MABADILIKO YA SAUTI KATIKA KUTAMKA

By , in MITIHANI SHAHADA on . Tagged width:
Kuna mabadiliko fulani katika sauti za kutamkwa za binadamu. Sauti hizo huwezi kuziona kama haujazichunguza vizuri. Jiulize kwanini
neno kama jenga, tukitaka kumtaja mtenda jambo hatusemi “mjengi”?
au neno iba kwanini hugeuka kuwa mwizi? yaani
sauti /b/ imegeuka kuwa /z/.
Kwa kutumia data ifuatayo tutabainisha mabadiliko ya
sauti yanayotokea na kwa njia hiyo basi tunaweza kusema kuwa mabadiliko hayo
hutokana na mabadilliko flani flani yaliyosababishwa na mazingira ya
kifonoloji, kimofolojia na kimofofonolojia. Ili kuelezea vizuri mabadiliko haya
hatuna budi kutumia mifano kadha wa kadha kutoka katika hii.
Data.
Iba
Wizi
Cheka
Mcheshi
Mguu
Miguu
Nkindiza
Nkindiza
Mkuki
Mkuki
Mvuvi
Mvuvi
Ulimi
Ndimi
Katika kujibu swali hili tumeligawanya katika sehemu
tatu. Katika sehemu ya kwanza tumetolea maana ya istilahi mbalimbali kwa mujibu
wa wataalamu mbalimbali. Istilahi hizo ni pamoja na maana ya fonolojia,
mofolojia na mofofonolojia, sehemu ya pili tumejadili kiini cha swali ambapo
tumeonesha mazingira mbalimbali ya utokeaji wa data tulizopewa na suluhisho la
wanamofofonolojia katika kutatua matatizo ya kimofofonolojia na sehemu
ya  tumehitimisha kazi na kutoa marejeo. Kwa kuanza na maana ya
istilahi hizo watalaamu wanatueleza kama ifuatavyo;
Massamba na wenzake (2004) wanaeleza kuwa; fonolojia
kama tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji
wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha
za binadamu. Hii ina maana kwamba fonolojia kama tawi la isimu hujishughulisha
hasa na zile sauti ambazo sauti ambazo hutumika kutofautisha maana za maneno
katika lugha mahususi.
John Habwe na Peter Karanja (2004) wanaeleza kuwa;
fonolojia ni utanzu wa isimu unaochunguza jinsi sauti za lugha zinavyofanya
kazi katika lugha mbalimbali. Fonolojia huchunguza jinsi sauti hizo
zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili
kuunda tungo zenye maana.
Hivyo kutokana na maana za wataalamu hawa tuanaweza
kueleza kuwa; fonolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi,
uchambuzi na ufafanuzi wa sauti katika lugha mahususi. Mfano Kiswahili,
Kiingereza Kichina, Kijerumani na Kihaya.
Baada ya kueleza maana ya fonolojia tuanagalie maana
ya mofolojia kulingana na wanataalamu mbalimbali.
Massamba na wenzake (2004) wanaeleza kuwa; mofolojia
ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa
maneno katika lugha.
John Habwe na Peter Karanja (2004) wanatueleza kuwa;
mofolojia ni neno linalotumiwa kumaanisha utanzu wa isimu unaoshughulikia
muundo wa maneno. Fasili hii inamapungufu kwani katika mofolojia
hatushughulikii miundo ya maneno katika lugha bali kinachoshughulikiwa ni
maumbo ya maneno. Miundo ya maneno katika taaluma ya isimu inashughulikiwa na
tawi na sintaksia.
Kutokana na fasili za wataalamu hawa tunaweza kueleza
kuwa; mofolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na
ufafanuzi wa maumbo ya maneno katika lugha. Baada ya kuangalia maana ya
fonolojia na mofolojia ifuatayo ni maana ya mofofonolojia;
Massamba (2010) akimnukuu Martinet (1965) ambapo
Martinet alinukuu kutoka kwa Trubetzkoy (1929) anatueleza kuwa; mofofonolojia
kama ilivyotumiwa na Trubetzkoy ilimanisha sehemu ya isimu ambayo ingeweza
kutumia mofolojia kuelezea tofauti fulani za kifonolojia ambazo zisingeweza
kuelezwa kwa kutumia data za kifonolojia peke yake.
