MAJINA YA KIPARE NA MAANA ZAKE

By , in Kavazi on . Tagged width:
Wapare kama walivyo Wanyakyusa hutumia majina yenye maana mbalimbali na kwa kiasi kikubwa huwa yanamrejelea Mungu. Baadhi ya majina hayo ni:
1.     ELIETI                      – MUNGU ANASEMA
2.     ELIETINIZE          – MUNGU ANASEMA NIJE
3.     ELITWAZA – MUNGU TUMEKUJA
4.     ELINAZA    – MUNGU NIMEKUJA
5.     ELITUWAHA  – MUNGU TUKO HAPA
6.     ELIMVONEIA    – MUNGU NIHURUMIE
7.     ELIENIGHENJA – MUNGU ANANISAIDIA
8.     ELIENITUJA – MUNGU AMENIFARIJI
9.     ELIATULIZA – MUNGU ANATULIZA
10.  ELINAFIKA – MUNGU NIMEFIKA
11.   ELIESIKIA – MUNGU ANASIKI/ANATUJALI
12.   NAMINAZI/ZA   – NAMI NIMEKUJA
13.   NAGHENJWA – NIMESAIDIWA
14.   NAMKUNDA – NIMEMPENDA (MUNGU)
15.  TWAZIHIRWA    – TUMEFURAHI
16.   NIARIRA            – NATARAJIA
17.  NIMZIHIRWA       – NAMFURAHIA (MUNGU)
18.  NIGHENJIJWA  – NILISAIDIWA (NA MUNGU)
19. NIMGURAELI       – NAMSHIKA MUNGU
20. GURACHEDI        – SHIKA CHEMA
21.  NAVONEIWA       – NIMEHURUMIWA
22.  NIMSEMBA      – NAMBEMBELEZA (MUNGU)
23.  NIVONEIA – NIHURUMIE
24.  NIMUINDAELI – NAMSUBIRI MUNGU
25.  NAZAHEDI       – NIMEKUJA PAZURI
26. TWAMZIA – TUMEMJIA (MUNGU)
27. KUNDAELI    – MPENDE MUNGU
28.  NARISHWA   – NACHUNGWA (NA MUNGU)
29.  NARISHWAHEDI   – NACHUNGWA PAZURI
30.  NAANJELA       – NAABUDU
31.  NIMUINDAELI     – NAMSUBIRI MUNGU
32.  NAFIKAHEDI      – NIMEFIKA PAZURI
33.  MBONEA              – HURUMA
34. YONAZA                – LEO NIMEKUJA
35.  NAMSHITU      – MSITU (Linahusishwa na msitu)
Yapo majina ya kipare yenye kuashiria misimu mbalimbali ya majira ya mwaka kama vile:
36.    NAVURI –  (Aliyezaliwa msimu wa vuli)
37.    NAISHIKA      – (Alizaliwa masika)
38. NAMBUA – (Alizaliwa msimu wa mvua, kwa mwanamke)
39.    SEMBUA     – (Alizaliwa kipindi cha mvua, mwanaume)
40.     NAMSI           – (Alizaliwa mchana)
41.     NAKIO            – (Alizaliwa usiku)
42.     NANZA          – (Alizaliwa kipindi cha njaa)
Wapare pia hutumia majina ya wanyama kama walivyo Wangoni ingawa majina yao hayako wazi kama ya Wangoni. mf
43.  NANKUKU            – KUKU
44.  MTHETHE            – MTETEA
45.   NGUVE                 – NGURUWE
46.   MASHUVE           – MANYANI
47.  KADEGHE            – KINDEGE
48.  KAGOSWE           – KAPANYA
49.  NKURUVI            – JOGOO
50. KATHUNI             – KASWALA
error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!