsi ya kuchunguza na kuzichambua hizo taarifa ili apate kufahamu ujumbe uliomo na utamu wake. Katika sehemu hii kutatolewa mwongozo wa namna ya kufundisha aina hizo mbili za fasihi.

 

Kwa nini fasihi ifundishwe?

Fasihi ni somo ambalo ni muhimu sana kwa sababu zifuatazo

Ø  Ni kioo cha jamii humfahamisha mwanafunzi kuhusu mila na  tamaduni za  jamii

Ø  Humuwezesha mwanafunzi kufahamu tamaduni za watu wengine. Hivyo, ataweza kuwaelewa na kuwavumilia watu  walio na amali tofauti na zao.

Ø  Husaidia  kukuza kiwango cha lugha cha wanafunzi. Katika fasihi kuna kuna  umbuji na matatizo ya namna kwa namna ya nahau na misemo. Hii hujenga ukwasi wa lugha ya mwanafunzi na kumzidishia uwezo wa kujieleza.

Ø  Hujenga uwezo wa mwanafunzi kuyatafakari mambo na kuchambua hali ilivyo katika maisha ya kila usiku. Fasihi humpa mwanafunzi jicho  la upekuzi.

Ø  Humtayarisha na kumsaidia mwanafunzi kukuza kipawa chake cha uandishi wa kubuni.

Ø  Humzusha mawazo kuhusu maswala nyeti yaliyoko katika jamii anamoishi mtu yatakayosaidia kuijenga jamii hiyo.

1.      Uchaguzi Wa Vitabu Vya Fasihi Shuleni

Ni vitabu gani vinavyofaa kutumiwa katika somo la fasihi?

Vitabu vinavyofaa kwa fasihi ni vile ambavyo:

Ø  Vitawaongezea wanafunzi maarifa na kuwa changamoto kwao ili watafakari mambo mbalimbali yanayomwathiri binadamu.

Ø  Vimeandikwa kwa lugha , nzuri yenye mnato lakini iliyo ya kiwango  kilichokusudiwa. vitabu hivyo vizingatie maudhui yasiyopitwa na nyakati na viwe vile vinavyoweza kupata ukubalifu kimataifa.

Ø  vinahusisha aina mbalimbali za vitabu, mathalan, tamthilia, riwaya, hadithi fupi, tawasifu na diwani.

Ø  Havizingatii tu  utamaduni fulani na kupuuza zingine

Ø   Vinahusisha aina mbalimbali za vitabu, mathalan, tamthilia, riwaya, hdithi fupi, tawasifu na diwani.

Ø  Havizingatii tu utamaduni fulani na  kupuuza zingine.

Ø  Vinaeleweka kwa urahisi na visiwe na utata kwa sababu ya msingi yake ya kijamii au utata wa kiisimu.

 

2.         Maswala Yanayozingatiwa Katika Ufunzaji Wa Fasihi

(a)   Nadharia

Ili mwalimu wa fasihi  afaulu kutoa tahakiki inayowafaa wanafunzi wake, lazima ajihami na silaha ya kufanya kazi hiyo; na silaha yenyewe ni nadharia za fasihi. Kila wakati, mwandishi au mhakiki anapotoa kauli yake huwa anaongozwa na  nadharia fulani kuhusu kile anachosema labda hata bila yeye kufahamu nadharia hizi. Sharti mwalimu ajitahidi kuzifahamu nadharia mbalimbali za fasihi ingawa anapofundisha hahitaji kumweleza mwanafunzi juu ya nadharia hizo.Zinabakia tu silaha yake inayomsaidia uchambuzi. Kuna nadharia nyingi za fasihi na kila siku nyingine zinazinduliwa.Mifano ya nadharia hizi ni udenguzi,udhanaishi,nadharia za kihistoria,mtazamo kike,uyakinifu wa kijamii,ubwege na upokezi. Mwalimu anapaswa kuchagua nadharia itakayofaa matini anayotaka kuhakiki.Uchaguzi huu utaelekezwa na matini husika pamoja na kile anachotafuta mhakiki.Aghalabu,matini nyingine huweza kuhakikiwa kwa kutumia nadharia zaidi ya moja.

(b)   Mtiririko

Katika kufundisha fasihi, hususan riwaya na tamthilia, mwalimu atalenga kuhakisha kwamba wanafunzi wanaupata vyema ule msuko wa matukio na  kuweza kuukumbuka. mwalimu anaweza kufanikisha jambo hili kwa  kufanya yafuatayo:

(i)                 Kuwaeleza wanafunzi  wasome  hadithi kimoyomoyo.

(ii)               Baada ya wanafunzi kujisomea hadithi zinazohusika, mwalimu atawaongoza kwa kusoma sehemu muhimu za vitushi vya hadithi.

