Malengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifa

Malengo ya kufanya Kiswahili kiwe lugha ya taifa nchini Tanzania yalielezwa na mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama ifuatavyo:

1.Kuwaunganisha watu wote waliopo ndani ya Tanzania.

2.Kuongeza na kusaidia ufanisi wa kazi mbalimbali katika jamii.

3.Ni ishara kuwa huru kama taifa.

4.Ni ishara ya kuonyesha uzalendo katika taifa letu.

5.Kuongeza ajira kwa kupata wataalamu watakaofundisha wageni.

6.Kuwapata wakalimani mbalimbali wa lugha ya Kiswahili.

7.Kusaidia kupata vijana wazalendo wa taifa letu.

8.Kuondoa matabaka miongoni mwetu kwa kutumia lugha moja tutakayoelewana.

9.Ili kutoa elimu ya ufanano nchini Tanzania.

10.Kupata nguvu ya pamoja kama taifa ili kupigania haki zetu.

Facebook Comments
Recommended articles