LEO KATIKA KAMUSI ‘Baadhi ya maneno yanayotumika vibaya’

By , in Kamusi on .

Karibu katika KAMUSI.

KAMUSINI LEO tunaendelea kusaidia kutoa uelewa kuhusu maneno ya Kiswahili.

Baadhi ya maneno yanayotumika vibaya
1. Mbele/Mbeleni
Neno mbele linaweza kuwa na maana ya siku au tarehe za usoni. Mfano: Tarehe ya uchaguzi imesogezwa mbele.
Mbele pia ina maana ya usoni mwa kitu au mtu, kama vile mbele ya macho, mbele ya watu. Lakini neno ‘mbele’ likiongezewa kipashio ‘ni’ na kuwa ‘mbeleni’, basi kwa silka na adabu za Waswahili neno hilo hugeuka kuwa tusi, lenye maana ya sehemu za siri za mwanamke. Hivyo, maneno mawili haya si vibadala, kila moja lina maana yake.
2. Husika
Sifa moja ya vitenzi vya Kiswahili ni kuchukua viambishi vya mtenda, wakati na mtendwa. Vipashio hivyo vina dhima, maana na matumizi maalumu vinapotumika, kama vile kubadilisha nafsi ya mtenda na mtendwa, ngeli, kuonesha umoja na wingi na wakati wa kutokea kwa tendo. Kwa mfano:
mtu – a_nayekusika – watu wa_naohusika
gari – i_nayohusika – gari zi_lizohusika
kazi – i_takayohusika – kazi zi_takazohusika
Kutumia neno husika bila kuliambatanisha na vipashio vyake vya mtenda, mtendwa na wakati ni kukiuka taratibu za sarufi ya lugha zilizokubalika bila ya kuwa na sababu za msingi.
3. Mrabaha
Baadhi ya watumiaji wa lugha ya Kiswahili kwa kutojua au kutokuwa makini wanalitamka neno hili kwa kuzibadilisha nafasi za silabi ‘ba’ na ‘ha’ na kulitamka #mrahaba, yaani linazalisha neno jipya ambalo hata halimo katika lugha.

Makala haya ya KAMUSI inakushajiisheni wafuatiliaje wa nakala haya hasa wanahabari kumanikia usanifu wa lugha ya kutangazia habari zao.

#Usithubutu Kupitwa na Makala ya Kamusi.

KAMUSI imeletwa kwenu kwa hisani ya BAKIZA #KamusiLaKiswahiliFasaha na #Tamthiliya ya NjeNdani.

Majid Mswahili
#Bwanakamusi.
Mchambuzi wa Lugha, Fasihi na Fasaha ya Kiswahili.

Tuandikie : majidkiswahili@gmail.com Au + 255 715 838480

Facebook Comments
Recommended articles