MASWALI NA MAJIBU -6: DARASA LA 3 & 4

By , in DRS 1-7 on .

MASWALI NA MAJIBU -6: DARASA LA 3 & 4

SEHEMU A: Jibu maswali kwa kuchagua jibu na kuandika katika sehemu iliyowazi.

 1. Piga yowe maana yake ni………………

(a) piga kelele (b) imba kwa sauti ya juu (c) furahi sana

 1. Wanyama pori ni wale…………………

(a) wanaofugwa (b) waishio porini (c) tembo na simba

 1. Neno keti maana yake ni……………………

(a) kaa chini (b) simama (c) andika

 1. Huyu kijana ni mwerevu. Neno huyu limetumika kuonesha…………….

(a) umbali (b) karibu (c) sifa

 1. Mama yake aliaga dunia Aga dunia maana yake ni………………

(a) fariki (b) aga watu (c) fanya sherehe

 1. Mtoto mwenye adabu…………………

(a) hupendwa (b) hupigwa na watu wengi (c) hulia hovyo

 1. Lipi kati ya mazao yafuatayo ni nafaka…………………..

(a) nazi (b) mbaazi (c) mahindi

 1. Mtu anayefanya kazi ya kufua na kupiga nguo pasi huitwa………………

(a) mpiga pasi (b) dobi (c) maridadi

 1. Wakatafakari maana yake ni…………….

(a) wakasahau (b) wakakariri (c) wakafikiri

 1. Shangazi aliweka fedha na funguo………..ndani ya pochi.

(a) yake (b) zake (c) wake

SEHEMU C: Jibu kwa kuchagua maneno katika kisanduku ulichopewa.

Usingizi ulipaa, fedha lukuki, walikaa chonjo, waliangua kicheko, walipigwa butwaa, walitega sikio, kufuja mali.
 1. Watu wote……..waliposikia Juma ameuawa na majambazi.
 2. Wanafunzi wote…………walipomwona mwalimu wao anacheza dansi.
 3. Alikuwa na……………lakini hakuwa na mipango mizuri ya matumizi.
 4. Baada ya kuota ndoto ya kutisha……….usiku wote.
 5. Wanakijiji………….kumsikiliza mgombea wa ubunge alipofanya kampeni yake.

SEHEMU D: Jibu swali 16-20 kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi. Andika kinyume cha sentensi hizi.

 1. Sitalala usingizi leo………………………..
 2. Chausiku hatarudi leo……………………

Kamilisha methali zifuatazo

 1. Mchagua jemba……………………..
 2. Jungu kuu……………………………
 3. Kila mtu humwabudu apitapo………………………

SEHEMU E: Vitendawili, Methali na Nahau

 1. Nyumba yangu ina mlango juu………………
 2. Haba na haba……………………
 3. Chapa mguu……………………..
 4. Kila niendapo hunifuata…………….
 5. Kula chumvi nyingi…………………

MAJIBU

 1. A
 2. B
 3. A
 4. B
 5. A
 6. A
 7. C
 8. B
 9. C
 10. B
 11. Walipigwa butwaa
 12. Waliangua kicheko
 13. Fedha lukuki
 14. Usingizi ulipaa
 15. Walitega sikio
 16. Nitalala usingizi leo
 17. Chausiku atarudi leo
 18. Si mkulima
 19. Halikosi ukoko
 20. Mlango
 21. Chupa
 22. Hujaza kibaba
 23. Tembea
 24. Kivuli
 25. Ishi niaka mingi
Facebook Comments
Recommended articles