MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI

By , in KISWAHILI KWA WAGENI WALIMU on .

UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI

MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI

 1. Malengo ya ufundishaji lugha kwa wageni

Lengo kubwa ni kwamba ili mwanafunzi aweze kujua lugha hiyo kwa stadi zote za lugha ile. Stadi za lugha ni 1. Kusikiliza 2.kuzungumza 3. Kusoma  4.kuandika 5. Sarufi 6. Utamaduni wa lugha ile

Malengo ya jumla ya kufundisha Kiswahili ni pamoja na:-

 • Kumwezesha mwanafunzi ili aweze kumudu lugha.
 • Kumwezesha mwanafunzi aweze kuwasiliana na wazawa wa lugha husika

LUGHA YA KWANZA

Stern (1983) anasema kwamba “lugha ya kwanza lugha ambayo mtoto hupata kutoka kwa mama yake mzazi angali mchanga.

LUGHA YA PILI

Stern (1983) anasema kwamba “ lugha ya pili si lugha ambayo mtoto/mtu aliipata alipoanza kukua na kupata lugha. Hii ni lugha ya kujifunza,kwa maana ya kwamba mtu huyu huwa tayari ana lugha nyingine.mfano. hapa Tanzania Kiswahili ni lugha ya pili kwa watu wengi

LUGHA YA KIGENI

Ni ile lugha ambayo unajifunza na kuitumia lakini wazungumzaji wake wako nje ya nchi au mbali na jamii anapokaa mwanafunzi huyo. Mfano lugha ya kiingereza ni lugha ya kigeni hapa Tanzania

MALENGO YA JUMLA YA UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI WA LUGHA YA KIGENI

Mara nyingi hii hutegemea taaasisi yenyewe lakini kuna malengo ambayo ni ya jumla:

 • Kutaka kuwasiliana na wenyeji wa sehemu /nchi husika
 • Kujiandaa kusafiri kwenda nchi nyingine kwa shughuli mbalimbali
 • Kwa ajili ya kufanya biashara
 • Kukidhi vigezo vya masomo
 • Kufanya utafiti katika taaluma husika
 • Ili kupata ajira nchi za ng’ambo

KITU GANI KIANZE KUFUNDISHWA SASA?

Onyo: usijaribu kumfundisha mwanafunzi sarufi za lugha hiyo kwanza, utamfundisha ikibidi lakini isiwe kipaumbele chako

 • Anza na salamu za kawaida, salamu katika utamaduni wa mwafrika ni kitu cha muhimu sana, hivyo fundisha salamu,maana lengo ni kwamba huyo mtu aweze kuwasiliana.

MALENGO YA UJUMLA YA UFUNDISHAJI LUGHA YA KISWAHILI KWA WAGENI

 1. Ili mwanafunzi wa Kiswahili ajue mambo yafuatayo:
 2. Aweze kumudu lugha ya Kiswahili
 3. Aweze kuwasiliana na watumiaji wa lugha ya Kiswahili
 • Ili wanafunzi waweze kung’amua mambo yafuatayo:- Namna ya kusema jambo gani? Mfano anataka kwenda chooni Asemee wapi? Kwa nini aseme? Kwa nani aseme? Mazingira gani aseme?
 1. Ili kuwapa wanafunzi mbinu mbalimbali za kujifunza lugha ya Kiswahili. Wanafunzi wafanye kwa vitendo ili waweze kujichukulia misamiati ya kutosha
 2. Wanafunzi wang’amue umuhimu wa lugha wanayojifunza
 3. ili wanafunzi waweze kutimiza malengo haya, mwalimu ni lazima wape wanafunzi:

kuchunguza®kugundua®kutalii kuhusu lugha ya Kiswahili

 1. wape uwezo wa kukuza lugha ya Kiswahili kila siku aweze kuongeza msamiati kwa kusoma vitabu mbalimbali vya hadithi
 2. wape nafasi kutumia mbinu mbalimbali lugha ili kukuza uelewa wao
 3. wape uwezo wa kukuza fikra zao na kudadisi
 4. wasaidie kufanya utumbuizi wa vipengele vya mfumo na utamaduni wa lugha ya Kiswahili

NADHARIA KUU ZA UJIFUNZAJI LUGHA

Kuna mambo mawili ambayo waalimu tarajili  wanapaswa kujua

 • mbinu za kujifunza lugha ya pili ni nyingi kama ilivyo waalimu wengi
 • manzingira halishi wakati wa ujifunzaji. Rogers (2001) anasema kwamba “ wakati wa ufundishaji wa lugha ya kigeni hutumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wafikie malengo yao”

Kuna nadharia kuu nne (4)za ujifunzaji lugha:

 • NADHARIA YA HULKA
 • Mwasisi wake ni Noamy Chomsky (1957)
 • Wazo kuu lake ni kwamba: binadamu huzaliwa akiwa na uwezo Yaani kwenye ubongo wake ana mfumo ambao huzaliwa nao kwa ajili ya kujifunza lugha. Ana kifaa kinachoitwa LAD (Kifaa cha upataji lugha)
 • Naye Brown (2000) aliunga mkono mawazo haya. Mwingine aliyeunga mkono ni Ellis (1997) walikuwa na hoja kwamba kuna kipindi mtu akifikia umri Fulani hawezi kupata lugha sawasawa na wazawa wa lugha husika. Umri huo ni kuanzia 0-miezi 18. Kwa mujibu wa wataalamu hawa mazingira hayana msaada wowote katika ujifunzaji lugha.

 

 • NADHARIA YA UTABIA (BEHAVIORISM)
 • Mwasisi wa nadharia hii ni B Watson. Wengine wanaoshadidia nadharia hii ni Leornald Bloomfied, O.N Mowrer, B.F Skinner na A.W Staats
 • Edward Thorndike (1935) alikuwa wa kwanza kabisa kutafiti zaidi. Kwa mujibu wa wanatabia ujifunzaji wa lugha ni mwigo kwa maana ya kwamba huiga kile kinachosemwa na watu wanaomzunguka
 • Aliyetafiti zaidi katika nadharia ya ujifunzaji ni Burrhus Frederic (F) skinner , Huyu alikubali ni mwigo lakini akaongeza kuwa ni uimarikaji wa tabia, hivyo mtoto mdogo hazaliwi na lugha bali huichota kutoka kwa wazazi wake
 • Wilga Rivers (1968)anasema mtoto hujifunza kupitia kujaribu na kukosea “trial and error’ huendelea kufanya hivyo mpaka anapofikia matamshi ya jamii nzima.
 • Nadharia hii inayapa mazingira nafasi kubwa katika ujifunzaji lugha
 • Je mtu akitengwa na jamii anaweza kuwa na lugha?

