LEO KATIKA KAMUSI ‘IPI NI TOFAUTI BAINA YA HULKA NA SILKA’

By , in Kamusi on . Tagged width:

Karibu katika KAMUSI.

IPI NI TOFAUTI BAINA YA HULKA NA SILKA.

KAMUSINI leo tunaangazia kuhusu dhana mbili nazo ni Hulka na Silka.

Watumiaji wengi wa lugha ya Kiswahili aghalabu huzitumia dhana hizi katika maelezo yao ya kila siku.

Hata hivyo, wapo baadhi ya wasema lugha huzitumia dhana hizi kwa kuzichanganya au kuzikanganya.

Malala haya ya KAMUSI inapenda kukuletea ufafanuzi kwa ufupi kuhusu dhana hizi.

Tuliyemwalika KAMUSINI leo ni Mzee Mudhihir. M. Mudhihir. Huyu ndiye BwanaKAMUSI wetu kwa Makala haya.

Mzee Mudhihir anaeleza kuwa ; Hulka ni mwenendo/tabia ambayo mtu anaipata kutoka katika mazingira anayokuwa nayo na kutoka kwa watu wanaomzunguuka.

Mazingira hayo hujumuisha wazazi, walezi , rafiki , taasisi za elimu, dini, michezo. Mazingira mengine ni mazingira ya kazi, safari, nk.

Aidha, Hulka inaweza kuwa sifa njema au mbaya. Husikika watu kwa mfano, Fulani ana hulka mbaya.

Kwa upande wa Silika (silka) , Mzee Mudhihir anaendelea kueleza Silka ni tabia/sifa ambazo mtu huzaliwa nazo kama vile furaha, huzuni, kupenda, kuchukia n.k. Kwa hiyo, inaweza kusemwa kuwa silka ni jambo la kimaumbile ( Kinasaba), hivyo mtu huweza kurithi silka kutoka kwa mzazi wake.

Kwa mintarafu hii , upo uwezekano wa kumfanya mja awe na hulka fulani lakini si silka. Kwa sababu silka mtu huipata tu kutokana na maumbile yake.

Makala haya KAMUSI yanahoji iwapo ni sawa kusema kuwa mtu fulani ana silka mbaya?

Je, una maoni gani kutokana na Makala haya ya KAMUSI hii leo.

Tunaomba maoni yako hapa katika ukurasa wetu au tuandikie kupitia : majidkiswahili@gmail.com au +,255 715 838480.

Kongole Maalum kwa BwanaKamusi wa Makala haya, Mzee Mudhihir, M. Mudhihiri ( Mwele bin Taaban).

Majid Mswahili
#Bwanakamusi.
Mchambuzi wa Lugha , Fasihi na Fasaha ya Kiswahili.

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!