MASWALI NA MAJIBU – 8: DARASA LA 3 & 4

By , in DRS 1-7 on .

MASWALI NA MAJIBU – 8: DARASA LA 3 & 4

 SEHEMU A: Chagua herufi ya jibu sahihi

 1. Mwanambee maana yake ni mtoto wa…………..

(a) mwisho (b) kwanza (c) pili (d) tatu

 1. Vaa miwani ni nahau inayomaanisha……………..

(a) lewa pombe (b) vaa vizuri (c) vinga (d) weka miwani machoni

 1. Neno lenye maana sawa na chumvi ni.

(a) sukari (b) munyu (c) chungu (d) kiungo

 1. Rubani hufanya kazi ya kuendesha…………..

(a) ndege (b) meli (c) bodaboda (d) treni

 1. Kisawe cha neno pangaboi ni ……………

(a) feni (b) panga (c) kitasa (d) ufunguo

 1. Kinyume cha neno “cheka” ni ……………….

(a) piga kelele (b) kaa kimya (c) chekelea (d) lia

 1. Mahali njia mbili zinapokutana huitwa……………….

(a) barabara (b) njia panda (c) kona ya njia (d) njia mbili

 1. Neno lenye maana sawa na dhiki ni…………….

(a) shida (b) raha (c) maudhi (d) karaha

 1. Watoto watatu wamefali mtihani. Neno lipi linaloonesha kiasi?

(a) watoto (b) wamefeli (c) ni (d) watatu

 1. Sehemu ambayo watu mbalimbali huuza vitu mara moja kwa wiki panaitwa……….

(a) gulio (b) soko (c) duka (d) kibanda

 1. Kitinda mimba maana yake ni mtoto wa………………

(a) kwanza (b) wa mwisho (c) anayezaliwa (d) yatima

 

SEHEMU B: Methali, nahau na vitendawili

 1. Aga dunia maana yake ni…………………….
 2. Nyumba yangu haina mlango…………………
 3. Ahadi ni ………………………………..
 4. Pata jiko………………………………..
 5. Kuku wangu katagia mibani……………….

 

SEHEMU C: Oanisha maneno ya fungu A na yale ya fungu B ili kupata maana.

ORODHA A                                         ORODHA B

 1. Msitu                   [        ]        Sehemu ya juu inayofunika nyumba
 2. Koboa                  [        ]        mbuzi dume
 3. Paa                      [        ]        asiyeweza kusema
 4. Bubu                    [        ]        miti mingi
 5. Beberu                 [        ]        ondoa maganda ya juu kwenye nafaka

 

SEHEMU D: Soma habari kwa makini kisha jibu maswali

Fisi ni mnyama wa porini. Ana madoa meupe na meusi. Mikono ya fisi ni mifupi kuliko miguu yake kwa hiyo akitembea anachechemea kidogo. Fisi hula mizoga ya wanyama wanaofugwa kama vile mbuzi, ng’ombe na kondoo wetu. Kaka alikuta kondoo ameuawa aliuliza, nani amemuua kondoo wetu. Tukajibu sisi hatujui labda wanyama wa porini.

MASWALI

 1. Mikono ya fisi ni mifupi kuliko miguu hivyo humfanya atembee kwa……..

(a) kurukaruka (b) kuchechemea (c) kasi sana (d) taratibu

 1. Fisi hupenda kula……………ya wanyama waliokufa.

(a) nyama (b) mboga (c) mizoga (d) maiti

 1. Fisi ni mnyama………………

(a) afugwae (b) baharini (c) mjini (d) porini

 1. Wanyama ambao fisi hupenda kuwashambulia ni……………..

(a) paka, mbuzi na kondoo

(b) ng’ombe, mbuzi na sungura

(c) mbuzi, ng’ombe na kondoo

(d) kondoo, paka na mbwa

 

MAJIBU

 1. B
 2. A
 3. B
 4. A
 5. A
 6. D
 7. B
 8. A
 9. D
 10. A
 11. B
 12. Kufikiri
 13. Yai
 14. Deni
 15. Kuoa
 16. Nanasi
 17. D
 18. E
 19. A
 20. C
 21. B
 22. B
 23. C
 24. D
 25. C
Facebook Comments
Recommended articles