Baada ya kuangalia maana za istilahi mbalimbali
zilizotumika katika swali hili, kifuatacho ni kiini cha swali kinachoonesha
mabadiliko ya sauti yaliyotokea katika data tuliyopewa ambayo ni mabadiliko
kifonolojia  pekee, kimofolojia pekee na kimofofonolojia.
Tukianza na mabadiliko ya kifonolojia pekee, haya
hutokea kwa namna tofauti au katika mazingira tofauti. Kwa mfano mazingira hayo
ni; udondoshaji, uyeyushaji, muungano wa sauti, nazali kuadhiri konsonanti na
konsonanti kuathiri nazali.
Hivyo kutokana na data yetu katika kubainisha
mazingira ya mabadiliko ya sauti  kifonolojia pekee ni kama
ifuatavyo;
                                        Mvuvi     /ɱvuvi/
Badiliko lililotokea hapa ni la kifolojia katika
mchakato wa usilimishaji wa nazali yaani konsonanti kuathiri nazali. Hapa
tunaona kuwa sauti ya midomo /m/ imesilimishwa na kubadili sehemu yake ya
kutamkia na kuchukua sifa ya midomomeno /ɱ/ baada ya kukabiliana na sauti ya
midomomeno /v/. Hivyo sauti /m/ imebadilika na kuwa /ɱ/.
Katika mabadiliko ya sauti ya sauti ya kitambaza /l/
kubadilika na kuwa kipasuo /d/ pia ni mabadiliko ya kifonolojia hii ni katika
neno;
Nlimi       huwa
/ndimi/
Utokeaji wake  ni kutokana na kanuni ya
nazali kuathiri konsonanti. Mazingira ya utokeaji wake ni sauti / /inapokabiliana
na nazali / / yenye sifa ya kutamkiwa sehemu moja
yaani kwenye ufizi hubadilika na kuwa / /.
Pia mabadiliko nazali /n/            kipasuo
cha kaa laini /ŋ/ ni ya kifonolojia ambayo utokeaji wake ni
wakiusilimishaji au kanuni ya konsonanti kuathiri nazali. Mazingira ya utokeaji
wake ni sauti ya nazali kuathiriwa na konsonanti inayoiandamia hivyo kuifanya
nazali kuifuata konsonanti mahali pa kutamkia. Mabadiliko hayo yameathiri sauti
ya nazali /n/ na kutamkwa kama nazali ya  kaa laini /ŋ/.
Hivyo katika uwakilishi litakuwa;
Umbo la ndani /ŋkindiza/
Umbo la nje  nkindiza.
Baada ya kueleza mabadiliko ya kifonolojia, tutazame
mabadiliko ya kimofolojia. Kutokana na data hii tunapata maumbo kama;
Mguu                mi-guu
Haya ni mabadiliko ya kimofolajia. Mazingira ya
utokeaji wake ni mabadiliko ya uongezaji au upachikaji wa  mofimu ya
umoja na wingi ambapo; mofimu m- ya umoja imebadilika na kuwa mofimu mi- katika
wingi.
M-guu     –   umbo
la umoja
Mi-guu  —   umbo la wingi.
Pia katika neno
mkuki          mkuki
mabadiliko yaliyotokea ni ya kimofolojia tu kwani hakuna mabadiko ya umbo na
kinachoonekana ni uwepo wa mofimu m- ya umoja katika umbo hili pamoja na mzizi
-kuki. hivyo kilichofanyika ni kuongeza -kuki katika mofimu hiyo ya umoja na
kupata neno m-kuki. Hivyo umbo hili linabakia na umbo lake ambalo hubakia kuwa
vilevile.
M-kuki      m-kuki maumbo
yote haya yako katika
umoja
Vilevile katika neno
M-dalasini          m-dalasini
hakuna mabadiliko ya kimofolojia bali umbo limeendelea kuwa vilevile la umoja.
Baada ya kuangalia mabadiliko ya kifonolojia na
kimofolojia katika data tulitopewa, kipengele kinachofuatia ni kubainisha
mabadiliko ya sauti yaliyotokea kwa mabadiliko ya kimofofonolojia.