 

 • NADHARIA YA UTAMBUZI
 • Nadharia hii iliasisiwa na Jean Piaget (1954)
 • Alidai kuwa binadamu anapozaliwa kuna kipindi maalum cha kupata lugha
 • Alidai kuwa kujifunza lugha ni sehemu ya makuzi ya binadamu, kwa kadiri unavyokua ndivyo unavyozidi kupata lugha
 • Alidai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya kuzaliwa.
 • Arth(2003) anadai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya kuzaliwa,kuanzia 0-miezi 18
 • Nadharia hii haipingani na umuhimu wa mazingira katika ujifunzaji lugha

 

 • NADHARIA YA UUMBAJI
 • Nadharia hii iliasisiwa na Jerome Brunner
 • Wazo kuu la nadharia hii inasisitiza nafasi ya mama katika upataji lugha ya kwanza
 • Mtoto hutengeneza lugha kutegemeana na mawasiliano ambayo mama yake anayatumia
 • Alidai, ili mtoto aweze kupata lugha ni lazima mambo yafuatayo yatimizwe
 • Muktadha
 • Tajiriba (experience)
 • Upangilifu (organization)
 • Kujenga mazingira ya upekuzi (udadisi_
 • Hukaza zaidi kuhusu mazingira katika ujifunzaji lugha
 • Mwalimu awatie moyo wanafunzi kugundua mfumo wa lugha wao wenyewe
 • Mwalimu na wanafunzi wanapaswa kutumia sana majadiliano

NJIA ZA UJIFUNZAJI LUGHA YA KISWAHILI

Njia za ufundishaji Kiswahili ni nyingi kama na waalimu nao walivyo wengi, lakini njia hizi itatengemea hali ya wanafunzi, hata hivyo njia zifutazo zinapendekezwa zitumike.

 1. Njia ya majadiliano-njia hii haifai kwa mwanafunzi ambaye ndio kwa mara ya kwanza anasikia Kiswahili. Lakini ni njia nzuri kwa mwanafunzi ambaye amewahi kusikia habari za Kiswahili
 2. Njia ya Mfano mwalimu aandae maswali, awaambie wanafunzi wajipe vyeo mfano mmoja anakuwa daktari mwingine anakuwa mgonjwa n.k
 3. Mchezo wa maswali. Kwa mfano. Kama wewe ungekuwa rais wa marekani ungefanyaje kuhakikisha unakomesha ugaidi duniani? Watajibu na kujipatia msamiati kibao
 4. Njia ya uigizaji-mwli awape wanafunzi mwongozo wa maigizo
 5. Njia ya maswali ya papo kwa papo (ana kwa ana) mfano: mimi ni Seni, wewe ni nani?
 6. Njia ya uwandani. Mfano ukitaka kuwafundisha misamiati ya sokoi wapeleke sokoni.
 7. Njia ya kutumia mazingira mbalimbali. Mfano kama mwalimu anataka kuwafundisha michezo wapeleke uwanja wa mpira
 8. Njia ya usomaji. Mfano kusoma pande nne za dunia,kuwapa matini mbalimbali wanafunzi
 9. Njia ya majadiliano funge. Yaani wanafunzi wanajadili vitu ambavyo vimewekewa mipaka

Angalizo:uteuzi wa njia ipi itumike itategemea aina ya wanafunzi na kazi zao!

HULKA/TABIA YA UANAFUNZI KUJIFUNZA LUGHA

Wanafunzi hutofautiana kulingana na hulka zao, mwalimu anahitaji kuangalia mielekeo ya  wanafunzi wake. Baadhi ya tabia zao ni kama vile: ucheshi, hasira, aibu, hasira za kutojua, hapendi kusahihishwa, mkimya nk

ATHARI ZA KIJAMII KUHUSU LUGHA/WANALUGHA

Kila jamii ina mtazamo wake kuhusu ujifunzaji lugha, mtazamo hasi ndio ambao huathiri ujifunzaji lugha na kupelekea kutopata motisha wa kujifunza lugha. Baadhi ya mambo yanayoathiri ni kama vile

 1. Nia au lengo la kujifunza lugha hiyo
 2. Jinsia; inasemekana wanawake wanaweza kupata lugha kuliko wanaume
 • Umri; umri mdogo ni rahisi kupata lugha kuliko umri mdogo
 1. Mazingira; mazingira mazuri yanavutia mwanafunzi kujifunza haraka
 2. Umilisi wa lugha kama akiwa na umilisi mdogo

Malengo ya mwalimu ni kuhakikisha anafanya mambo yafuatayo:

 1. Kuwatia motisha wa kujifunza lugha
 2. Kumsaidia kuondokana na hasira
 • Kuondoa dhana potofu ya ujifunzaji lugha. Mf. Kuna wanaoamini kwamba Kiswahili ni lugha ya kiislamu
 1. Kuondoa utata katika vipengele vya kisarufi
 2. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika

Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara zinazotumika katika jamii. Hivyo mwalimu anapaswa awaeleze mambo yafuatayo;

 1. Baadhi ya utamaduni huangalia usoni, tabasamu na kujiamini
 2. Matumizi ya mkono wa kushoto au wa kulia
 • Kuonyesha vidole-jamii zingine haziruhusu kabisa
 1. Namna ya kusimama na kuelezea jambo

Ili kutimiza hayo yote mwalimu lazima awe na sifa zifuatazo:

 1. Awe muwasilishaji mzuri
 2. Awe na mpangilio mzuri
 • Awe mstahimilivu
 1. Awe na ujuzi wa kufundisha
 2. Awe na uhusiano mzuri na wanafunzi
 3. Awe na maarifa ya somo

SIFA ZA MJIFUNZAJI LUGHA

 1. Awe na utayari wa kujifunza lugha ya Kiswahili bila kulazimishwa
 2. Afanye mazoezi ya kuitumia lugha hiyo
 3. Atumie akili kupambanua dhana mbalimbali ili kugundua mambo ambayo jamii Fulani inayafanya
 4. Awe na uhuru wa kuzungumza lugha hiyo
 5. Awe na ratiba ya kujifuza
 6. Aweze kulinganua na kulinganisha lugha anayojifunza
 7. Awe na ukarimu ili aweze kuwa na uhusiano na jamii husika
 8. Awe mtendaji
 9. Azingatie ubora ili aweze kujifunza zaidi

MOTISHA

Ni tabia au msukumo katika kutimiza malengo fulani. TUKI (2004) wanadai kuwa motisha ni kitu kama fedha inayotolewa ili kumtia mtu hamasa kujifunza jambo.

Hata hivyo, si lazima umpe kitu bali unamtia moyo mwanafunzi na kumsaidia. Mwalimu anapaswa kutumia motisha chanya sio hasi. Mfano hutakiwi kuchapa fimbo

Brown (1994) anasema kuwa motisha;

 1. Ni kiwango cha uchaguzi ambacho unafanya kuhusu lengo unalotaka kufikia
 2. Jitihada atumiazo mtu kufikia malengo hayo

SKINNER &WATTSON-hawa wanaangalia zawadi na uhimizaji kwa wanafunzi pamoja na adhabu ili kufifisha na kujenga hali fulani

AINA ZA MOTISHA

 1. Mwamko wa mjifunzaji mwenyewe
 2. Mazingira mazuri ya kufundishia Kiswahili mfano, darasa, nje n.k
 3. Jamii inayomzunguka ni motisha pia
 4. Mwalimu anaweza kuwa motisha kwa mwanafunzi
 5. Zana/vifaa vya kujifunzia pia ni motisha

MOTISHA IPO KATIKA MAKUNDI  MAWILI

 1. Motisha wa ndani-
 • Haitegemei vitu vya nje ya yenyewe
 • Hiki ni kile kinachoonekana kwa mjifunzaji lugha mwenyewe
 • Hii haibadiliki kulingana na muktadha wowote ule
 1. Motisha wa nje
 • Ni aina ya motisha ambayo mwanafunzi hutegema kupewa, kupata, kusikia au kuona
 • Hivi vitamsaidia katika kujifunza lugha

