MASWALI NA MAJIBU- 10: DARASA LA 3 & 4

By , in MITIHANI DRS I-VII on . Tagged width: ,

MASWALI NA MAJIBU- 10: DARASA LA 3 & 4

SEHEMU A: Andika neno linaloonesha mtendaji

           Kitendo                                   Mtendaji

 1. Vua samaki …………………
 2. Jenga nyumba …………………
 3. Suka nywele …………………
 4. Fuga mifugo …………………
 5. Pika chakula …………………

SEHEMU B: Chagua herufi ya jibu sasa

 1. Kila siku nina amka…………..ili kufanya usafi

(a) alasiri (b) alfajiri (c) jioni

 1. …………..yashule yetu ni shati jeupe na sketi ya bluu.

(a) vazi (b) sare (c) rangi

 1. Wakulima huhifadhi mazao yao katika…………

(a) duka (b) ghala (c) shamba

 1. Kibogoyo ni mtu…………..

(a) asiye na macho (b) ambaye ni mvivu (c) asiye na meno

 1. Baba anafanya kazi inayompatia……………kikubwa.

(a) mapato (b) kipato (c) jasho

SEHEMU C: Methali, vitendawili  na nahau

 1. Mwenda pole…………………..
 2. Kupata jiko…………………….
 3. Kipara cha babu kinafuka moshi……………
 4. Baada ya dhiki……………………..

SEHEMU D: Umoja na Wingi

            Umoja                                               Wingi

 1. Tongotongo                                      ……………………..
 2. ……………                                                vichaka
 3. Mlemavu                                            ………………………

SEHEMU E: Kinyume cha maneno

 1. Panda…………………………
 2. Usiku…………………………
 3. Chota…………………………

SEHEMU F: Andika wakati uliotumika

 1. Mama alipika ugali…………………..
 2. Watoto wanacheza mpira…………….
 3. Shangazi atapata maua………………..

SEHEMU G: Pigia mstari neno lililotofauti na mengine

 1. Nanasi, papai, samaki, topetope
 2. Mbuzi, ng’ombe, kondoo, mjusi

MAJIBU

 1. Mvuvi
 2. Mwashi
 3. Msusi
 4. Mfugaji
 5. Mpishi
 6. B
 7. B
 8. B
 9. C
 10. B
 11. Hajikwai
 12. Kuoa
 13. Ugali
 14. Faraja
 15. Matongotongo
 16. Kichaka
 17. Walemavu
 18. Shuka/vuna
 19. Mchana
 20. Mwaga
 21. Uliopita
 22. Uliopo
 23. Ujao
 24. Samaki
 25. Mjusi