MASWALI YA KISWAHILI KWA SHULE ZA MSINGI

By , in MITIHANI DRS I-VII on . Tagged width:

SEHEMU YA KWANZA: SARUFI

Sarufi, ni dhana pana sana ambayo inajumuisha taaluma ya uchambuzi wa lugha katika kiwango cha umbo sauti (fonolojia), umbo neno (mofolojia), miundo ya maneno (sintaksia) na umbo maana (semantiki).

Nitaanza kuangalia maswali ya somo la Kswahili kwa mwaka 2012. Mtihani huu ulitungwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na kuwekwa kwenye tovuti yao ili wadau mbalimbali wapitie maswali haya na kuwasaidia wanafunzi wao.

 Katika mtihani wa somo la Kiswahili kwa Darasa la VII, yafuatayo ni maswali yaliyoulizwa: Nitaanza na kipengele cha sarufi.

A- Sarufi ni mojawapo ya kipengele cha lugha.

Maswali 50 yaliulizwa katika mtihani wa Kiswahili. Mbali na sarufi, vipengele vingine vilivyozingatiwa  ni utungaji, mashairi, ufahamu, matumizi ya lugha kama nahau, methali na misemo.  Kipengele cha sarufi kilikuwa na maswali 20 kati ya 50. Maswali hayo 20 yalikuwa ni kama ifuatavyo:

Swali la 1:

Katika maneno yafuatayo lipi ni nomino dhahania?

 • Unakuja
 • Umeenea
 • Utalima
 •  Uelewa
 •  Ulisoma

Lengo la swali hili ni kupima uwezo wa mtahiniwa kutambua aina za nomino.

Watahiniwa walipotoshwa na umbo ‘U’ lililojitokeza katika kila neno, hivyo kuwafanya washindwe kuyatofautisha. Umbo hili hutumika kuwakilisha nafasi ya pili ya upatanishi wa ngeli. Kwa hiyo nomino dhania ni uelewa.

 

Swali la 2

Wingi wa neno paka ni upi?

 • Mipaka
 • Paka
 • Mapaka
 •  Vipaka
 •  Wapaka.

Swali hili lililenga kupima uwezo wa kutumia maneno katika umoja na wingi

Jibu sahihi ni Paka na asilimia 62.4 ya watahiniwa walichagua neno Paka.

Swali la 3

“Akiondoka Sulubu kazi zote zitalala”

Neno Sulubu ni la aina gani?

 • Kielezi
 • Kivumishi
 •  Kiwakilishi
 •  Nomino
 •  Kiunganishi.

Swali lililenga kupima ujuzi wa aina za maneno na lilimtaka mtahaniwa kutambua aina gani ya neno katika tungo hiyo.

Jibu sahihi ni nomino. Watahiniwa walikosa ujuzi wa kutambua aina za maneno zikiwemo nomino za pekee ambazo zinapoandikwa huanza na herufi kubwa hata kama neno liko katikati ya maneno mengine.

 

Swali la 4

“Ili tuendelee————kufanya kazi kwa bidii.”

Neno lipi linakosekana kukamilishha sentensi hiyo?

 • Ni budi
 •  Hatuna budi
 •  Tuna budi
 •  Kuna budi
 •  Hapana budi.

Swali lililenga kupima matumizi ya nahau ya Kiswahili ambapo asilimia 43.55 ya watahiniwa walijibu kwa usahihi. Muundo sahihi wa maneno ni “Hatuna budi”.

 

Swali la 5

“Mvua ilinyesha jana usiku kucha.”

Katika sentensi hiyo kikundi cha kielezi ni kipi?

 • Mvua ilinyesha jana
 •  Ilinyesha usiku kucha,
 • Ilinyesha jana
 •  Jana usiku kucha.

Swali lillenga kupima uwezo wa kutumia sarufi ya lugha.

Asilimia 15.83 walichagua  kwa usahihi ‘jana usiku kucha’ kama kikundi kielezi.

Hii inaonyesha kuwa mada ya sarufi ya lugha haikueleweka vizuri kwa watahiniwa walio wengi.

Swali la 6

“Baba alilima shamba”

Sentensi hii ipo katika kauli gani?

 • Kutenda
 •  Kutendwa
 •  Kutendeshwa
 • Kutendeka
 • Kutendea.

Jibu la swali hili ni kauli ya kutendwa.

Swali hili lililenga kupima ujuzi wa kauli za vitenzi. Watahiniwa wengi alijibu kwa usahihi swali hili. Ni asilimia 72.46 waliojibu kwa usahihi

Swali la 7

“Adili alikuwa anaimba tangu ujana yake.”

 ‘Alikuwa’ ni aina gani ya kitenzi?

 • Kisaidizi
 •  Jina
 •  Kishirikishi
 •  Kitegemezi
 •  Kikuu.

Swali lililenga kupima uwezo wa watahiniwa kutambua aina za vitenzi vya Kiswahili.

Jibu sahihi ni Kisaidizi. Kimetokea kabla ya neno ‘anaimba’ ambapo ni kitenzi kikuu.

Swali la 8

“Mchungaji alivaa suti maridadi sana.”

Katika sentensi hii neno lipi limetumika kama kivumishi?

 • Suti
 • Alivaa
 •  Maridadi
 •  Mchungaji
 •  Sana.

Swali hili lililenga kupima ujuzi wa watahiniwa kuhusu aina za maneno hasa dhana ya kivumishi. Watahiniwa waliojibu kwa usahihi ni wale waliochagua neno ‘maridadi’ Hawa ni 38.50 tu ya wale waliochagua jibu kwa usahihi.

Swali la 9

Kitenzi ‘anapigwa’ kipo katika kauli gani?

