MASWALI NA MAJIBU-7: DARASA LA 3 & 4

By , in DRS 1-7 on .

MASWALI NA MAJIBU-7: DARASA LA 3 & 4

SEHEMU A: Chagua jibu sahihi

 1. Haraka haraka haina……………………

(a) papara (b) baraka (c) haraka

 1. Fikiri kabla ya ………………..

(a) kutenda (b) kutendwa (c) kuhisi

 1. Mbwa ni …………..wa nyumba yetu

(a) msumbufu (b) mnyama (c) mlinzi

 1. Juma alimuua mbwa wake kwa………………

(a) bomu (b) risasi (c) bunduki

 1. Wezi walishindwa kuiba nyumbani kwa Juma kwa sababu ya………..wa fensi yake.

(a) ukali (b) ukubwa (c) ujanja

 1. Mtu anaposema vijana wale ni chanda na pete maana yake ni………………

(a) majirani (b) marafiki (c) kuwa na joto (d) wanaishi karibu karibu

 1. Kinyume cha nahau vunjika moyo ni………………………….

(a) tia for a (b) mezea mate (c) tia moyo (d) kata tamaa

SEHEMU B: Chagua muundo sahihi kukamilisha sentensi.

kabla ya, baada ya, kwa ajili ya, bila shaka, huna budi, mara kwa mara

 

 1. Wingu jeusi limetanda angani kote…………….mvua itanyesha sasa hivi.
 2. Ukitaka kufaulu ……………kusoma kwa bidii.
 3. ………………kumsubiri muda mrefu, hatimaye mgeni aliwasili.
 4. ………………kuanza kujibu swali lolote lile ni vizuri kulisoma tena na tena.
 5. Anafaulu kwa sababu hupitia masomo yake…………..
 6. Wageni wote tayari wameshawasili……….mkutano.

SEHEMU C: Oanisha maneno ya orodha A na yale ya orodha B

             ORODHA A                           ORODHA B

 1. Kushirikiana           (        )        Kuweka vitu tayari
 2. Ndugu                      (        )        Watu waliozaliwa pamoja
 3. Shabaha                  (        )        kufanya pamoja
 4. Kuandaa                 (        )        kusudi, lengo
 5. Kuogopa                 (        )        kukamata kitu
 6. Kutundika mtini  (        )        kuwa na hofu
 7. Shika                       (        )        kuning’iniza juu ya mti

SEHEMU D: Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali

Sijali hakuwa mwangalifu wa maisha yake, siku moja alichomwa na mwiba mguuni. Majirani zake walimwambia aende hospitalini lakini hakujali. Mwishowe mguu ulivimba na kidonda chake kuoza na kutoa harufu. Hali ilipokuwa mbaya alitafuta msaada na kwenda hospitali. Maskini Sijali mguu wake ulikuwa umeoza na dawa pekee ilikuwa ni kuukata. Ama kweli mdharau mwiba mguu huota tende.

Jaza nafasi zilizoachwa wazi.

 1. Sijali hakuwa………………….wa maisha yake.
 2. Kina nani walimwambia Sijali aende hospitali?…………….
 3. Kutokana na kisa cha Sijali andika maana ya methali mdharau mwiba mguu huota tende………………..
 4. Mguu wa Sijali ulikuwa umekwisha……………na ukatakiwa……………
 5. Umejifunza nini kutokana na habari hii uliyosoma?………………

MAJIBU

 1. B
 2. A
 3. C
 4. C
 5. B
 6. B
 7. C
 8. Bilashaka
 9. Huna budi
 10. Baada ya
 11. Kabla ya
 12. Mara kwa mara
 13. Kwa ajili ya
 14. C
 15. B
 16. D
 17. A
 18. F
 19. G
 20. E
 21. Mwangalifu
 22. Majirani
 23. Anayedharau tatizo mwishowe hujuta
 24. Oza na kukatwa
 25. Mdharau mwiba mguu huota tende
Facebook Comments
Recommended articles