Mwalimu wasaidie wanafunzi kutumia lugha kulingana na muktadha. Hapa kuna mambo ya kuzingatia:-

 1. Akili ya mwanafunzi: lazima utambue tofauti zao katika akili zao ili kujifunza lugha
 2. Kipaji chao-kuna wengine wana vipaji vya kujifunza lugha
 3. Umri-watu wazima huchelewa kujifunza lugha
 4. Jinsia-inasemekana wanawake wanaweza kupata lugha haraka kuliko wanaume
UFUNDISHAJI LUGHA KIMAWASILIANO
 • Ni muhimu kuhakikisha kwamba katika kujifunza lugha ufundishaji uwe wa mawasiliano
 • Ni mbinu ya kufundisha lugha ngeni na lugha ya pili
 • Husisitiza mwingiliano maathiriano kama mbinu ya kujifunza lugha

KAZI ZA LUGHA

 • Van (1975) anasema kuwa kazi ya lugha ni:
 1. Kutoa habari
 • Kusimulia
 • Kuuliza
 • Kutoa taarifa
 1. Kutafuta taarifa za kitaaluma
 2. Kuelezea mihemuko na misisimko. Mfanoo mapenzi, misisimko
 3. Kuelezea masuala ya uadilifu.mfano kuomba msamaha, ibada etc
 4. Kwenye mambo ya ushirikiano. Mfano kuamkia watu, kujitambulisha nk

Angalizo: hata kama mwanafunzi ana malengo mengine ya kujifunza lugha hiyo ni lazima umfundishe umuhimu wa lugha hiyo kulingana na muktadha

MASHARTI YA KUZINGATIA

 1. Azingatie majukumu ya kijamii mfano ataanzaje kuzungumza na mtu asiyemjua? Watu wengine ni wenye mamlaka Fulani, hivyo kuna namna ya kuzungumza nao
 2. Majukumu ya kisaikolojia-mfano asipendelee upande wowote mfano CHADEMA CUF na CCM
 3. Mazingira ya lugha ilipo. Je ni lugha ya taifa? Watu wanaokuzunguka wanatumiaje?

Angalizo: lugha sio sarufi tu au fonolojia bali ni chombo cha mawasiliano, hivyo inahitaji kufundishwa kimawasiliano zaidi

MUKTADHA WA UFUNDISHAJI LUGHA

 • Haya ni mazingira halisi ambapo tukio la ufundishaji lugha hufanyika kwa kuzingatia wadau wakuu watatu
 1. Mwanafunzi
 2. Mwalimu
 3. Jamii
 • Pamoja na motisha ufundishaji uzingatie sana mambo yafuatayo:
 • Utoaji wa kazi na mazoezi mengi
 • Tumia lugha katika mazingira halisi na yanayostahili ukilenga kwenye stadi nne za lugha
 • Matumizi ya lugha kwa kuzingatia muktadha
 • Utumizi wa mazingira halisi ya darasa.mfano picha, katuni. Nk
 • Himiza ushirikiano miongoni mwa wanafunzi baina yao na baina yako mwalimu
 • Tumia mbinu zaidi ya moja. Mfano vikundi, majibizano nk (rejea mbinu)
 • Fafanua kwa uangalifu masuala ya kisarufi
 • Ajue maono ya mwanafunzi. Mfano huzuni, ucheshi nk
 • Kuunda mazingira ya utani darasani

UFUNDISHAJI WA DARASA MSETO

 • TUKI (2013) Mseto ni hali ya kuwa na mchanganyiko wa makabila mbalimbali kutengeneza kitu fulani
 • Hapa ni mchanganyiko wa darasa lenye wanafunzi wanaotoka sehemu mbalimbali na wenye umri tofauti, malengo tofauti nk
 • Hivyo mwalimu inakubidi utofautishe sana katika ufundishaji wako na uwe makini ili usije ukawakwaza wanafunzi wengine

NAMNA YA UFUNDISHAJI DARASA MSETO

 1. Lazima mwalimu uwe na maarifa ya wanajamii mfano utamaduni wao. Kama ni wazungu, wachina nk jua utamaduni wao
 2. Uwe na usisitizaji wa lugha lengwa. Kama ni Kiswahili basi pendelea kutumia Kiswahili ili usiwakwaze sana. Hata hivyo lazima wawe na lugha ambayo wewe unaijua
 3. Tumia vitendo halisi, ishara nk
 4. Arika wageni mbalimbali waje waeleze kuhusu lugha na mazingira
 5. Puuza(ignore) malengo ya wanafunzi
 6. Ufundishaji wa masuala ya utamaduni lazima ufungamane na muktadha husika

SIFA ZA MPATAJI LUGHA

Mpataji lugha ni lazima awe na sifa kuu mbili tu:

 1. Umilisi wa kiisimu
 • Ni uwezo alio nao mjifunzaji lugha ambao unamwezesha kutofautisha viambo, miundo tofauti ya lugha na msamiati wa lugha
 • pia kuweza kutamka lugha ile.
 1. Umilisi wa kiisimujamii
 • Ni umilisi ambao mtumiaji wa lugha hupata lugha inayomwezesha kujifunza lugha na kuzingatia muktadha

NADHARIA /MBINU /MIKABALA ZA KUJIFUNZA LUGHA YA KIGENI

 • Nadharia ni mkondo wa mawazo unaotumika kuelezea jambo
 • Mtesigwa(2009) anasema “ nadharia ni kiunzi cha mitazamo, mawazo au vitendo vinavyohusisha uchunguzi, mpangilio na uchanganuzi wa matukio katika kukabili suala fulani kisayansi

       ®kuna mambo mawili ambayo lazima tujikumbushe:

 1. Njia za ufundishaji lugha ya kigeni ni nyingi kama waalimu walivyo wengi
 2. Kumbuka hali ya darasa. Tumia njia mbinu zaidi ya moja darasani, usitumie njia moja tu.
 • Rogers&Richards (2001)wanasema kuwa tunapojiandaa kwenda kufundisha tunahitaji kujiuliza maswali yafuatayo:-
 1. Malengo ya ufundishaji lugha lengwa(LL) ni yapi? Mfano labda lengo lao linaweza kuwa wanataka kuzungumza tu.
 2. Upi ni msingi asili wa lugha lengwa na unaathiri vipi njia za kufundisha. Mfano kaida za lugha ya Kiswahili ni zipi?
 3. Ni misingi ipi inatumika kuchagua mambo katika ufundishaji lugha?
 4. Ni misingi ipi ya upangiliaji wa mada. Mfano kwa kuzingatia suala la utamaduni, mfano salamu nk
 5. Je lugha mama ya mwanafunzi ina jukumu gani katika kujifunza lugha? Mfano miundo ya lugha mama inafanana na lugha lengwa?
 6. Je wanafunzi binafsi watumie mbinu zipi katika kujifunza lugha hiyo?
 7. Je ni mbinu na vitendo vipi hufanikisha vizuri ujifunzaji lugha ya pili (kigeni)?