(iii)             Kuwa na vipindi vya wanafunzi vya kuzisikiliza kanda na vipindi vya redio kuhusu vitabu vinavyohusika.

(iv)             Kuwauliza wanafunzi maswali yatakayorejesha kwenye hadithi.

(v)               Kuwahusisha wanafunzi kutoa muhtasari wa kila onyesho.

(vi)             Kusimulia hadithi za kikufu. Hii ina maana kwamba mwanafunzi mmoja ataanza kueleza sehemu ya hadithi iliyosomwa kisha anakatishwa ghafla ya mwingine anayeombwa kuiendeleza hadithi.

(c)    Wahusika

Mwalimu ana jukumu la kuhakikishakuwa wanafunzi wanaelewa wahusika waliotumika katika kitabu. Anaweza kuwaongoza  kufikia lengo hili kwa kuwahusisha wanafunzi kufanya yafuatayo:

 

(i)                 Vikundi vya wanafunzi vijadili maswali mbalimbali yatakayotolewa na mwalimu kuhusu wahusika fulani. Kwa mfano, kwa nini Ame na Zidi wanabadilika mara kwa mara katika tamthilia ya Amezidi?

(ii)               Makundi ya wanafunzi yaigize sehemu za  kitabu walichosoma.

(iii)             Wanafunzi waliocheza nafasi  za  wahusika fulani waulizwe maswali kuhusu vitendo walivyotenda, maneno waliyosema nadharia walizokuwa nazo.

(iv)             Kuendesha mjadala darasani kuhusu mhusika fulani. Katika riwaya ya Siku Njema tunaweza kupata mada hii. Kongowea Mswahili ni mhusika asiye na uhalisia

(v)               Wanafunzi wahusishwe katika zoezi la aundishi wa kubuni ambapo watamchukua mhusika mmoja kutoka kwa hadithi waliyosoma na kumweka katika mazingira tofauti.

d) Maudhui

Maudhui ni yale muhimu yanayojitokeza katika kazi za fasihi. Mwalimu hapaswi kuwaeleza wanafunzi maudhui yanayopatikana katika kitabu walichosoma. Ni bora ikiwa atawaelekeza tu ili wayagundue na kuyafahamu hayo maudhui wenyewe. Mwalimu anaweza kufanya yafuatayo:-

            i.            Kuwaongoza wanafunzi kuchambua maandishi waliyosoma kwa kujibu maswali kama. Ni jambo gani linalotajwa kila mara katika sura hii? Nani anaonekana kujali sana jambo hilo? Ana mwelekeo gani kuhusu jambo hilo limeshatajwa hapo mbeleni katika kitabu hiki? Lilielezwaje wakati huo? Unafikiri mwandishi ana mwelekeo gani kuhusu jambo hili mwelekeo wako ni upi?

          ii.            Wanafunzi wawekwe katika vikundi na wajadili na kuorodhesha maudhui yanayojitokeza.

        iii.            Wanafunzi waandike insha zinazohusu masuala tata na telezi katika maudhui ya kitabu walichosoma.

e) Mbinu

Mwalimu anatakiwa kuwa ameshawafundisha wanafunzi mbinu mbalimbali zinazotumika katika fasihi kabla ya kuwauliza kuzitambua. Haya huwa katika masomo ya utangulizi yanayokuja kabla ya uchambuzi wa matini za kifasihi. Kwa mfano:-

              i.            Jazanda

            ii.            Majazi

          iii.            Methali

          iv.            Kejeli

            v.            tamthilia tangulizi

          vi.            Viona mbele na viona nyuma

        vii.            Sadfa

      viii.            Ndoto

f) Mfunzo

Hakuna haja ya kusoma kitabu cho chote cha fasihi ikiwa hakutawepo juhudi za kupata mafunzo fulani yanayohusiana na maisha. Mwalimu atawasaidia wanafunzi kwa kufanya yafuatayo:-

        i.            Kuwauliza maswali kwa mfano “Ungefanya nini kama ungekuwa mhusika fulani?” Umeshamwona mtu aliyemkubwa na hali kama hii? Jamii inafunzwa nini katika kisa hiki?

      ii.            Majadiliano katika vikundi

    iii.            Uandishi wa kubuni kwa mfano kiandike kisa cha tamthilia ya Amezidi kama kilichotokea katika kitongoji chenu.

Baada ya kutalii kwa kujumla yanayohitaji kuzingatiwa katika ufundishaji wa fasihi, sasa tutarejelea ufundishaji wa kila utanzu. Sehemu hii itazingatia ufundishaji wa fasihi simulizi, riwaya, tamthilia na mashairi.

