MASWALI NA MAJIBU- 4: DARASA LA 3 & 4

By , in DRS 1-7 on .

MASWALI NA MAJIBU- 4: DARASA LA 3 & 4

SEHEMU A: MISAMIATI: Chagua jibu lililosahihi

 1. Kamchape aliwakumbuka sana marehemu watoto wake akashikwa na ……………na kuomboleza.

(a) amaki (b) mwaliko (c) hatimaye (d) fumanizi

 1. Ali …………pesa katika kiganja cha mkono na kukimbia hadi dukani.

(a) adhimisha (b) hamaki (c) shuhudia (d) fumbata

 1. …………..mvua zikanyesha na watu wakapanda mbegu za kila aina.

(a) fukuto (b) hatimaye (c) maarufu (d) mara nyingi

 1. Juma alipigwa………….kuonekana katika eneo la shule kwa sababu ya wizi.

(a) tetemeko (b) marufuku (c) mara nyingi (d) wizi

 1. Kila tarehe 14 Oktoba tuna………….kumbukumbu ya kifo cha hayati Mwalimu J.K. Nyerere.

(a) adimisha (b) adhimisha (c) azimisha (d) kimbilia

 1. Huyu ni ………….wa hapa kijijini kwetu.

(a) mkungu (b) mkonge (c) mkunga (d) mkenge

 1. Huu ………..mpaka wa shule yetu.

(a) ndimo (b) ndiyo (c) ndio (d) ndiko

 1. Sikukuu ya Idd baba alichinja ……………mkubwa.

(a) faali (b) fahari (c) fahali (d) faili

 1. Tulikaribishwa kwenye ………ya harusi.

(a) kalamu (b) karamu (c) kaumu (d) mwito

 1. Alimeza ………….mbili za dawa.

(a) temba (b) mtembe (c) tembe (d) tumba

 

SEHEMU B: Nahau na methali

Mfano: Kufa maji ………….kufia ndani ya maji

 1. Mkono wa birika………………………..
 2. Unga mkono……………………………..
 3. Mtoto wa kikopo……………………….
 4. Ana mkono mrefu……………………..
 5. Kutoa rambirambi………………………
 6. Zimwi ……………………………………
 7. Kuku mgeni……………………………..
 8. Nina chemchemi isiyokauka………………
 9. Ukumbuu wa babu mrefu…………………
 10. Ukiona vyaelea……………………………

SEHEMU C: UFAHAMU: Soma kifungu cha habari kisha jibu maswali yanayofuata.

Mara tu mvua za vuli zilipoanza Mzee Lazaro “alipaza” sauti yake juu na kusema “…hameni wote mliojenga na kuishi mabondeni” watu walitahamaki kuona hakuna aliyesikia tamko hilo la Mzee Lazaro. Mvua zilipozidi kumiminika ndipo mjomba alisema “asiyesikia la mkuu huvunjika guu” watu wengi waliaga dunia na wengine kukosa mahali pa kuishi na kupoteza samani zao za ghali na kujutia kwa kutosikia sauti ya busara ya Mzee Lazaro.

MASWALI

 1. Ni ipi maana ya methali “Asiyesikia la mkuu huvunjika guu”.

(a) asiyesikia ya wakubwa atapata matatizo

(b) asiyesikia ya watu ataweza kuvunjwa mguu

(c) asiyesikia ya watu ana mkosi

(d) asiyesikia la mkubwa atafukuzwa kazi

 1. Neno “samani” lina maana ipi?

(a) vitu vya ndani (b) vitu ghali (c) vitu vya thamani (d) vitu vyao

 1. “Waliaga dunia” neno hili lina maana gani?

(a) kufariki (b) kuondoka duniani bila kuaga (c) kutoroka (d) kupotea

 1. Waliopuuzia sauti ya Mzee Lazaro walipoteza nini?

(a) samani zao (b) vitu vya mbali (c) kwenye maji (d) sauti

 1. Mara tu mvua zilipoanza Mzee Lazaro ………….sauti yake juu.

(a) aliangusha (b) alipoteza (c) alipaza (d) alilia

 

MAJIBU

 1. A
 2. D
 3. B
 4. B
 5. B
 6. C
 7. C
 8. C
 9. B
 10. C
 11. Mchoyo
 12. kubaliana naye
 13. mtoto wa muhuni
 14. mwizi
 15. kutoa mchango msibani
 16. halikuli likakwisha
 17. hakosi kamba mguuni
 18. mate
 19. barabara
 20. vimeundwa
 21. B
 22. A
 23. A
 24. A
 25. C
Facebook Comments
Recommended articles