MAANA YA MANENO

By , in Kamusi on . Tagged width:

1. Shwari…………. Utulivu, isiyo na shida
2. Ghali…………. enye gharama kubwa, siyo rahisi
3. Pweza………. kiumbe wa baharini mwenye umbo laini la duara na mikono minane anayeishi chini mwa bahari
4. Uadui……….. hali ya kufanyiana mambo mabaya baina ya watu wa pande mbili. Ukosaji wa huruma, tabia ya kutenda mambo ya ukatili
5. Mzigo……….. kitu chochote kinachofungwa na kubebwa
6. Dereva…….. mtu anayefanya kazi ya kuendesha vyombo vya usafiri kama vile gari na pikipiki
7. Sherehe……. tafrija inayoambatana na shamrashamra inayofanywa ili kuadhimisha tukio fulani la furaha
8. Njaa……….. hisia anayoipata mtu kama matokeo ya mwili kuhitaji chakula
9. Zizi………… boma lililojengwa kama ua linalotumika kwa ajili ya mifugo
10. Kijana…… mtu wa jinsi ya kike au kiume ambaye si mtoto wala si mtu mzima

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!