Ufundishaji wa fasihi simulizi  

Kufundisha fasihi simulizi kunategemea sana kuifahamu dhana yenyewe ya fasihi simulizi na taaluma zake. Fasihi simulizi ina tanzu za mashairi, methali, nyimbo, mafumbo ngano, visasili, maghani na misemo. Lakini ikiwa ni fasihi simulizi kwa Kiswahili tutarejelea fasihi ya kabila jingine lolote tukitumia lugha ya Kiswahili. Ufundishaji wetu unatakiwa umwezeshe mwanafunzi kuwa na nadharia madhubuti za kumfanya aitambue dhana ya fasihi simulizi na kanuni mbalimbali zinazoitawala dhima na thamani yake katika jamii. Pili, ni kuwa na sehemu ya umbuji, utumizi na uenezaji wa fasihi hiyo.

 

Itambidi mwalimu achague mada za kufundishia somo lake kwa kutegemea uwezo na kiwango cha wanafunzi wake. Kwa mfano vipengele vinne vifuatavyo vinaweza kufuzwa katika kidato cha kwanza:-

            i.            Fasihi ni nini?

          ii.            Fasihi simulizi  ni zipi?/

        iii.            Tanzu za fasihi simulizi ni zipi?

        iv.            Thamani za fasihi simulizi ni zipi?

Ili kufaulu, ni vizuri kuanza na mambo yanayofahamika. Kila hatua moja inayoeleweka, itumiwe kupanua na kujenga hatua  inayofuata. Kwa mfano, wanafunzi watoe mifano ya methali ya vitendawili kisha ichambuliwe na kujadiliwa.Mbinu nyingi zaweza kutumiwa kufundishia fasihi simulizi. Jambo la kimsingi ni kuwa mwalimu na mwanafunzi washiriki katika utendaji kwani fasihi simulizi huhusisha utendaji mwingi kwa mfano:

(i)                 Mwalimu na mwanafunzi wajadiliane kuhusu vipengele mbalimbali vya fasihi simulizi.

(ii)               Wanafunzi watoe mifano kutoka kwa jamii zao.

(iii)             Wanafunzi wajadili wao kwa wao katika vikundi.

(iv)             Mihadhara ya wataalam wa fasihi simulizi au wasanii iandaliwe.

(v)               Wanafunzi wahudhurie shughuli za kitamaduni zinazozingatia na kutumia fasihi simulizi.

(vi)             Kuandaliwe warsha za utunzi, uchunguzi au uhakiki wa fasihi simulizi za darasa, shule moja au zaidi.

(vii)           Kuandaliwe tafrija ambazo zitaonyesha matumizi na ibara za fasihi simulizi

(viii)         Walimu na wanafunzi wajenge kumbukumbu ya uchunguzi wa fasihi simulizi ambayo wanaweza kuitumia katika shughuli zao za marejeleo.

Ufundishaji wa mashairi

Sehemu ya mashairi imeteteresha nguvu za walimu wengi katika kufundisha Kiswahili. Matokeo ya ufundishaji wao ni kwamba hata wanafunzi wameyaona mashairi kuwa ni magumu, makavu na yasiyo na mvuto. Baadhi ya walimu hulifanya somo la mashairi lionekane kuwa gumu na kavu kutokana na uteuzi mbaya wa mashairi na mtindo usiofaa wa kufundisha. Walimu hawa huchagua mashairi bila kujali kiwango cha wanafunzi pamoja na tajriba zao katika maisha. Athari ya jambo hili ni kukatisha wanafunzi tamaa na kuwafanya wachukie somo la mashairi. Ili kuwafanya wanafunzi walipende somo la mashairi, mwalimu anashauriwa achague mashairi yatakayowapendeza na kulingana na kiwango chao.

 

Mwalimu anapofundisha mashairi haifai awashirikishe wanafunzi moja kwa moja katika kuyachambua. Ni bora ayatangulize kwa utaratibu unaolenga kuwawekea misingi ya kuwawezesha kuelewa na kufurahia somo la hilo ushairi. Njia kadha wa kadha zinaweza kutumika katika kufundisha mashairi. Lakini ni bora kuelewa kuwa ufundishaji wo wote unapaswa kutekeleza shabaha nne.

 

Kwanza, ni kumfanya mwanafunzi avutiwe na ayapende mashairi, pili ni kumsaidia ayaelewe mashairi, tatu ni kumpa nafasi ya kufafanua na nne, kama ana kipawa au ameingiwa barabara na ushairi atunge mashairi ili aendeleze kipawa hicho. Misingi ifuatayo inaweza kutumiwa kufundishia ushairi.

a) Mvuto

Kufundisha mashairi kuanzie kwa kusoma mashairi maalum yanayoweza kuwavutia wanafunzi. Baada ya kufanya hivyo wanafunzi wapewe nafasi ya kutafakari kuhusu ushairi. Ni bora kuwauliza juu ya mambo yanayowavutia katika mashairi waliyoyasoma.