 • Kutenda
 •  Kutendwa
 •  Kutendea
 •  Kutendeka
 •  Kutendesha.

Jibu sahihi ni kutendea.

Swali hili lililenga kupima maarifa ya dhana ya kutendwa. Asilimia 47.9 waliweza kujibu swali hili kwa usahihi.

Swali la 10

Kisawe cha neno bahati ni kipi kati ya maneno yafuatayo:

 • Tunu
 •  Sudi
 •  Shani
 •  Huba
 •  Hidaya.

Swali lililenga kupima uwezo katika kutumia msamiati. Asilimia 18.46 ndio walioweza kuchagua jibu sahihi ambalo ni Sudi.

Maneno mengine yanakaribia kimaana. Swali hili ni miongoni mwa maswali ambayo watahiniwa wengi hawakujibu kabisa.

Swali la 11

“Maandishi yanasomeka vizuri”

Sentensi hii iko katika wakati gani?

 • Ujao
 •  Uliopita
 •  Mazoea
 •  Uliopo
 •  Timilifu.

Swali linalenga kupima uwezo wa mtahiniwa katika kutumia njeo kwa wakati.

Jibu sahihi ni wakati “uliopo” ambalo ni jibu sahihi kwa kuwa kitenzi ‘yanasomeka’ kina umbo la ’na’ ambalo ni umbo la wakati ‘uliopo’.

 

Swali la 12

“Makubi   ni mtoto wa mjukuu wangu.”

Makubi ni nani kwangu?

 • Kilembwekeze
 • Kijukuu
 •  Kilembwe
 •  Kitukuu
 •   Mtukuu.

Jibu sahihi ni kitukuu

Swali lililenga kupima ujuzi wa mtahiniwa kuhusu matumiizi ya msamiati unaoonyesha uhusiano wa watu katika jamii kinasaba. Asilimia 46.63 walichagua neno kitukuu ambalo ni jibu sahihi.

Swali la 13

“Sipendi uongo”

Sentensi hii ipo katika nafasi ipi?

 • Nafasi ya kwanza katika wingi
 • Nafasi ya tatu katika umoja
 • Nafasi ya kwanza katika umoja
 • Nafasi ya tatu katika wingi
 • Nafasi ya pili katika umoja.

Swali hili lililenga kupima ujuzi katika sarufi ya lugha. Asilimia 45.91 ya watahiniwa walichagua “Nafasi ya kwanza katika umoja”. Hili ni jibu sahihi.

 

Swali la 14

Neno “poni” lina maana sawa na neno lipi kati ya maneno yafuatayo:

 • Posho
 • Rahani
 • Mali
 • Mkopo
 • Pesa

Swali linalenga kupima uwezo katika matumizi ya msamiiati wa Kiswahil  sanifu. Neno sahihi ni rahani. Asilimia 21.48 ya watahiniwa walichagua neno rahani.

 

Swali la 15

“Shuleni kwetu kuna upungufu wa ——————–“Ni neno gani linakamilisha utungo huu kwa usahihi?

 • Thamani
 • Thamini
 • Dhamini
 • Zamani
 • Samani

Swali hili linapima uwezo katika matumizi wa lugha. Neno sahihi hapa ni samani. Asilimia 40.58 walijibu kwa usahihi kwa kuchagua neno samani.

Athari za matamshi zinaweza kuchangia katika kujibu  swali hili kwa wale waliochagua ‘zamani’ badala ya ‘samani’.

Swali la 16

“Mtoto ametengeneza toroli ya mti”. Wingi wa sentensi hii ni upi?

Swali hili linalenga katika kupima ujuzi katika mada ya upatanishaji wa kisarufi.

Tungo zilizotolewa ni:

 • Watoto wametengeneza toroli za miti
 • Watoto wametengeneza matoroli ya miti
 • Watoto wametengeneza matoroli za miti
 • Watoto wametengeneza matoroli ya mti
 • Watoto wametengeneza toroli ya mti

Jibu sahihi ni “Watoto wametengeneza toroli

 ya miti.” Neno matoroli si sahihi.Toroli linatumika kwa umoja na wingi.

Swali la 17

“Muda mfupi atakuwa anaingia uwanjani.”

Sentensi hii ipo katika wakati gani?

 • Wakati uliopo
 • Wakati uliopita
 • Wakati ujao
 • Wakati timilifu
 • Wakati wa mazoea

Swali lililenga kupima ujuzi katika njeo ya wakati. Asilimia 42.28 ya watahiniwa walichagua “Wakati ujao”.

Watahiniwa walishindwa kufahamu vipengele vya nyakati.

Swali la 19

“Juma ameondoka hivi punde”. Maneno “Hivi punde” yana maana gani?

 • Haraka
 • Muda mfupi
 • Karibuni
 • Kwa pupa
 • Kwa haraka

Swali lililenga kupima uwezo wa kutumia aina za maneno na hasa vielezi.

Asilimia 53.04 ya watahiniwa walichagua jibu sahihi kuwa ni “karibuni”.

Swali la 20

Neno lipi ni kisawe cha neno ‘adili’?

 • Ujinga
 • Wema
 • Uovu
 • Ujasiri
 • Ukatali

Lengo la swali hili ni kupima uelewa wa mtahiniwa kuhusu visawe vya maneno. Jibu sahihi ni ‘wema’.

Asilimia 47.9 walichagua neno wema ambalo ni jibu sahihi.

Watahimiwa wengi walishindwa kuelewa maana ya neno ‘adili’ ili kuweza kupata kisawe sahihi.

Kwa jumla kipengele cha sarufi ni changamoto kwa walimu wengi na hivyo kuweza kuwaathiri wanafunzi.