NADHARIA ZA KUJIFUNZA lugha

 1. Mbinu ya tafsiri sauti
 2. Mbinu ya moja kwa moja(direct method
 3. Mbinu ya usomaji(reading approach method)
 4. Kusikia na kusimulia (audiolingual method)
 5. Kushirikisha jamii (community language learning method)
 6. Mbinu ya ukimya (silence method)
 7. Mbinu ya mawasiliano (communicative language approach)
 8. Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)
 9. Mbinu ya utambuzi (communitive code method)
 10. Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)
 1. Mbinu ya tafsiri sarufi
 • wakati mwingine hujulikana kama mbinu ya kimapokeo. Huu ni mkabala ambao ufundishaji wa lugha ya kigeni umejiegemeza katika sarufi ya lugha ya Kiratini. Iliasisiwa/anzishwa na Meidinger (1783) na Ploetz (1849) wakati ule iliaminika kwamba lugha ya kiratini ndiyo lugha pekee.
 • Nafasi ya lugha mama ilipuuzwa kwa kiasi kikubwa na ilijikita katika sarufi ya Kiratini, na hivyo mwalimu alipaswa kujikita katika kufundisha sarufi ya Kiratini na vipengele vingine vilipuuzwa
 • Huu ulikuwa ni mkabala elekezi-yaani unawaelekeza watu namna ya kutumia lugha na sivyo wanajamii wanavyotumia lugha hiyo
 1. Mbinu ya moja kwa moja(direct method)
 • Iliasisiwa na Gouin(1880)
 • Nadharia hii inazingatia uzungumzaji wa lugha husika
 • Mbinu zilizopaswa kufundishia ni zile zilizohamasisha wanafunzi kuzungumza. Mfano mbinu ya majadiliano,uigizaji,maswali katika vikundi
 • Masomo yalianza kwa hadithi fupi halafu wanafunzi wanauliza maswali kuhusu hadithi waliyosimuliwa na mwalimu aliwaambia watoe maoni yao kuhusu hadithi hiyo.
 • Matumizi ya vielelezo vilitumika zaidi. Mfano picha, ramani, katuni n.k
 • Kipengele vya sarufi kilifungushwa kwa kufuata muktadha halisi ambamo lugha inatumika
 • Kipengele cha utamaduni kilifundishwa kwa uchache sana
 1. Mbinu ya usomaji (reading approach method)
 • Mbinu hii inatumika kufundishia kwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya kigeni ambao hawatarajiwi kutoka nje ya nchi ambapo lugha hiyo inatumika
 • Malengo yake huwa kuendeleza uwezo wao wa kusoma ile lugha
 • Vipengele vinavyofundishwa ni vile vinavyohusu usomaji, hivyo vipengele vingine havihusiki. Mkazo wake ni kwamba anayejifunza lugha aweze kusoma vitu vingi kwa wakati mmoja.
 • Mbinu hii haimpi mjifunzaji lugha uwezo wa kuzungumza lugha husika bali ni kuisoma tu.
 1. Kusikia na kusimulia (audiolingual method)
 • Nadharia hii ilitokana na haja ya ukarimani nchini marekani miaka 1940.
 • Iliasisiwa na Bloomfield (1942) na Fries (1945)
 • Msingi mkubwa wa nadharia hii ni kile kinachosemwa
 • Maandishi hayakupewa fursa kubwa bali kile kilichosemwa ndicho kilikuwa cha muhimu sana. Bloomfield alisema kuwa lugha si katika maandishi bali ni kile ambacho kinasemwa.
 • Inahusisha kusimulia mada mbalimbali na kupima uwezo wa kusikia
 • Walipenda sana kutumia miziki, nyimbo, usimulizi na ughanaji
 • Walisisitiza stadi ya kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika
 • Waliongeza kitu kingine cha kuona
 1. Kushirikisha jamii (community langaage learning method)
 • Iliasisiwa na curran (1976)
 • Dai la nadharia hii ni lugha ni watu, kwa maana ya kwamba huwezi kutenga jamii na lugha
 • Walidai kwamba ili uweze kumfundisha mwanafunzi mgeni basi nenda kwenye jamii husika
 • Walidai pia kwamba kama utaamua kufundishia darasani bali darasa lako lifanye angalau lifanane fanane na jamii ya lugha husika
 • Ili uweze kufundisha watu ni lazima ushirikishe watu wanaotumia lugha hiyo.
 • Mwanafunzi atapata vichocheo vya aina nyingi katika jamii na kubaini ni mambo gani yanafaa na mambo gani hayafai
 • Nadharia hii inaipa kipaumbele jamii kama chombo muhimu katika kujifunza lugha
 1. Mbinu ya ukimya (silence method)
 • Nadharia hii inaamini kwamba kila lugha ina mfumo wake tofauti na lugha nyingine, hivyo ufundishaji wa lugha ya pili ulenge kumfanya mjifunzaji wa lugha kuwa mmilisi au kukaribia kuwa mmilisi wa lugha anayojifunza
 • Nadharia hii inadai kwamba ujifunzaji wa aina yoyote ile unahusisha vitu viwili.

Kichocheo®      Mwitikio®       mgeuko

(Mwalimu)      (mwanafunzi)-(anabadilika)

 • Ili kuweza kutimiza hili, mwalimu anahitaji kujenga mazingira ya utani katika darasa jambo ambalo litaleta matokeo mazuri ya umilisi wa lugha husika
 • Nadharia hii inamhitaji mwalimu kufanya tathimini kwa wanafunzi wake ili kubaini kama kuna badiliko
 1. MBINU YA UTAMBUZI (COMMUNITIVE CODE METHOD)
 • Nadharia hii inatokana na ukosoaji/udhaifu wa nadharia ya mbinu ya sarufi na ile ya moja kwa moja
 • Ilianzishwa mwaka 1970
 • Wanadai kwamba mwanafunzi apewe vipengele vyote vya lugha kwa ujumla mwanafunzi kumpa maarifa mapana kuhusu lugha, kumpakanuni za msingi kuhusu lugha, halafu yeye mwenyewe kulingana na utambuzi wake aweze kuielewa lugha.
 • Uwafundishe kanunu za msingi. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili ni lazima ujue ngeli za majina-hii itakusaidia kutumia nomino katika mazingira tofauti tofauti, vitenzi-waeleze namna ambavyo vinaweza kukaa peke yake kama sentensi
 1. Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)
 • Nadharia hii pia hujulikana kama mkabala asilia.
 • Iliasisiwa na James Asher 1969
 • Inatilia mkazo mfumo na muundo wa lugha.
 • Kama ilivyo nadharia ya usikizi nadharia hii pia inasisitiza umuhimu wa kumudu mazungumzo kama sehemu ya umilisi wa lugha
 • Ufundishaji uhusishe mazoezi ya kurudia rudia ambayo angalau unamfanya mwanafunzi kumudu anachojifunza
 • Nadharia hii inasisitiza matumizi ya vitendo na ishara mbalimbali kama nyenzo mojawapo katika kujifunza lugha.
 1. Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)
 • Ilianzishwa na Lonzano georgi (1979)
 • Nadharia hii inayapa mazingira bora ya ujifunzaji lugha kama nyenzo muhimu mojawapo katika kujifunza lugha. Hii inamaanisha kwamba mazingira yanayotumika kujifunzia lugha ni lazima yamkumbushe mwanafunzi kile alichojifunza jana yake
 • Wanaelezea namna ya mkao wakati wa kufundisha wanafunzi wageni. Mkao katika darasa uwe ni wa kutazamana, maana yake vikae kwa duara.
 • Wanasisitiza matumizi ya mziki laini na mziki nyororo
 1. MBINU YA MAWASILIANO (COMMUNICATIVE LANGUAGE APPROACH)
 • Inasisitiza maingiliano na maathiriano katika ya mwalimu, mwanafunzi na jamii
 • Wanakaza kwamba kujifunza lugha ni kujifunza kuwasiliana.
 • Kujua lugha kwa hakika sio kujua kanuni za lugha ile bali ni kujua namna ya kuwasiliana na watu wa jamii ile kwa kuzingatia mikitadha mbalimbali ambamo lugha hiyo inatumika
 • Ni nadharia ambayo imeshaididiwa na wataalam wengi akiwamo Noamy Chomsky
 • Hii ndiyo nadharia ambayo inafaa kutumia kwa ajili ya kujifunza lugha