Njia zifuatazo zinaweza kutumika kuleta mvuto katika somo la ushairi.

 

        i.            Kusoma mashairi, kukariri na kuyaimba kwa mahadhi mbalimbali mashairi yanayopendeza kusomwa hivi na vikundi vya wanafunzi ni yale ya ngonjera

      ii.            Kutumia picha. Picha huvuta nadhari. Kama shairi lahusu viraka au uzee, mwalimu atafute picha kubwa inayoonyesha hali izungumziwayo.

    iii.            Kukusanya na kusoma mashairi kuhusu mambo mbalimbali kutoka kwenye vitabu na magazeti  ya Kiswahili.

    iv.            Wanafunzi wanaweza kukusanya mashairi wanayoona yanawavutia. Haya yanaweza kuchapwa kuandamana na picha za washairi hao maalum walioyatunga.

      v.            Wanafunzi wanaweza kujaribu kutambua mambo yanayosisimua katika ushairi na uhuru wa ushairi, mafumbo na urari.

b) Kuelewa

Haitoshi tu kutoa mazoezi ya ufahamu kutokana na mawazo makuu ya ushairi, mbinu nyingine zinaweza kutumika kukuza uelewaji wa mashairi. Wanafunzi wakijadiliana kuhusu mashairi hayo watayaelewa vizuri. Mwalimu anaweza pia kupanga uigizaji wa mashairi wanayosoma wanafunzi. Wanafunzi watapata nafasi ya kuona na baadaye kuzungumza na kujadiliana juu ya uigizaji huo.

c) Ufafanuzi

Ieleweke kwamba uchanganuzi wa mashairi unashirikisha yafuatayo

        i.            Uhuru wa kutumia lugha

a)      Mpangilio wa maneno ni kinyume ya jinsi yanavyopangwa katika maandishi ya kawaida

b)      Kiswahili cha mkato mkato au kuremba maneno

c)      Lugha ya mafumbo

d)     Msamiati unaotumika

ii) Muundo wa shairi

Mwalimu anaweza kuwataka wanafunzi wajibu maswali kama yafuatayo:

Ø  Shairi hili lina umbo gani? (Ni la unne, utatu, utano?)

Ø  Mpangilio wake ukoje?

Ø  Mwandishi amefuata utaratibu gani ili kuwasilisha ujumbe wake?

Ø  shairi lenyewe linafululiza moja kwa moja au limegawika katika sehemu mbalimbali?

Ø  Ikiwa shairi limegawika katika sehemu mbalimbali, hizo sehemu zinatengana vipi?

Ø  Muundo wa shairi hili unamguso gani wa hisia kwa msikilizaji?

Maudhui

Mwalimu ana jukumu la kuhakikisha kwamba wanafunzi wanazifahamu kunga mbalimbali za ushauri ili waweze kufahumu mashairi wanapoyasoma. Aidha, mwalimu ahakikishe kwamba wanafunzi wanaweza kutambua na kueleza maudhui ya shairi wanasoma. Ikiwa shairi lina maudhui mengi ni wajibu wake kuwaongoza wanafunzi kuyatambua maudhui hayo.

 

Mashairi huwa na maadili fulani kwa jamii. Baadhi ya washairi huyataja maadili wanayokusaidia moja kwa moja. Hata hivyo wakati mwingine inambidi msomaji mwenyewe kufikia uamuzi juu ya maadili yaliyokusudiwa.

d) Utunzi

Utungaji wa mashairi bora ni kipawa walicho nacho waandishi wachache. Yarahisishwe iwezekanavyo hasa pale mwanzoni. Yanaweza kuwa ya namna zifuatazo

i.                    Mwalimu anaweza kuwapa mshororo mmoja au miwili kisha akisaidiana nao, watunge mshororo wa tatu

ii.                  Wanafunzi waongozwe kutunga ubeti mmoja wa shairi na baadaye beti zaidi.

iii.                Mashairi yajadiliwe na kutungwa katika vikundi.

iv.                Walio na vipawa, wahimizwe kuendelea kutunga.

Kutamatisha somo la ushairi

Mwalimu anaweza kulitamatisha somo la ushairi kwa njia mbayo wanafunzi wake watafaidika. Kwa mfano yale yaliyo muhimu yakaririwe, shairi likaririwe au liimbwe kwa mahadhi mbalimbali.

 

Ufundishaji wa riwaya na tamthilia

Madhumuni ya sehemu hii ni kupendekeza na kujadili njia mwafaka ambazo zinaweza kutumiwa kusoma na kuvielewa vitabu vya riwaya na tamthilia. Hili limefanywa kwa kuzingatia ukweli kwamba tamthilia na riwaya na tanzu zenye mambo mengi yanayoweza kujadiliwa pamoja.