Kutokana na data yetu maneno;
Iba                kuwa
mwizi
Cheka           kuwa                mcheshi
Haya ni mabadiliko ya kimofofonolojia. Sababu ya
kuwepo kwa  mchakato huu ni uwepo wa mbadilishano wa sauti ambayo
hayakuweza kufafanuliwa kwa utaratibu wa fonolojia pekee na utaratibu wa
mofolojia pekee hivyo kukawa na hitaji kubwa kuwa na kiwango kingine cha kuweza
kutatua changamoto hiyo. Kwa hiyo kuibuka kwa mofofonolojia kulikuwa na lengo
la kumaliza changamoto hiyo iliyokuwepo.
 Hivyo katika mabadiliko iba
kuwa          mwizi, sauti ya
kipasuo cha midomo /b/ kubadilika kuwa sauti ya kikwamizi cha ufizi /z/ imesababishwa
na kuwepo kwa irabu /i/ ya unominishaji mwishoni mwa sauti /b/.
kutokana na kitendo cha kuiba tunapata nomino “mwibi” kutokana na mofimu
mu-ib-i hapa konsonanti ya kipasuo cha midomo /b/ hudhoofika na kuwa konsonanti
ya kikwamizi cha ufizi /z/ katika mazingira ya kutanguliwa na irabu ya
unominishaji /i/.
                     iba    /wizi/
Pia katika neno cheka  kuwa   mcheshi mabadiliko
yaliyotokea hapa ni ya kimofofonolojia ambapo sauti ya kipasuo cha kaakaa laini
/k/ inabadilika na kuwa suati ya kikwamizi cha kaka gumu /∫/ baada ya kufuatiwa
na irabu ya unominishaji /i/.
                           Cheka   kuwa
/mče∫i/
Uwepo wa mabadiliko sauti na umbo ambayo hayawezi
kuelezwa, kwa mchakato wa fonolojia na  mchakato wa kimofolojia ndipo
palipoibuka mchakato wa kimofofonolojia.
Katika utatuzi wao wanamofofonolojia walikuja na dhana
ya umbo kiini. Umbo kiini hili liliwakilisha fonimu mbili. Waliteua umbo kiini
kwenye neno la msingi. Na liliwekewa mabano mchirizi { }.
Kwa mfano katika   cheka      kuwa
mcheshi
  Neno la msingi ni “cheka” ambapo
waliteua sauti {K} kuwa umbo kiini. Fonimu {K} iliteuliwa
kuwakilisha /k/ yenyewe katika neno cheka ambalo ni kitenzi na
inawakilisha sauti  /∫ / kwenye “mcheshi” ambayo ni nomino.
                                                                                           /k/
                                                                      {K}
                                                                                           /∫/
Umbokiini   {K}   linawakilisha
sauti  /k/ na /∫/
Pia katika neno iba na wizi umbokiini ambalo
liliteuliwa ni {B} ambayo kuwakilisha sauti /b/ na sauti sauti /z/.
                                                                                              /b/
                                                                        {B}
                                                                                           /z/
Baada ya utatuzi huu baadhi ya
wataalamu  walitoa maoni yao juu ya umbokiini. Baadhi yao ni Linhtner
(1970) akinukuliwa na Massamba (2010) anaeleza kuwa umbo kiini sio halisi ni la
kidhahania na kinasibu kwani halioneshi mchakato na namna ambavyo sauti na umbo
hubadilika na kuwa katika sauti nyingine na kitu gani hasa husababisha
mabadiliko hayo ya sauti. Umbokiini huishia tu katika kuteua sauti moja
kuwakilisha sauti nyingine. Basi huo ukawa udhaifu wa dhana ya umbokiini.
Hitimisho kutokanana wanamofofonolojia kushindwa
kutatua matatizo ya kifonolojia. Hivyo wakaibuka wanafonolojia zalishi ambao
waliokuja na mitazamo mipya katika utatuzi wa matatizo ambayo yalishindwa
kutatuliwa na wanamofofonolojia ambapo walikuja na misingi mipya na mihimili ya
kufuata ili kubainisha mabadiliko yaliyokuwa yanatokea yaliyoshindwa kuelezeka.
 Marejeo.
Habwe, J. na P,
Karanja (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers
Ltd.
Massamba, D.P.B.
na wenzake (2004) Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA): Sekondari na
Vyuo. Dar es Salaam. TUKI.
Massamba, D.P.B.
(2010) Phonological Theory: History and Development. Dar es Salaam:
TUKI.

 

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!