VIWANGO VYA WANAFUNZI

 • Hapa inamaanisha uwezo alio nao mtu wa kutumia lugha Fulani.
 • Viwango hivi viliwekwa na shirika/taasisi moja isiyokuwa ya kibiashara wala kiserikali liitwalo Interagence Language Round Table (ILRT)
 • Kulingana na shirika hili wajifunzaji lugha wako katika viwango vitatu
 1. Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level
 2. Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level
 3. Wanafunzi wa daraja la juu (DAJUU) Advanced Level
 1. Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level

Daraja limegawanyika katika viwango hivi

 • Kiwango cha 0-®mwanafunzi hawezi kabisa kuzungumza lugha
 • Kiwango cha +0-®mwanafunzi amekaririshwa tu mahitaji muhimu akibadilishiwa tu basi Amepotea
 • Kiwango cha 1-®mwanafunzi anaweza kusitahimili mazungumzo ya ana kwa ana ila hawezi kuanzisha mazungumzo
 • Kiwango cha +1-®huyu anaweza kuanzisha mazungumzo yeye mwenyewe, hata hivyo ni kwa ajili ya kukidhi matarajio yake
 1. Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level
 • Daraja la 2-lugha si kamilifu lakini anaeleweka kwa urahisi
 • Kiwango cha 3-anaweza kuzungumza lugha kwa muundo sahihi, ana msamiati wa mazingira fulani fulani tu ili kukidhi mahitaji ya kitaaluma
 • Anaweza kukithi mahitaji ya kitaaluma
 • 2+®Lugha yake si kamilifu lakini anaweza kueleweka kwa urahisi
 • 3®mwanafunzi ana uwezo wa kuzungumza lugha kwa usahihi, ana msamiati toshelevu kwa mazingira fulani fulani tu.
 • 3+®mwanafunzi ana uwezo wa kuzungumza lugha kwa muundo sahihi na ana uwezo wa kukidhi mahitaji ya kitaaluma
 • 4®mwanafunzi ana uwezo wa kutumia lugha kwa usahihi na ufasaha katika viwango vyote vya lugha. Yaani fonolojia-matamshi, sintakisia-miundo, mofolojia-maumbo
 • Huweza kutoa maana ya viambo mbalimbali kulingana na muktadha
 • 4+®uwezo wa mzungumzaji wa kiwango cha juu kabisa katika mawanda yote lugha: yaani fasihi na isimu
 • Ana uwezo wa kutumia kwa kuzingatia utamaduni wa lugha husika
 • Anaelekea kulingana na wazawa wa lugha husika
 • 5®usitadi wa lugha alio nao ni wa kiwango cha mmilisi wa lugha aliyeboboea
 • Ana sifa za kudhihilisha wakati wa lugha anayojifunza.

TATHMINI YA VITABU VYA KUFUNDISHIA KISWAHILI KWA WAGENI

Suala la uteuzi wa vitabu vya kufundishia lina ugumu unaotokana na mambo yafuatayo:

Yaani malengo tofauti ya:

 • Malengo tofauti ya wanafunzi
 • Malengo tofauti ya taasisi
 • Malengo tofauti ya waajiri
 • Malengo tofauti ya waalimu
 • Malengo tofauti ya wazazi/walezi

Tutafafanua utofauti huo kwa namna ifuatayo:

 • Malengo tofauti ya mwanafunzi:-mfano viwango tofauti vya wanafunzi
 • kitabia, kiuchumi, kiuelewa, kiutamaduni,kiumilisi
 • viwango tofauti za wanafunzi mfano kiwango cha kati,juu nk
 • tofauti za kimaamzi. Mfano taasisi moja tu ihusike katika uandaaji wa vitabu vya kufundishia mfano wizara ya elimu
 • uzingatizi tofauti wa vitabu. Mfano,bei, mwonekano, upatikanaji wake

NAMNA YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO

 • Malengo ya kozi inabidi yaangaliwe
 • Wanafunzi walengwa ni akina nani?
 • Mkabala utakaotumia kufundishia
 • Stadi za lugha. Je kitabu kimekidhi stadi zote za lugha?
 • Ubora wa mazoezi yaliyotolewa ndani ya kitabu
 • Mfuatano wa masomo/mada. Ngumu? rahisi? Nk
 • Msamiati
 • Hali ya jumla ya kiisimu jamii. Je kitabu kimetumia lahaja, lugha rasmi, vigezo vya kiutamaduni
 • Muundo mzima wa kitabu. Chapa yake ni ndogo au kubwa?

KITABU BORA CHA KUFUNDISHIA LUGHA KWA WAGENI KIWE NA SIFA ZIFUATAZO

 1. Kila somo/kitabu kiwe na lengo mahususi la kumsaidia mwanafunzi kuwasiliana
 2. Kila kitabu kiwe na matini ya lugha kama izungumzwayo na wazawa
 3. Kila kitabu kiwe na kielelezo cha mazingira halisi. Mfano salamu
 4. Msamiati na sarufi ukidhi matakwa ya wanafunzi
 5. Utumizi wa vilelezo halisi kama vile picha,magazeti, tangazo, kadi nk
 6. Kila kitabu lazima kiorodheshe sauti zilizo katika lugha husika ili aweze kuzielewa.

MAELEZO YA MJIFUNZAJI LUGHA

UCHAMBUZI WA DOSARI

Maana yake:

 • Uchambuzi wa dosari ni njia ya kuainisha, kupambanua na kufafanua dosari mbalimbali za wajifunzaji wa lugha ya kigeni/lugha ya pili
 • Suala la uchambuzi wa dosari liliasisiwa na Corder (1967) ambapo yeye anaeleza maana ya dosari kuwa ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za lugha lengwa
 • Mambo yanayoshughulikiwa na wanausasanyuzi; wanashughulikia mambo makuu manne
 1. Jinsi mjifunzaji anavyoilewa lugha ya kigeni anayojifunza
 2. Jinsi mjifunzaji anavyojifunza lugha ya kigeni/mbinu anazotumia
 3. Matatizo anayokabiliana nayo wakati anajifunza lugha ya kigeni
 4. Kung’amua mchakato/kutambua michakato inayotumiwa katika kujifunza lugha ya kigeni

UMUHIMU WA DOSARI/DHIMA YA DOSARI KWA WAJIFUNZAJI LUGHA YA PILI

 • Dosari zinazofanywa na wanafunzi wanaojifunza lugha ya kigeni hutumiwa kama kioo kinachoakisi hali halisi iliyofikiwa na wajipatiaji wa lugha ya pili.
 • Dosari hizi humpatia mwalimu nafasi ya kutathimini jitihada zilizofikiwa na wanafunzi wake kwa minajili ya kuboresha au kuendeleza mbinu za ujifunzaji lugha na humsaidia mwalimu kubadilisha vifaa anavyotumia katika ufundishaji.
 • Kwa ujumla umuhimu wa dosari unaangaliwa katika namna kuu nne
 1. Kwa upande wa mwalimu
 • Huonyesha jitihada zilizofikiwa na wanafunzi na kusaidia kuboresha
 1. Kwa watafiti
 • Huonyesha jinsi lugha inavyopatikana/inavyoamiliwa
 1. Kwa mwanafunzi
 • Humsaidia mwanafunzi kujua ruwaza/partern ya maendeleo ya mwanafunzi alipofikia
 1. Kwa waandaa mitalaa
 • Huwasaidia kuboresha uandaaji wa vitabu na machapisho mbalimbali kwa kujifunza

AINA ZA DOSARI

Aina hizi za dosari zimeainishwa kutokana na mbinu wanazotumia wanafunzi kujifunza lugha.