Kama ilivyoelezwa hapo awali ufundishaji wa riwaya na tamthilia au fasihi yo yote unahitaji mwongozo wa nadharia fulani ya uhakiki. Kimsingi, riwaya na tamthilia hutegemea nyenzo kuu maalum ili zijengeke. Ni kazi ya mwalimu kutumia mifano mbalimbali ili kuwafahamisha wanafunzi nyenzo hizo. Mwalimu atapaswa kushughulikia dhamira na maudhui, wahusika, mtiririko wa matukio, mazingira au mandhari, muundo na mtindo.

 

Katika kufundisha kipengele cha mazingira au madhari, mwalimu atilie maanani kwamba misingi ya fasihi imejikita katika jamii. Mwandishi ni mtu aliyezaliwa na jamii fulani, katika mazingira fulani, wakati fulani. Yale yote anayozungumzia yanatokana na tajriba yake katika jamii. Mwalimu wa fasihi awaelekeze wanafunzi katika muktadha wa kijamii na kihistoria ambao mwandishi anauzingatia katika kazi yake. Ili wanafunzi waielewe vyema tamthilia na mashetani ya Ibrahim Hussein, itabidi mwalimu aifunze kwa kurejelea historia ya Tanganyika na Unguja kabla na baada ya mapinduzi ya Januari 1964 na Azimio la Arusha la 1967.

 

Ikiwa ni wahusika, mwalimu azingatie vile wanavyojitokeza katika hadithi. Awasaidie wanafunzi kuutambua wasifu wan je na wa ndani wa wahusika hao. Wana sura au maumbile gani? Wana tabia gani? wametumiwaje? wana dhamana zipi? tabia/ wasifu wao itaonekana kwa kuzingatia vitendo vyao, lugha yao, mavazi yao, uhusika wao na wahusika wengine, na maelezo yanayolewa na wahusika wengine au mwandishi juu yao. Wanafunzi waelekezwa kuwatambua wahusika wakuu, wadogo, bapa, mviringo, foili, shinda na wengineo Mwalimu awape nafasi ya kujadiliana masuala nyeti yanayohusu wahusika.

 

Mwalimu ajailiane na wanafunzi kuhusu mtiririko wa matukio katika vitabu wanavyosoma. Baadhi ya maswali yafuatayo yanaweza kuzingatiwa

i.                    Kisa kinahusu kina nani?

ii.                  Ni matukio yapi yanayorejelewa?

iii.                Ni nani anayeelekea kutawala matukio?

iv.                Matukio haya yanasababishwa na nani?

v.                  Matukio haya yana uhusiano gani na yaliyotangulia/ yanayofuata

Kwa mujibu wa mafunzo haya, mwalimu aingize wazo la upeo au kilele. Mwalimu pia awaelekeze wanafunzi  kuitambua lugha ilivyotumiwa kujenga mtiririko, kisa, na hata kuibusha hisia  na maudhui mbalimbali.

hatimaye, kwa kuzingatia vipengele vyote vilipitiwa, mwalimu awasidie wanafunzi kuyatambua maudhui kwa  kuwapa maswali yanayowaelekeza kwa mfano:

Ø  Ni maudhui  gani yanayojitokeza katika katika kazi hii?

Ø  Maudhui ya kazi hii yanakuzwaje  na wahusika?

Ø  Maudhuiya kazi hii yaendelezwaje na lugha na mtindo uliotumika?

Ø  Ni migogoro gani inayojitokeza katika kazi hii?

Ø   Je migogoro hiyo imesuluhishwa?

Ø  Tunapata funzo gani katikakazi gani?

Fasihi inatakiwa ifundishwe kwa mtindo utakaowapa wanafunzi nafasi ya kuishi ukweli na uhalisia wa matukio mbalimbaliyasimuliwayo. Stadi zote za lugha kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika) zihusishwe. Wanafunzi wasikilize maelezo ya mwalimu, vipindi vya redio au kanda za  kaseti kisha wajadiliane kuhusu waliyoyasikia. Wasome vitabu na majarida mbalimbali, na  mwisho waandike na hata kuigiza waliyoyasoma.

 

Uchambuzi Wa Makosa Na Usahahihishaji

 

1.      Uchambuzi wa  makosa ya  wanafunzi

Wanafunzi wote wanaofundishwa lugha hufanya makosa. Makosa wanayofanya ni ya aina nyingi.  Baadhi ni ya maelezo, mengine ni ya matamshi, mengine ni uchunguzi au uteuzi wa msamiati, ilhali mengine ni ya kisarufi.

Walimu wana fikra mbalimbali kuhusu makosa yanayofanywa na wanafunzi wao. Walimu wengi huona kuwa, makosa ya wanafunzi wao bado hawajaimudu miundo fulani ya lugha. Kwa baadhi ya walimu, makosa yanatokana na kutojali kwa wanafunzi.

