MASWALI NA MAJIBU -5: DARASA LA 3 & 4

By , in DRS 1-7 on .

MASWALI NA MAJIBU -5: DARASA LA 3 & 4

SEHEMU A: Chagua jibu sahihi

 1. Ipi kati ya sentensi hizi ni sentensi inayoonesha wakati ujao:-

(a) zena atakuja kwetu (b) zena anakuja kwetu (c) zena alikuja kwetu (d) zena huja kwetu.

 1. Kaka alichinja sungura jana. Sentensi hii ipo katika wakati gani?

(a) uliopita (b) ujao (c) mazoea (d) uliopo

 1. Badili kuwa hali ya mazoea, “Mkulima analima”……….

(a) mkulima analima (b) mkulima hulima (c) mkulima alilima (d) mkulima atalima

 1. Wingi wa neno kijiko ni………………………

(a) majiko (b) vijiko (c) mavijiko (d) vikijiko

 1. Baba …………..mama ni wazazi wangu.

(a) ni (b) wa (c) ya (d) na

 1. Wagonjwa wamelazwa…………………….

(a) nyumbani (b) wodini (c) hodini (d) chumbani

 1. Jua huchomoza asubuhi upande wa ………….

(a) Mashariki (b) juu (c) magharibi (d) kulia

 1. Mtu ambaye hasikii huitwa……………..

(a) bubu (b) kiwete (c) kiziwi (d) kilema

 1. Samaki wa maji chumvi wana ……………nzuri.

(a) mabaka (b) ladha (c) chumvi (d) rangi

 1. Vitabu ……….juu ya meza.

(a) viko (b) vino (c) vimekaa (d) zipo

 

SEHEMU B: Jaza nafasi iliyoachwa wazi

 1. Umoja wa neno “mvi” ni……………
 2. Waislamu daima ………………kwenye misikiti.
 3. Andika neno moja tu kutokana na kundi hili. …………..(Machungwa, nyanya, ndizi, nanasi)

SEHEMU C: Chagua jibu sahihi kwenye mabano

 1. Rehema ni bingwa wa……….mashairi (kughani, kugairi, kukubali)
 2. Hapo…………………za kale binadamu alifanana na sokwe. (mwanzoni, zamani, mwishoni, katikati)
 3. Mchwa huishi kwawingi na kuzaliana kwenye…………..(mzinga, zizi, kichuguu, kichukuu)

SEHEMU D: Methali, Nahau na Vitendawili

 1. Kamilisha methali hii:- Mvumilivu hula mbivu……………
 2. Toa maana ya nahau hii:- Kula chumvi nyingi…………….
 3. Tegua kitendawili hiki. Kila mtu humwabudu kila apitapo………….
 4. Andika kinyume cha neno baridi…………………..

SEHEMU E:UFAHAMU: Soma habari ifuatayi kisha jibu maswali

Chakula bora ni muhimu sana kwa wagonjwa na hasa magonjwa ya muda mrefu kama vile UKIMWI, kifua kikuu na saratani. Mgonjwa anayekula vizuri, dawa hufanya kazi vizuri. Lishe bora kwa kweli, ndiyo dawa ya magonjwa kwa sababu mwili hujenga kinga.

Mtu asiyekula chakula cha kujenga mwili ni sawa na kujenga nyumba isiyo imara ambayo wakati wowote inaweza kubomoka.

 1. Dawa bora ya wagonjwa ili waweze kujenga kinga za mwili ni …………

(a) lishe bora (b) kuepuka magonjwa ya UKIMWI (c) kwinini (d) panado

 1. Magonjwa ya muda mrefu yaliyotajwa katika habari hii ni…………..

(a) Malaria na UKIMWI (b) kuharisha na Saratani (c) kifua kikuu, saratani na UKIMWI (d) UKIMWI, saratani na kwashakoo

 1. Dawa hufanya kazi vizuri zaidi kwa………………

(a) wagonjwa wa muda mrefu (b) kujenga nyumba bora (c) kukosa chakula bora (d) kula chakula bora

 1. Mtu aliyekula chakula cha kujenga mwili ni sawa na………..

(a) kufa haraka (b) kujenga nyumba isiyo imara (c) kukosa chakula bora (d) UKIMWI

 1. Mwandishi amesema katika habari kuwa chakula bora ni muhimu kwa……

(a) watoto (b) wanafunzi (c) wagonjwa (d) wazee

 

MAJIBU

 1. A
 2. A
 3. B
 4. B
 5. D
 6. B
 7. A
 8. C
 9. B
 10. A
 11. Mvi
 12. huswali
 13. matunda
 14. kughani
 15. zamani
 16. kichuguu
 17. mbivu
 18. kuishi miaka mingi
 19. mlango
 20. joto
 21. A
 22. C
 23. D
 24. B
 25. C
Facebook Comments
Recommended articles