 1. Dosari majumui/majumuisho
 • Hizi ni dosari ambazo mwanafunzi hutumia kanuni ya jumla ya lugha ya kwanza na kuitumia katika lugha ya pili. Hii inasabisha kukiuka matumizi ya lugha lengwa. Mfano katika lugha ya kiingereza vitenzi vingi huongeza “ed” mwanafunzi wa mswahili wa kiingereza anaweza kupata shida kwani anaweza kuwa anaongeza ed katika kila kitenzi jambo ambalo sio sahihi.
 1. Uepukaji/avoidance
 • Ni ule utaratibu wa mjifunzaji lugha ya kigeni kujaribu kuepuka matumizi ya kanuni/maumbo/miundo fulani ya lugha. Kwa mfano mwanafunzi anajaribu kuepuka matumizi ya neno fulani anatajaribu kuliepuka hilo neno na kutumia neno lingine jambo ambalo litasababisha makosa.
 • Hata hivyo si rahisi kujua kama mtu fulani amekwepa matumizi ya neno fulani
 1. Urahisishaji
 • Mwanafunzi anapoamua kurahisisha muundo wa lugha fulani hujikuta katika dosari
 1. Uhawilishaji
 • Uhamishaji wa miundo na kaida za lugha ya kwanza kwenda lugha ya pili. Miundo hii inapohamishwa basi hukiuka miundo ya lugha ya pili.
 • Kwa mfano baadhi ya jamii ya watanzania hukiuka sana kanuni za Kiswahili. Mfano Wanyakyusa wa hawawezi kusema “chama” bali “kyama” pia Wakinga hawawezi kusema “viatu” bali wanasema “fyatu”
 1. Utumizi ziada/over use
 • Ni kuongeza matumizi yasiyohitajika katika utumizi wa lugha

MISINGI YA UAINISHAJI WA DOSARI

Hapa ni kwa kuzingatia Nyanja kuu za lugha:

 1. Dosari za kifonolojia/ukiushi wa matamshi-lugha zingine zina toni zingine hazina.
 2. Dosari ya kimaumbo/kimsamiati-yaani upangaliaji wa vipashio vinavyounda maneno. Mfano uwingi wa nomino za kiingereza hupachikwa mwisho tofauti kabisa na lugha ya Kiswahili ambapo haitabiliki. Mfano pia katika lugha ya Kiswahili neno moja linaweza kuwa na sifa ya kuwa sentensi, mfano “ninasoma” jambo ambalo kwa kiingereza haiwezekani kuwa neno moja “ I read”
 3. Dosari za kimuundo-taratibu tofauti tofauti zinazotumika kuunda vipashio. Kila lugha ina utaratibu wake. Mfano. My brother-yangu kaka-mfumo huo hauwezekani kuwa sawa
 4. dosari za kimaana/kisemantiki- maana huwa ni tofauti tofauti
 5. Dosari za kipragmatiki-hii ni miktadha mbalimbali mfano sokoni, kanisani

dosari kulingana na athari za kimawasiliano

Ni uainishaji wa dosari kulingana na uelewekaji/kutokueleweka kwa ujumbe uliotolewa na mjifunzaji lugha. Kwa kuzingatia kigezo hiki tunapata aina mbili za dosari.

 1. Dosari za kimalimwengu/global errors-ni dosari ambazo zinafanya usemi uliotolewa na mjifunzaji lugha kutoeleweka kabisa
 2. Dosari za kienyeji/local errors-ni semi zinazotolewa na mjifunzaji wa lugha ya pili ambazo haziko sahihi lakini zinaeleweka na msikilizaji. Mfano “I angry” mfano mwingine ni “ninataka kura”-akiwa jikoni au akiwa katika jukwaa anasema “ninataka kula”- hizi zinaeleweka na wasikilizaji japo haziko sahihi.

USHUGHULIKIAJI WA DOSARI ZA WANAFUNZI

 • Kila mwanafunzi wa lugha ya pili huwa ana dosari katika kujifunza lugha ya pili. Ni jambo la msingi kushughulikia dosari za wanafunzi, lakini angalia ni wakati gani ushughulikie dosari hizo, hii ni kulingana na muktadha wa darasa: aina ya wanafunzi; haiba yao, mihemko, aina ya dosari, umri n.k. Hata hivyo ikiwezekana dosari hizo ziweze kushughulikiwa ili kusaidia zisijirudie rudie.
 • Wataalamu wengine wanaona kwamba dosari zisishughulikiwe. Mfano Krashen na Terrell(1983) husema kuwa mwanafunzi aachwe mwenyewe atazidi kugundua dosari hizo na atashughulikia mwenyewe.
 • Kathleen Bailey (1985)anapendekeza uamuzi wa aina saba
 1. Puuza dosari hizo
 2. Dosari zishughulikiwe papo kwa papo
 3. Kuhusisha wengine katika kurekebisha dosari hizo. Mfano miongoni mwa wanafunzi hao hao unaweza kuhusisha na wakakosoana wenyewe
 4. Kuhusisha wanafunzi mahususi-yaani kumtumia mwanafunzi wa karibu na mwenzake kumsahihisha mwingine.
 5. Kumrudia mfanyaji dosari/ mfano unaweza kumwambia “unaweza kufikiri zaidi juu ya hilo?”
 6. Kuwaruhusu wanafunzi wengine kutoa tathmini.
 7. Kumpa nafasi ya kujaribu tena na tena mfanyaji wa dosari baada ya vitendo fulani kufanyika ndani ya darasa.