 

Baadhi ya walimu na watafiti wa masuala ya lugha ya pili, wanafikiri kuwa makosa ni muhimu kwani huonyesha njia anazopitia mwanafunzi katika ujifunzaji wake. Maoni ya kikundi hiki ni kuwa, makosa yakichambuliwa vizuri yanaweza kumsaidia mwalimu kuimarisha ufundishaji wake wa lugha.

 

a) Hatua muhimu katika uchambuzi wa makosa

i. Ukusanyaji wa makosa

Mwalimu hukusanya makosa wanayoyafanya wanafunzi wake kila siku. Haya yanaweza kuwa makosa ya kimaandishi au ya kimazungumzo. Kiasi cha makosa kitakachokusanywa kitamtegemea mwalimu mwenyewe. Mwalimu anaweza kuamua kukusanya makosa kwa wiki moja au mbili, au kutokana na kazi mbalimbali za wanafunzi katika darasa lake.

      ii.            Uainishaji wa makosa

Mwalimu anapomaliza kuyakusanya makosa, yeye huingilia jukumu la kuyaainisha. Katika hatua hii makosa hupangwa kwa kufuatia mantiki fulani kwa mfano, makosa yanayotokana na athiri za lugha mama:-

Ø  Nipatieko mbira nicheseeko

Ø  Yeye hunywa sigara nyingi

Ø  Sisi hukulanga chakula mingi.

Ø  Yeye ni mtu mwenye anapenda pombe sana

Makosa ya ujumlishaji wa sarufi ambapo viambishi muhimu vya lugha hudondoshwa

Ø  Aliruka kwa mguu –moja

Ø  Tulikata miti –tatu

Ø  Nilinunua visu –tatu

Ø  Nyumba tuna –ishi ni nzuri sana

Ø  Mungai na Mwangi –napigania kiti

Makosa ya kifonolojia ambapo sauti za Kiswahili hubadilishwa na sauti za lugha mama:-

Ø  Chakura chote kimeriwa na paka

Ø  Nasikia laa ndani ya loo

Ø  Alisema kwamba yeye akuwa mwogo.

Ø  Alimlipia mke wake mbuzi mbili na kondoo watatu kama mahali.

Makosa yanayotakana na uteuzi mbaya wa msamiati:-

Ø  Mbuzi wake walikula maji mingi

Ø  Kikombe chake kimekufa

Ø  Daniel alipinduka na kuumia vibaya sana.

Makosa ya kisaikolojia ambapo mwanafunzi hubadilisha vipengele vinavyopatikana katika lugha yake na vingine vinavyopatikana katika lugha ya pili anayojifunza:-

Ø  Alihumia sana alipojifunza

Ø  Alihapa kwamba hakuwa mwizi

    iii.            Kutafuta chazo cha makosa

Mwalimu anapomaliza kuanisha makosa katika viwango mbalimbali, hujaribu kutafuta chanzo halisi cha makosa hayo. Akishajua hayo, mwalimu atakuwa na nafasi nzuri ya kuwarekebisha wanafunzi wake. Atajua ni maelezo na mazoezi ya aina gani atakayowapa.

 

    iv.            Kutathmini makosa

Katika hatua ya mwisho mwalimu hutathmini makosa aliyoyakusanya miongoni mwa wanafunzi wake. Mwalimu huhesabu na kujua ni makosa yapi yanayotokea kwa wingi katika kazi na mazungumzo ya wanafunzi. Mwalimu pia atajua ni makosa yapi yenye uzito kuliko mengine na hapo kuamua yanayopaswa kupewa nafasi ya kwanza katika urekebishaji. Sababu muhimu ya chambuzi wa makosa wa aina hii ni kujaribu kuelewa mikakati wanayotumia wanafunzi katika ujifunzaji wao. Kwa mfano, wanafunzi anayefanya makosa yafuatayo atamfundisha mwalimuwake nini?

 

Umoja                                     Wingi

Dada                           Wadada

Ndugu                                     Wandugu

Mwanafunzi anayafanya makosa ya aina hii si mjinga. Anazifahamu baadhi ya kanuni za kugeuza nomino kutoka umoja hadi wingi. Kwa mfana, anajua kwamba katika ngeli ya M-wa wingi wa majina huonyeshwa kwa kutumia kiambishi wa-kwa mfano

Mtoto-             Watoto

Mtu     –           Watu

Mwanafunzi aliyetoa mifano yenye makosa hafahamu kikamilifu mipaka ya maneno ambayo yanapaswa kuwa na kiambishi wa-katika wingi hajui kwamba maneno kama ‘dada’ ‘na’ ndugu hayapaswi kupewa wa-katika wingi wake. Ni juu ya mwalimu kumfahamisha mwanafunzi huyo kanuni zilizo sahihi na kumpa mazoezi ya kutosha.

Ingawa uchambuzi wa makosa ni jambo muhimu ufundishaji wa lugha, siyo jambo rahisi wakati mwingine kupata chanzo kimoja cha kosa. Tuchukue kwa mfano, mwanafunzi anayetumia kiambishi (-nga) katika sentensi zake.

Anakujanga kwetu

Makosa ya aina hii yanaweza kuwa na vyanzo viwili. Mwanafunzi anaweza kuwa amethiriwa na lugha yake ya kwanza ambapo kitendo kinachofanyika kila siku au kila mara huasiriwa na kiungo (-nga). Matumizi hayo pia yanaweza kutokana na lugha kama inavyosikika mitaani. Mwanafunzi anayetumia kiambishi (nga) huenda asiwe na kiambishi kama hicho katika lugha yake kwanza, lakini huenda akawa anaitumia lugha kama anavyoisikia ikizungumzwa mahali anakoishi. Jambo hili linatuonyesha kuwa tunapaswa kuwa macho tunapojaribu chanzo cha kosa la mwanfunzi. Tusiwe wa kutaja chanzo cha kosa kabla ya kufanya utafiti wa kutosha.

 

Kwa ujumla, uchambuzi wa makosa wanayofanya wanafunzi utamfaa mwalimu wa Kiswahili ikiwa utamsaidia mwalimu huyo kutafuta suluhisho la matatizo yawanfunzi wake, na ikiwa utamsaidia mwalimu kujitayarishia vizuri ufundishaji wa vikundi vingine atakavyofundisha baadaye.

 

Usahihishaji

Usahihishaji ni hatua ya ufundishaji inayofuata punde wanafunzi wanapomaliza kufanya jaribio au mtihani. Mwalimu anapaswa kuwa makini anaposahihisha, la sivyo, kazi nzuri ya kufundisha aliyoifanya itaharibika. Sharti azingatie malengo ya usahihishaji na ateue na kutumikaza mikakati ya usahihishaji kwa makini ili wanafunzi wadaidike.

 

a)      Malengo ya usahihishaji una malengo manne makuu.

i.                    Kuongoza na kuwashauri wanafunzi

Usahihishaji wa kazi ya wanafunzi ni wa manufaa kwani huwaelekeza kutambua makosa waliyoyafanya. Licha ya kutambua makosa, wanafunzi hupata fursa ya kusahihisha makosa yaliyotokea. Kazi kuu ya mwalimu hapa ni kuwapa wanafunzi mbinu zitakazowawezesha kutorudia makosa kama hayo tena.

 

ii.                  Kutathmini ufundishaji

Usahihishaji una lengo la kumwezesha mwalimu kufahamu kama ufundishaji wake ulifaulu au haukufaulu. Mwalimu anaposahihisha kazi za wanafunzi atatambua ni dhana na mbinu zipi.

–          Amefundisha na wanafunzi wamezimiliki vilivyo.

–          Amefundisha lakini bado wanfunzi wengi wana matatizo nazo.

–          Jahafundisha lakini wanfunzi hawana shida nazo

–          Hajafundisha na wanafunzi wanatatizika nazo.

Habari hizi anazokusanya mwalimu wakati anaposahihisha kazi za wanafunzi huwa za manufaa sana anaporatibu kazi za siku za usoni. 

 

iii.       Ukadiriaji

Kila mara mwalimu anaposahihisha huwa anatuza na kurekodi alama za wanafunzi. Rekodi anayoweka humsaidia kukadiria maendeleo ya wanafunzi. uwezo wa mwanafunzi akiulinganisha na wanafunzi, uwezo wa mwanafunzi akiunganisha na wanafunzi wengine darasani, na nuwezo wao kwa mujibu wa viwango vya mitihani ya kitaifa. Shida kubwa inayojitokeza katika usahihishaji ni kuwa aghalabu walimu wengi huzingatia lengo la ukadiriaji na kupuuza hayo malengo mengine. Sharti mwalimu atofautishe kati ya tamrini za kufundishia na tamrini za kukadiria uwezo wa wanafunzi.

 

iv.       Motisha

Usahihi mzuri ni kichocheo kinachozidisha maradufu juhudi za wanafunzi ambaye daima kazi yake haisahihishwi na mwalimu au husahihishwa vibaya huwa hana motisha ya kustawisha utendaji wake. Lakini mwanafunzi anapobaini kuwa mwalimu ana makini na husahihishaji kazi yake na kumwelekeza vizuri, anapaswa nguvu na kujitahidi katika somo linalohusika. Mwalimu anapaswa kujua namna ya kutuza na kusifu kazi nzuri na kukosoa kazi isiyo nzuri bila kumwaziri mwanafunzi.