 

Mwisho wa yote lazima vitu vifuatavyo viwe vimejitokeza:-

 1. Usahihi na uhalali wa dosari uwe umedhihilika
 2. Sehemu na mahali dosari imefanyika iwe imebainishwa wazi wazi. Mfano kama ni kwenye neno, tungo nk
 3. Nafasi ya kurudia na kujirekebisha kwa mfanyaji dosari iwe imetolewa
 4. Mifano mbalimbali ya dosari na usahihi wa semi uwe umetolewa na kuonyeshwa kwa uwazi
 5. Aina ya dosari iwe imeonyeshwa. Mfano kama ni dosari ya kimpangilio, kimatamshi nk
 6. Marekebisho yawe yamefanywa kwa mifano anuai
 7. Mhusika awe amesifiwa/kama ameepuka hizo dosari

MAMBO YANAYOATHIRI UJIFUNZAJI/UPATAJI LUGHA YA PILI/KIGENI

 

Mambo hayo ni yale ama yanayomwezesha au yanamkwamisha mpataji lugha kupata lugha. Tutaangalia kwa mujibu wa Martland (1997)

 1. Umri
 • Mtu mwenye umri mdogo ana ahueni zaidi katika kujifunza lugha kuliko mtu ambaye umri umeenda. Mtoto ambaye hajabalehe mfano miaka kabla ya tisa (9). Hii inatokana na kwamba mtu mzima tayari anakuwa na lugha nyingine ambayo inasigana na lugha anayojifunza
 1. Hali ya kiuchumi ya mjifunzaji lugha:
 • Mtu wa tabaka la chini hawezi kutumia vitu vya kisasa ili kupata lugha, maana vifaa hivyo ni vya gharama kubwa.
 1. Hali ya darasa:
 • Darasa ambalo limejengewa mazingira ya utani, wanafunzi wanamudu haraka sana kupata lugha.
 • Hii inajumuisha michezo mbalimbali katika darasa hilo
 1. Msaada wa kifamilia/community support:
 • Ikiwa mwanafunzi lugha anayojifunza inatumika ndani ya jamii hiyo, atapata haraka sana lugha kuliko mwanafunzi ambaye anajifunza lugha ambayo wazungumzaji wake hawako hapo.
 • Mfano: Mtanzania anayetaka kujifunza kiingereza anapata shida kwa sababu wazungumzaji wake wako nje ya nchi
 1. Motisha:
 • Motisha ni kipengele muhimu sana katika ujifunzaji lugha
 • Mwanafunzi aliye na motisha ya ndani atapata lugha haraka kuliko anayepata motisha ya nje. motisha
 1. Kiwango cha elimu:
 • Mtu mwenye kiwango kikubwa cha elimu ana uwezo mkubwa sana wa kupata lugha kuliko mtu ambaye hana elimu kabisa.
 1. Matarajio:
 • Kama mjifunzaji lugha ana lengo la kufanya utafiti sehemu fulani, matarajio yake ni kujifunza lugha na kuimudu ili akafanye kazi yake.
 • Kama mwanafunzi hana matarajio yoyote basi itakuwa ngumu kupata lugha.
 1. Haiba
 • Wanafunzi wacheshi hupata lugha haraka kuliko wanafunzi ambao sio wacheshi.
 • Wachesi hupenda kujichanganya sana.
 1. Mtazamo wa utamaduni wa ujifunzaji lugha ya kigeni/pili.
 • Mwanafunzi kama ana mtazamo hasi na lugha anayojifunza basi itakuwa ngumu sana kupata lugha.
 • Mtazamo chanya ndio utakaomsaidia mjifunzaji lugha kupata lugha.
 1. Uwezo wa kumudu lugha ya kwanza:
 • Uwezo wa lugha ya kwanza una kawaida ya kuathiri umuduji wa lugha ya pili, hasa inapotokea kwamba lugha ya kwanza ni tofauti kabisa na mfumo wa lugha ya pili. (Nozalle (2012)
 1. Viigwa (role models in the community)
 • Hii ni kwamba kuna mtu gani katika jamii ambaye ni mtu maarufu unataka uzungumze kama yeye? Hii itakusaidia kwa sababu mjifunzaji lugha atajaribu kujitahidi azungumze kama mtu huyo.
 1. Muktadha/mazingira
 • Mazingira ni muhimu katika upataji lugha

TOFAUTI ZA UPATAJI WA LUGHA YA KWANZA NA LUGHA YA PILI/KIGENI

 

Kuna tofauti kubwa kati ya upataji wa lugha ya kwanza na lugha ya pili. Kila mtu ana lugha ya kwanza. Wataalam wanaokuwepo hapa kushadidia hili ni Ellis (1994) na Bley Vroman (1988)

Hawa wanabainisha hoja tisa, kama ifuatavyo:

 1. Mafanikio kwa ujumla: mtoto anapopata lugha ya kwanza huipata lugha ile kwa usahihi katika Nyanja zote, japo anaweza asiweze kutofautisha uchambuzi kiisimu lakini wapataji lugha ya pili hupata mafaniko katika maeneo fulani fulani tu katika lugha wajifunzayo.
 2. Kushindwa(failure): katika upataji wa lugha ya kwanza kushindwa hakupo labda kama ana ulemavu fulani lakini kwa wapataji lugha ya pili kushindwa ni jambo la kawaida
 3. Utofauti baina ya wajifunzaji/wapataji lugha (variation): wajipatiaji wa lugha ya kwanza hawana tofauti yoyote katika upataji lugha, yaani wakifikia umri fulani labda kama miaka 3 hivi wote watakuwa wamepata, kama atakuwa hajapata lugha mpaka miaka 9 basi huyo atakuwa na matatizo (msukuku-kukoma kujifunza lugha (fossilization )lakini lakini wajifunzaji wa lugha ya pili kuna tofauti kubwa sana, utakuta mwishoni mwa kozi mmoja amemudu na mwingine bado
 4. Malengo/goals: lengo la mjipatiaji lugha ya kwanza ni umili wa lugha hiyo katika viwango vyote lakini lengo la mjipatiaji lugha ya pili ni kupata maudhui na umilisi kidogo
 5. Usukuku(ukakamaaji): suala la usukuku halipo kwa mtoto anayejipatia lugha ya kwanza lakini kwa mjipatiaji lugha ya pili hii ni hali ya kawaida kabisa(soma Han1998-2013).
 6. Uvumbuzi/ughamuzi: wajipatiaji wa lugha ya kwanza huendelea kujipatia lugha ya kwanza katika ughamzi bwete (kujisahihisaha dosari pasipo kujua) lakini mpataji lugha ya pili huwa katika ughamzi tambuzi.
 7. Maelekezo/instruction: ujipatiaji wa lugha ya kwanza hauhitaji maelekezo, labda kidogo kwa ajili ya kuchochea lakini mjipatiaji wa lugha ya pili anahitaji maelekezo ya kina na sahihi na kwa utaratibu maalumu.
 8. Uthibitisho hasi:katika ujipatiaji wa lugha ya kwanza usahihishaji wa dosari haumsaidii mpataji wa lugha ya kwanza kupata lugha ile lakini katika upataji wa lugha ya pili ni muhimu kufanya masahihisho ili kumpa mwelekeo sahihi.
 9. Athari hisivu (affective factor): mjipatiaji wa lugha ya kwanza hakuna kitu kinachomwathiri kujipatia lugha ya kwanza, mfano hafikilii kwamba atakosea, atachekwa bali yeye hutamka tu lakini katika ujipatiaji wa lugha ya pili athari hisivu zina msaada sana katika kupata lugha. Mfano mwanafunzi mcheshi, hucheka atapata lugha haraka kuliko mkimya.
 10. Muda: mtoto huchukua muda mfupi kati ya miezi 36 anakuwa mmilisi wa lugha lakini mjipatiaji wa lugha ya pili hutumia muda mrefu sana. Inachukua miaka kama tisa

UTAYARISHAJI WA MBINU ZA UFUNDISHAJI

 

 1. UTAYARISHAJI WA SOMO:
 • Hapa tunaangalia muundo wa andalio la somo (lesson plan) unahitaji kuangalia mambo haya:
 1. Muda
 2. Mada
 3. Malengo-ie kitu gani kitokee katika somo hilo. Mfano mwisho wa somo mwanafunzi aweze kutaja aina ya ‘nomino’
 4. Mazingira/muktadha-darasa, aina ya wanafunzi.
 • Shajala
 • Logbook
 • Mhitasali

MUUNDO WA ANDALIO LA SOMO

Andalio la somo linatakiwa kuwa na mambo yafuatayo

 1. Malengo ya jumla (main objective)-haya ni mabadiliko ya muda mrefu yanayotakiwa kutokea kwa muda mrefu. mfanoMwanafunzi aweze kutathimini….mwanafunzi aweze kufahamu…
 • Mara nyingi malengo haya hayabadiliki
 1. Malengo mahusus/malengo wezeshi
 • Haya ni malengo ya muda mfupi
 • Haya ni malengo ambalo ni la kudumu lakini lengo lake ni kusaidia lengo la jumla
 • Tofauti kati ya malengo mahusus na malengo ya jumla ni kwamba malengo ya jumla hayapimiki ilhali malengo mahusus yanaweza kupimika
 • Malengo mahususi ni mabadiliko ya muda mfupi ilhali malengo ya jumla ni mabadiliko ya muda mrefu

 Mwanafunzi aweze kutaja viungo vya binadamu vilivyo katika kichwa…mwanafunzi aweze kulinganisha na kulinganua

Mwanafunzi aweze kuonyesha viungo vya mwili..

Kubainisha viungo vya mwili

 1. Mada kuu.
 • Kila unapoenda kufundisha lazima kunakuwa na maada. Mfano wa mada ni Usafiri wa Anga
 1. Mada ndogo:
 • Kama mada yako itakuwa hapo juu, mfano Usafiri wa Anga, mada ndogo inaweza kuwa,kuwasili kwa ndege, kukata tiketi, kufika uwanja wa ndege, mahali uwanja wa ndege ulipo, hali ya miundombinu kwenda uwanja wa ndege nk
 • Kama ikiwa mada kuu ni familia: basi mada ndogo yaweza kuwa aina za familia
 1. Zaka za kufundishia
 • Hakuna somo lisilo na zana za kufundishia. Mfano kama ni usafiri wa anga. Unaweza kuchora picha ya mwanza, kuwapa ramani nk.
 1. Utaratibu wa somo/yaani darasani
 • Somo lolote linakuwa na:
 1. Utangulizi-tanguliza somo lako, kama sio mara ya kwanza wape chemsha bongo, kama ni kwa mara ya kwanza unaweza kuanza na hadithi. Hii itakusaidia kuvuta usikivu wa wanafunzi. Pia unaweza kuwaruhusu wanafunzi wakuulize maswali kuhusu wanaelewa nini kuhusu kile unachoenda kukifundisha
 2. Uwasilishaji wa kiini cha somo:- unaweza kuandaa maswali, unaweza kuandaa makundi ya wanafunzi wachache wachache.
 3. Utumizi/utendaji wa wanafunzi. Hapa mwalimu unategeneza mazoezi, kazi binafsi, mazoezi mengine ambayo watafanya wenyewe, maswali ya papo kwa papo au mazungumzo
 4. Kazi ya nyumbani
 • Haifai hata kidogo kuwafundisha wanafunzi wageni kumaliza kuwafundisha na kuwaacha bila kuwapa zoezi lolote la kufanya
 • Zoezi hilo lihusishe vile ambavyo mwanfunzi amesoma darasani.
 • Mfano wa zoezi: Mtafute mtu yeyote kule mitaani muulize maswali haya. Wewe ni nani, unasoma? Umeoa? Je unapenda nini? Nk
 • Hii itakusaidia sana kujua wapi palipo na udhaifu ili uwee kuwasaidia wanafunzi kama hajaelewa.
 1. Tathmini
 • Ni lazima kujitathimini wenyewe kama wameelewa au la.

UONGOZI WA DARASA/UTHIBITI WA DARASA

 1. Upangaji wa darasa/ je darasa limepangiliwaje? Je watu wote wako sana?
 2. Mbinu za ufundishaji/mbinu zinazopendekezwa ili uweze kulitawala darasa ni mbinu shirikishi. Usiwe mwongeaje tu wewe mwenyewe. Pia tumia mbinu za kuona.
 3. Uimara wa mwalimu/lazima mwalimu ujiamini katika ufundishaji wako. Usionyeshe kuyumba hata kidogo, kumbuka mara utakapoyumba hawatakuamini tena hata kama ukifundisha vizuri. Kama wakikuuliza swali ambalo hulijui jaribu kuwashirikisha, kama na wao hawajui basi waambie utawapata jibu siku nyingine. Unahitaji kuwa msafi. Uwe mbunifu.
 4. Mwonekano wa darasa/ lazima darasa liwe linaonekana. Kusiwepo na sauti nyingine inayoingia ndani
 5. Matumizi ya ubao au power point. Vionekane vizuri
 6. Sauti ya mwalimu-je sauti yako inasikika vizuri? Hakikisha sauti yako inasikika kwa wanafunzi wote. Uwe na uwezo wa kuimudu lugha vizuri.
 7. Ukubalifu wa mambo ambayo hukufundisha/hukupanga kuyafundisha..kama wanafunzi wakitaka kufundishwa kitu Fulani ambacho wewe hukujiandaa kuwafundisha, itategemea hali ya darasa

UTAYARISHAJI WA MITIHANI

Huu ni mchakato wa upimaji wa maarifa/ujuzi ambao wanafunzi wameupata tangu mwanzo wa kozi hadi mwisho wa kozi. Kipengele hiki ni cha muhimu sana hivyo lazima lifanyike kwa ustadi na ubunifu mkubwa.

Malengo ya mitihani lazima yalenge kupima mambo manne

 1. Ulenge kupima maarifa na ujuzi aliyopata mjifunzaji lugha.
 2. Kupima mbinu mbalimbali alizotumia mwalimu kufundishia kama zimeeleweka au la.
 3. Mitihani imelenga kupima mitaala
 4. Mitihani inapima uwezo wa kuchochea kujifunza maarifa mapya.

AINA ZA UPIMAJI

 1. Upimaji rasmi-huu ni upimaji unaofanyika mwisho mwa kozi na hufanyika mara moja tu. Hupima viwango vyote ambavyo alijifunza mwanafunzi.
 2. Upimaji usio rasmi-mwanafunzi anapimwa wakati somo linaendelea,mfano mazoezi, mitihani nk. Mara nyingine upimaji huu huitwa upimaji umbaji

KANUNI ZA UPIMAJI

 1. Kuwapa wanafunzi muda wa kujiandaa-wape muundo wa mtihani ulivyo
 2. Hakikisha jaribio lako linapima wanafunzi kitu walichojifunza
 3. Hakikisha kwamba jaribio lako lina uhalisia/reality
 4. Hakikisha kwamba jaribio lako/mtihani wako linachochea utendaji

***ili kutimiza haya, unapaswa

 1. Hakikisha unaondoa utata katika mtihani huo/maswali yawe bayana/yawe wazi.
 2. Muda wa kufanya mtihani huo uzingatie
 3. Kuwepo na umakini katika uandishi/ avoid typing errors.
 4. Hakikisha haurudii majaribio
 5. Hakikisha wanafunzi wako hawaibii/kuangaliziana katika mtihani/cheating

***mwisho wa somo la Kiswahili kwa Wageni***

Facebook Comments
Recommended articles