 

b)     Mbinu za ushahihishaji

Mbinu zinazotumika katika usahihishaji hutegemea sana aina ya maswali yaliyoulizwa. Kuna maswali ya kuchagua jibu sahihi, ya ufahamu, ya ufupisho, ya matumizi ya lugha na ya insha. Insha hujumuisha matumizi ya vipengele vyote vya lugha na huwa ni kigezo mwafaka cha kupimia uwezo alionao mwanafunzi wa lugha. kutokana na ukweli huu ni vizuri kufahamu jinsi insha inavyosahihishwa.

 

i). Namna ya kusahihisha insha

Katika kusahihisha insha mwalimu anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-

Maelezo/Maudhui

Hiki ndicho kiini cha insha kama ni insha ya methali, ya mjadala, ya usimulizi, ya barua au kubuni, mwandishi atatoa hoja zake kulingana na mahitaji ya insha anayoandika. Msahihishaji anahitaji kuona kama mwandishi anazo hoja za kutosha na kama amefuata muundo ufaao kwa aina hiyo ya insha.

 

 

Msamiati

Msamiati hurejelea lugha ambayo mwandishi anaitumia. Lugha inayofaa ni ile inayofafanua habari zinazoelezwa. Msahihishaji atapima jinsi mwandishi alivyotumia msamiati unaofaa, semi na fani nyinginezo za lugha.

Mtindo

Mambo yanayochunguzwa hapa ni kama mitindo sentensi, uandishi wa aya, matumizi ya alama za kuakifisha, mchanganyo wa semi halisi na semi taarifa, matumizi ya takriri na tanakali za sauti.

 

Sarufi

Baadhi ya makosa ya sarufi anayoadhibiwa ni kama:-

Ø  Mabadiliko ya umoja na wingi katika ngeli tofauti tofauti.

Ø  Mwafaka kati ya nafasi mbalimbali na matumizi ya vitendo mbalimbali.

 

Umoja                         Wingi

Ø  Nafsi ya kwanza               Mimi                            Sisi

Ø  Nafsi ya pili                       Wewe                          Nyinyi

Ø  Nafsi ya tatu                     yeye                             Wao

Ø  Matumizi ya vihusishi kama ‘amba,’- na’enye’ katika ngeli mbalimbali

Ø  Matumizi ya viunganishi

Ø  Matumizi ya vivumishi.

Maendelezo/ Hijai

Baadhi ya makosa y amaendeleo yanayoadhibiwa ni

Ø  Kuwacha ua kuongeza herufi

Ø  Kutenganisha herufi za maneno moja.

Ø  Kuunganisha maneno mawili

Ø  Kukata neon visivyo (mwisho wa mstari).

ii. Ushauri wa jumla kuhusu usahihishaji

Mwalimu anaposahihisha insha, itafaa akizingatia malengo ya usahihishaji wake. Ikiwa lengo ni kumwongoza na kumshauri mwanafunzi, mwalimu anaweza kufanya yafuatayo.

Ø  Aonyeshe makosa yote yaliyo kwenya kazi.

Ø  Apige mstari makosa yote  na  kuwauliza wanafunzi wayaasahihishe.

Ø  Arekebishe  baadhi ya  makosa na kupiga mstarichini yam engine.

Ø   Ateute makosa machache yaliyo nyeti na  kuyarekebisha.

Ø  Aamue kutoandika lo lote kwenye kazi atoe  maelezo fika kuhusumakosa yaliyomo.

Ø  Asahihisheakitumia alama za msimbo zinazoeleweka na wanafunzi.

Kwa mfano

S          –           kosa la sarufi

M        –           Kosa la mendelezo

Ms       –           kosa la msamiati

Mt       –           kosa la mtindo.

(iv) Matumizi ya kadi za marekebisho

kadi ya  marekebisho huwa  kadi kubwa  kubwa  ambayo upande mmoja ina mafundisho kuhusu kipengele fulani cha lugha, na upande wa pili kuna tamrini zinazokusudiwa kumzoesha mwanafunzi kutumiakipengele hicho kwa usahihi. Vile vile kunakadi ndogo za majibu zitakazomwezesha mwanafunzi kusahihisha kazi aliyoifanya na kurekodi alama alizopata.

Kadi kama hizi huwa zimetungwa kimbele zikiwa zinazingatia maeneo aambamo makosa mengi hufanyika kwa mfano, muundo, msamiati, uakifishaji na hijai. Wakati wa kusahihisha kazi ya mwanafunzi, mwanafunzi mwalimu hupiga mstari chini ya makosa yanayorudiwarudiwa sana na kuandikanambari ya kadi inayohusika kwenye pambizo ya karatasi.

MWISHO WA MODULI

 

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!